Massimo yaanda mbio za baiskeli Dodoma

KLABU ya mbio za baiskeli ya Massimo ya mjini Dodoma, imeandaa shindano maalum kwa ajili ya Siku ya Ukimwi Duniani zitakazofanyika Desemba Mosi, mwaka huu mjini humo.
Kwa mujibu wa mratibu wa mbio hizo za kilomita 135, Nicola Morganti, uandikishaji wa washiriki utafanyika siku moja kabla ya shindano kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Hata hivyo mshauri huyo wa klabu ya Massimo alisema bado wanahitaji kwa udi na uvumba wadhamini wa mbio hizo za aina yake.
“Udhamini ni tatizo, inatufanya tushindwe kufanya mambo makubwa zaidi, lakini kwa kadri ya uwezo wetu tunajitajidi kuandaa ili kuendelea kuyafanya kuwa ya kila mwaka,” alisema Morganti ambaye ni raia wa Italia.
Mbio hizo ambazo mshindi wake atajinyakulia kitita cha sh 100,000, zimepangwa kuanzia Dodoma Mjini na kufuata barabara ya Dar es Salaam hadi eneo la Mbande, linalotenganisha wilaya za Dodoma na Kongwa.
“Kutokana na kukosa wadhamini, hata zawadi zetu zimekuwa ndogo, lakini tukipata wa kutuokoa angalau kwa wakati huu, mambo yanaweza kuwa mazuri zaidi katika mashindano yetu na ustawi wa mbio za baiskeli kwa ujumla nchini,” alisema Morganti, akiongeza kwamba, mshindi wa pili atajipatia sh 75,000 wakati mshindi wa tatu atajinyakulia sh 50,000.
Washiriki wawili watakaoshika nafasi za nne na tano kila mmoja atajipatia sh 25,000, wakati watakaoshika nafasi kati ya sita na 10 kila mmoja atapata sh 10,000. Kifuata jasho cha sh 5,000 kitakwenda kwa washiriki watakaoshika nafasi kati ya 11 na 20.

KWA MAWASILIANO ZAIDI;
The Team Leader
Luis Musisi
0757622633
P.O. BOX 2938
Dodoma
The Advisor,Nicola Morganti,0782490917,
dodocola@maf.or.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...