kaka michuzi,
jana mgomo uliendelea hapa chuoni (Ardhi) ila ilipofika mida ya mchana hivi kwa wale wenye akaunti crdb waliekewa hela zao za project,sasa najiuliza hivi,kwanini linapokuja suala la fedha kwenye taasisi za elimu ya juu hazitoki mpaka watu tugome??
Kwa upande mwingine leo jumatano wanafunzi wote tumeingia madarasani huku tukisubiri muongozo kutoka kwa wanaharakati wetu(sio viongozi) kwani mpaka sasa viongozi wetu wa serikali ya wanafunzi hawajatuonesha ushirikiano wowote kuhusu matatizo yetu, sanasana wametubandikia orodha ya majina ya wanafunzi ambao hawajalipa fedha yao ya serikali tunayooiita 'union fees'
Kwakweli najiuliza viongozi wetu wamegoma kutupa ushirikiano kwakuwa hatujalipa hela au??mimi sidhani kama hiyo ni sababu,kwani hata katika semester zilizopita hela tumekuwa tukilipa kwenye serikali yetu lakini matatizo yapo palepale,,wengi wao ni puppet yani hawawezi kujiongoza wenyewe.
kwa ufupi tu ni kwamba tunasubiri wanaharakati wetu waliojitoa muhanga kwa ajili yetu watuambie nini kitafuata ama baada ya mgomo wetu huo wa siku mbili.kazi njema kaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hizo pesa mngepewa tu bila kugoma, ni kwamba tu hamna uvumilivu, na mmeshaingiwa na kaugonjwa ka kuamini kwamba kupata pesa za field ni lazima mgome kwanza. Hivi mnadhani mnapokuwa mmegoma, kama hizo pesa hazipo zitapatikana wapi? Huko zilikopatikana pesa za kuwapa baada ya kugoma ndiko zingepatikana pia za kuwapa hata kama msingegoma. Mnaposomeshwa, wasomeshaji wenu (waalimu, na wadhamini) wanataka mpate elimu bora. Hakuna asiyeelewa kuwa field ni muhimu. Kama wasingeona umuhimu wa hiyo field wasingeiweka kwenye curriculum, na sijui kama isingekuwepo hiyo mngejuaje kuna suala la field na hela zinatakiwa! Kwa vile wasomeshaji wenu wanaujua umuhimu wa field, hiyo hela wangewapa tu muende field. Na hata kama msingegoma, ingechukua muda huohuo kupatikana hizo hela za field. Mimi nadhani huko vyuoni sasa hivi tuna kizazi cha vijana waliokosa busara, akili zao zimejaa "bongo fleva" tu, ni kama watoto wadogo kabisa. Tabia ya mtoto mdogo wa miaka 3 au 4 hivi ni kwamba huwa hafikirii zaidi ya kile kitu anachohitaji kwa wakati ule. Kama amezoea kupewa uji saa 4 asubuhi, basi muda ukifika akisikia njaa anataka uji wake. Hata kama mama amepoteza kazi kwa hiyo hana hela ya kununua unga na baba ni mgonjwa kalazwa hospitali, mtoto hana habari, anataka uji wake. Na ataangua kilio kwelikweli, haelewi kabisa kwa nini asipewe uji wakati ana njaa! Hayo mazingira yaliyosababisha uji usipatikane siku hiyo hawezi kuyaelewa, akili yake bado changa, kwa hiyo mtoto huyo tunamsamehe. Sasa hawa vijana wa vyuo vikuu vya siku hizi naona akili zao ziko kama za hao chekechea. Nadhani inafaa wawekewe bembea huko vyuoni na wapangishwe foleni za kupewa uji kila asubuhi, ndio kiwango cha uelewa wanachotuonesha. Kila siku migomo tu, tena ya kijinga kabisa kama zile temper tantrums za watoto wa chekechea! Na huko vyuoni wanashindwa nini kuweka sheria kali, kwamba anayegoma afukuzwe tu moja kwa moja bila kurudishwa, hata wakigoma wote, fukuza wote walimu waende likizo au wafanye kazi nyingine (ziko nyingi tu) hadi next academic year, na sheria iwekwe kwamba aliyekwisha kufukuzwa kwa sababu ya migomo asirudi tena hata kwa ku-apply, atafute vyuo vingine huko duniani kwa hela yake mwenyewe. Tuone kama hawatashika adabu. Tutapata hasara kiasi ya mwaka mmoja, bora, lakini watakaofuata watafyata.

    Nakuomba ndugu Michuzi, najua una access na Mzee wetu muungwana JK, naomba umpendekezee jina langu anipe madaraka ya u-VC kwenye chuo kimoja, miaka 3 tu nitawale kwa mkono wa chuma, uone mabadiliko. Na digrii zitapatikana za kiwango cha juu sana, maana nitakuwa sina utani, machezo wala huruma. Kazi itakuwa moja tu, kusomesha wanaotaka kusoma, na kuondoa "makapi" au "magugu" yote ya wapenda vurugu wanaosumbua wenzao. Hawa watoto wa siku hizi ukiwaongoza kidemokrasia wanakuona mdebwedo! Ukimchekea nyani shambani utavuna mabua!

    Brian J.Y. Kithuku

    ReplyDelete
  2. TIT FOR TAT........kama nyinyi hamjalipwa hela mkagoma sasa kwanini serikali ya wanafunzi wasigome kutoa ushirikiano wakati nyinyi hamjawalipa union fee???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...