Wadau,
nawaombeni munisaidie kwenye hii mada; nimeombwa niongelee juu ya economic development in tanzania hapa kwenye chuo kikuu huku czech republic, before colonisation and now. sina moja. naombeni michango yenu.
natanguliza asante zangu.
nana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Nana anahitaji msaada na ni kweli ukiwa ughaibuni halafu data huna za nchi yako inakuwa tatizo at times. Tungeomba E-mail ya Nana tumshauri ila kwa sasa anaweza kutumia website ya serikali hasa aangalie Ministry of Planning and Economic Empowerment then aangalie data kutoka web. ya National Bureau of Statistics; www.nbs.go.tz
    Mimi Mdau Mnzava, Ernest

    ReplyDelete
  2. http://unpan1.un.org/intradoc/groups/public/documents/AAPAM/UNPAN028082.pdf

    ReplyDelete
  3. Hakuna Mtu anaitwa Nana from Tanzania hapa Czech Republic. Kama anahitaji hizo nondo aje kwangu nitampa. Watanzania wote tuliopo hapa twafahamiana.

    ReplyDelete
  4. kama kuna mtanzania anayeitwa Nana hapa Czech Republic basi hajawasiliana na watanzania walio hapa,sio kosa inawezekana hukujua jinsi ya kuwatafuta.kuna Prof wa Uchumi mtanzania hapa Czech na anaweza kukupa details za uchumi unazohitaji.andika anuani yako humu ndugu zako tutakutafuta na msaaa inshaalah utapata...zemarcopolo.

    ReplyDelete
  5. Of course, "NANA" is jina la kuombea msaada,hasa ukizingatia nature ya msaada unaoombwa.Huyu mtu ni wale tuliokuwa tunawaita VILAZA pale UDSM.Yaani siamini kama mtu anayedai kuwa chuo kikuu atakwama kwenye mada nyepesi kama hii,ambayo ni miongoni mwa zilizozoeleka hapa kwenye pubs kwa wale "waliokwepa umande".We NANA,usiwe mzembe,tumia internet kuchangamsha ubongo wako na usiikwepe maktaba ya chuo (kama ipo,maana huko Czech nako kama hakutabiriki).Pole NANA,ndio ukubwa huo,next time ukibabatizwa scholarship,angalia kwa makini kama utaimudu.

    ReplyDelete
  6. Mas Pravdu Vule acha masifa wewe, sio lazima umjyue kila mtu alieko chekirepabubliki. Pili nana anaeza kuwa ametumia alias name si lazima atumie jina kamili, tatu kama una nondo si useme tu zinapatikana wapi ili nana asome kisha kisha akazitafute mwenyewe?

    Na wewe Nana moja ya sababu ya wewe kwenda shule ni wewe kutafuta material kwa ujanja wako sio kuomba omba material kwenye net. Elimu yako mama fanya fanya ujanja ndio mana ya kusoma hiyo!

    ReplyDelete
  7. JITUKABEJA! Hahahahaaa

    ReplyDelete
  8. Ningependa sana uongelee pia juu ya "perspective" mpya ya kuangalia uchumi usiopimika kutokana na "market value". Huu si uchumi wa njia za panya (underground economy)!

    Kwa mfano, rafiki yako akija kukutembelea, utamchinjia kuku hata mbuzi kwa ajili yangu. Kuna "goods" na "services" nyingi sana ambazo haziwezi kupimwa ki-soko. Ukitaka kujenga nyumba, unaalika jirani na marafiki kukusaidia.

    Kwa kifupi, uchumi wa namna hiyo si wa "barter" bali unatokana na mfumo wa kuwa "both the producer and consumer of goods and services".

    Mihogo, viazi, mahindi, maharage, machngwa, ndizi, na kadhalika, zinatoka mashambani moja kwa moja hadi mdomoni bila kupitia "Kariakoo Market au
    "supermarket ya Shoprite" (CHEKA)!

    Uchumi wa namna hii umekidhi sana mahitaji ya "survival" yetu kabla ya ukoloni (na hata sasa) na kutufanya kuwa "resilient" maishani.

    Wenye kupendelea "perspective" hii, wanauita mfumo wa uchumi huo kuwa "prosumerism": Wazalishaji wanakula vile wanavyozalisha (wanakuwa "prosumers", kwa mfano wakulima wetu huko vijijini.

    Kutoka na hilo, ni vigumu sana kuweza kukadiria "gross national product" ya "the total market value of all the goods and services produced by a nation during a specified period."

    Bila hata ku-"regurgitate" matakwimu mengi, nadhani ukiendeleza pointi hiyo, inaweza kuinua hadhi ya kile utakachokizungumzia.

    Nakutakia kila la heri!!!

    ReplyDelete
  9. Nana, elimu ni kushea material. Hebu tafuta kitabu cha Prof Abdul Sheriff (1987). Slaves, Spices & Ivory in Zanzibar. Kimechapishwa na James Currey (Oxford), Mkuki na Nyota Publishers (Dar es Salaam), Ohio University Press (USA) na E. A. E. P (Nairobi). Unaweza pia kukitafuta kutoka kwa African Books Collective Ltd, Oxford, UK. Kwa kutumia kitabu hiki na sources nyingine utaweza kutengeneza sythesis ya kuvutia kuhusu Economic Development in Pre-Colonial Tanzania.

    Kila la kheri.

    ReplyDelete
  10. nana Internet hamna huko Czech? mbona kila siku tunafanya jusi tu ni memaliza research yangu ya mchango wa mwanamke katika third world countries. Na wala sikuomba msaada...please usituangushe...do your homework okay

    B ya kwako ni nzuri kuliko A ya mwezio ....hehehehehheeeeeeee

    ReplyDelete
  11. huyo anayesema hakuna nana czech republic, mbona mie nipo brno, na siyo mwanafunzi ndo maana hunijui, lakini nimealikwa kama mtanzania, kutoa speech of economy in my country. sio vibaya kuomba msaada, na kumsaidia mtu siyo mpaka umjue. nashukuru kwa the first two people, they gave me a very useful website. thanks.
    nana

    ReplyDelete
  12. Nana Mtanzania mwenzetu, kama kweli upo Brno na unadai kuwa watu (watanzania) siyo lazima wakujue, then sioni sababu yako wewe kuomba msaada wa watanzania ambao si lazima wakujue. Sasa hapo Brno ulipo ndipo alipo Prof wa uchumi (Mtanzania) anasomesha ktk chuo kikuu kimojawapo hapo Brno kama alivyokuelekeza ZEMARCOPOLO. Kama unaishi karibu na HLAVNI NADRAZI then kwa tram hadi chuoni kwake ni four stops.
    ALL the best Nana na acha ghadhabu.
    NB: email yangu ni revdevm@yahoo.co.uk
    BY the way tarehe 08.12.2007 kuanzia saa 10 jioni, FRED's corner , Dejvicka - PRAGUE, tutakuwa na uhuru dei yetu. Karibu ujumuike nasi watanzania wenzako.

    ReplyDelete
  13. Oyaa masela acheni tabia ya kijinga ya kuongea majineno utadhani mnataka kuharisha hii web tuitumie kwa ajili ya manufaa yetu ni isigeuke kama sehemu ya kusengenyana na kuongea mijineno ambayo haina kichwa wala miguu.Heshima ni kitu ya bure hata kama nana ni mbongo au myaudi lakini mshikaji kauliza ajibiwe acheni ushamba ambao hauna kichwa wala miguu bali masifa na kujifanya unajua kuongea!Mimi nafikili kuna mijitu mingine haina cha kuandika na inaandika utafikili ina uhalisho wa maneno, Guys get a grip and get real!this is not a place for messing around.

    ReplyDelete
  14. Huyu Gangwemsemakweli nakifiri ndo anayetaka kuharisha. Mbona naona jamaa wote wanaongea point na mna ya kumsaidia huyo "myaudi". So Gangwemsemakweli be realistic.

    ReplyDelete
  15. NANA UNATAFUTA RAFIKI WA INTANETI AU WAKUSOMA NAE...NENDA KWENYE UHURU DEI WAMESHA KUKARIBISHA.

    ReplyDelete
  16. Nana, pole kwa kupewa assignment hiyo lakini nakushauri get into Google and type Marc Wuyt utapata papers zake nyingi za kichumi hasa kuhusu Tanzania particularly hito topic uliyopewa
    Vilevile log to www.esrf.or.tz
    Nakutakia kila la heri katika changamoto hiyo

    ReplyDelete
  17. kama una nia ya kusaidia utafanya hvyo kama wengine walivyofanya....lakini kumkandia na kumkebehi mwenzenu sio ustaraabu....she is desperate, she needs help and the first thought which came to her was this blog...what is the big deal jamani? Lets share and in a postive way...Pole Nana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...