Brother Michu,
Salaam Alaykum.Naomba nifikishie salamu zangu za pongezi kwa uongozi mzima wa ATC hususan rubani wa leo aliyetajwa kwa jina la Muze.
Katika hali isiyo ya kawaida nikitokea Dar kuja Arusha leo asubuhi, Rubani huyu aliamua kwa makusudi mazima kutupitisha juu ya mlima kilimanjaro ili kila mtu aliyekuwemo kwenye ndege auone kwa karibu saaaaaaana mlima huo na aliuzunguka kwa karibu dakika kumi hivi ila kila mwenye camera aweze kuchukua picha hiyo adimu kwa karibu na kwa ufasaha.
Bahati mbaya kinyamkwemba changu nilikuwa nimekisahau dar hivyo sikuweza kufotoa hiyo picha ili nishee na wadau wa blog hii but it was veeeery exciting!!!
Nilipenda maneno ya rubani " COURTESY OF AIR TANZANIA TO PROMOTE OUR MOUNTAIN AND WITNESS HOW GLOBAL WARMING AFFECTS THE SNOW TOP OF KILIMANJARO PLEASE HAVE A CLOSER LOOK AND IF POSSIBLE TAKE A PHOTOGRAPH FOR THOSE WITH CAMERA"
shukrani ATC
Mdau,
Mani-yuu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. I had a similar experience mwaka juzi nikisafiri katika Precision Air kwenda Arusha. It is indeed very exciting!! I feel your pain Mani-Yuu!

    ReplyDelete
  2. inatia moyo kuona ndege za tanzania zimefikia hatu nzuri, ya kutitangaza nchi. ni view nzuri, hasa kwa wageni, na lazima tujivunie. hongera kwake pilot.
    nana

    ReplyDelete
  3. Nina uhakika Rubani huyu alikuwa na nia nzuri. Lakini, wakati ana zungumzia tatizo la global warming alafu anatumia dk kumi kuzunguka mlima je na yeye si anachangia tatizo hilo?

    Fikiria kama ndege zote zinazopita hapo zitafanya hivyo CO2 si itachangia zaidi tatizo? Nchi zingine zinazungumzia kuongeza ushuru wa usafiri wa hewa kwa sababu uchangiaji wa tatizo la hali ya hewa yeye anafanya kinyume chake. mat

    ReplyDelete
  4. kweli wa kupewa hongera ni pilot lakini sio ATC,kumradhi kwa hilo! kwa juhudi zake na ustadi wake wa kutoa service makini akaamua kukunja karibu na limilima letu, kilimanjaro ili wateja wake wapate uhondo huo! juhudi binafsi kama hizi zinatakiwa kuigwa na Watanzania wote ili kuweza kufanikisha maendeleo kwa mfano muda wakufika ndege zetu utaboreka katika kuchukua abiria na kuwafikisha wanakokwenda katika utaratibu uliopangwa!

    Evan wa Mwanza

    ReplyDelete
  5. alimaliza mafuta ya bure tu kwa kupenda sifa, ndo maana nauli zinapanda bei sababu ya sifa kama hizi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...