habari toka mwisho wa reli zinasema treni la abiria toka kigoma limekwama sehemu za kaliua siku ya nne leo na wadau wanasota ile mbaya. hii ni mara ya tatu kwa usafiri huu kuleta noma toka ulipoanza upya tokea stesheni ya dar kwenda bara siku ya novemba 1, 2007

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. yaani katika huo mwezi 1, train kasheshe mara 3,,mbona mambo, halafu eti bongo tambarare, mmh bora nibebe boksi langu nchi za watu huku...haya weee, kufikia mwakani mwezi kama huu, litakuwa limechemsha mara ngapi?
    3*1=3(novemba)
    3*12(mwaka)=36times + kipindi cha mvua mara (x)??unpredictable
    TRAIN CHOKA MBAYA..

    ReplyDelete
  2. Unategemea nini? Reli toka alivyojenga mjeremani kabla ya vita kuu ya kwanza ya dunia!! Na somo la kukarabati au kukaravati hata sijui hapo neno gani nitumie (Michuzi yule mwalimu wako wa kiswahili fasaha yuko online anisaidie kidogo)bado halijaeleweka vizuri.

    Miundominu ni tatizo hasa reli, na mabehewe yenyewe, halafu na watu nao kwa kuiba mataruma ya reli!! Hii yote imeletwa na biashara ya chuma chakavu, mwe!

    Wewe nawe unashobokea nchi ya watu!!! ina wenyewe hiyo USIONE VYALEA! Pengine walikufa watu kujenga hayo mamiundominu unayijifagilia nayo tena kutoka huko visiwa vya carribean!!

    ReplyDelete
  3. hao wahindi wawekezaji inaonekana ni matapeli tuu hawana lolote na sijui kama wataleta chochote cha maana katika usafiri wa Train,angalia hata trains zenyewe ni zile zile tuu,hawa wapuuzi wamekuja kukusanya pesa za ticket tuu,yaani viongozi wetu ni mbumbumbu sana huwezi kuamini wanachofanya hao matapeli wao wameshindwa...ni aibu tupu na inatia hasira sana na hawa mbulukenge,walishindwa kuendesha ATC wakaja makaburu wakajichotea bila kutuletea huduma yeyote ya maana na sasa wamejiondokea na pesa kibao,angalia TANESCO ni upuuzi mtupu...jamani mimi naona bora mzungu arudi tumpe kila kitu atuendeshee mpaka ikulu la sivyo maendeleo tusahau

    ReplyDelete
  4. Bongo tambarare weweeeeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  5. mr chuzzi,"mimi fikiri bongo tamberere,pana iko jua train only lay dat.mimi iko tuma juma inende engelia lafu mimi iko fanyasawa"!!!!!!!!!!!!ok?
    mgosi nilisema huyawezi ni afahali uje msufini uuze kachori zakona samosa upate tiketi ya kurudi bombay...!!!!!!utupunguzie kiwingu.

    ReplyDelete
  6. Kwanini isikwame wakati inatembea kama Jyoti.

    ReplyDelete
  7. TRC imekuja baada ya TTCL, Urafiki, ATC na listi bado inaendelea. Tatizo sio kwamba eti reli ni ya kizamani, jamani katika Africa kuna mtu anafahamu kuwa kuna wakati reli iliyokuwa na ufanisi zaidi ilikuwa ya Sudan? wa nini wakati nchi yenyewe uimekuwa vitani forever, sababu ni kwamba waliamua kijeshi kuwa lazima ifanikiwe. Sisi nyumbani hata wakati tunafanya ubinafsishaji wa TRC (kama ambavyo tulivyofanya mashirika mengine hapo ju na mengine mengi tuuu) hatukuwa tunajua ni nini kile tunataka, au wadhungu wanasema "performance criteria/index". Sasa TRC wamepewa wakubwa kutoka nje kuongeza ufanisi. Lakini jamani, ufanisi utaongezwa na mtu/kampuni yenye ufanisi....... Hao jamaa bwana ni kalaghabaho kinoma. Wewe ukiambiwa India ni nchi yenye kampuni/shirika moja lenye wafanyakazi wengi kuliko popote duniani utakubali? Hilo shirika/kampuni ni Indian Railways, hilo likampuni lina wafanyakazi 1,000,000.....Ufanisi?? hapo usiulize nenda kaangalie kwa macho yako.... kasheshe mtiiindo mmoja.

    Mungu Ibariki Tanzania na Watu Wake...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...