Hi Michu,
Naomba unipostie hii article kwenye blog yako ili niweze kujua watanzania wenzangu wanaoishi hapa UK wanalionaje swala hili, mimi binafsi naona ni ubaguzi na unyonyaji wa waziwazi, akhsante.

'NO RECOURSE TO PUBLIC FUNDS' ni sentensi fupi tu ambayo inaonekana kwenye visa yangu, na to be frank, sikujali sana kutafuta maana ya maneno hayo miaka mitano iliyopita waliponigongea.Hii sentensi inamaanisha siwezi ku claim benefit, tax credit wala housing assistance. Jamani huu si unyonyaji? Ukizingatia wageni kama mimi tunatwanga mzigo kila siku, tena masaa kibao na kuna mizungu haifanyi kazi kabisa, inaishi kwa kutegemea hizo benefits tu, some of them have never done any paid work in their lives. Ni kama wanakula jasho letu tu, tax tunazolipa makazini ndo walipwa wao, huu nauona kama ubaguzi pia. So so unfair.
Kana-Ka-Nsungu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. I have one short answer for you, If you do not like it COMEBACK HOME else leave by their rules, It is what it is. You got to do what you got to do pal.

    ReplyDelete
  2. Piga ze boxxxiz mzee!! Unalia lia nini kwani ulilazimishwa kwenda huko?

    Kama unaona sio fea warudishie viza njoo Bongo ule vumbi.

    ReplyDelete
  3. KILA NCHI INASHERIA ZAKE HAMNA UNYONYAJI WOWOTE. HUKO NCHI YAO NA LAZIMA UFATE MASHARTI YAO KAMA UNAONA UNANYONYWA PANDA PIPA RUDI HUKU MINAZI MIREFU.SWALI DOGO NAKUULIZA KAMA HIO SHERIA UNGEJUA TOKA MWANZO UNGENGATAA VIZA YAO?NA HIZO HELA WANAZOPEWA RAIA WAO POWA TU INAMAANISHA WANAWAJALI WANANCHI WAO.MCHEZA KWAO UTUZWA HAO WAKO KWAO HAPO NDIO WAMETUZWA NA WEWE RUDI NYUMBANI UJE KUTUZWA.JIFUNZE KUSHUKURU CHOCHOTE UNACHOKIPATA KWANI KUNAWAZAKO HATA ROBO YA HIO UNAYOPATA HAWANA.KAMA UNAONA KIPATO KIDOGO KULIKO HUKU NYUMBANI BASI RUDI NYUMBANI.

    ReplyDelete
  4. unamaliza lini kusoma?rudi yumbani gemu ni nzito hii,wageni tupo wengi wanaamua kwa upande wao,pole sana-Tukupya Tuli nkakoloboji,London

    ReplyDelete
  5. Hey! unavyofanya kazi una kibali cha kazi? Kama unacho basi unaruhusiwa kufile tax zako...lakini kama kibali huna basi you have no saying....Na kama umjanja bazi raie dependants uwe unakatwa tax kidogo tu kwa vile hutaifile at the end of the year...

    Benefits ni za wazawa wao wewe una kwenu mambo yakikushinda rudi kwenu..wanamaana hiyo...their plate is full they don't want any more of you there

    ReplyDelete
  6. Mjini shule kulala na njaa uamuzi wako. Ukishindwa kurudi minazi mirefu tafuta mbinu za kupata benefit. Akili kichwani

    ReplyDelete
  7. Hivi wewe ulipoandikiwa hivyo kwenye viza yako kwa nini hukuhoji pale pale umekaa wee mpaka miaka mitano imepita ndio unahoji kulikoni?

    Si ndio nyie kwenye blogu humu mnatamba huko maisha mazuri bongo mavumbi, sijui kuchafu. Sasa unategemea huo usafi na hiyo miundombinu na uzuri wotee huo mnaojisifia mnafaidi utakuwa maintaned na nini kama si hayo makodi. Wenyewe wana mzigo wa kulea wazee wao ambao ni wengi kuliko vijana, bado na vijana wao wasiotaka kufanya kazi hizo ambazo nyie mnafanya tena wakupe na fund uhamie moja kwa moja? Hiyo ni njia ya kukwambia you are not part of us, rudi kwenu.

    Kama unaona unaweza kuishi hapo bila hizo benefits fine lakini kama maisha magumu, ndugu yangu anza kuapply kazi bongo ujirudie zako ukale mishikaki ya mahindi na samaki wa kukaanga wenye vumbi!

    ReplyDelete
  8. Siku zote kama wewe ni mgeni katika nchi ya watu, mazingira ya ile nchi uliyoko yanakuwa na disadvantage kwako. Sijui sheria ya Immigration za U.K lakini kwa U.S. sheria za uhamiaji haziwapi favor wageni. Kwa mfano:
    Kama ni ada kwenye vyuo vikuu vya majimbo, wageni (non immigrants) tunalipa zaidi ya in state na out of state rates.
    Kazi..ili ufanye kazi kihalali (kama ni mwanafunzi, nje ya campus) lazima uwe na work permit ambayo its only good for 1 year na ikiisha lazima u-i renew, na haina guarantee kama utapewa U.S. Citizenship and Immigration Services (USCSI) wanaweza kukunyima vile vile na fee yako ya $220 inakunywa maji.
    Drivers license ndizo hizo zimeanza kuwa issue kwa ajili ya mambo ya Terrorism, sasa hivi kwa baadhi ya States kama vile, MN ukiomba license na wewe ni mwanafunzi wa kigeni lazima waweke tarehe ambayo I-20 yako ina expire. Hii ni kuwarahisishia kazi Polisi incase siku ukikamatwa na makosa ya barabarani huku una records mbaya...at the same time ume over stay visa kuwa deported.
    Kwa hiyo in general maisha ya wageni(non immigrants) ni magumu na hizi sheria zimewekwa PURPOSELY ku discourage wageni. Ukiwa mgeni huwezi ku qualify kwa housing assistance, wala food stamps, wala welfare. Ila kitu kimoja ninachoipendea hii system ni kwamba hata kama ukiwa illegal ukapata medical emergency na hauna dime...utatibiwa na bills zako za hospitali zitakuwa written off. Thats the only place ambayo wageni wanapata break...vinginevyo mambo ngumu tu.
    Ila kama unajua ni nini unatafuta...ukavumilia, ukachapa kazi, shule, whatever brought you abroad, after a certain period of time kwa kweli mambo yatabadilika.

    ReplyDelete
  9. Hi Kana-Ka-Nsungu
    ningekua mimi wewe,ninge funga mdomo wangu nikaendelea kuiba.Mpaka umepewa stamp ina sema no recourse to public funds ina maana umekuja kutembea au ki uanafunzi,na kama ni student umepewa masaa 16 kwa wiki ya kufanya kazi,na mwanafunzi anakuja kwa ku dhaminiwa,mbele ya mzungu ni kwamba mdhamini wako anakulipia huitaji kufanya kazi kwahiyo mzungu kakupendelea kukupa masaa 16 yakufanya kazi.Hizo public funds unazoona una haki nazo acha nikwambie huna haki,wenye haki ni wazawa na wanao ishi nchini permanently wewe obviously una bangaiza kazi na visa mshikemshike kwenye ku renew,why dont you just quit whining and keep hiding till the day they deport you.

    ReplyDelete
  10. kazi bila vibali hizo,wengine tumo humuhumu hatuna mihuri kama hiyo

    ReplyDelete
  11. pole sana,
    mimi nina permanent residence, ambapo ninaishi nchi hii kama raia mwenzao sasa. lakini sina mafao yoyote ninayopata kama social support, napata medical care ya bure tuu kama wananchi wote, but im not entitled to get the unemployed benefit!!! ni sheria za nchi, huwezi shindana nazo, its either do or dont.

    ReplyDelete
  12. Huyu ni michuzi kaandika miswahada yake hamna cha mtu aliyekaa miaka mitano aje kulalamika leo...wageni ndio wanaona shida. kama wewe umekaa miaka mitano bado hujavumbua njia ya kuishi hapa na mpaka leo upo hapa unalalamika basi rudi nyumbani mjini hukuwezi...

    ReplyDelete
  13. mhhh hata huku japan ni hayo hayo, mgeni hana benefits zozote!!!

    ReplyDelete
  14. mhh mambo ya mamtoni hayooo

    ReplyDelete
  15. ISSA NAOMBA KUIMBA WIMBO WA ZAMANI KIDOGO.

    KANA KANSUNGU AEEE KANA KANSUNGU KALAGESYE X2

    AKA KAWIMBO BADO NINAKAKUMBUKA..

    ReplyDelete
  16. Sheria za upendeleo kwa raia wa nchi zipo kila mahala hata hapo Tanzania pia.
    Ukijiunga na chuo chochote hapo Tanzania mgeni lazima utalipa karo zaidi ya raia wa Tanzania.
    Pia ukitembelea mahoteli makubwa ya hapo Tanzania gharama za malazi zinategemea kama wewe ni raia wa Tanzania au mgeni, mgeni hutozwa bei kubwa kuliko raia wa Tanzania.
    Hiyo ni mifano michache hivyo 'unashangaa nini???' ndo kilimwengu hivyo ndugu yangu hakuna unyoyaji.
    Mdau
    Cancun, Mexico.

    ReplyDelete
  17. Michuzi sasa unataka kuwa urojo mbona hupost mada za maana tukajadili unatuletea upumbavu wa mtoto wa mama alieenda kujaribu maisha majuu, si arudi anataka benefit ye'mwingereza? Miaka mitano ya ujinga wake ndo leo anatuletea hapa!. shwini.

    ReplyDelete
  18. kama upendi rudi kwenu ukadahi public funds za bongo

    ReplyDelete
  19. Jamani inanifurahisha sana kusoma comment zenu wote. U dont know, but i believe this will help young people in this country wenye mawazo kwamba ukishapanda pipa mambo yako mswano..wenzenu wanataabika jamani!Sasa wewe ulieleta hii mada ndio unasikitisha kupita neno lenyewe!Hii ni type ya ile mijitu ambayo haina shukrani,at the end of the day,inataka haki sawa na wenye kwao..na hii ndio ile mijitu ambayo inasahau ilikotoka kwa urahisi!hebu rudisha makalio huku maana umeshajichokea!inaonekana ulienda kusoma but ndio nyie nyie kila siku mko mwaka wa kwanza mxiiiiiiiiiiiiiiiii^&^$%#^*&&*

    ReplyDelete
  20. kaka?please come back home!akufukuzae si lazima akwambie ondoka matendo yake tu utayaona!njoo nyumbani ule maboga na mafenesi bei chee kuliko kuganda kwenye vinchi vya watu hata mafenesi unauziwa bei ghali wakati huku bei karibu na bure hata mchunga,bamia,tembele huko hakuna.Rudi nyumbani tunakusubiri ndugu yetu.

    faza hausi.

    ReplyDelete
  21. we anon wa 8:10 AM,sasa unatuletea porojo,unaishi uingereza hii au upo kwa wala vumbi,ukiwa huishi ki halali kweli ntakufahamu huna entitlement ya benefit lakini una fanya kazi wewe unemployment benefit ya nini?social fund originally ziliwekwa kwa ajili ya the old,sick and for the unempolyed,sasa ni kwa ajili ya hizo group hapo juu,na SINGLE MUMS and the IDLE.Sasa wewe unaetwambia unapata medical care vingine hupati kivipi unless ur a single guy,kuwa single man in this country it's a disadvantage but to be fair to the British system once you live in their country legally you are treated as one of the citizen or maybe even more,wenye kulalamika hawajui pakutafuta msaada,kama huelewi nini uko entitled to andika status yako ya nchi iko vipi na marital status yako iko vipi then watanzania wenzio tutakushauri wapi uende kwa ajili ya msaada kama nilivyokwaambia if you are single man there's little you can get but for you to get unemployment benefit you have to be unemployed not in work and want benefit utakua una commit Benefit Fraud. Mwana Masanja

    ReplyDelete
  22. WEWE UNAYESEMA SHERIA ZA NCHI UGENINI ZIKO AGAINST WAGENI KLA MAHLI UNAKOSEA SANA, KWASABABU KWA WALA VUMBI WAGENI( WANAWAITA WADHUNGU) WANA HAKI ZOTE, MISHAHARA MIKUBWA KULIKO WALA VUMBI, HAWALIPI KODI, NA WANAKWENDA WANAKOTAKA. YAANI WANAHAKIKISHA WADHUNGU HAWALI VUMBI KAMA WAO!

    ReplyDelete
  23. wewe kwanza umeshakua illigeal visa ya miaka mitano walikupa au umejiengezea mwenyewe?

    Rudi home we huna fadhila...kazi umpata shukuru mungu tax waachie waliokuajiri as a token of your appreciation

    ReplyDelete
  24. RUDINI KWENUUUUUUUU KWANI MNANG'ANG'ANIA UKO KISA NINI HASWAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA?

    ReplyDelete
  25. nipo bongo,maisha matamu,benefits njenje..ulaya naenda kutembea na kupiga kitabu only..bongo for life..taabikeni kihivyo kwa ubishi ati ooh nipo ulaya..ni hayo tuuuu

    ReplyDelete
  26. Wewe anon Dec 6, 9:45 am unajifanya mambo supa subiri siku ya kupasuliwa kichwa badala ya mguu hapo Muhimbili shenzi type!! Ushatoka hapo kwenye comfort zone yako ukaona watu wanavyoishi kwa shida.... Hebu donate madawati basi kwenye shule uliyosoma au funga bakuli lako!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...