JK akimsindikiza mkewe Mama Salma Kikwete katika uwanja wa ndege wa Tabora jana ambapo mama Salma alielekea Mwanza kuhudhuria tamasha la vijana kupinga ukimwi kama mgeni rasmi na Rais Kikwete kubaki Tabora ambapo maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yalifanyika kitaifa mkoani humo.
Akiwahutubia vijana katika uwanja CCM Kirumba huko Mwanza,Mama Kikwete aliwaasa vijana hususan wanafunzi wa kike kuvikataa vishawishi vya fedha na zawadi kutoka kwa watu wanaotaka kuwarubuni kimapenzi na alitoa wito kwa viongozi wa serikali na mshirika ya umma kuimarisha kampeni ya upimaji na ushauri .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Nimelipenda sana shati la JK.Hiyo ndio inatakiwa.Vaa african wear.Sio kila kukicha watu..oh vutton,,ooh hilfiger..Kapendeza hajapendeza???

    ReplyDelete
  2. afadhali sasa Bw.JK ameonyesha mfano kwa viongozi wetu kwa kujimwaga adharani na mkewe mkononi hii inaonyesha mfano mzuri kuwa siyo tu kumwambia mkeo chumbani kuwa unampenda bali onyesha hata mbele ya kadamnasi kila mtu akuone naamini busu litakuwa next siku moja mbele ya kadamnasi.endelea kuonyesha njia kama first family.

    ReplyDelete
  3. Safi sana mgawanyo wa kazi. Lakini walikuwa wanashangaa nini?

    ReplyDelete
  4. Michu! ehe, umesikiliza ule wimbo wa Jide na Mad Ice ''nishike mkono''?
    ..nishikee mkono ohoo kwani wewe ndio wako, mpenzi tafadhari usiniache mbali...uende kote uendako moyo wangu upo kwako nimekuridhia we ndio wangu wa kweli...habari ndio hiyo wabeba maboksi bongo ni kama huko tu cha msingi ujipange

    ReplyDelete
  5. Michuzi, naenda nje ya point kidogo, NAOMBA KUTOA PONGEZI

    Hongera Bibie Faraja Kota kwa kutunza heshima yako na kupata mume, Hongera Mhe. Lazaro Mbunge wa Singida kwa kufunga ndoa na Bibi Faraja Kota Miss Tanzania wa miaka ya nyuma. Hongereni sana!!

    Tunaomba picha jamani Michuzi najua umepata tenda ya kupiga hizo pics

    ReplyDelete
  6. Hii michuzi imetulia sana! Waosha vinywa poleni. O'C - Sinza

    ReplyDelete
  7. Hongera Lazaro, hicho chombo si cha kitoto ngoma imetulia.

    ReplyDelete
  8. Duuh Jk Na my wife wake(First lady) wamependeza sana,keep it up mr. prezidaa panga vitu wenye wivu wajinyonge......

    ReplyDelete
  9. anon wa nne hapo juu.kushikana mikono kwa hao wawili kinahusiana vp na wabeba mabox,its pathetic,eti oh tambarare ,tambarare kushikana mikono au?watu mnaongea tuuu jinsi mnavyomind mabox kila pahali lazima myataje,nimeskia wamepunguza bei za visa sijui kweli,ni bora kwenda kuomba kuliko kudaydream mabox,maana ukishapata utayaona mabox for real.mi siko maboksini ,lakini naona sasa inakuwa too much,ndo maana wanasema tunayamind ,kama Bongo nitambarare tuwaonyeshe how tambarare it is,kwa jinsi sisi personally tunavyoishi ,sio kutumia mikonos ya rais na mywife wake.Ah saa nyingine tunaongea pumbaaa.Inachefua.

    ReplyDelete
  10. hii poa sna nakuomba kikwete zidisha mapenzi maana huu ni mfano na watu muige maana kila siku wanawake mnatunyima raha sana wanaume wa kiafrica mnatuacha nyuma kikwete nipenda salma shika mama uvevaa kieshima nimependa kama mama wa kislam kichwa umefunika mzee shati limekupendeza sana . hii wale wezi wa wanaume za watu acheni mke wake mnamuona wezi poleni sana

    ReplyDelete
  11. Huyu mama amenenepa sana na ni hatari kiafya. Anahitaji kuangalia afya yake au anaweza kuishi maisha yasiyo na raha.

    ReplyDelete
  12. we jamaa wa Sunday, December 2, 2007 9:17:00 PM EAT usijifanye ww ndio unajua sana mambo ya afya, mwanamke wa kiafrica unene ni asili yetu

    ReplyDelete
  13. haya ,huyu mama kunenepa yamekujaje ,unamfahamu huyu mama kama hajawa first lady weye.nikikwambia amepungua utasemaje? kama hivyo vibabu mnavyovichambisha msipobeba maboksi ndo vinataka mkondeane kama mnakwashakoo mkome,huyu mama ndio mwili wake na kwa ufahamu wangu mdogo nadhani amepungua.shuuuu ,michu wape hiyooo .

    ReplyDelete
  14. Michu hii picha inaendelea mmeifinya..inaelekea alimpa busu kabla ya kupanda ndege.mdau Holland

    ReplyDelete
  15. Safi sana JK, na hiyo jeans ndo umeuwa kabisaaaa

    ReplyDelete
  16. jamani go east go west home is the best....... Anagalia hapo mheshimiwa alivyomshika mama hana wasiwasi yani yupo powaaaaaaaaaaaaa kwamba niwakwake
    hehehhehe nasikia raha ile mbaya

    ReplyDelete
  17. Poa sana ni nkewe lakini mama wait mbona zipo juu jamani. Mazoezi kigodo jamani tunataka lenywe AFYA.

    ReplyDelete
  18. Oooh big up mr prezidaa you shew us how to be close to our wives mmmwaaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  19. WAMEPENDEZA SANA. Wenye vijiba vya roho huwa hawakosi la kusema. They make a very good couple. NIMEPENDA SANA

    ReplyDelete
  20. Jamani rais wetu yuko so romantik, ni mambo ya watoto wa pwani hayo. Hongera Mama Salma.

    ReplyDelete
  21. ovyoooooooooooooo kwa waweka comments kazi hamna ila comment za kijinga losh wazushi wote nyie kwani kushikana mikono imeanza leo cha ajabu kiko wapi??????????

    ReplyDelete
  22. anon wa "mambo ya watoto wa pwani.."Mimi nimezaliwa na kukulia Dar je nakwalifai kuwa mtoto wa Pwani?

    ReplyDelete
  23. JK UMETOKA NA MAMAA SIO HONGERA MEPENDEZA..UNATEGEMEA MTOTO HIVI KARIBUNI.."..USIONE VYAELEA VIMEUNDWA..

    ReplyDelete
  24. Mwanamke wa kiafrika unene wa ugonjwa? Wrong perception. Mama kanenepa vibaya sana na amevimbewa na ninakuhakikishia she is sick. Na wewe ni kibunengo nini? Prove me wrong.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...