WAZIRI Mkuu Edward Lowassa anaondoka Dar es Salaam leo (Jumamosi Des. 1, 2007) alasiri kwenda Vienna mji mkuu wa Austria kuhudhuria mkutano mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO).

Lowassa ambaye ataongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo wa Desemba 3 hadi 7, 2007, atakuwa mmoja wa wazungumzaji wakuu katika mkutano huo wa 12 wa UNIDO.

Wazungumzaji wengine ni Rais Ernst Koroma wa Sierra Leone; Waziri Mkuu Tertius Zongo wa Burkina Faso; Waziri Mkuu Zeljko Sruranovic wa Montenegro na Waziri Mkuu Lansana Kouyate wa Guinea.

Wengine katika ujumbe wa Waziri Mkuu Lowassa ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Hezekia Chibulunje na Balozi wa Tanzania kwenye Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva, Uswisi, Marten Lumbanga.

Waziri Mkuu Lowassa anatarajiwa kurejea Dar es Salaam Desemba 6, 2007.
(mwisho)

Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021,
DAR ES SALAAM
Jumamosi Des. 1, 2007

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AKAWAELEZE KUWA TANZANIA TUMEPIGA HATUA KUBWA SANA KWANI TUMEVUKA HATUA YA VIWANDA SASA TUNAVIGEUZA KUWA MAGODAUNI YA WAWEKEZAJI WA KICHINA.

    ReplyDelete
  2. Viwalo vimeanza kuchoka anaenda shopping, who cares?

    ReplyDelete
  3. At least Ujumbe wa PM hauna kundi kubwa la vigogo, kama bwana masifa JK anayependa U-mwinyi kwa kupenda kufuatwa na kundi la wapambe...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...