Tarehe 21/12/2007 ilitimia miaka miwili kamili tangu Rais Kikwete aapishwe kuwa Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika kuzingatia miaka hiyo miwili Rais Kikwete alikutana na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini ambapo alifanya mahojiano nayo.


Ifuatayo ni sehemu ya mwanzo tu wa mahojiano hayo. Unaweza kuyasikiliza mahojiano hayo kwenye tovuti yetu mpya ya http://www.klhnews.com eneo la Podcasts.

Title: KLH News Episode: Mahojiano ya waandishi na Rais Kikwete
http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/eg/2007-12-25T22_31_31-08_00
Enjoy!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. JAMANI MIMI NINA ISHI HAPA BOSTON NIMEZUNGUKA KTK HOSPITALI NYINGI HAPA KUULIZIA KUHUSU GOV.BALALI LAKINI KILA NINAPOKWENDA KTK MAHOSPITALI WANAYOFIKIA SANA WAGENI HAKUNA MTU MWENYE JINA KAMA HILO. KWAHIYO NAOMBA MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA KUHUSU JINA LA HOSPITALI ALIOLAZWA KAMA KWELI MTU HUYU YUKO HOSPITALI NAOMBA TUWWASILIANE KTK MTANDAO HUU TAFADHALI.

    ReplyDelete
  2. POLE SANA MDAU. BALALI AMELAZWA BOT TWIN TOWERS HOSPITAL, BOSTON TEXAS, USA. ROOM NO. 2

    ReplyDelete
  3. We annon wa kwanza hapo juu achana na Balali. Unataka umfanye nini? Sisi tunamsubiri huku bongo aje ajibu mashtaka. Wewe unasema unamtafuta huko, wa nini? Ndiyo umbea na ushambembe huo!

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli, mimi yangu macho tu. Hiyo miaka miwili kwangu naona kama karne tatu...................! Ikifika kumi sijui itakuwaje? I hope nitakuw abado mzima nianze upya!

    ReplyDelete
  5. Anon wa hapo juu kanichekesha..na post yake..miaka miwili anaona karne..ni kweli hata mimi yaani naona kama vile huyu jamaa amekaa miaka ishirini!

    Kwa kweli uongo dhambi, JK amekuwa nibonge la dissapointment katika maraisi tuliowahi kupata!!

    Anyway happy New Year JK! Salaam haigombi bwana!

    ReplyDelete
  6. wewe anony wa 12:11 kumbe wewe ndo unawezakuwa shambenga mtu kavurunda pesa za walipa kodi afu tunadanganywa ati kalazwa Boston akitibiwa tuambiwe yu hospitali gani tuliopo hapa Boston tukampe pole kama kweli ni mgonjwa na vilevile tuambiwe anasumbuliwa na maradhi gani si longolongo tu za kuanmbiwa ati anaumwa!Kwa mtaji huu Bongo hatutafika popote!Angalieni wenzetu Rwanda sasa hivi wako mbali sana kwa sababu rais wao yuko very makini na maswala kama hayo!Sasa wewe unafikiri atarudishwaje sisi wadau tusipopiga kelele!Ni kale kale ka ugonjwa ketu ka kusahau umesahau ya ZITO KABWE na BUZWAGI ni nini kinaendelea sasa hivi kama si Zito kupiga aram pale Bungeni leo kungelikuwa na kamati ya kuchunguza mikataba ya Madini?

    ReplyDelete
  7. Kwakweli JK anaumiza wabongo hasa masikin kwani vitu vimepanda bei mno! na uchumi haujapada sema tu waandishi wa habari ndo wanamfaigilia na kumpa chati, lakini hakuna lolote bora mkapa! mambo wa2 2liyaona na si kusikia!

    ReplyDelete
  8. tumechoka mwee!!!

    ReplyDelete
  9. We annon unayeulizia alipo Balali, unataka ukampe pole? Unadhania atakugawia alichoiba? Wewe la msingi weka presha huku home jamaa arudishwe bongo kushitakiwa. Siyo eti unamtafuta ukampe mkono, wa nini? Kama alivyosema annon mwingine, ni dalili ya ushambenga na unafiki hiyo. Rudi home hapa tumshitaki na siyo kwenda kumwangalia. Utasaidia nini ukienda kumwangalia? Hayo Mobox yanapunguza uwezo wa kufikiria?

    ReplyDelete
  10. Na wewe annon uanyetaka kumwona Babali, Rwanda wako mbali ya wapi? Mbali kutoka wapi? Usivamie propaganda za West ukazibeba kama zilivyo, Rwanda na majitran i zao wote wamechoka kama nini! Kinachopigiwa upatu pale ni mfumo uliorudi kwenye line baada ya mauaji ya 1994. Mfumo huo sisi tulishapita muda mrefu sana. Tupo katika mfumo wa kuiba, au UFISADI! Kwa hiyo usije sikia eti Rwanda wako mbali, ukadhinia kwa kuwa wewe uko Boston basi wako mbali nawe! Soma katika line na si kurukia sentences!

    ReplyDelete
  11. Mhh, annon wa Boston nawe kituko! Unajua kwamba Mashariki ya DR CONGO kna Wahutu million saba wanasubiri zamu yao ya kuchukua nchi kama walivyofanya Watusi walioko madarakani?!! Sasa huwezi fananisha issue za kule na Tanzania. Wewe sasa hivi jadili suala la maendeleo ya nchi na miaka mwili ya Kikwete.

    ReplyDelete
  12. Jamani naomba tuzidi kuwasiliana mwenye taarifa kuhusu Bw.Balali naomba sana tafadhali tuwasiliane ili niweze kuwasiliana na mwanasheria wangu ili nianze kumbana huku huku kabla ajakimbilia bongo kwa maana ushahidi wote unaweza kupatikana kirahisi kutoka dar es salaam na huku itakuwa raisi kumbana kwani ni vigumu kutumia aina yeyote ya vitisho tofauti na Tanzania. kwahiyo naomba sana mwenye taarifa za huyu mtu tuwasiliane ili niwasiliane na mwanasheria wangu tumwanzie huku huku. mwanansheria huyu ni Mtanzania na amesoma hapa na amekubali kuifanya kazi hii bure kwa kuonyesha mapenzi makubwa na nchi yake. tunajiandaa kumfungulia kesi muda wowote tutakapopata taarifa zake kamili.
    kwahiyo kwa wale wote wenye uchungu na nchi yetu sasa ndio wakati wa kufanya kweli na kuacha maneno matupu kwani tutaomba sana ushirikiano wenu ktk hili.

    ReplyDelete
  13. Yeah tunamtaka huku huku twende na wanasheria akipurusuka tu akarudi bongo hawatamfanya chochote huyu....Si tumewaona wote...huyu wetu tuachieni sisi....kalazwa wapi au kaamua kujificha na mahela yote ...mbona namepeleka barua baada ya uchunguzi kuisha.....this time noooooooo .....

    yeah mimi siishi boston lakini nitamfungia safari...atueleze ukweli na tujue anaumwa nini..

    ReplyDelete
  14. UMEME BEI JUU

    2007-12-28 08:35:14
    Na Joseph Mwendapole


    Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), imeliruhusu Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kupandisha bei ya umeme.

    Kuanzia mwezi Januari mwakani bei ya umeme itaongezeka kwa asilimia 21.7, wakati ile ya kuwaunganishia wateja wapya itaongezeka kwa kati ya asilimia 66 na 215.

    Mwezi Agosti mwaka huu, Tanesco iliomba kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 40 na asilimia 281 kwa wateja wapya wanaounganishiwa umeme.

    Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Haruna Masebu, alisema mamlaka hiyo imeona kuwa bila kufanya hivyo Tanesco haiwezi kujiendesha.

    Alisema bei ya umeme wa matumizi madogo ya kaya umepanda kutoka Sh. 40 kwa uniti moja hadi kufikia Sh. 49, wakati Tanesco ilipendekeza bei iwe Sh. 56.

    Alisema kwa matumizi makubwa ya kaya bei imepanda kutoka sh. 128 kwa uniti hadi kufikia Sh. 156. Tanesco yenyewe ilipendekeza Sh. 179.

    Bw. Masebu alisema matumizi ya kawaida gharama za huduma kwa mwezi zimepanda kutoka Sh. 1,892 hadi kufikia Sh. 2,303.

    Alifafanua kuwa kwa wateja wanaotumia msongo mkubwa gharama za huduma kwa mwezi imepanda kutoka Sh. 7,012 na kufikia Sh. 8,534.

    Kuhusu wateja wapya wanaounganishiwa umeme, alisema wenye matumizi ya kawaida ambao watatumia mita za kawaida (Single Phase) umbali usiozidi mita 30 watalipia Sh. 342,619 badala ya bei iliyopendekezwa na Tanesco ya Sh. 469,393.

    Alisema watakaounganishiwa umeme kwa kutumia mita za LUKU watalipa Sh. 385,682 tofauti na bei iliyopendekezwa na Tanesco ya Sh. 469,393.

    Watejawatakaounganishiwa umeme umbali wa mita 30 umeme mkubwa (Three Phase) kwa kutumia mita za kawaida watalipa Sh. 880,772 na Tanesco ilikuwa imependekeza bei iwe Sh.1,065,735.

    Bw. Masebu katika kundi hilo, alisema wateja watakaounganishiwa kwa kutumia mita za LUKU watalipa Sh. 772,893.

    Alisema watakaounganishiwa umeme umbali wa mita 70 Single Phase nguzo moja na mita ya LUKU watalipa Sh. 1,145664.

    Bei iliyokuwa imependekezwa na TANESCO ni Sh. 1,388,972.

    Alisema watakaounganishiwa umbali wa mita 70 Three Phase kwa kutumia mita za LUKU watalipa Sh. 1,799,062 kinyume na Sh. 2,180,188 zilizopendekezwa naTanesco.

    Mkurugenzi huyo alisema watakaounganishiwa umbali wa mita 120 Single Phase kwa kutumia mita za LUKU watalipa Sh. 1,696,120 na si sh. Sh. 2,054,999 zilizokuwa zinapendekezwa na Tanesco.

    Alisema wateja wa umbali wa mita 120 Three Phase kwa kutumia mita za LUKU watalipa Sh. 2, 604, 391 na Tanesco ilipendekeza iwe Sh. 3,154, 635.

    Alisema walifanya tathmini ya kina kwa kuzingatia maoni ya wadau mbalimbali nchini kabla ya kutoa uamuzi huo.

    Alisema baada ya kupata maoni ya wananchi na kufanya uchambuzi wa kina, EWURA ilibaini kuwa hoja ya TANESCO ina mantiki na ni halali.

    Alisema nyongeza ambayo imeidhinishwa kwa bei ya umeme na gharama za kuwaunganishia wateja wapya italiwezesha shirika hilo kulipa gharama zake za uendeshaji na ukarabati wa miundombinu.

    Alisema ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 21.7, italiwezesha shirika hilo kupata Sh. bilioni 56, ambazo litazitumia kujiimarisha kiutendaji.

    Bw. Masebu alisema shirika hilo litafanya utafiti wa kutambua viwango vya upotevu wa umeme wa kiufundi na wa kibiashara katika mfumo wake.

    ReplyDelete
  15. Hii ya TANESCO mi hata siijadili, kwan hao EWURA tuliotegemea watusaidie ndo hao wametutosa, mi bado niko na DALALI wa majengo ya BOT, sory, I mean BALALI gavana wa BOT.

    Eti kuna jamaa mmoja wa BOSTON aliniambia laimuona mtu kama Balali akifanyiwa PLASTIC SURGERY ya kubadilisha sura then arudi bongo bila kujulikana.

    Eti aliskia kama akisema kua mpango huo uliratibiwa na serikali na kwamba ukifanikiwa bas itatangazwa kua ye ndio alioiba hivyo anatafutwa kumbe jamaa atakua yuko bongo tu anakula kuku kwa Mrija, Bia kwa uma.

    Mi nimeskia tu, sasa sijui ni kweli ama vipi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...