kuwa kiongozi wa nchi, hata kama umestaafu, kuna raha na karaha zake. hapo mzee mzima akibuzibuzi mitaa ya ukerewe hivi karibuni na manyigu kibao...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. wala vumbi najua sasa hivi mmelala ila nataka kuwaambia tuu huyo ndiyo alikuwa raisi wetu na wakati wa uongozi wake mambo yalikuwa ni matawi ya juu sana maana box lilikuwa linalipa kwa week moja unaweza kumsomesha mla vumbi yeyote chuo kikuu cha huko kwenu na ukampa pesa ya kula na beer
    wenu mbeba box

    ReplyDelete
  2. Ulaniwe weye kiumbe usiye na heshima wala adabu waweza kututukana wazee wako,na huku ndiko alikozaliwa baba na mama yako.babu zako na hata weye mwenyewe!Vumbi halali yetu hongera sana kwa kuishi Marekani ambako nadhani kwenda huko ulitenda dhambi ya UONGO(Kusema Uongo) kudanganya pale US Embassy ili upate visa!

    ReplyDelete
  3. Hivi jamani hii hoja ya boks na kuosha vibibi itaisha lini? naona kuna watu imewachoma sana kiasi kwamba wanajikuta kutoa dukuduku lao hata kama topic haina mwelekeo.Ebu jiulize ziara ya Clinton Ukerewe na boksi vinauhusiano? We piga boksi lako ili mradi unachanga sio unacheza poa ukifanya vitu tunakupa shavu kwani nani anajua siri ya matajiri.Kuna mheshimiwa mmoja anatesa kwa sasa lakini kaosha sana glass Italy miaka ya 80.fungeni hii topic.

    ReplyDelete
  4. Mdau Mbeba Box usijali sana Obama anakuja atarudisha tena enzi za neema.

    Na sisi wala vumbi huku tutaneemeka pia manaake mtakuwa mnanatumia hizo green bucks na bei ya mafuta itakuwa nafuu manaake wataaacha mavita ya kijinga jinga.

    Hakikisha Obama anapita

    ReplyDelete
  5. Hivi wewe Mbeba Box unajiona umefika sana kuishi Marekani sio. Wewe si wa kwanza kufika Marekani lakini kwa upumbavu wako basi nafikiri ndio umekuwa wa kwanza kusema maneno yako.
    Isitoshe watu kama ninyi mara nyingi ni wazamiaji tu. Watu wastaarabu hawawezi sema maneno kama hayo rafiki yangu.
    Wenzako tulioko mamtoni hatubebi mabox lakini bado nawaheshimu watanzania waliko nyumbani kama ninavyojiheshimu. Kamwe maneno kama hayo ya dharau hayawezi nitoka kinywani. Tena natamani nirudi nyumbani nikalione lile vumbi unalolisema kwani huko ndipo nilipokuwa.

    Ila sishangai sana kwani najua hujasoma, na isitoshe kwa bahati mbaya yawezekana maisha unayoishi huko ni heri wale unaowaita wala vumbi ambao ni wajomba zako, mama zako, baba zako, au hata mkeo ambaye sifikiri kama yupo kwani hakuna msichana mwenye akili timamu atakayekubali kuolewa ma mtu mwenye akili finyu na aliyokosa ustaarabu kama wewe.

    Anyway, nina kampuni Marekani, waweza nitafuta nikupe kibarua kwani yawezekana ni mbeba box mzuri. Ila sitavumilia utomvu wa nidhamu maana nitatoa taarifa kwa mandata wakurudishe huko unapopadharau kwani nina amini huna MAKARATASI.

    teh... teh... teh....

    Anyway, ukikua utaacha. Kuwa na busara.
    Kimbia mzigo maana nasikia leo mabox kibao halafu wenzako wamesha kamatwa. Kwa hiyo kuwa mwangalifu.
    hahahahahaaaaaaaaaaaaaa
    Kazi njema.

    ReplyDelete
  6. Jamani miaka yangu mitatu yakuishi Ughaibuni nilikuwa sijawahi piga boksi.lakini juzi usiku nilipelekwa kwenye box,bwana siyo mchezo,maana kipindi hiki chakaribia na Chrismass mawine kibao,leo sina hamu,nasubiri viza yangu iishe nirejee nyumbani nikale kuku,boksi halina mpango kabisa.Yaani mwili wote teketeke,uzito wa mizigo unazidinguvu ya nguvu mwili bwana hata baunsa mchizi Kidume hafui dafu

    ReplyDelete
  7. wala vumbi wote nashukuru sana kwa maoni yenu ila ukweli ndio huo,Clinton alikuwa anatuweka matawi ya juu,nasikia huko siku hizi hata kuoga ni shida maji hakuna,huku bwana kila nyumba ina maji pipe mbili ya moto na baridi masaa 24 na barua hatufuati posta wanatuletea mpaka nyumbani,nitaendelea kuwaletea na mengine
    wenu mbeba box!

    ReplyDelete
  8. Ndugu wala vumbi na wanaojifanya wabeba box kumbe ni wala vumbi nashukuru kwa maoni yenu,mpaka sasa nishapiga double kama sita hivi na mjue hicho ni kichele cha nguvu,sina mengi ila ndugu zangu na mama wake mkao wa kula maana sikukuu ndiyo hiyo,mnaokwenda shule January pesa inakuja na wala endeleeni na wivu kama kawaida yenu na hamtaendelea ng'o na kama paper nilibamba long time kutoka mtoto wa kizungu,leo niko off naenda kununua pamba
    wenu mbeba box!

    ReplyDelete
  9. we anony hapo juu huna lolote, kwa nini unangoja visa iishe? kama box huliwezi rudi anytime. Au unajitetea kabla hujarudishwa ili ukifika wajue uliamua mwenyewe. Wakerewe wengine hamna lolote, usiwaongelee wengine.. Anony wa juu kabisa poa babu. Walianza wenyewe kutuita wabeba box, walihakikisha vipi wakerewe wote wanabeba?? Tulikubali as a joke..lakini naona nyani haoni k****** huliona la mwenzie. Vumbi mtakula sana...teh teh
    MKEREWE MASHUHURI

    ReplyDelete
  10. Wewe usemaye Obama aweza kuwa Raisi Marekani unaota ndoto za mchana.

    Sifa za Raisi wa Marekani japokuwa hazijaandikwa lakini zimeandikwa kwenye mioyo ya wamarekani ni:

    1.Awe Mzungu
    2.Awe mwanaume
    3.Awe Mkristo
    4.Awe anatoka Dhehebu la Baptisti ili kujihakikishia ushindi wa wazi kinyume cha hapo ushindi ni wa shida sana na si rahisi kabisa.

    Katika sifa hizo tatu Obama ana sifa moja tu ya kuwa mwanaume.

    Hata mke wa Clinton ambaye kagombea Uraisi anapoteza tu wakati wake na kuzuga tu dunia ione kama wanawake marekani nao waweza gombea uraisi lakini hamna kitu ni porojo tu za kisiasa.

    Wanawake hawana sehemu katika Uraisi wa Marekani na uwezekano wa kushinda haupo pamoja na bla bla za vyombo vya habari ambavyo hulipwa ili vimtangaze mgombea vizuri haisaidii.

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  11. Wabeba ma-box kazi kwenu!

    ReplyDelete
  12. Michuzi naona hapa hii Wi Fi ya starbucks ilikuwa inagoma maana nilipita hapa kununua coffee nikaamua nifungue laptop yangu nikutumie picha,anyway ngoja nikale pamba za nguvu Macys nasikia NIKE wametoa ndula mpya na jamaa wa Chicago nasikia mna bash la nguvu Uhuru day nitatia timu kichaa wenu na wale wala vumbi salaam zenu najua mmelala mapema maana hakuna cha kufanya umeme shida,hivi joto na mbu halafu hakuna umeme...damn i cant imagine hiyo pain.
    wenu mbeba box!

    ReplyDelete
  13. Usisahau na kununua eneo lako la kuzikiwa kabisa usitukane mamba kabla hujavuka mto maana hiyo ndiyo fainali. Mkipatikana na umauti ( Mungu apishie mbali maana huwa kasheshe) Mzikane huko huko kusiko vumbi na kwenye maji ya moto na baridi na umeme wa kumwaga, msirudi kwenye mavumbi, Kutafuta nini, shida duniani na shida mpaka kaburini? Kwanza Kinondoni kumeshajaa itabidi wawapeleke vijijini kwenu (maana huko sijui kutakuwa na nini kama Dar yenyewe ni mavumbi matupu.

    Tuachieni siye na shida zetu na mavumbi yetu ya kumwaga lakini aah hatuishi kwa viza wala visa.

    ReplyDelete
  14. Ehhhh aaaahhh
    yaani wewe anon wa kwanza nakufagilia ele mbaya
    hao wala vumbi wanapowasemaga watu wanaoishi nje wote wanabeba mabox na kutukandia leo wakisemwa kidogo wanaanza !!! hasa huyo anon wa pili
    oh mmezaliwa huku mama yako anaishi huku, kwani mnapotusema kila siku na kutudharau kwenye blogu hii, kwani hatukuzaliwa huko?
    mkuki kwa nguruwe sio?
    mkituheshimu na sisi tutawaheshimu fanya kile ambacho unataka wengine wakufanyie. halafu sio wote tunaobeba box .
    wewe kula vimbi tu huko huna lolote

    mdau Canada

    ReplyDelete
  15. Nyie wabeba mabox nawaonea huruma sana, first of all sio kila mtu ambae yupo bongo amechoka na sio kwamba hatuwezi kwenda huko. I have lived in the States for 4 years got my degree and bounced back to Tanzania, na sikufanya kazi wala nini. Pole zenu mnaohenyeka huko mnabeba mabox for years shule mna soma semester 1 on semester nyingine off and sometimes mwaka mzima mnakuwa off. I know tons of people huko ambao wamekaa miaka 7, 8, 9 hawana Certificate yeyote, kingereza hawajui wanakalia kwenda kwenye party Labor Day DC, May Columbus, Thanks giving Dallas. I have been to tons of countries but my HOME TANZANIA is the best. Na siku mnaporudigi nyinyi na kutukuta sisi tumeendelea huwa mnatia huruma pole zenu. Kwenda kwenye ma party sio issue I used to go to all those party's and am sure there is nothing new than showing off. And who said we can't shop from here?// Remember we have internet and credit cards and we can shop on line......Plus few of us can fly out of country just to go shopping and for vacation anywhere we want in the world.......IT PAINS DOESN'T IN

    ReplyDelete
  16. Guys what's the big deal?? Kubeba box na kula vumbi yote maisha. Unapiga box, unakula vumbi then baadae unakula vumba. Au sio?

    Mzee Koloboi you are in for a BIG surprise. Obama anachukua hata kama hutaki. Watch this space.

    ReplyDelete
  17. Guys what's the big deal?? Kubeba box na kula vumbi yote maisha. Unapiga box, unakula vumbi then baadae unakula vumba. Au sio?

    Mzee Koloboi you are in for a BIG surprise. Obama anachukua hata kama hutaki. Watch this space.

    ReplyDelete
  18. We anony wa 9:41 unatamba kwamba hujafanya kazi? wenzio wakifanya kazi ndo wanatamba, halafu unaona kuwa "few of you" ndio mnaweza kusafiri na kufanya shopping ni fahari wakati nchi nyingine kwao fahari ni majority kuweza kusafiri na kufanya shopping, Sasa hata ukipewa dhamana si ndo utaona fahari kuwaumiza wananchi na few of you kuweza kutanua?

    Jamani tujifunze kuthamini kazi, tujifunze kuona kazi ndio fahari badala ya kutamba eti sijafanya kazi.

    Halafu mbona wenzenu wameichukulia kubeba boksi vizuri tu, sasa kula vumbi bongo kuichukulia kiulaini kwani shida iko wapi? kwani hakuna vumbi bongo? na kama lisipotamkwa hilo waziwazi ni lini litapatiwa ufumbuzi? au wewe unaona kula vumbi pia fahari?

    Hata kama una kiyoyozi kwenye gari unataka kubisha ukishuka hakuna vumbi? juzi juzi tu msafara wa raisi ulipata ajali kwa sababu vumbi lilikuwa kubwa na mmoja wa madereva hakuona mbele, sasa kama hata raisi vumbi analila itakuwa wewe? embu msilete hizo zenu za kulikana vumbi wakati wote macho mekunduu kwa ajili ya vumbi. Muangalieni mbeba boksi akijaga ile sehemu nyeupe ya kwenye macho huwa inakuwa imebaki nyeupe.

    ReplyDelete
  19. Anon dec 4 at 4.44
    huyo Obama unayemzungumzia wewe ana sifa zote hizo kasoro ya kwanza anayo half maana mama yake mzungu.
    kwahiyo tunampa at least 85 %
    halafu wewe anon dec 4 1:28
    mimi nataka kujua hiyo kampuni yako marekani ni ipi?
    yakupukuchua maharage au? tuambiage basi na sie tutume resume zetu
    huna lolote kutuzingua tu hapa

    mdau namba moja

    ReplyDelete
  20. Nini shida? Kwa nini tuna dharauliana? Sio kwamba sisi tulio nje ni bora kuliko nyie mlioko nyumbani. After all, huko tunakokuita kwenye mavumbi ndio tulikotokea na ndipo tutakaporudi eventually.
    I think hii nguvu tunayotumia kila wiki (I say this kwa sababu kila wiki kuna haya malumbano ya wabeba mabox vs. wala vumbi hapa Michuzi blogsite), hii nguvu ingeweza kufanya greater good for our country, kama vile kukemea uzembe, ufisadi, na vile vile humu humu tunaweza kuunda vyombo vya kusaidia mashule, hospitali zetu nk.
    Sio kila mtu aliyeko nje ni mbeba mabox na sio kila aliye nyumbani ni mla vumbi. Kuna watu wako nyumbani na mambo yao ni mazuri mno, na kuna watu huku nje ambao kila kitu kipo kwenye mstari. Vile vile kuna watu wanao struggle pande zote. Maisha ni popote. Sio lazima uje U.S. na si lazima uishi Tanzania.
    Sasa kwa nini tunadharauliana? I think this is absurd...and instead we could do some constructive things for our nation as a whole.
    Michuzi please end this debacle.

    ReplyDelete
  21. we anony wa Dec 4 9.41pm u just talking rubbish, probably u've been here only 4 a day n' 2 u sounds 4yrs.u cant speak english urself yet enough speaking 4 wabeba mabox...huna lolote no chance 4 u to stay any longer, huna lolote unajidai unaipenda vumbi...teh kula vumbi kulaleki.

    Maboksi oyeee

    ReplyDelete
  22. dah,kweli mkataa kwao ni mtumwa,hv umesahau kwamba ulizaliwa kwenye nyumba ya nyasi futi kumi na mbili,choo cha shimo tena nje ya nyumba unaenda na kikopo mkononi kwa ajili ya kuchamba, leo unawatukana mama zako,baba zako pamoja na wajomba zako kwamba ni wala vumbi?

    Laana inakufuata weye,unajiona umefika hapo USA?Na ukipatwa na umauti unawasumbua watu wengine waanze kukuchangia rambirambi na kusafirisha mwili wako hadi huku kwetu kwa wala vumbi na unatusumbua sisi wala vumbi kukuhifadhi kwenye nyumba ya milele.
    Usitukane mamba kabla hujavuka mto ndugu yangu ila ushauri wangu kwako ni kwamba NUNUA MAPEMA KIWANJA KWA AJILI YA KABURI LAKO KWA KUWA BONGO IMEJAA SASA HV UTAENDA KUZIKWA MSATA USIPOKUWA MAKINI.

    ReplyDelete
  23. naomba kuuliza wadau maana mi bado ni mshamba,hv mchawi wa bongo anaweza kumloga mtu anayeishi ukerewe???Pia michuzi swala la wabeba mabox na wala vumbi lifutwe maana hakuna mpya kila siku wabeba mabox oh wala vumbi kila mtu anayajua maisha yake hakuna haja ya kutambishiana kupitia blog.MICHUZI FUNGA SWALA HILO.

    faza hausi.

    ReplyDelete
  24. kudadadeki!!!! wabeba mabox mnatusaidia sana hata viji-ada vya shule mnatutumua so tunashukuru kwa hilo.Pia wabeba box msikandie sana wala vumbi kwa kuwa huku pia ni kwenu japokuwa huko uzunguni mmeenda kutafuta kitabu pamoja na kutafuta maisha.wala vumbi oyeeee!!! wabeba box oyeeeeeee.

    ReplyDelete
  25. Ah mfyooo.... kula pepo kula vumbi mavumbini utarudi tuuu. punda la dek... ah! ehee kulaleki.nyumbani ni nyumbani tuuuuuuuu.

    mla vumbi.

    ReplyDelete
  26. PhatLorenzo kasema neno la maana, sasa umefika wakati wa kupanga mikakati ya kupunguza mavumbi au umaskini huko kwetu. Hivi jamani tuchukulie mfano wa nchi kama Senegal ukienda utakuta wamefanya vitu vya maana, hao hao wasenegali walioko nje ya Senegal hizo remmittances zao ndio zinajenga Senegal, vijana wa kirundi na kinyarwanda nao wako busy kutengeneza kwao sie tumekalia kuzomeana humu huyu anakula vumbi huyu anabeba box.

    Jamani wakati umefika tuamke hata hao w9ja nao wana vyama vyao vya kuendeleza wanakotoka kwao, kiko kimoja kinaitwa Africa in diaspora, na wana miradi kibao ya maendeleo huko makwao hiki kina wa9ja wengi lakini nafikiri kimejumuisha wawest Africa wengine.
    Hebu nasie wabongo tuanze kujadili namna ya kufanya mambo ya maendeleo huko kwetu. Tunaweza kuwaomua kuwa na Tanzania in diaspora na kuamua kufanya shughuli za maendeleo nyumbani hata hao wanaotutukana tuna beba mabox wataona faida ya mabox yetu na watatuheshimu kwa kuwa tunafaida na nchi yetu. Si lazima tufanye makubwa hata wenzetu walianza kidogo kidogo, kuna watoto kibao vijijini ambao wazazi wao wanashindwa kuwalipia ada ya shule hivi tukiamua kwa mwaka tunawalipia ada watoto hata 10 kwa kuanzia, si tutakuwa tumefanya la maana, au kusaidia miradi ya maji au umeme wa solar vijijini vitu ambavyo tukiwa na umoja tunaweza kufanya.

    Hii kila siku ya nani zaidi hata haimsaidii mtu yeyote inabaki tu malumbano yasiyo na kichwa wala miguu. Hebu tuamke walioko huku ughaibuni na walioko nyumbani pia.

    ReplyDelete
  27. mimi ugomvi wangu na wala vumbi ni tabia yao ya kishamba ya kudharau kazi na kuita watu majina ya madharau,kumbe wangejua kazi ni kazi na ni kitu cha kuheshimu sana na wajue ndugu zetu wengi wanaenda shule kwa hizi kazi zetu,wala vumbi msipojifunza kuheshimu kazi mnazofanya hata kama ni ndogo na mnaziona hazifai mjue vumbi na maisha ya tabu bila umeme na maji ni yenu milele,mkiona mitaa ya huku misafi mnafikiri kasafisha CEO au vipi? haya endeleeni kusubiri wote muwe CEOs na kutucheka sisi wala vumbi then tuonane baada ya miaka 5 tupeane report...jifunzeni kuheshimu kazi
    wenu mbeba box!

    ReplyDelete
  28. Wazee nimesoma habari za leo kuwa msafara wa raisi umepata ajali huko mkoani pwani, na chanzo cha ajali hiyo ni pale madereva wa hayo magari kula vumbi kishenzi na kushindwa kuona mbele. Sasa jamani kama Msafara wa raisi ya jamhuri unakula vumbi je itakuwaje kwa wananchi wengine?

    ReplyDelete
  29. Anony wa wednesday 5th umecema kweli kwamba nguvu itumikayo kulumbana kati ya wabeba mabokisi na wala vumbi ni heri sana ingelitumika kwa manufaa ya upande mmoja hususan wa wala vumbi.... baci uanzishwe mfuko wa wabeba mabokisi ambapo wataiamo dola humo kwa mradi wa kuondoa ama kupunguza vumbi Bongo... akaunt hii aitunze Br Michu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...