THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Archive for September 2007

ohoooo...kinshasawadau wengi wamenitaka nibandike tena picha hizi za kinshasa, sababu kuu ikiwa wameshazisikia sana lakini hawajaziona, na kila wakipekua globuni hawazipati. tarishi hauwawi - nawasilisha...


nyumba ya milele ya mzee kadumaHatimaye Mzee Godwin Kaduma aliyefariki alhamisi iliyopita jijini Dar amepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele leo huko kujijini kwake Itamba, Iringa, ambako mdau Maggid Mjengwa aliyetuletea picha hii alituwakilisha. picha zingine nenda http://mjengwa.blogspot.com.
MOLA AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU - AMINA


noti


mdau william mjema aliye tampere, finland, katika kupekuapekua vitabu vyake kakuta noti hii ambayo anasema ilikuwa inatumika enzi hizo...


mapambo


ukichagua kuja kuoa ama kuolewa bongo usiwe na wasi juu ya ukumbi wala mapambo ama keki. hela yako tu...


kili


mdau wa marangu katuletea hii tuone kili ulivyo leo


baruamonica


keki ya monica makundi. anapatikana ivy6mak@yahoo.com


uraia nchi mbili wanukia...


jk akipokea zawadi ya mpira toka kwa zamunda, mbongo anaeishi marekani hivi majuzi.

Serikali yapania uraia wa nchi mbili

Na Mobhare Matinyi, New York

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, amesema serikali itahakikisha sheria ya uraia wa nchi mbili inapitishwa kwa manufaa ya Watanzania na taifa na si vinginevyo.

Akizungumza na baadhi ya Watanzania waliokutana naye mjini New York wiki iliyopita katika hoteli ya Grand Hyatt, Waziri Membe alisema lengo la serikali ni kuwasaidia Watanzania na si kugawa uraia wa Tanzania kwa wageni wenye uraia wa nchi zao.

Alisema haingii akilini ni kwa nini Mtanzania wa kuzaliwa anyang’anywe uraia wa Tanzania kwa kuwa amechukua uraia wa nchi nyingine kutafuta faida za kielimu, ajira au hata matibabu.

“Ni kwa nini tumuadhibu huyu Mtanzania wa kuzaliwa kwa kuwa tu amechukua uraia wa nchi nyingine ili apate elimu ama ajira na kusaidia ndugu zake waliobaki Tanzania?” alihoji Waziri Membe.

Waziri alisisitiza kuwa sheria hiyo itakapopitishwa haitatoa mwanya kwa kila mtu kuuvamia uraia wa Tanzania bali itawalinda Watanzania wanaotaka kuchukua uraia wa nchi za nje kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Akitoa mfano mmojawapo bila kutaja majina ya wahusika, Waziri Membe alisema anaifahamu familia moja ya Watanzania ambayo ililazimika kuchukua uraia wa Kanada kwa sababu za matibabu, na kwamba kuwanyang’anya uraia watu hawa ni kuwaadhibu bila kujali uhai wao.

Alieleza kuwa familia hiyo ina watoto wawili ambao matibabu yao hugharimu dola 2,000 kwa kila mmoja kwa mwezi, na kwamba kwa kuchukua uraia wa Kanada, matibabu hayo yanakuwa bure. Alihoji je, ni haki kuwanyang’anya uraia wao wa Tanzania?

Akitoa mfano wa manufaa yanayopatikana Ghana, Waziri Membe aliwaambia Watanzania hao kwamba ni muhimu kwa Tanzania kutumia raia wake walioko nje kwa manufaa ya taifa na siyo kuwabagua.

“Mwaka jana pekee wananchi wa Ghana walioko nje waliingiza dola bilioni 2.5 kwa njia mbalimbali halali,” na akaongeza: “Taifa dogo kama Komoro, mwaka jana lilipata dola milioni 89 kutoka kwa wananchi wake walioko Ufaransa pekee.

Akifafanua zaidi, Waziri Membe alisema wakati akiwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kipindi kisichofikia miaka miwili, Tanzania ilitoa uraia kwa wageni 101 na kushangaa ni kwa nini Watanzania wa kuzaliwa wapoteze uraia wao.
Waziri Membe aliwataka Watanzania kujenga umoja thabiti na kuwahakikishia kwamba serikali itakuwa pamoja nao ili kuleta maendeleo kwa taifa, na kwamba mawazo kuwa usalama wa taifa utakuwa hatarini si la jambo kuhofia iwapo sheria itatungwa vizuri.

Tanzania ina raia wake waliosambaa nchi mbalimbali duniani huku idadi kubwa ikiwa katika nchi za Kiarabu za Ghuba ambako wakati serikali ikiongeza ofisi moja ya Ubalozi nchini Oman miaka michache iliyopita ilikadiria kuwa kuna Watanzania laki tano.

Nchi nyingine ambazo Watanzania wanakadiriwa kuwa wengi ni za Marekani Kaskazini na Ulaya Magharibi ambako wako kwa maelfu, ambao wengi wao hukabiliwa pia na utata wa uraia wa watoto wao wanaozaliwa ugenini.

Mjadala wa suala la uraia wa nchi mbili umekuwa ukiendelea nchini katika siku za karibuni ambako kumeibuka kambi za wanaopinga kwa madai ya kulinda maslahi ya nchi na wanaounga mkono kwa madai hayo hayo ya kulinda maslahi ya nchi.vayle springs
vitu vya wapambaji namba moja bongo, vayle springs


fleti


mwanadada akiwa fleti kufuatia msongamano wa jana kwenye uzinduzi wa mfuko wa uadilifu, uwajibikaji na uwazi bustani ya mnazi mmoja gadeni


wanja


wanja letu la ndege halijachacha kiivyo. hapa ni katika lonji ya mwisho kabla hujakwaa pipa. ukiondoa odogo wake sijaona tofauti sana na lonji za nchi zingine - karibuni waoshazzzzzzzz...


aminamwakilishi wa umoja wa afrika katika umoja wa mataifa mh. amina salim ali. huyu ni mwanamke mwingine wa shoka anayeiweka bongo katika ramani ya kimataifa pamoja na kina dk.rose-asha rose migiro ambaye ni naibu katibu mkuu umoja wa mataifa pia profesa anna tibaijuka bosi wa shirika la kimataifa la makazi (unhabitat) na kadhalika


uzinduzi


makamu wa rais dk. ali mohamed shein akikata riboni ya kitabu kama alama ya kuzindua rasmi mfuko wa uadilifu, uwajibikaji na uwazi leo bustani ya mnazi mmoja gaden. sherehe hizo zilifana hadi ulipofikia wakati wa burudani ambapo msongamano ulisababisha kuahirishwa kwa shoo ya ze comedy


ze comedyze comedy wakingoja uamuzi wa wakubwa baada ya onesho lao lililotaka kufanyika bustani ya mnazi mmoja gaden kusherehekea uzinduzi wa mfuko wa uadilifu, uwajibikaji na uwazi kuingia kashkash kutokan na msongamano wa watu mbele ya makamu wa rais ali mohamed shein aliyekuwa mgeni rasmi. msongamano huo sio tu ulitishia usalama wa viongozi bali pia hata watazamaji walikuwa na wakati mgumu. sherehe hizi ziliandaliwa na sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma na lengo la mfuko huo ni kusaidia taasisi za umma, sekta binafsi, vyama visivyo vya kiserikali na vyama vya kitaaluma nchini viweze kuwa na uwezo wa kusimamia uadilifu, uwajibikaji na uwazi.


kandoro


ilibidi mkuu wa mkoa wa dar mh. abbas kandoro atumie busara ya kuwataka ze comedy angalau wasalimie tu wananchi badala ya kuahirishwa onesho lao kavukavu. hatua hiyo ilifaa kwani baada ya kusalimia kwa mbwembwe zao na kuondoka hali ikarejea kuwa shwari


mtoto


mtoto wa nani huyu jamani eeee.....


nyomi


washabiki wakifurahia shoo ya ze comedy ambayo haikuweza kuendelea kutokana na msongamano


wajameni tulieniiiiiii....


ze comedy na polisi wakijaribu bila mafanikio kutuliza umati


umati


umati uliohudhuria uzinduzi wa mfuko wa uadilifu, uwajibikaji na uwazi leo mnazi mmoja


umati


umati uliohudhuria uzinduzi wa mfuko wa uadilifu, uwajibikaji na uwazi leo mnazi mmoja


benzi


ze comedy wakiwasili mnazi mmoja leo


seki


prodyuza wa ze comedy seki akitelemka mnazi mmoja akiongoza kikosi chake cha kuvunja mbavu


joti
joti akifanya vitu vyake leo mnazi mmoja kwenye uzinduzi wa mfuko wa uadilifu, uwajibikazi na uwazi


ze comedy


trupu zima la ze comedy leo katika bustani ya mnazi mmoja gaden likipungia mashabiki waliofurika kushuhudia uzinduzi wa mfuko wa uadilifu, uwajibikaji na uwazi


makamu


makamu wa rais dk.ali mohamed shein akiondoka mnazi mmoja baada ya kuzindua mfuko wa uadilifu, uwajibikaji na uwazi kwenye sherehe zilizoandaliwa na sekretarieti ya maadili ya uongozi wa umma leo


taarifa ya serikali dhidi ya tuhuma za dk. slaa


SERIKALI imetoa taarifa kujibu shutuma za rushwa kwa viongozi na watendaji wakuu wa serikali zilizotolewa na Mbunge wa Karatu kwa kupitia CHADEMA Dk. Wilbrod Slaa hivi karibuni.

Taarifa hiyo iliyotolewa Ijumaa Sept. 28, 2007 na Waziri ya Habari, Utamaduni na Michezo Mh. Muhammad Seif Khatib (pichani) imesema shutuma hizo hazina msingi wowote na zinastahili kupuuzwa.

"Tafsiri pekee na mantiki ya kutolewa kwa tuhuma hizi wakati huu ni kuwa hili ni jaribio la kuwavunja moyo wananchi kuhusu manufaa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005," imeeleza.

Imesema kwmba Serikali inapinga vitendo vya rushwa nchini "kwa nguvu zake zote" na kama Dk. Slaa na wenzake wana lengo la kupiga vita rushwa basi tuhuma hizo wangezifikisha katika vyombo vinavyohusika ili zishughulikiwe.

Dk. Slaa, akiwaongoza wanasiasa wenzake kadhaa wa kambi ya upinzani, walitoa tamko hadharani Septemba 15 mwaka huu kwenye viwanja vya Mwembeyanga, wilaya ya Temeke, mkoani Dar es Salaam, kuwatuhumu viongozi kadhaa wa umma kuwa wanashiriki vitendo vya rushwa.

Kufuatia tuhuma hizo, gazeti la kila wiki la MwanaHalisi linalotolewa jijini Dar es Salaam, limekuwa likisambaza tuhuma hizo bila ya kutafuta ukweli wake, taarifa imesema.

Taarika kamili ya Serikali inatarajiwa kuchapishwa ikiwa ni tangazo katika magazeti kadhaa ya kila siku Jumamosi Sept. 29, 2007.

Taarifa imesema Serikali ya Tanzania wakati wote imekuwa ikitekeleza mipango na mikakati mbalimbali ya kupambana na rushwa, awamu ya kwanza ya mwaka 1997/2004 na awamu ya pili mwaka 2005/2010.

Imenukuu Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005, Ibara ya 110, inayoelezea mapambano dhidi ya rushwa na tamko la Rais Jakaya Kikwete dhidi ya rushwa katika hotuba yake ya kuzindua Bunge Desemba 29, 2005.

Serikali imeanzisha Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye Wilaya zote nchini, imeshughulikia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na inashirikisha wananchi katika mapambano dhidi ya rushwa, imesema.

"Serikali isingebuni na kutekeleza mikakati hii kama isingekuwa na nia ya dhati ya kupambana na tatizo la rushwa [WINDOWS-1252?]nchini…Serikali haikutarajia kwamba watakuwepo miongioni mwetu watakaotumia fursa hizi kuibua taarifa za uzushi kwa lengo la kuchafua majina ya wenzao ili kujipatia umaarufu wa kisiasa wasioustahili," imeongeza.

Taarifa imesema Serikali inaelewa kwamba Dk. Slaa na wenzake ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 wakitegemea kushinda lakini walishindwa na wananchi kuichagua CCM.

Imesema wananchi wanayaona mafanikio mengi katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba wanachokitafuta wale walioshindwa ni kile walichokikosa na hivyo wanajaribu kuwahadaa na kuwachanganya wananchi.

"Serikali ya Awamu ya Nne ni imara na iko makini kutekeleza ahadi zake zote ilizowaahidi wananchi wakati ilipokuwa inawaomba ridhaa ya kuingia madarakani.

"Hivyo ni vyema wananchi wakatambua kwamba wapinzani hawa hivi sasa wanatapatapa na wanataka kutuondoa katika lengo letu la kuwaletea maisha bora Watanzania," imeongeza.


wafanyabiashara


baadhi ya wafanyabiashara wa bongo walioongozana na jk marekani. toka shoto ni issack mwamasika, gerald mongela, emily mwenewanda, mary malekia, elvis musiba, joachim lyimo, veronica lyimo na mulamu nghambi


chesi


vijana wa zenji wakicheza mchezo wa chesi ambao unaenea kwa kasi visiwani humo


shabikikuna wadau wameomba kuiona picha hii ya shabiki wa simba na mbuzi wake wakiwa neshno enzi hizo wakati simba na yanga walipokuwa na unazi uliotukuka. taarifa mpya ni kwamba baada ya kuvurunda kwenye michezo ya awali ya ligi kuu, simba imeongeza nguvu benchi lake la ufundi kwa kumrejesha jamhuri kihwelo 'julio' kama kaimu kocha mkuu na yanga wanafikiria kumrejesha kundini kocha jack chamangwana ambaye muda wote huu alikuwa kando akifundisha timu ya watoto wa wana jangwani


hotuba ya jk umoja wa mataifa


STATEMENT BY H. E. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA,
AT THE 62ND SESSION OF THE UNITED NATIONS

GENERAL ASSEMBLY, NEW YORK,
27th SEPTEMBER 2007

Your Excellency Srgjan Kerim, President of the United Nations General Assembly;
Your Excellency Ban Ki-moon, Secretary-General of the United Nations;
Excellencies Heads of State and Government;
Distinguished Representatives;
Ladies and Gentlemen.

Let me begin by congratulating you, Dr. Kerim, for your well deserved election as President of the 62nd Session of the General Assembly. You can
count on Tanzania’s full support and cooperation as you discharge your mandate. I also commend your predecessor, Madam Shaikha Haya Rashed Al Khalifa, for having skillfully presided over the 61st session.
We congratulate Mr. Ban Ki-moon for his unanimous election as the eighth Secretary General of the United Nations, which reflects his distinguished diplomatic track record, integrity and commitment to international diplomacy.
I also thank him for the honour and trust he has bestowed upon my country, by appointing an accomplished Tanzanian academic and diplomat to the post of UN Deputy Secretary General. I take this opportunity to once again congratulate Dr. Asha-Rose Migiro, for her appointment to this high office. I trust that such a combination of diligence and devoted leadership will steer this important institution towards greater heights of success.

Climate Change
Mr. President;
I highly commend the Secretary General for his decision to convene the High Level Event on Climate Change four days ago. The meeting gave us an opportunity to discuss the state of health of our common planet. It also gave us the opportunity to renew our commitment to take the necessary steps to correct the mistakes we have done.
The recent report by the Intergovernmental Panel on Climate Change (IPCC) has confirmed that warming of the earth’s climate system is indisputable and is attributable to, by and large, human activities.
Africa and many Small Island States contribute the least to the greenhouse gases that cause this phenomenon; yet, significant impact of climate change is evident on our countries. Most countries are experiencing severe floods, frequent and prolonged droughts, reduced water supply, decline in crop yields, rising sea levels, and an increase in water borne diseases. These impacts of climate change can affect African countries’ ability to achieve the Millennium Development Goals (MDGs). Climate change threatens to undo the results of decades of development efforts.
In Tanzania, for certain, the impact of global warming is real and visible. There has been a steady increase in temperature for the past 30 years, adversely affecting almost all sectors of the economy.
Severe droughts have been recurrent in the past few years. Water levels in Lake Victoria and Lake Tanganyika have dropped significantly. There has been a dramatic recession of 7 km of Lake Rukwa in the Western part of the country in the past 50 years. About 80 per cent of the glacier on Mount Kilimanjaro, the highest in Africa, has been lost since 1912.
We have prepared a National Adaptation Program of Action. There is a national programme of planting over 200 million tree seedlings per annum besides having reserved 24 percent of our territory for national parks and 38 percent for forest reserves.
We trust that countries like Tanzania, which have reserved such large tracts of land for protection of wildlife and forests, including an ambitious tree planting programme for global good, would be adequately compensated for their significant contribution to carbon sequestration.
We have prepared a National Adaptation Program of Action (NAPA) and undertaken an indepth analysis of the impact of climate change on agriculture, health, water as well as a technological needs assessment for adaptation and poverty reduction.
Tanzania hopes that the Climate Change Adaptation Fund would be successfully negotiated and concluded together with other proposed innovative sources of financing discussed during the High Level Event earlier this week.

Mr. President;
Since the causes and consequences of climate change are global, international cooperation and partnership in addressing them is imperative. Tanzania supports the Clean Development Mechanism (CDM), which assists developing countries to achieve sustainable development and requires developed countries to fulfill their commitments under the Kyoto Protocol.
So far Africa has the least number of CDM projects. Of the over 800 projects around the world, Africa has about 20 projects only. This inequitable distribution is of concern to us and must be resolved in order for it to contribute meaningfully to the sustainable development of Africa.
I wish to emphasize that international collective action is critical in developing an effective response to global warming. Indeed a review process to consider further commitment of the Parties under the Kyoto Protocol beyond 2012 is urgent and necessary. Tanzania promises to participate actively at the Bali Summit.

UN Reforms/One UN
Mr. President;
Tanzania welcomes the recent milestones in the UN reform process namely the establishment of the Peace Building Commission, the Human Rights Council and the Central Emergency Relief Fund. We attach great importance to these new initiatives and we want to contribute to their success.
In its report of November 2006 entitled, “Delivering as One”, the UN Panel on System-wide Coherence made valuable recommendations, including the establishment of a “One UN” system at the country level. For, we in Tanzania, believe that the development coordination agenda is best served when we have at the country level one programme, one budgetary framework, one leader, and one office.
Tanzania is pleased to be among the eight “One UN” pilot countries. The One UN Programme is for us a logical development from the United Nations Development Assistance Framework (UNDAF), a framework that is fully aligned with our national priorities. The efficiencies in aid delivery expected through “One UN” will certainly contribute to enhancing our capacity to attain the MDGs.
I call upon member states to give our organization, the United Nations, the resources it needs to implement this pilot project. The project should not fail for lack of resources. I also urge the Bretton Woods Institutions to take a keener interest in this initiative and join in the efforts to realize its objectives.
The need to make the UN Security Council more representative is an age old demand of all of us. Time has come to walk the talk. We need to move from rhetoric to action. Now is the time. Tanzania assures the entire UN membership our whole-hearted support and cooperation in this process.

Millennium Development Goals (MDGs)
Mr. President;
We are now halfway through the time-line of 2015 set for achieving the Millennium Development Goals. Yet we are not half-way in realizing the targets as spelt out at the Millennium Summit of 2000. We are in this unfortunate state of affairs because the additional resources expected and promised by the developed countries have not come forth. I urge this august General Assembly to renew its appeal to the developed nations to deliver on their promise.
In this regard, we welcome the initiative mentored by the Norwegian Prime Minister Mr. Jens Stoltenberg to launch a global campaign to mobilize resources for achieving the MDG 4 on reducing infant mortality rates and MDG 5 on reducing maternal mortality rates. Tanzania supports the effort and we are happy to be associated with it. I appeal to all of us to support the initiative. It is our hope that, developed nations will support the campaign by providing the required resources.
On the same vein, we commend Secretary General Ban Ki-moon for establishing the African MDG Steering Group. Africa is excited about it. We trust that it will give new impetus in assisting Africa attain all MDGs.
We also welcome the historic decision taken by the President of the General Assembly to convene a special summit of leaders to discuss the MDGs during this session. We support this wise decision of our President for we believe it will provide the needed momentum for the timely achievement of the MDGs in Africa.
Regional Issues: Africa
Mr. President;
Tanzania has played, and will continue to play, its historic role in the search for peace, security, stability and development in Great Lakes region. I thank the United Nations and the Group of Friends of the Great Lakes for their support to the processes of the International Conference on the Great Lakes. As we all know, at the Nairobi Conference held in December, 2006, an historic Pact on Peace, Security, Stability and Development in the Great Lakes Region was signed. A new era of hope, collective security and cooperation for development was ushered in. For sure, if the letter and spirit of the Pact are implemented, the Great Lakes Region will be a completely new place from the one we are used to know.
We are happy that member states have committed to ratify the Pact by the end of this year. This will enable the Pact to come into force. We look forward to continued support from the UN, friends of the Great Lakes and the international community at large as we endeavour to get durable peace, stability and sustainable development.
Mr. President;
Burundi and DRC
We are happy with the tremendous progress made in Burundi. Peace has been restored and life has come back to normal. Tanzania will continue to work with the region and South Africa to ensure the full operationalization of the peace agreement signed between the Burundi government and the FNL-Palipehutu.
We are concerned with the fluidity of the situation in North Kivu. We hope wisdom will prevail on the parties concerned to give peace a chance. The people of the DRC deserve it. We in Tanzania promise to play whatever part may be required of us.
With restored peace in Burundi and many parts of the Democratic Republic of the Congo (DRC), it is incumbent upon us in the international community to encourage and assist refugees to go back to their respective countries. This is what the Tripartite Commissions involving Tanzania, UNHCR and the respective countries of Burundi and DRC have been doing. Our joint Commissions have been encouraging repatriation of refugees on voluntary basis and we have been assisting those who came forward. The results are encouraging but things could be better. A word of encouragement from this organization could make a difference.
Mr. President;
Tanzania believes that the return of refugees to their country of origin is a sovereign right which should not be denied. It is also the ultimate testimony and guarantor of the peace so attained. It is not fair, it is not right for people to continue to live in refugee camps after peace has been restored in their countries of origin.
Situation in Darfur
Mr. President;
The current progress with regard to Darfur gives us hope. The adoption of Security Council Resolution 1769 to deploy a hybrid force of peacekeepers from the African Union and the United Nations, and the renewed political dialogue among the parties to the conflict, holds promise for the stalled peace process and the humanitarian crisis that unfortunately persists there.
Tanzania applauds the unique partnership which has evolved between the African Union and the United Nations. We stand ready to contribute troops to the hybrid force.
Somalia
Mr. President;
We are encouraged by recent developments with regard to internal political dialogue in Somalia. We are equally happy with the attention given to Somalia by the Security Council and the United Nations Secretary General. We welcome the recent Security Council resolution 1772 (2007) which supports the political process in Somalia and the role of AMISON. As member of the Somali Contact Group, Tanzania promises to continue to be pro-active and offers to contribute in the training of the Somali military.
Western Sahara
Mr. President;
The United Nations should remain seized with the issue of Western Sahara. Tanzania reaffirms its support for the inalienable right of the people of Saharawi to decide and choose the way forward. We urge the United Nations to intensify its efforts to find an honourable and just solution to this longstanding decolonization issue.
The Middle East
The crisis inside the Palestinian territories is a matter of great concern to us. Tanzania remains supportive of efforts aimed at creating two states, Israel and Palestine, living side by side, at peace with each other. This presents, in our view, the best hope for sustainable peace in the region. We applaud and welcome the renewed international interest and effort in line with the relevant UN resolutions.
Lebanese Situation
The Lebanese government and peoples need and deserve the continued support of the UN and all of us in the international community as they reconstruct and stabilize their country. In this regard, Tanzania is glad to be a party to the efforts being expended by the United Nations, through our modest contribution to the Interim Force in Lebanon (UNIFIL). We are ready to increase our contribution whenever required to do so.
Conclusion
Mr. President;
In conclusion, Mr. President, Tanzania reaffirms its belief in and commitment to multilateralism and the United Nations. You can count on Tanzania’s continued support to this organization and the ideals it stands for.
I thank you.


msaada kwenye tuta...

mdau mwenzetu Sankofa anashindana kwenye mtanange wa filamu bora afrika mashariki. anakuomba uende www.zafaa.com halafu bonyeza link ya NOMINATE, kwenye category ya BEST DOCUMENTARY FEATURE pigia kura filamu ya PLAY YOUR PART ili ishinde tuzo. Hii ni filamu yake hivyo sambaza kampeni hii kabla hapajakucha. haya shime wadau na tuendeleze libeneke la kusapotiana kama wanavyofanya wenzetu!!!
asante


mirahabamojawapo ya kazi kubwa ambazo marehemu godwin kaduma alipigamia na kuhakikisha inatekelezwa akiwa kama mwenyekiti wa chama cha haki miliki (cosota) ni utoaji wa mirahaba kwa wasanii kutokana na matumizi ya kazi zao. hapa ni dokta remmy ongalla akipokea mrahaba wa kazi zake kwa mara ya kwanza toka aanze shughuli za muziki bongo miaka ya 80. hii ilikuwa ni mwaka jana na zoezi hili linaendelea hadi leo


KUNRADHI

KUTOKANA NA MSIBA MZITO ULIOTUKUMBA WA KUONDOKEWA NA MPENDWA WETU HAYATI MZEE GODWIN KADUMA, KWA HESHIMA NA TAADHIMA NDUGU WADAU KWA MOYO MZITO NAOMBA KUSITISHA SHAMRA SHAMRA ZA SHEREHE ZA KUTIMIZA MIAKA MIWILI YA GLOBU HII NILIYOPANGA IDUMU KWA MUDA WA SIKU TANO KUANZIA SEPTEMBA 25, 2007.
HIVYO KWA UNYENYEKEVU NAOMBA KUSITISHA MVUA YA SALAMU ZA PONGEZI NYINGI ZIKIWA ZIMEAMBATANA NA PICHA TOKA KILA PEMBE YA DUNIA ZILIZONINYESHEA TOKA JUZI NA KUNIFANYA NIJISIKIE KUHEMEWA KWA FURAHA KUONA NAMNA WADAU MNAVYOUNGA MKONO GLOBU YENU HII YA JAMII.
HIVYO NAOMBA NIPOKEE HIZO SALAMU KWA PAMOJA NA KUSEMA AHSANTE KWENU NYOTE MLIOTUMA NA AMBAO MLIKUWA MNATAKA KUTUMA. MOYO MLIOUONESHA NI CHANGAMOTO KUBWA SANA KWANGU KUKAZA BUTI NA KUENDELEZA LIBENEKE ILI NIHITIMISHE MATARAJIO YENU. NAMI NAAHIDI KUFANYA HIVYO, INSHAALLAH, TUOMBE AFYA NA UZIMA.
NI IMANI YANGU MTANIELEWA NA KUKUBALI OMBI LANGU. KWA MARA INGINE NASEMA AHSANTE SANA WADAU WOTE, MUNGU AWAJAALIE KATIKA SHUGHULI ZENU ZA KILA SIKU.
MICHU


buriani mzee kaduma


wachache, kama wapo, wameshawahi kumuona marehemu mzee kaduma akiwa amenuna

marehemu mzee kaduma akimkabidhi jk risala aliyosoma siku ya ufunguzi wa tamasha la utamaduni na sanaa chuo cha sanaa bagamoyo mwaka jana

popote palipokuwa na ngoma ama mambo ya sanaa sio tu alikuwa hakosekani bali alikuwa katikati ya eneo la tukio

aliheshimika na kila mtu, hasa kwa vile naye aliwaheshimu wote - wakubwa na wadogo

mzee kaduma daima alikuwa smati na anaondoka akituachia majonzi mazito ya kupotelewa na lulu ya sanaa na utamaduni iliyotukuka.

MSANII mkongwe wa sanaa za maonesho nchini, Mzee Godwin Zilaoneka Kaduma, aliyefariki dunia jana mchana kwa maradhi ya kupooza (stroke) anatarajiwa kusafirishwa leo Ijumaa kuelekea nyumbani kwake Bagamoyo na baadaye kijijini kwake Itamba, Iringa, kwa Mazishi.
Enzi za uhai wake marehemu mzee Kaduma aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa la Lugha ambayo kwa sasa imebadilishwa na kuwa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni.
Baada ya kustaafu Serikalini marehemu mzee Kaduma aliendelea na shughuli za sanaa akiwa kama kiongozi na mtendaji katika sanaa za maonesho ikiwamo ngoma na maigizo.
Alikuwa mwanzilishi wa Kituo cha Sanaa za maonesho Tanzania (TzTC) na Taasisi ya sanaa za maonesho Mashariki mwa Afrika (EATI) ambapo pia alikuwa Katibu Mtendaji wa kwanza wa asasi hizo.
Aliamua kupumzika kuzitumikia asasi hizo mwaka 2003, ambapo aliendelea na shughuli zake za kawaida za kufundisha masuala ya sanaa katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo akiwa kama mkufunzi mwalikwa katika Idara ya tamthiliya ambapo alikuwa akifundisha somo ya uandishi wa michezo ya kuigiza kazi aliyokuwa anaedelea kuifanya hadi kifo kilipomkuta.
Marehemu Kaduma pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Hakimiliki (Cosota) hadi kufa kwake, kazi ambayo aliifanya kwa ufanisi na uelewa kiasi hata kuamsha wasanii katika kuona umuhimu wa chombo hicho na kujisajili wao na kazi zao kwa wingi kuliko wakati wowote wa uhai wa Cosota.
Kwa mara ya mwisho, marehemu mzee Kaduma alifanya onesho akiwa msanii wa kujitegemea mwezi Juni mwaka huu, wakati wa semina maalum ya kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, iliyoandaliwa na Mfuko wa Utamaduni Tanzania ambapo alitamba na shairi la 'Naililia Tanzania'.
*KWA MUJIBU WA RATIBA ILIYOTOLEWA USIKU HUU NA KAMATI YA MAZISHI INAONESHA MWILI WA MAREHEMU MZEE KADUMA UTAAGWA ASUBUHI SAA 4 KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI, KABLA YA KUPELEKWA NYUMBANI KWAKE BAGAMOYO AMBAKO UTAAGWA NA WAKAZI WA HUKO NA SAA NANE SAFARI YA KUMSAFIRISHA ITAANZA SAA 8 MCHANA KUELEKEA KIJIJINI KWAKE ITAMBA, IRINGA, KWA MAZISHI
MOLA AILAZE PEMA PEPONI ROHO YA MPENDWA WETU MZEE KADUMA
AMINA

utemi


barabara za dar si magari tu yaliyo mengi bali pia madereva watemi. jamaa mwenye ki rav 4 alikatiza boda kukwepa foleni na kukutana na magari yanayoenda alikotoka. kuambiwa apishe akaleta utemi. na mwenye shangingi naye kumbe mtemi. ilikuwa raha ya aina yake na hadi naondoka sehemu ya tukio jamaa alikuwa bado kadindisha na mwenye shangingi akawa anakula naye sahani moja...


tuzo ya sokoine

coventry


Kaka michuzi mimi na wadau wenzangu wa coventry tunaitakia mafanikio mema hii blog yetu kwa kutimiza miaka miwili, umekuwa kiunganisho kizuri sana cha habari kwa wananchi wa tanzania ndani na nje ya nchi naweza kusema kwako tunapata habari haraka sana kuliko hata kwenye vyombo vya habari vingine tanzania, nitaweza kukupa mfano zile habari zilizosemwa ati mpanjia amekufa kuna watu walikuwa wananitumia msg niwachekie kwa michuzi blog kwa hiyo tunakushukuru sana mungu akupe afya njema.


Lizzie,

coventry(england)


rai ya leoiringa


Wanafunzi wa shule ya msingi St. Dominic Savio ya Iringa wakimshangilia balozi wa redds Victoria Martin alipowatembelea hivi karibuni alipokua kwenye ziara ya semina za mikoni kuhusu shindano la ubunifu wa mitindo ya mavazi ya kiafrika (Rafda).


kariakoo


kariakoo inazidi kubadilika. hapa ni kona ya mitaa ya swahili na msimbazi


azaniabenki ya azania ni mojawapo ya taasisi za fedha zinazokuja juu kwa kasi na kusambaza huduma zake karibu na wadau. hapa ni mtaa wa msimbazi beneti na klabu ya simba. zamani mambo kama haya yalikuwa katikati ya jiji tu...


madafuzzzzz leo