October 2007

richard na mai waifu wake rikki. mambo yakienda mswano wapendanao hawa huenda wakawa pamoja bada ya wiki hii ambapo mchezo wa big brother africa II uitafikia tamati. shime shime mdau usiache kumpigia richard kura ashinde kwa kubofya linki hiyo hapo chini. wenzetu wa angola wamegangamala kumpigia tatiana na nigeria wanampa shavu offuneka. fanyeni hima tuwapige bao la kisigino...


mfungwa haruna gombellar akionesha nondozzz zake za sheria shahada ya kwanza baada ya kutunukiwa leo. makamu mkuuu wa chuo kikuu huria profesa tory mbwete amesema kwamba tukio hili la kihistoria liliwezekana baada ya chuo kuwekeana mkataba na wizara husika ili kumruhusu mwanafunzi wao abukue. mkuu wa jeshi la magereza afande nanyaro amesema hakukuwa na tatizo kwa gombeller kujisomea kwani kama ni msongamano magerezani upo kwenye sehemu za kulala tu, lakini mchana wafungwa huwa na nafasi kibao za kufanya shughuli kama hiyo ya kujisomea. gombellar ameweka historia kuwa mbongo wa kwanza kutwaa nondo akiwa kifungoni. maelezo ya kesi yake haikutolewa na afande nanyaro amesema hilo halikuwa swala kwa leo na pia ni siri ya mfungwa.


mkuu wa chuo kikuu huria mh. john samwel malecela akimtunuku shahada ya kwanza ya sheria mfungwa anayetumikia kifungo cha miaka 50 katika gereza la ukonga haruna gombellar (54) katika hafla ya kutunukiwa shahada ya kwanza ya sheria katika hitimisho la mahafali ya 19 ya chuo hicho yaliyofanyika maalumu kwa mfungwa huyo kwenye bwalo la maafisa wa magereza ukonga, dar, leo.
gombellar ambaye alianza kutumikia kifungo hicho mwaka 1998, alipata nafasi ya kusoma mwaka 1999 ila masomo alianza rasmi miaka mitatu ilopita baada ya patashika za kisheria kufikia muafaka kati ya chuo na wizara ya mambo ya ndani.


gazeti jipya la 'raia mwema' limetinga mitaani leo. gazeti hilo la kiswahili na litalotoka mara moja kwa wiki, linaongozwa na qiji wa habari jenerali ulimwengu akisaidiwa na nguli johnson mbwambo na john bwire ambao wote wamejitoa toka magazeti ya mtanzania, rai na dimba waliyokuwa wakiyaendesha kwa muda mrefu kabla ya kunuliwa na mdau mwingine



Habari kaka Michuzi,

Leo nimepita sehemu huku Kibaha na kumkuta mwanamuziki maarufu, Freddy Saganda, aliyeimba wimbo ule wa kichaga "Masawe Alikuwepo" na pia mpiga guitar wa Zemkala Group na pia Shada Group ya Kalola Kinasha.
Huyu mdau amenambia kwamba amejichimbia huku Kibaha kwenye studio mpya kubwa za Usanii Production akifanya Music production pia akifanya ubunifu wake wa sanaa ya muziki.
Anadai amepapenda hapa Kibaha na ni hizo studio za kisasa zinazomfanya awe huru na kufanya kazi kwa ufanisi kuliko studio alizowahi kukutana nazo mpaka sasa. Studio hizi zinafanya Music, Graphics na Video production.Tusubiri vitu vyake.
Mdau Godfrey


Kibaha Kontena
no image
ATTENTION EVERYONE
We have a new film club in Dar es Salaam. Movies are shown every Thursday at what used to be Smokies Tavern, from 08H00 onwards.
This Thursday at 8 in the evening and weather permitting we will be showing Robert Altman's anarchic comedy M.A.S.H.
Bring drinks, snacks, and friends along
Karibuni wote....
Nassos

nyota wa liberia george weah alipokuwa bongo na timu ya taifa ya nchi yake aliongea na waandishi ukumbi wa habari wa maelezo. yeye alitangulia na ndege yake na alikuwa akifanya mazoezi na veterani wetu pale lidaz

HATIMAYE KWA MAJAALIWA YAKE MANANI LEO MCHANA NIMEFANIKIWA KUITOA ILE ZAWADI YA $500 KWA MDAU ALIYEBAHATIKA KUWA WA MILIONI 2 KATIKA GLOBU YETU HII YA JAMII, BRIAN MARIKI, KUPITIA KWA MAMA YAKE MZAZI MAMA MARIKI NA KUSHUHUDIWA NA MWANAKIJIJI MAGGID MJENGWA KUFUATIA MAELEKEZO YA MSHINDI MWENYEWE BAADA YA URASIMU KWENYE TAASISI ZA KUTUMA PESA NJE YA NCHI KUTAKA KUCHELEWESHA HAKI YAKE.


NAMPONGEZA BRIAN KWA KUNYAKUA ZAWADI HIYO, NAMSHUKURU MAMA MARIKI KWA KUJA KUPOKEA ZAWADI HII KWA NIABA YA MWANAWE ALIEKO MASOMONI HOUSTON, TEXAS, NA NAMPA TANO MWANAKIJIJI MAGGID KWA KUAHIRISHA KWAKE SAFARI YA KURUDI IRINGA ILI KUSHUHUDIA TUKIO HILI LA KIHISTORIA. ASANTE SANA MAGGID!


PIA NASEMA AHSANTE SANA SANA KWA KAKA RODRICK MWAMBENE NA KAMPUNI YAKE YA COMPUTERCONSULT LTD KWA KUDHAMINI SHINDANO HILO NA HILI LINALOENDELEA LA KUTABIRI MSHINDI WA MECHI YA MANCHESTER UNITED NA ARSENAL WIKIENDI HII




brian, mdau wa milioni 2 ambaye amejishindia kitita cha $500 (kulia) akiwa na baba yake balozi richard mariki alipowatembelea huko houston, texas. shoto ni jesse, mdogo wake brian, na wa pili kulia ni walter kaka yao mkubwa
MWANDISHI wa habari mwandamizi Godfrey Mhando (63) amefariki dunia leo asubuhi jijini Dar es Salaam kwa matatizo ya moyo.
Mhando ambaye hadi kifo chake alikuwa mhariri msanifu (sub-editor) wa gazeti la KULIKONI, linalochapishwa na Kampuni ya Media Solutions Limited alifariki leo asubuhi muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali ya Burhani.
Familia ya marehemu ikielezea kuhusu kutokea kwa kifo chake, ilieleza kuwa Mhando leo asubuhi alikuwa amejiandaa kuelekea kazini, lakini kabla hajaondoka nyumbani, alijisikia vibaya, hasa kubanwa na kifua na mapigo ya moyo kuongezeka, ndipo alipopelekwa hospitali ya Madonna, iliyopo Tabata.
Hata hivyo, madaktari walishauri apelekwe hospitali ya Amana, ingawa familia iliamua kumpeleka hospitali ya Burhani ambako alifariki dunia hata kabla ya kuanza kupatiwa huduma.
Mhando aliwahi kuajiriwa na Kampuni ya magazeti ya Chama Cha Mapinduzi ya Uhuru na Mzalendo ambako alifanya kazi kwa muda wa miaka 30 kabla ya kustaafu mwaka juzi kujiunga na Media Solutions Limited kama mwajiriwa wa muda (part-time staff).
Alizaliwa mwaka 1944 jijini Dar es Salaam na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya Mchikichini kuanzia mwaka 1952 hadi 1955 na kuendelea na shule ya kati ya wavulana ya Uhuru hadi mwaka 1959 alikohitimu.
Kuanzia mwaka 1960 hadi mwaka 1964 alijiunga na Shule ya Sekondari Kiungani, Zanzibar na baadaye kwenda Chuo cha Kimataifa cha Mawasiliano ya Umma cha Szechoslovakia ambako alisoma uandishi wa habari na kutunukiwa stashahada.
Alirejea nchini na kuanza kazi Uhuru na Mzalendo akiwa mwandishi wa habari na mwaka 1990 hadi 1991, alikwenda Ujerumani kwa masomo ya Sayansi ya Jamii katika chuo cha Magdeburg ambako alitunukiwa stashahada.
Mhando ameacha mke na watoto kadhaa. Taratibu za mazishi zinapangwa na familia ya marehemu Mhando nyumbani kwake Tabata Segerea, eneo la Mangumi.

UTAWALA
Media Solutions Limited
30 Oktoba, 2007

leodegar chilla tenga

kamati ya shirikisho la soka nchini imemteua rais wake leodegar chilla tenga kugombea nafasi ya uenyekiti wa shirikisho la soka kwa nchi za afrika mashariki na kati a.k.a cecafa katika uchaguzi mkuu utaofanyika desemba 7 kabla ya kuanza kwa michuano ya nchi hizo jijini dar. shime mabalozi wa nchi hizo mpigieni kampeni tenga ashinde tuendeleze soka la eneo hili la afrika

miss tz 2007 richa adhia mchana wa leo ameagwa rasmi siku moja kabla hajaelekea sanya, china, kuiwakilisha nchi kwenye fainali za miss world kwenye hafla ilofanyika kituo cha uwekezaji na kuhudhuriwa na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, mh. bernard membe.
akiongea kwenye hafla hiyo mrembo huyo amesema amejiandaa vya kutosha baada ya kupewa mafunzo mbalimbali, na amewataka wabongo wamuombee dua njema kwenye kinyang'anyiro hicho.
amewashukuru wadau mbalimbali waliomsaidia kwenye maandalizi ikiwa ni pamoja na wazazi wake na wadogo zake, dk. ramesh shah ambaye ni mshauri mkuu wa kamati ya miss tz, waandishi wa habari na wananchi wote kwa jumla pamoja na mbunifu mustafa hassanali ambaye amesema ndiye aliyemtayarishia nguo za wakati wa shindano la miss tz na pia atazovaa huko china.

waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh. bernard membe anamvisha beji yenye bendera ya taifa miss tz 2007 richa adhia ikiwa ni ishara ya baraka za serikali kwa mwakilishi wetu kwenye miss world huko sanya, china, hapo desemba 1 mwaka huu.

waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa mh. bernand kamilius membe anamkabidhi mizz tz 2007 richa adhia bendera ya taifa katika hafla ya kumuaga iliyofanyika leo kwenye kituo cha uwekezaji, dar. wanaoshuhudia ni mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji mh. emmanuel ole naiko (shoto) na mkurugenzi wa kamati ya miss tz hashim lundenga

waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh. bernard membe akiongea wakati wa hafla ya kumpa baraka za serikali na kumkabidhi bendera ya taifa kwa miss tz 2007 richa adhia mchana wa leo kwenye makao makuu ya kituo cha uwekezaji, dar. kwenye hotuba yake hiyo amesema serikali itatumia mbinu mpya kuitangaza nchi, ikiwa ni pamoja na kutumia fani ya urembo na warembo katika kunadi vivutio vya kitalii kibao vilivyopo bongo. mrembo huyu anatarajiwa kuondoka kwenda sanya, china wiki hii tayari kuingia kambi ya miss world ya mwezi mzima kabla ya fainali zinazotarajiwa kufanyika huko desemba 1.
no image
A husband and wife are waiting at the bus stop, with them are their 8 children.

A blind man joins them after a few minutes. When the bus arrives, they find it overloaded and only the wife and her 8 children are able to fit in the bus. So the husband and the blind man decide to walk.

After a while the husband gets irritated by the ticking of the stick of the blind man and says to him, "Why don't you put a piece of rubber at the end of your stick, that ticking sound is driving me crazy!"

The blind man replies, "If you would have put a rubber (condom) on the end of YOUR stick, we'd be sitting in the bus right now, so shut up and walk .
no image
KAKA MICHUZI! NIMEPOKEA E-MAIL HII TOKA KWA RAFIKI ZANGU WA U.K, HEBU MSAIDIE HUYU JAMAA KUPATA MWENZA KUPITIA BLOG YAKO JAMANI. AMEKUWA WAZI MNO HADI INAFURAHISHA.
"TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA"
Habari za masiku,
Samahani kwa kutokupa jina langu halisi,kwani nnachotaka kukueleza sitakupa jina langu kamili lakini naomba msaada wako nikifanikiwa siku moja ntajitambulisha kwa jina kamili live wakati tunakunywa chai au bia sehemu, naomba uifoward hii email kwa Watanzania unaowafahamu ili the right person awasiliane na mimi, ifoward bila editing tafadhari na asante.
Mimi ni Mtanzania mwenye miaka kati ya 35 na 43,sina tatizo la kulipa bill zangu wala maisha ya kawaida. Nilitambua kuwa nipo positive mwaka 2002 (nna virusi vya Ukimwi) nnatumia dawa na nnapata matibabu kama inavyositahili, nafanya kazi kama kawaida na hakuna dalili yoyote itakayomwezesha mtu asiyetumia vipimo au hasiye na hali kama yangu kutambua kuwa nnaishi kwa matumaini.
Tatizo nililonalo ni upweke na pia sipendi wala si vizuri kuwa na uhusiano na mtu asiye positive kama mimi nnachoomba ni itume hii email kwa watanzania unaowajua nao wataiforward mpaka mwenye hali kama yangu atakaponijibu kwa hii address: jameskisalu@yahoo.com
Ningependa mtu atakaenijibu asiwe na itikadi kali ya aina yoyote. Naomba aliye na upweke na aliye serious tu ndio anijibu na si kujaribu hili kujua undani wangu wakati wala hana shida kama yangu kwani atapoteza muda wake na wangu na hata akinijua haitasaidia chochote.
Tuvumiliane kwani wote bado tunapenda kuishi kwa raha na amani, hata kama wengine tupo positive.
Nimetumia njia hii kwani nahitaji Mtanzania Mwenzangu.
“SAMAHANI NI KWA WANAOISHI UNITED STATES OF AMERICA TU”.
Ahsante Sana.

Habari kutoka kwa A.Y ni kwamba msanii huyu mkali anatarajia kuzindua documentary “UNDANI WANGU”, Website www.ay.co.tz na Nguo zitazokwenda kwa jina la “A.Y COMMERCIAL WEAR”.
Tarehe 16/11/2007
Venue:Club Maisha
Wadhamini ni Straight Muzik wakishirikiana na Lips Entertaiment
DocumentaryInaelezea safari nzima ya maisha ya A.Y kama live shows zake,historia ya muziki wake,maisha nje ya muziki,ushauri na mitazamo ya wadau,maisha yake ya kimapenzi.
Clothing line: Pia AY anatarajia kutoa nguo zake week hii jumamosi zikiwa zinajulikana kwa jina la “ A.Y commercial wear”.Zina ubora wa hali ya juu kabisa na zitapatikana katika duka la Zizzou Fashion kabla uzinduzi huo.Washabiki na wapenzi wa A.Y wataweza kupata T.shirts za Kiume,Tops za Kike,Kofia za kike na kiume zenye nembo yake. Website.
Siku hiyo A.Y atazindua tovuti yake ya www.ay.co.tz ambapo atakuwa msanii wa kwanza kuzindua tovuti yake rasmi kwenye siku hiyo maalumu.Katika website yake kuna mambo mengi ndani yake.utapata kuona video zake mpya,habari zake,ratiba ya ziara zake za kimuziki,picha mbali mbali,pia kuna sehemu inayofanya shabiki ukawasiliana na A.Y kwa barua pepe na mambo mengine mengi ya kuvutia.
Wasanii wanaotamba afrika ya mashariki kutoka Kenya,Uganda na Tanzania wataosindikiza usiku huo watatangazwa kipindi kifupi kijacho.
no image
wadau wa bongo mnaolalamika hamna nyenzo majumbani kazi kwenu....
AFFORDABLE TECHNOLOGY 4 AFRICA-USA

NOW OPEN FOR BUSINESS

( OUR WEBSITE COMING SOON)

1. USB FLASH 1GB $ 20, 2GB $ 30, 3GB $ 40 etc.

2. USED, REFURBISHED, OR NEW LAPTOPS P 3/4 FROM $ 300 AND UP.

3. USED, REBURBISHED, OR NEW PC P2,3 AND 4 FROM $ 200 AND UP( WITH NO SCREEN), FROM $ 400 AND UP(WITH LCD SCREEN).

4. USED, REFURBISHED, OR NEW LCD SCREEN(15”-19”) FROM $ 200 AND UP.

5. WE CAN ALSO PROVIDE USED OR NEW MEDICAL AND LAB EQUIPMENTS.

PLEASE CHECK WITH US FOR ALL YOUR NEED IN TECHNOLOGY OR ELECTRONICS AT A VERY AFFORDABLE PRICES.

PRESS YOUR ORDER DIRECT AT
1.technology4africa@gmail.com
2. 255-717-796761
3. 255-717-422242
4. 255-755-971825.
haya tena, ni kipindi cha lala salama kwenye jumba la big brother africa II ambapo kwa mara ingine tena bongo inawakilishwa kwenye hatua hii ya fainali na kijana richard na utaratibu wa kupiga kura umeanza rasmi leo wa kuchagua mshindi wa dola 100,000 kwa siku saba zijazo.

shime wadau na tumpe tafu richard kwa kumpigia kura kwa wingi ili ashinde nasi tujidai. ni rahisi sana kupiga kura. we nenda tu http://www.mnetafrica.com/bigbrother/vote.asp na fanya vitu vyako. haya tena wadau, umoja ni nguvu na wenzetu wanalijua hilo na wanalitekeleza kwa vitendo...

magwiji wa muziki bongo. toka shoto ni kikumbi mwanza mpango a.k.a king kikii, shem ramadhani karenga na ramadhani mtoro ongara a.k.a dokta remmy. pamoja na kutumikia fani hiyo kwa umri wao wote lakini wengi kama wao wana hali duni na serikali inabidi iamke kwani ufisadi kwenye muziki upo mwingi kuliko inavyodhaniwa hasa ukizingatia kwamba sheria ya hakimiliki ipo toka enzi hizo lakini haina meno kwani hakuna alieng'atwa nayo hadi dakika hii

Msanii wa muziki wenye vionjo asilia vya kitanzania na ambaye alivuma nakibao cha Sumu ya Teja Vitalis Maembe akiwa jukwaani kuliongoza kundi zimala Maembe & The Bagamoyo Spirit wakati wa mwendelezo wa tamasha la utamaduniwa Mtanzania mjini Bagamoyo.


Msanii huyo alifanikiwa kwa kiasi kikubwakukonga nyoyo za kila aliyehudhuria onyesho lake kutokana na umahiri wake wakuimba nyimbo zinazoigusa jamii kwa karibu, vilevile wasanii anaoshirikiananao wengi wao ni vijana wadogo ambao waliushangaza umati uliojitokeza kwauwezo wao wa kupiga ala na kucheza.


Ni wazi kuwa Tanzania imesheheni vipaji lukuki kutoka kwa wasanii wenye uwezo wakuipeperusha bendera yetu vilivyo.Kinachohitajika ni kwa wadau kutoa sapoti ya hali na mali ili wasanii hawawaweze kufaidika na kazi zao ukizingatia kuwa wengi wao wamejiajiri wenyewehivyo kuipunguzia mzigo serikali.


Hivi sasa Maembe ametoa albamu yake yapili ijulikanayo kama Imbila na hivi karibuni itaingia sokoni hivyo endeleakufuatilia CHUZI NEWS kwa taarifa zaidi.



hawa ni baadhi ya wanafunzi wa tsj wa 1994-96 ambao darasa lao la diploma ya uandishi wa habari ndilo lililokuwa la mwisho kabla chuo kuhamishiwa kijitonyama kutoka ilala shariff shamba. waliosimama toka kushoto ni bakari mkhondo ambaye yupo uhuru na mzalendo, hanna maige (rtd) munde mirambo (yuko london), carol bennet (sina uhakika aliko), amabilis batamula (femina), bahati iddi nzimano (dada wa tabora asiye na mikono alikuja kutembelea chuo), fatma msiyu (sina uhakika aliko) farida kipingu 'mnyarugusu' (yupo dar), nelly mtema (daily news), saida msumi (channel 10) mwajuma (msaidizi wa bahati), kohiya kibanga (yupo dar).
chini toka shoto: semkae kilonzo (karudi bongo majuzi), esther banda (yuko kwao zambia), mdau (anabangaiza dar) na asha muhaji (posta, dar). mchakato unafanyika alumni hii na zinginezo za chuo hicho kukutana pamoja siku za karibuni
no image
Maoni yangu ni tofauti na yako ingawa yanalenga haja ya kupunguza msongamano hapo Jijini. Hii inawezekana kabisa. Mapesa ya kufanya hivyo yapo kwani Tanzania yetu si masikini; ni tajiri. Tunafuja mapesa yetu bure.

Fikiria, hao mawaziri karibu sitini ni wa nini, kama sio ku-“exercebate the so-characterised” umasikini wetu? Hawa “mawaziri” na “wizara” zao wanamaliza mapesa kwa mishahara ya wafanyakazi, kuwapamba kwa magari ya fahari na majumba, marupurupu, ubadhirifu, ufisadi, na kurudufisha huduma.

Tulishindana na Benki Kuu ya Dunia, washauri wetu wa uchumi, kututaka tupunguze sekta ya serikali (umma) ambayo ilikuwa imeota kitambi. Tukashauriwa kuipeleka “gym” ikafanye mazoezi ya kukonda; ikakonda! Lakini sasa tumerudia yale yale ya kuota kitambi, tena kikubwa zaidi! Ikiwa kitambi kwa binadamu leo hii ni “skandali”, basi hata kitambi cha serikali nacho ni “skandali”!

Najua nchi kongwe (kama Uingereza, Ujerumani, Ufaransa) zilikuwa tayari na dola (the state) kabla vyama vya siasa kuanzishwa. Nchi changa (kama Tanzania) zilikuwa ni lazima ziunde vyama vya siasa ili zijenge “the state” ambayo ingejenga nchi. Matokeo ya kuota kitambi hicho yalikuwa ni mafanikio ya kujenga nchi.

Leo hii eti tunaambiwa mambo yamebadilika. Kuna kuoana baina ya sekta ya serikali na ile ya binafsi. Ndoa hiyo ndio kitovu cha maendeleo ya kujenga nchi….bado tunajenga nchi mpaka leo!

Kurudia ya Jiji la Dar, tunalipendelea sana jiji hili. Linazidi knawili. Wengine kati yetu wanalifananisha na New York au Shanghai kwa madhari yake. Tuliache Jiji hili lilivyo bila ya kulinyonga. Lakini Jiji la Dar limeshindwa kudhibiti wingi wa magari kwenye barabara zilizotengenezwa wakati wa Gavana akiwa ndiye mwenye gari, na wakati wa kutaka kutoka na gari hilo, barabara zilifungwa.

Mpaka sasa, serikali imekataa kuhamia Dodoma; inazidi kujenga nyumba za mawaziri na maafisa wa serikali Dar! Nchi imetumia mapesa mengi kwa ajili ya hayo “Makao Makuu Dodoma” toka enzi za “Sir” George Clement Kahama! Na “over cost” yake inazidi kila mwaka, licha ya ufisadi wa wafanyakazi wake kukopa mapesa na kujijengea majumba yao. Hii inajulikana hata kwa TAKUKURU! Tuache kuhamia Dodoma!

Itatubidi tuunde “our own format of decentralisation”, ambayo ni “home grown” ili kuendeleza baadhi ya miji yetu mingine na kupunguza msongamano wa magari jijini Dar na taabu nyinginezo.

Lakini tuendeleze miji mingineyo kwa kuhamisha wizara fulani kutoka Dar es Salaam. Kila mwaka tuhamishe kundi moja la wizara. Baada ya miaka kama kumi hivi, Tanzania itakuwa imebadilika sana!

Niruhusu nifupishe orodha ya wizara zetu ziwe wizara 15 tu. Orodha iwe fupi kama mini-sketi lakini ndefu kiasi cha kusetri huduma za lazima, kama ifuatavyo:

Dar es Salaam: Fedha na Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Mipango (Mipango, Uchumi, Uwezeshaji na Kazi); Habari, Utamaduni na Michezo; Nje (Mambo ya Nje, Mashirika ya Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Mashariki); na Ulinzi na JKT.

Dodoma: Uhusiano wa Ndani (Muungano, Siasa na Uhusiano wa Bunge); Elimu (Elimu, Ufundi, Sayansi na Teknolojia; pamoja na kuwa Makao Makuu ya Vyama vya Siasa ili viwe karibu na Bunge “tukufu”.

Arusha: Maendeleo (Makazi, Jamii, Jinsia na Watoto); Sheria (Katiba na Utawala Bora); Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa Nairobi na Kenya Kusini.

Mwanza: Afya na Ustawi wa Jamii, na Mazingira Nishati, Madini na Miundombinu, ikiwa ni pamoja na kuwa jiji la kuhudumia biashara ya Ziwa Victoria, Rwanda, Uganda, na sehemu za Kenya Magharibi. Mwanza iwe senta ya madini.

Kigoma: Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijana, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa biashara ya Ziwa Tanganyika, na DCR Mashariki, Burundi na hata Rwanda.

Mtwara: Uzalishaji (Viwanda, Biashara na Masoko). Mtwara hauna budi kupewa hadhi mpya kama senta ya huduma za mpango wa “Mtwara Corridor” – kwa ajili ya Malawi na Zambia na sehemu za Msumbiji Kasikazini. “Daraja la Umoja” kwenye Mto Ruvuma ili kuunganisha Tanzania na Msumbiji sasa linajengwa baada ya kulisubiri kwa miaka mingi tangu Awamu ya Kwanza – wakati Msumbiji inapata uhuru wake! Mtwara iwe senta ya gesi.

Mbeya: Ardhi, Maji, Mifugo, Kilimo, Chakula na Ushirika; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa nchi za Malawi na Zambia. Ni kitu cha kutia shime kuona kuwa uwanja wa ndege wa kimatiafa unaendelea kujengwa mjini Mbeya. Uwanja huu utasaidia pia kuinua maendeleo kwa mikoa ya kusini, ikiwa ni pamoja na kuinua hali ya utalii kwa mikoa hiyo ya kusini.

Miji hiyo iwe na wizara ambazo nimeziunganisha. Tuwe na Mawaziri Wadogo 15 tu wakisaidiwa na nyongeza ya Makatibu Wakuu, endapo italazimika. Wizara hizi zitagawanya katika mafungu matano.

Kila fungu la wizara zilizotawanyika lisimamiwe na afisa mwenye sifa za nidhamu na uchapaji kazi (mwenya madaraka makubwa zaidi ya makatibu wakuu) ili kuweza kufuatililia maazimio na miradi mbali mbali ya serikali kulingana na manifesto ya chama tawala (na kudhibitiwa na “chama tawala kivuli” kikisaidiana na vyama vingine vya siasa.

Naona kumekuwepo na kuteuliwa kwa maafisa wapya wa kumsaidia Waziri Mkuu katika kusimamia mipango ya sera za serikali.

Hii itasaidia sana kuangalia ni vipi tunavyotekelza yale ya Hotuba Rais aliyotoa alipokifungua Bunge la Awamu ya Nne. Na itawasaidia sana Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kuweza kufuatilia, kukagua na kudhibiti miradi na maazimio yaliyowekwa.
Born Again Pagan
no image
watani wa jadi simba na yanga leo wamezabwa faini ya shilingi 500,000 kila mojakutokana na timu hizo kufanya vurugu wakati wa mechi yao iliyochezwaJumatano iliyopita mjini Morogoro.

katika mchezo huo ambao Simba ilishinda bao 1-0 mashabiki wa Yanga waliwekavizuizi vya viti kwa lengo la kuzuia magari ya viongozi wa Simba nawachezaji tukio ambalo lilisababisha kushambuliwa kwa mawe, chupa za maji navimiminika vingeni gari la wachezaji wa Simba na mchezaji Haruna Moshialijeruhiwa.

yanga imepigwa faini ya shilingi 500,000 na imetakiwa kulipa gharama za uharibifu uliotokana na vurugu hizo ikiwa ni pamoja na matibabu ya mchezaji Haruna Moshi baada ya kuwasilishwa na kuthibitishwa na tff.

simba, ambao nao walihusika na vurugu kwa kurusha mawe, chupazilizojaa maji na vimiminika vingine na kusababishwa mchezo kusimama nayo imetozwa faini ya shilingi 500,000 na faini hizo ni kwa mujibu wa kanuni ya 31(1) na 66 ya tff.
no image
Dear colleagues,
My office has just received brochures, leaflets and other publications indicating study opportunities in Flanders, Belgium 2008/09. The opportunities listed below are supported by the Flemish Interuniversity Council, VLIR.
The International Course Programmes (ICPs) for the year 2008/09 include:
1. MSc Biostatistics
2. MSc Aquaculture
3. MSc Environmental Sanitation
4. MSc Nutrition & Rural Development (Human Nutrition)
5. Master of Nematology
6. Master in Physical Land Resources
7. Master of Food Technology 8. Master of Human Ecology
9. Master of Molecular Biology
10. Master of Ecological Marine Management
11. Master of Water Resources Engineering
12. Master of Human Settlements
13. Master in Development Evaluation and Management
14. Master in Globalisation and Development
15. Master in Governance and Development in Sub-Sahara Africa.
International Training Programmes (ITPs) for 2008 include:
1. Bee-keeping for Poverty Alleviation
2. Audio Visual Learning Materials - Production & Management
3. Governing for Development: Opportunities and Challenges for Development Actors under the New Aid Paradigm
4. Dairy Technology: From Rural to Industrial Level
5. Scientific and Technological Information Management in Universities and Libraries
6. Optimisation in Diagnostic Radiology.
For more information, brochures, etc. please contact:
The Co-ordinator SUA - VLIR Ex post Programme
P. O. Box 3082
Chuo Kikuu
MOROGORO
Attention: Peter W. Mtakwa, PhD
phone:
+ 255 23 260 4214;
+ 255 23 260 3511/14 ext 4525;
+ 255 786 073391
fax: + 255 23 260 4214

mdau katutumia hii ya wanandoa mashombe wa kiingereza ambao wamejaaliwa kuzaa mapacha ambapo kurwa na dotto hao ambao wote ni wasichana mmoja mzungu mmoja ni mmatumbi pyua. wataalamu wanasema hii inatokea kwa nadra sana kwa kipimo cha mtukio milioni moja kwa tukio moja kama hili. wadau, hii imekaaje?

Maendeleo ya mwakilishi wa bongo Angel Kileo ni mazuri na amepewa nafasi kubwa na wataalam ya kuwania taji. Tovuti moja la masuala la urembo (GrandSlam Beauties)imemweka Angel katika Top 20 kama mwafrika pekee. http://www.grandslambeauties.org/me07/me2007-hotpicks.htm

Nchi za Afrika zinazoshiriki katika Miss Earth ni Botswana, Congo, Ethiopia, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria, Sierra Leone, South Africa, Tanzania, Uganda na Zimbabwe. Nchi zingine za kiafrika ambazo ziliahidi kutuma warembo na ambao hawajafika ni Tunisia, Zambia na Cameroon.

Pia waandaji wa Miss Earth wametangaza kuanzishwa kwa tuzo la "Beauty for a Cause" ambalo latatunukiwa mrembo ambaye amefanya kazi nzuri ya kijamii ya kusaidia kuokoa mazingira. Angel Kileo amefanya kazi kubwa ya kupandikiza mikoko (mangrove tree) ufukweni mwa bahari huko Ununio. Kutoka bara la Africa warembo waliofanya kazi ya mazingira zaidi ya Angel Kileo ni mrembo wa Botswana na Afrika Kusini. Angel Kileo pia atashiriki katika mashindano ya vipaji (talent

Ndugu wapendwa,Sasa radio yenu ya TIMES FM 100.5 imewaletea kipindimaalumu kabisa LIVE from USA kiitwacho Sunday NiteSlow Jams.


Kipindi hiki kitarushwa kila siku za Jumapili kuanzia saa 2:00 (8pm) hadi 6:00 (12 Midnight) USIKU hivyo mnaombwa msikilize kipindi hiki mashuhuri kabisa kutoka huko USA.


Kipindi kitapiga nyimbo laini zikiambatana na salamuORAL EXPRESSIONS au DEDICATIONS hivyo tumia nafasi hiyo kumkumbuka umpendaye popote pale DUNIANI.


pigasimu sasa +1 877 2090631 kutuma salamu zako aukuchagua nyimbo au Ingia katika WEB www.slowjams.com


NA HAPO utatuma salamu zako ambazo zitasikika kote DUNIANI na hapa Nyumbani kupitia radio yako yenye MGUSO WA JAMII " TIMES FM 100.5" iliyopo Dar essalaam.Anza sasa kutuma salamu na tafadhari watumie wengine ujumbe huu ili nao wafaidi kusikiliza kipindi hiki.


Mgori JT

Senior Marketing Officer

Sunday Nite Slow Jams-Tanzania

0773 223152,

0784 291697
no image
Barrick Gold Tanania yatimua wafanyakazi 900
Oktoba 29, 2007
Kampuni ya Barrick Gold Tanzania leo imetangaza kuwa imewasimamisha kazi wafanyakazi takribani 900 katika mgodi wa wa Bulyanhulu uliopo Wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga.

Wafanyakaazi walioathirika na kusimamishwa kazi ni wale waliojisusisha na mgomo batili ulioitishwa na Chama cha Wafanyakazi wa Migodi na Ujenzi (TAMICO) jioni ya tarehe 24,October,2007.

Menejimenti ya mgodi wa Bulyanhulu imetoa taarifa kwa wafanyakazi wote ikiwaataarifu kuwa, wafanyakazi wote walioshindwa kurudi kazini kama walivyoagizwa wamesimamiswa kazi na nafasi zao zitatangazwa upya.

Menejimenti pia imefafanua kuwa waajiriwa wote wa hapo awali hawatabaguliwa kwa namna yeyote na kwamba kila mmoja anayo haki ya kuomba kazi kwa nafasi zitakazo tangazwa upya.

“Nasikitika sana kwamba TAMICO hawakuwa wastahimilivu, tumejaribu kwa kiasi kikubwa kutafuta suluhisho ili kuzuia vurugu za aina yeyote lakini wenzetu wa TAMICO wakafanya maamuzi kwa nia isiyo njema” alisema Greg Walker, Meneja wa Mgodi wa Bulyanhulu.

Hasara iliyopatikana katika Mgodi wa Bulyanhulu kutokana na mgomo huo inakadiriwa kuwa zaidi ya dola za kimarekani USD $ 5.2 milioni. Hasara hiyo inategemewa kuongezeka mpaka pindi mgodi huo utakapoanza kuendeshwa kwa ufanisi kama hapo awali.

Kipaumbele kilichopo kwa sasa ni kuhakikisha kuwa mgodi unarejea kufanya kazi haraka iwezekanavyo ili kukidhi na kutimiza wajibu wetu kwa jamii inayozunguka mgodi, wafanyakazi wetu, wabia wetu kibiashara na serikali kwa ujumla.

Ili Shughuli zetu ziendelee kufanyika katika hali ya amani, Uongozi wa mgodi wa Bulyanhulu unaona haja ya kutekeleza marekebisho ya mfumo wa uendeshaji ambayo yatainufaisha kampuni na wafanyakazi wake.
Kuhusu Barrick Gold.

Barrick Gold Tanzania inaendesha migodi mitatu ya Bulyanhulu, North Mara na Tulawaka, ambapo hivi karibuni itaanza ujenzi kwenye mradi wa Buzwagi.
Maeneo ya migodi ya Barrick inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye sekta hii muhimu ya madini nchini Tanzania, huongeza nafasi za ajira, ukuaji uchumi na kuboresha huduma ya elimu na afya kupitia miradi inayobaki kuwa endelevu.

Kampuni ya Barrick ni mchangiaji mkubwa katika hazina ya Serikali, kupitia mishahara, mrahaba na kodi.
Imetolewa na;
Teweli Kyara Teweli
Uhusiano & Mawasiliano
Barrick Gold Tanzania,
Plot 1736, Hamza Aziz Road,
Msasani Peninsula
P. O. Box 1081, Dar es Salaam
United Republic of Tanzania
Kwa mawasiliano zaidi;
É +255 22 2600604
È +255 767 308600
*
tteweli@barrick.com



KUTOKANA NA MALALAMIKO YA WADAU WA BONGO KWAMBA WAMEONEWA BAADA YA MDAU WA UGHAIBUNI KUIBUKA MDAU WA MILIONI 2 KATIKA GLOBU HII YA JAMII NA KUJINYAKULIA $500, MDHAMINI AMETOA $500 INGINE YA KUSHINDANIWA NA WADAU KWA NAMNA AMBAYO HATA WALIO BONGO WATANUFAIKA.

SHINDANO JIPYA LITAHUSU MECHI YA LIGI KUU UINGEREZA KATI YA MANCHESTER UNITED NA ARSENAL WIKIENDI IJAYO. UNACHOTAKIWA KUFANYA, BILA KUJALI UKO WAPI DUNIANI HUMU, NI KUTABIRI MSHINDI WA MECHI HIYO NA ATASHINDA KWA MAGOLI MANGAPI


MDAU ATAKAYEPATIA KUTABIRI MSHINDI ATAKUWA NANI NA KWA MAGOLI MANGAPI ATAPEWA HIYO $500.


KWA KUZINGATIA KWAMBA HILI SHINDANO LA SAFARI HII HALIHUSU MUDA AMA UDHAIFU WA NYENZO, HII IMEKUJA KAMA NAFASI YA WADAU HATA WA BONGO KUSHIRIKI BILA MALALAMIKO KWANI WANA WIKI NZIMA YA KUTUMA UTABIRI WAO HUMU. HIVYO WADAU WA BONGO ACHENI KULALAMIKA NA NAFASI IKO WAZI KWA YEYOTE KUJISHINDIA $500 ZA UBWETE.


KUMBUKA: MSHINDI NI YULE ATAYETABIRI MSHINDI KATI YA MANCHESTER UNITED NA ARSENAL PAMOJA NA IDADI YA MAGOLI YA USHINDI. UKIPATIA UMEULA.


MASHARTI: MDAU YEYOTE POPOTE ALIPO DUNIANI ANARUHUSIWA KUSHIRIKI KATIKA SHINDANO HILI. ENDAPO KAMA WATATOKEA WASHINDI ZAIDI YA MMOJA ITACHEZESHAW DROO YA KUMPATA MSHINDI MMOJA. MSHIRIKI LAZIMA ATUMIE ANUANI YAKE YA EMAIL. NA HAIRUHUSIWI KUPITIA MLANGO WA NYUMA (KUNITUMIA EMAIL MOJA KWA MOJA) NA LAZIMA INGIZO LIONEKANE SEHEMU YA MAONI KWENYE GLOBU
MSTARI MFU: DAKIKA MOJA KABLA YA KIPYENGA CHA KWANZA KULIA SIKU YA MECHI


MDHAMINI: NI YULE YULE COMPUTERCONSULT LTD YA DAR NA ZAWADI IMESHATOLEWA NA INASUBIRI MSHINDI TU...





T

Umoja Entertainment ,Safiri Soundz & New Jersey Kenyans
Introduces For The First Time :
I'mm a Flirt SaturdayClub Rio Grande 196 Union Ave
Paterson NJ
Saturday November 3rd 2007
Music By Dj One & Surprise Guest Dj
This One is for The Bad... and....... Naughty
Doors Open at 9pm till 3am,
Cover $ 10 (All Nite)Drink Specials Before Midnite,
Ample Club Parking
Event Sponsors: Kiboko Lager & Uhuru Apparells
For More info & Past Events pics :www.umojaentertainment.com
Event Affiliates ; Umoja Ent, Rio Grande, Safiri Soundz, Kenya
USA Events & Sauti Jerzee


The horrifying sight which traumatized shoppers and office workers in the centre of Luxembourg City last week has now been labeled as a protest against racism. The Belgian woman of Congolese origin who set herself alight in the middle of Place d'Armes told witnesses that she was! doing it to protest against racism, moments before she carried out the desperate act which has left her in hospital fighting for her life.
Maggy Delvaux-Mufu, a mother of three in her forties, alerted several national newspapers late on Tuesday morning last week that she would be burning herself alive on place des Martyrs at 12.45 am, before setting out accompanied by her husband to walk through the centre of town to her macabre rendezvous. The police were alerted and officers were deployed to the Rousegärtchen.
But the woman changed her plan when she came across a group of journalists gathered to cover an event organized by the 'Movement écologique' on Place d'Armes, opposite the Cercle municipal. She soaked herself in petrol before confronting the members of the press, announcing that she was about to sacrifice her life to protest against racism. Moments later, she struck a match, turning herself into a human torch in front of hundreds of people.
Delvaux-Mufu' s husband and passers-by jumped on the burning body, attempting to stifle the flames with coats and jackets. The sce! ne made several people feel unwell and many witnesses who filled the square at lunchtime were traumatized by the woman's shrieking screams of unimaginable pain. The flames were already extinguished when police, rescue services and the fire brigade arrived at the scene. One person is reported to have vomited after seeing the woman being transported into an ambulance. The events in Place d'Armes have also started a controversy regarding the authorities' lack of psychological support for witnesses.
Delvaux-Mufu was taken to the Bon Secours hospital in Metz , where she is being treated in a specialized ward for burns and is fighting for her life. Grand Duchess Maria Teresa visited the woman and her family at the hospital last week.
RTL television was the first to run a news flash about the incident on its website on Tuesday afternoon last week. 352 reported the bulletin in its news in brief section, shortly before going to print. Events preceding the incident only came to light later on in the week.
The 42-year-old Belgian citizen and her husband had been facing financial difficulties. They had recently indebted themselves by buying a Citroën garage in Oberwampach, before realizing they were missing the documents that would allow them to set up a business. Delvaux-Mufu wrote a letter to Le Jeudi recounting her story of bureaucratic difficulties and economic despair. "I'm against all forms of violence, but day after day, my family and I have to endure moral violence, discrimination, insults and much more from Mr Juncker's administration" , she said in the letter published last week.
Money problems had driven the woman to desperately plead her case at the Prime minister's office early on the same day of the incident. Her threat to burn herself alive on Place des Martyrs after being turned away by the authorities caused government officials to contact the police. A city-wide search was organized, but nobody could foresee the woman would change her plans."