THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Archive for November 2007

raha na karaha


kuwa kiongozi wa nchi, hata kama umestaafu, kuna raha na karaha zake. hapo mzee mzima akibuzibuzi mitaa ya ukerewe hivi karibuni na manyigu kibao...


spia

ukiondoa vitabu vya riwaya za ujana kama vile james hardley chase, mickey spillane ama mills & boon nina imani wadau wengi wamenufaika na majarida ya spia kwa kuwa sio tu yalifurahisha bali pia yalikuwa nyenzo muhimu katika kujifunza lugha na kupenda kusoma. inasikitish kuona hakuna tena mfano wake na ndio maana mapenzi ya watu kupenda kusoma zaidi ya magazeti yamepungua. tembelea nyumba nyingi bongo utakuta ni wachache wenye shefu za vitabu ama majarida.


mabweni


jk akikagua mabweni mapya ya chuo cha ualimu cha vikindu wilayani mkuranga leo katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoa wa pwani


vikindu


jk akikata utepe kufungua mabweni ya shule ya ualimu ya vikindu huko mkuranga leo

kwenye siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya wiki moja mkoa wa pwani


TANZIA

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni Kanali Mstaafu Godfrey Kajana Makaya amefariki dunia.
Taarifa kutoka kwa mtoto wa Marehemu, Bi. Doreen Makaya imearifu kuwa Kanali Makaya alifariki Ijumaa saa nne na dakika ishirini katika hospitali ya Aga Khan Jijini Dare-es salaam.
Kanali Mstaafu Godfrey Makaya alifanyiwa upasuaji mdogo wa Henia mapema tarehe 19 mwezi Novemba mwaka huu na kuruhusiwa kutoka hospitali tarehe 25 mwezi Novemba Mwaka huu. Hali yake ya afya ilibadilika ghafla hapo jana, akiwa katika hospitali ya Aga khan alipokwenda kwa ajili ya kwa ajili ya check up ya maendeleo ya operesheni aliyofanyiwa.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa alitakiwa arudi baadaye ili kumuona daktari majira ya saa nane mchana lakini akiwa anatembea kurudi kwenye gari, hali yake ilibadilika ghafla na kufariki muda mfupi baadaye majira ya saa nne na dakika ishirini asubuhi katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar-es-salaam.
Kanali Mstaafu Godfrey Makaya aliiongoza Wilaya ya Kinondoni kwa Kipindi cha zaidi ya miaka kumi na saba mfululizo kwa kuchaguliwa na wananchi na hadi mauti yalipomkuta alikuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni na Mjumbe wa Tawi la Sinza D.
Kanali Mstaafu Godfrey Makaya alizaliwa tarehe 01/09/1944. Alijiunga na jeshi la Wananchi tarehe 01/11/1966 na kustaafu mnamo tarehe 09/12/1997 akiwa Mkuu wa Chuo cha Mgambo Mbeya.
Mazishi yatafanyika jumatano tarehe 05/12/2007 kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar-es-salaam kwa heshima zote za kijeshi baada ya kutolewa heshima za mwisho nyumbani kwake Sinza Madukani Mjini Dar-es-salaam. Martehemu ameacha watoto kumi na sita na wajukuu 29.


mission band


huko birmingham (ya marekani) kundi la mission band linaendeleza libeneke la muziki wa injili kwa kwenda mbele likiwa ni la wabongo watupu. kundi hili lina tovuti yake www.themissionband.org kwa habari zaidi na kama kuna maswali nenda admin@themissionband.org


jumanne


Hi Michuzi!!
Mdau Jumanne akipiga mikonozz baada ya kupata nondo ya BSC Hons in computer science kutoka Chuo kikuu cha Thames valley university, UK. pichani yupo na dada zake Mariam (kulia) na Johari.


enzi hizo09/09/1984: waandishi waandamizi wakiwa katika mji wa mpakani wa rukunyu, kizila, bukoba, kikazi. toka kushoto ni isaack nantanga (maelezo), moshy kiyungi (maelezo), alfred hilary (redio tanzania), nathan rwehabura (rtd, mwanza), ignace karege (rtd, mwanza) na salca rweyemamu (uhuru na mzalendo)


dully sykes atamba holland


msanii dully sykes akifanya onesho lake huko holland ijumaa ilopita ambalo limetajwa kuwa bomba kiasi cha wadau kuomba wansimooo kabla hajaondoka kuelekea nchi ingine


redds


meneja wa kilaji cha redds mpeli nsekela (mwenye shati) akiwa na wadau walioshinda bahati nasibu ya redds na kujipatia tiketi ya kwenda sanya, china, kushuhudia miss world majuzi


mchongo

Wadau wenzangu mnaoishi nje ya nchi,
salam.
Hapa ninakutumieni tovuti yenye orodha ya makampuni yenye nafuu katika simu za VOIP.http://progx.ch/home-voip-prixbetamax-3-3-2.html
Pia, unaweza kujisajili kwa kutumia anwani pepe yako nao watakufahamisha punde gharama zitakapobadilika.
Tovuti hii pia inapatikana kwenye kisehemu cha "tovunganishi" katika (Tovuti Unganishi = Web Link) www.nukta77.blogspot.com na www.nukta77.com
Shime tuhabarishane na kusaidiana Wadau.
"Siasa si hasa bali visa na mikasa",
Salam zangu,
Subi.


selous


Pole na kazi Bw. Michuzi,
Naomba kushae na wadau, Picha za Wanyamapori wa Pori la Akiba la Selous. Sifa moja ya wanyama waliopo katika Pori hili ni kuwa wanaishi katika mazingira ambayo bado hayajaharibiwa na shughuli za binadamu, ni wapole kama utakavyoona, tupo nao kama ng`ombe.
-Mteleka, S.


ajira na upanuzi wa TGDLC


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mh. Hawa Ghasia akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa Kituo cha Mtandao cha Kenya uliofanyika hivi karibuni Dar. Kushoto ni Balozo wa Kenya nchini, Boaz Mbaya, na Katikati ni Mkurugenzi wa Tanzania Global Development Learning Centre (TGDLC) Charles Senkondo.


Mfumo mpya wa ajira serikalini
Na Pascal Mayalla


Serikali haitaajiri watumishi wa umma wa kuanzia ngazi za maofisa waandamizi, bali sasa nafasi za kazi katika ngazi hizo, zitakuwa ni za uteuzi na zitagawiwa kwa watu wenye sifa walio ndani ya utumishi wa umma kinyume na ule utaratibu wa kuzitangaza kwa ushindani wa uwazi kwa kila mtanzania mwenye sifa kuwa na haki ya kuomba.
Uamuzi huo, umetangawa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bibi Hawa Ghasia, katika hafla ya kumuaga Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji msataafu, Lameck Mfalila, makamishina wa tume hiyo na wafanyakazi waliostaafu, iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Waziri Ghasia emesema, uamuzi huo wa serikali, unafuatia mabadiliko ya Sheria ya Utumishi Namba 7 ya Mwaka 2002, yaliyofanywa na Bunge hivi katika kipengele cha ajira katika utumishi wa umma kwa ngazi za maofisa waandamizi sasa sio za ushindani wa wazi.
Waziri Ghasia amesema, lengo la mabadiliko hayo ni kuipunguzia serikali mzigo wa kuendesha mafunzo ya mara kwa mara kwa maofisa wanaoajiriwa toka nje ya serikali, na kusisitiza kuwapandisha vyeo maofisa wa serikali wenye sifa na utendaji wao unajulikana kutaleta tija zaidi kuliko kuajiri watanzania wenye sifa ambao utendaji wao haujulikani.
Hata hivyo Waziri Ghasia amesema uamuzi huo hauna maana kuwa watanzania wenye sifa walio nje ya serikali sasa hawana nafasi tena katika uongozi wa utumishi wa umma, ila bado watanzania wenye sifa wataendelea kuajira katika utumishi wa umma pale ambapo hakutakuwa na watumishi wa umma wenye sifa zinazotakiwa.
Naye Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bibi Thecla Shangali, amewasisitizia watumishi wa umma kuzingatia taratibu sheria na kanuni katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili utendaji wa serikali upate mafanikio yaliyokusudiwa na kuleta tija kwa maendeleo ya taifa.
Mwenyekiti mstaafu wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu, Lameck Mfalila, amesema anajivunia sifa ya kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa tume hiyo iliyoundwa mwaka 2002 na mafanikio makubwa ya tume hiyo iliyoyapata katika kipindi kifupi ambapo ni pamoja na kubadilisha sura na mitazamo ya watumishi wa umma toka utumishi wa zamani ambao ni utumishii tuu mpaka sasa kwenye utumishi wa umma unazingatia matokeo huku ukifanya kazi kibiashara kwa kufuata kanuni za mikataba ya huduma kwa wateja.
Jumla ya makamishna watano wa tume hiyo ewamestaafu na mwenyekiti wao sambamba na wafanyakazi 3 wa tume hiyo akiwemo, Naibu Katibu wa tume hiyo, Bibi Prisilla Ole Kambainei.


Upanuzi wa TGDLC
Kituo cha Tanzania cha Taaluma ya Maendeleo kwa njia ya Mtandao cha Tanzania Global Development Learning Centre (TGDLC), kinakabiliwa na changamoto kubwa ya kusambaza huduma zake zifike mikoani ili Watanzania wengi zaidi waweze kufaidika na huduma zinazotelewa na kituo hicho kuliko hali ilivyo sasa ambapo huduma za kituo hicho ziko jijini Dar es Salaam pekee.
Changamoto hiyo imetangazwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo hicho, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. George Yambesi wakati wa hafla fupi ya kumuaga Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Kituo hicho Bibi Mollel, ambaye sasa ni Katibu Mkuu ofisi ya Makamo wa Rais.
Bw. Yambesi amesema, tangu kuanishwa kwa kituo hicho mwaka 2000, tayari kimeishapata mafanikio makubwa kwa kuendesha kozi na mijadala mablimbali ya kimataifa kwa njia ya mtandao wa video hali iliyopelekea kuokoa mabilioni pya fedha za kigeni ambazo zingetumika kuwapeleka maofisa hao nje ya nchi.
Amesema kufuatia mafanikio hayo katika medani za kimataifa, kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya kusambaza huduma zake mikoani ili kuwafikia Watanzania walio wengi zaidi na kuzidi kuokoa fedha zinatakozotumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti Msataafu, Bibi Mollel, amesema anajisikia faraja sana kuwa sehemu ya mafanikio makubwa ya kituo hicho katika kipindi cha uongozi wake, na kusisitiza ana imani kubwa na uongozi wa kituo hicho chini ya Bw. George Yambesi kwa sababu anamfahamu vizuri, amefanya nae kazi kwa karibu hivyo mafanikio ya kituo hicho yatapanda kwa kasi zaidi.
Bibi Mollel aliipogeza menejimenti na wafanyakazi wa kituo kwa moyo wa dhati wa kujituma katika kazi, kuwa na ushirikiano wa hali ya juu miongoni mwao na katika kuhudumia wateja wao na kueleza kuwa ndiyo siri kubwa ya mafanikio ya kituo hicho.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Bw. Charles Senkondo, amesema kituo chake kimeipokea changamoto iliyoko mbele yake kwa moyo mmoja na kuanza kuifanyia kazi mara moja na kusisitiza kuwa kituo chake tayari kimeishafanya mipango mkakati wa kusambaza huduma zake mikoani kwa kuanzia na mikoa ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Tanga, Mbeya na Morogoro.
Bw Yambesi amechukua nafasi ya mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kituo hicho toka kwa Bibi Mollel kwa mujibu wa sheria ya kituo hicho ambapo mwenyekiti wake wa bodi, ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Mwisho.


maharage


Waziri Mkuu Mh. Edward Lowassa akizungumza na balozi wa Tanzania katika Muungano Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), Juma Maharage baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dubai akiwa njiani kuelekea Vienna Austria kuhudhuria mkutano wa Shirik la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) jana.


dk. shein


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano unaozungumzi juu ya masuala ya utafiti wa uchumi kwa Afrika, mara baada ya kufungua mkutano huo asubuhi ya leo katika Hoteli ya kilimanjari kempisk jijini Dar es salaam.


mwalukasa uko wapi?

Michuzi,
Msaada kwenye tuta. Namtafuta bwana BONIFACE MWALUKASA (au maarufu kama BONI) mkazi wa maeneo ya Ubungo hapa Dar es Salaam.Alikuwa dereva wa teksi anapaki kituo cha taksi jirani na baa ya Machange Kinondoni.Simu yake haipatikani kwa muda mrefu sasa,na nina ujumbe muhimu sana kwake.Naomba msomaji yeyote wa blogu hii anayemfahamu amjulishe awasiliane nami kwa namba 0713543505
-TICHA


maggid


napata dina la mchana na mwanakijijji wa ipogole maggid mjengwa ambaye kaja kutoa tongotongo kidogo hapa jijini


juu kwa juu


baada ya mababa wa jiji kupiga marufuku shughuli za harusi bichi la aga khani siku hizi misafara hupita juu kwa juu ambapo walipa kodi wanajiuliza waiiiiiiiiiiiiii?????


chokoraa


repa nyota wa twanga pepeta khalidi chokoraa aliyekuwa mgonjwa kwa wiki kadhaa usiku wa kuamkia leo aliibiuka mango garden akiwa na shuka na mto na kula mzigo huku akisema kwamba katoka kitandani kuja kuburudisha wapenzi wake na kwamba sasa amepona


jk na mama


JK akimsindikiza mkewe Mama Salma Kikwete katika uwanja wa ndege wa Tabora jana ambapo mama Salma alielekea Mwanza kuhudhuria tamasha la vijana kupinga ukimwi kama mgeni rasmi na Rais Kikwete kubaki Tabora ambapo maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yalifanyika kitaifa mkoani humo.
Akiwahutubia vijana katika uwanja CCM Kirumba huko Mwanza,Mama Kikwete aliwaasa vijana hususan wanafunzi wa kike kuvikataa vishawishi vya fedha na zawadi kutoka kwa watu wanaotaka kuwarubuni kimapenzi na alitoa wito kwa viongozi wa serikali na mshirika ya umma kuimarisha kampeni ya upimaji na ushauri .


RICHA PWAA!


Mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya urembo wa dunia miss world huko china,Richa Adhia ameshindwa kabisa kufurukuta.
Mshindi wa kwanza ameibuka Miss China, Zi Lin Zhang.Wa pili ni Miss Angola,Micaela Reis akifuatiwa na Miss Mexico.Carolina Moran Gordillo.
Miss World 2007,Zin Lin Zhang kutokea China.Mshindi wa pili,Miss Angola Micaela Reis kutoka Angola.Mshindi wa tatu,Miss Mexico,Carolina Moran Gordillo.


tanzia

Mdau Mwanga Kirahi wa London anasikitika kutangaza kifo cha mama yake mzazi kilichotokea leo asubuhi huko Tarime, mkoani Mara. Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho huko huko Tarime.
Kwa niaba ya wadau wote natoa mkono wa rambirambi kwa Mwanga Kirahi kwa msiba huu mzito na kuomba Mungu ailaze pema roho ya mpendwa mama yetu - Amina

Kwa mawasilano na kumpa pole piga simu
no +44 7950302881


lowassa aelekea vienna

WAZIRI Mkuu Edward Lowassa anaondoka Dar es Salaam leo (Jumamosi Des. 1, 2007) alasiri kwenda Vienna mji mkuu wa Austria kuhudhuria mkutano mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO).

Lowassa ambaye ataongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo wa Desemba 3 hadi 7, 2007, atakuwa mmoja wa wazungumzaji wakuu katika mkutano huo wa 12 wa UNIDO.

Wazungumzaji wengine ni Rais Ernst Koroma wa Sierra Leone; Waziri Mkuu Tertius Zongo wa Burkina Faso; Waziri Mkuu Zeljko Sruranovic wa Montenegro na Waziri Mkuu Lansana Kouyate wa Guinea.

Wengine katika ujumbe wa Waziri Mkuu Lowassa ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Hezekia Chibulunje na Balozi wa Tanzania kwenye Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva, Uswisi, Marten Lumbanga.

Waziri Mkuu Lowassa anatarajiwa kurejea Dar es Salaam Desemba 6, 2007.
(mwisho)

Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021,
DAR ES SALAAM
Jumamosi Des. 1, 2007


nondozzz


WADAU TOKA KUSHOTO CALVIN JILALA, BISHOP ALOYSIUS BALINA, SUSUMA WA SUSUMA AND EDWARD KONDELA TOKA CHUO KIKUU CHA SAINT AUGUSTINE UNIVERSITY OF TANZANIA WAKIPOZI NA BABA ASKOFU BAADA YA KULA NONDOZZ ZAO ZA BA in MASS COMMUNICATION MAJUZI


MKUTANO WASHINGTON DC

UONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA WASHINGTON DC NA VITONGOJI VYAKE UNAPENDA KUWAFAHAMISHA WANACHAMA NA WATANZANIA WOTE KUWA MKUTANO ULIOKUWA UFANYIKE JUMAMOSI DESEMBA 1,2007 UMEAHIRISHWA HADI DESEMBA 15,2007 KUTOKANA NA MHESHIMIWA RAIS YASSIN NJAYAGHA KUPATA DHARURA.
BAADHI YA AJENDA ZITAKUWA NI PAMOJA NA
1.RIPOTI YA UONGOZI ULIOKO MADARAKANI
2.KUUNDWA KWA KAMATI YA UCHAGUZI
TAARIFA IMEIDHINISHWA NA UONGOZI ATC METRO


tarishi hauwawigi...

Bwana Michuzi,
Nimesoma kwa makini habari yenye kichwa cha habari noma kwenye blog yako. Nikiwa kada mwenye uchungu wa nchi hii nimeonelea nami niweke mambo sawa kwa kujibu kila lililosemwa, na ushahidi nnao. Ni kwamba, Bwana Michuzi, yote yalosemwa ni uongo wa mchana usiokuwa na kichwa wala miguu. Hao bwana asikudanganye mtu, ni wenzetu ambao sasa wamegundua matumaini waliokuwa nayo yametoeka baada ya nyota ya CCM kurudia kung'ara. Wamepoteza muelekeo hawana pa kushika.Hivyo wameamua njia hii ya uongo na kupakana matope.Bahati mbaya nayo haitasaidia kwa sababu ni uongo wa kitoto. Na wewe Bw. Michuzi usipoibandika hii kitu hapo chini nitajua kuwa na wewe ni hao hao kwani ilitoka kwenye mtandao huo huo ila mahasidi wakaminya na kukuletea ya upande mmoja tu, nawe ukaingia geji. Washindwe!
Si Mwingine ila ni mimi,
Mdau Nambari wani wa Nambari wani

1.Hadithi ya Bw.Gogo: JK hana swahiba Bagamoyo anayeitwa Gogo ambaye kanunuliwa gari ya Nissan na kuzunguka misikitini nchini kuhamasisha Waislamu kumuunga mkono JK wakati wa mchakato wa kutafuta uteuzi ndani ya CCM.Ama kweli njia ya muongo ni fupi.Mchakato ulikuwa ndani ya CCM hapakuwepo na haja ya kuzunguka misikitini.Kutafuta nini?Hakuna kura kule? Mwandishi amethibitisha asivyokuwa mwana CCM ingawaje anajifanya ni mmoja wao. Pia amethihbitisha asivyomfahamu JK.Yeye(JK) si mdini na hakuna wakati wo wote ametumia Uislamu wake kutafuta kura kabla, wakati na hata baada ya mchakato.Yuko hivyo hata sasa na atabaki hivyo kesho na kesho kutwa.
2.Kutekwa Anna Kilango: Anadai "ana ushahidi wa kuhusu Ana Kilango kutekwa ENEO LA GAIRO nje kidogo ya mji wa Morogoro,kuibiwa shilingi milioni mbili na kufanyiwa mambo mabaya." Mtu mwenye kudai kuwa na ushahidi anashangaza pale anaposhindwa kujua kuwa Gairo si nje kidogo ya mji wa Morogoro bali ni kilomita 125 kutoka Morogoro.Pia kwamba Ana Kilango hakutekwa Gairo. Kesi iliendeshwa hadharani Mahakamani asibabaishe watu kuwa anazo habari za siri za kutoa.Kama kweli anao ushahidi zaidi ya ule wa Polisi mbona hakuwapa Polisi wakati kesi inaendeshwa mpaka ikaisha zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa. Hata kama alishindwa kuwapata Polisi angempa habari hiyo Ana Kilango au Mzee Malecela ambao wangemshukuru sana kwani wangenufaika nayo sana kwa maana ya kesi na siasa wakati ule. Kutunga na hata kutoa uongo huo sasa hauna tija na wala hautambabaisha mtu ye yote.JK
hakuhusika na wala hakuna rafiki yake aliyehusika na tukio hilo la ujambazi.
3.Ngono na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda mwaka 2004: Huyu mtu anastahili kupuuzwa na kudharauliwa kwa uongo wa kijinga. Mwaka 2004 Uganda haikuwa na Waziri wa Mambo ya Nje mwanamke.Waziri alikuwa marehemu Wapakabulo na baada ya kufariki yeye akateuliwa Bw.Sam Kutesa anayeendelea mpaka sasa. Hili la JK kufanya ngono kwa siku mbili mfululizo na kushindwa kwenda mkutanoni halina msingi wowote. Rais Museveni hajaandika barua ya aina hiyo kwa sababu haikuwepo sababu ya kufanya
hivyo.
4.Fedha Chafu: CCM wala JK hawajapokea hata senti moja kutoka kwa Rais Joseph Kabila. Hapakuwa na haja ya kufanya hivyo. JK na CCM haijachangia hata senti tano kwenye uchaguzi wa Joseph Kabila na Chama chake. Hawajahi kuombwa na hivyo hawakuwa na sababu ya kufanya hivyo.Serikali ya Tanzania ilitoa mchango kwenye mpango wa SADC kuisaida Tume ya Uchaguzi ya DRC uliobuniwa na kuchangiwa na nchi wanachama wa SADC. Michango
iliratibiwa na ilitolewa kupitia Sekretariet ya SADC Gaborone, Botswana. Kamwe mchango huo haukupelekwa kwa mgombea ye yote binafsi, bali kwenye Tume tena kwa kuwapatia vifaa vilivyohitajika kufanikisha uchaguzi.
5.Millennium Towers Hotel: Madai ya JK kuwa na swahiba yake Jack Gotham katika hoteli hiyo na kufanya vitendo vya ngono na msichana wa UDSM ni uongo mtupu.Kwanza JK hana uswahiba na Jack Gotham. Ni watu wanaofahamiana lakini si watu waliowahi kuwa pamoja wakati wo wote katika hotel hiyo kwa ajili hiyo inayodaiwa.Hawako karibu kiasi cha kufikia kufanya hayo yanayosemwa.Ni maneno ya hasidi mwenye nia mbaya tu kwa JK. Lakini hapa amechemsha.
6.Klabu karibu na Red Cross: JK hajawahi kutembelea klabu hiyo maisha yake yote.Hata yeye haijui jina kama vile ambavyo hata mwandishi haijui.Isitoshe hajawi kukaa pamoja na vijana hao katika klabu au bar au mahali pengine po pote.Hivyo basi kuhusishwa na mkutano na vijana aliowataja mwandishi katika klabu hiyo na hadithi zote zinazodaiwa kutokea kwa ajili hiyo ni mambo
yasiyokuwa na hata chembe ya ukweli.Ni mambo ya kugushi tu.Hakika mwandishi hamfahamu JK ndiyo maana amesema mambo ambayo hata mtoto anajua uongo.JK hakuwa na matembezi ya klabu wala bar yo yote hapa jijini.
7.Kuoa mke kutoka Uarabuni: JK ana mke mmoja tu Salma. Hana mke mwingine, si kutoka Uarabuni wala kwingineko. Hadithi ya kuoa mke mpya ni upuuzi mtupu. Hii ni Bongoland kama mwandishi kakutana na tapeli shauri yake.Siku nyingine akikutana nae amtake ushahidi wa ndoa. Morogoro kuna kijana kawaibia watu wengi kwa kujiita mdogo wa JK aitwaye Yusufu. Alikamatwa na sasa anatumikia kifungo.
8.Hoteli ya Serengeti: Kwa kuwa suala la kuoa mke mpya ni jambo la uongo hivyo hadithi ya JK kuchukua eneo Serengeti la kujenga hoteli kwa ubia na mke huyo si jambo la kweli.JK hajengi hoteli po pote pale.


miss tz 2007miss tz 2007 ni richa adhia ambaye hivi tunavyoongea yamebaki masaa machache kabla hajapanda jukwaani kwenye kinyang'anyiro cha miss world 2007 huko sanya, china. tumuombee ushindi binti yetu huyu anayetuwakilisha.
MUNGU MBARIKI RICHA
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE
AMINA


miss tz 2006


wema sepetu ndiye aliyenyakua taji la miss tz 2006


miss tz 2005


mrembo nancy sumari ndiye aliyekuwa miss tz 2005 ambapo hadi sasa hakuna ambaye amekuwa mwenye fanaka kama yeye baada ya kushinda miss world africa kwenye mashindano hayo


miss tz 2002


miss tz mwaka 2002 hakuwa mwingine ila bibie angela damas


miss tz 2001


happiness magese (namba 5) ndiye alishinda taji la miss tz mwaka 2001


miss tz 2000


jaquiline ntuyabaliwe ndiye aliyekuwa miss wa milenia kwa kupasiwa taji na hoyce mwaka 2000


miss tz 1999


mshindi wa miss tz 1999 alikuwa hoyce temu anayetajwa kuwa ndiye miss aliyechangamka zaidi


miss tz 1998


miss tz 1998 alikuwa basila mwanukuzi


miss tz 1997saida kessy ndiye aliyeshinda mwaka 1997 na kufungua pazia la washindi kupewa zawadi ya gari


miss tz 1996


shose sinare ndiye aliyeibuka miss tz 1996


miss tz 1967


hivi ndivyo mambo yalivyokuwa mwaka 1967 siku miss tz ya kwanza ilipofanyika hoteli ya kilimanjaro na mshindi akiwa bibie theresa shayo (5) ambapo baada ya hapo yakapigwa marufuku kabla ya kuibuliwa tena na kina lundenga mwaka 1994


noma

Michuzi,
Kila siku tunasema wewe ni kada wa CCM unaminya. Sasa kuna hii email inazagaa kila sehemu kuhusu swahiba'ako JK. Kama kweli wewe si kada na una ubavu ibandike kwenye globu yetu ya jamii. Hapo nitaamini wewe huna noma wala nini na ni mshikaji. Hakyanani tena we kama mwanaume ibandike hii
-Mdauz,
Ukerewe
Baada ya kusoma kwa makini kwa siku nne mfululizo, kwenye forum yetu hii tukufu, na baada ya kuona kuwa uongozi wa forum hii tukufu umeamua kuwa kila anayeona uovu wa viongozi wa kisiasa na haswa wenyeviti wa vyama vya siasa ana haki ya kuleta ujumbe wake hapa bila kubugudhiwa kitu ambacho nakiheshimu sana kwenye ujenzi wa demokrasia na pia haki ya kupata habarikwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania ibara ya 18.
Na pia nimeguswa kuandika ujumbe huu kutokana na kile nilichokiona kwenyegazeti la majira la jana (front page) na pia kauli iliyotolewa na katibumkuu wa CCM ndugu Makamba kuunga mkono hoja iliyowekwa hapa forum na wanachadema! Kama ilivyorushwa kwenye taarifa ya habari ya channel ten janasaa moja jioni .
Makamba alisema kuwa viongozi wa upinzani waache kurusha mawe ile hali waowako wakiishi kwenye nyumba za vioo!nimeshtuka na kuogopa kama huyu ndioanatakiwa kuonyesha njia ya kuweza kufikia maisha bora kwenye taifa hili , nashindwa kuamini kuwa huyu ndio dereva wa chama tawala !
Leo nimeona niweke ushahidi wangu hapa juu ya ufisadi wa ziada na au uovuuliotendwa na JK pamoja na timu yake wakati wa kuwania kuteuliwa na chamachake, na pia jinsi alivyotumia cheo chake cha waziri wa mambo ya nje kuendekeza ngono na kulisababishia taifa hili madhara makubwa ikiwa nipamoja na mahusiano ya kidiplomasia kuwa mabaya.

Naanza kuweka hoja zangu na ushahidi wake kama ifuatavyo

1.Kikwete wakati anagombea kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM ,aliunda timu za aina mbalimbali ila kwa hapa nazungumzia timu yake ya uharamia ambayo aliiunda, aliunda timu ya kuwafanyia maasi wagombea wenzake na mojawapo ni hii iliyokuwa inaongozwa na mtu anayeitwa Gogo kutoka kule Bagamoyo.
Huyu alinunuliwa gari aina ya Nissan patrol ,na ndio mwanzo alitumika kupitakwenye misikiti mbalimbali na kutengeneza mtandao wa kiislamu,ila huyu Gogondio alihusika na aliongoza kikosi kilichohusika kumpora mke wa mzee Malecela fedha taslimu zaidi ya milioni mia mbili wakati anatoka dar kwendadodoma kwa ajili ya kampeni. ENEO LA GAIRO.

Gogo akiwa na vijana wenzake walimteka mama Kilango nje kidogo ya mji wamorogoro na kumpora fedha hizo na pia kumfanyia mambo ya ajabu ambayo kwamtu mzima kama mimi siwezi kuyaandika hapa.(ushahidi upo na nitautoa muda wowote kama utahitajika hapa ,niandikie kwenye PM yangu.)

2.Akiwa waziri wa mambo ya nje mwaka 2004 alipokwenda nchini marekanikuiwakilisha nchi kwenye kikao cha UN alifanya ngono na aliyekuwa waziri wamambo ya nje wa Uganda kitu kilichowafanya kutokuweza kuhudhuria mkutano kwa siku mbili mfululizo, na ndipo rais museven alimwandikia rais mkapa rasmimalalamiko yake na pia alimtimua kazi waziri huyo .

Hili linaifanya nchi yetu kutokuwa na mahusiano mazuri na serikali ya Ugandana haswa kati ya Kikwete na Museven na hili limechangia kwa kiasi kikubwahata kutokufikiwa kwa shirikisho kwani Museven anaamini kuwa hawawezi kujadili mambo serious na JK kutokana na kutokwenda kuwakilisha nchi nabadala yake ikawa ni kwenda kufanya ngono na waziri aliyetumwa na nchinyingine bila hata aibu.

3.Kikwete akiwa na swahiba wake wa karibu anayeitwa Jack Gotham,wakiwamaeneo ya millennium towers hotel kijitonyama ,walimchukua binti wamfanyibiashara mmoja wa jijini ambaye alikuwa anasoma shahada ya kwanza chuo kikuu cha DSM na kufanya naye ngono hapohapo hotelini na kumfanya kuchelewakwenda kwenye ziara za kampeni kwani kipindi hiki kilikuwa ni wakati wamchakato wa kampeni ukiwa unaendelea.

Huyu anaacha hata masuala ya maana na kwenda kumchukua binti wa rafiki yakeambaye amemchangia kiasi kikubwa cha fedha za kampeni zake na kufanya nayengono.

4.Fedha chafu.Kikwete aliingiza nchini kiasi kikubwa sana cha fedha chafu kutoka kwenyenchi za uarabuni na nyingine alizitoa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Congo(DRC)kutoka kwa Joseph Kabila na fedha hizi ziliingizwa kupitia mkoani Kigoma na nyingine ziliingilia mkoani Mwanza .Ujumbe wa watu wa kongo uliongozwa na Luten Jenerali Peter Gessimba Gabonneakiwa na wasaidizi wake watatu ambao walikuwa ni viongozi wa jeshi tiifu kwaKabila.Fedha hizi zilitolewa kwa masharti kuwa endapo angeshinda ni lazimaahakikishe kuwa Kabila naye anashinda kule Congo kitu ambacho alikifanya nahata kutumia pesa za taifa hili kwa ajili ya uchaguzi wa congo kwa wale mnaokumbuka Asha Rose Migiro alisema kiasi cha pesa zilizotolewa na misaadamingine ……..

5.Ngono.JK akiwa na maswahiba wa mwanae wa karibu waitwao Benno (huyu kwa sasaanagombea ujumbe wa NEC ndani ya chama chetu),Said (huyu ni msaidizi maalumuwa kumsaidia mzee Makamba) ,Mussa (huyu alikuwa ni kiongozi mwandamizi wa mbio za mwenge mwaka huu), na Sisko (huyu ni chief protocol wa ikulu)wakiwakwenye club mojawapo jijini dar,(ipo mkabala na red cross-barabara yaAlhassan mwinyi) kabla ya mchakato wa kampeni kuanza rasmi walimchukua binti anayeitwa Hadija ……aliyekuwa anasoma UDSM na pia ni mfanyibiashara wa mjiniArusha, ila alikuwa pia ni mke wa aliyekuwa meneja msaidizi wa kituo kimojacha kimataifa nchini , na kufanya naye ngono .

Kitendo hiki kilimfanya Hadija kuachika /kuachwa na mumewe na kumnyanganyamagari pamoja na mtaji kitu kilichopelekea binti huyu kuishi kwa taabu hadiJK alipoweza kushinda urais wa nchi na kumpangishia nyumba maeneo ya Kijitonyama ambako anaishi hadi sasa.Pia JK alimwamuru Benno ambaye ni afisa mwajiri wa jumuiya ya UVCCMkumwajiri bint huyu makao makuu na kwa sasa ameajiriwa kama katibu wauhamasishaji wa taifa cheo ambacho hakipo hata kwenye katiba ya umoja huo, kwa toleo la 2003 ambalo ninalo hapa.

6. Ngono ,Alifanya ngono iliyoligharimu taifa hili zaidi ya shilingi milioni mia nneNa themanini, (480 milioni) akiwa kule Zanzibar Hotel Kempinski palealipokuja na mkewe mpya kutoka uarabuni na kukaa naye kwenye mapumziko hayo ambayo yaliliingizia taifa hasara hiyo kwa muda wa siku 9 tuu.Mkuu wetu wa nchi anatumia rasilimali zetu kwa ajili ya kujistarehesha yeyebinafsi na wanawake zake kutoka huko uarabuni.

7.Ubadhirifu.Aliweza kujichukulia eneo ndani ya mbuga za wanyama kule Serengeti na sasaanajenga hotel ya kisasa nah ii anaijenga yeye kwa ubia na mke wake huyo wauarabuni akishirikiana na mashemeji zake hao , swali la kujiuliza ni je?huu mkataba hautaishia kwenye kuliuza taifa hili? Mke anaenda kupewa mahari ya rasilimali zetu? Kama kila rais akioa ni shartiatoe sehemu ya mbuga zetu je? Mpaka lini tutakuwa tunachezea taifa kwa faidaza kuoa ama kupata ngono!

Huyu ndio mwenyekiti wa chama chetu na bado tunamwona kama malaika aliyetokambinguni kama sio kuzimu!

Nitakuja na taarifa pia za kina juu ya ndugu Nchimbi ambaye naambiwa kuwaanaweza kuwa ndio katibu mkuu wa chama chetu, jambo ambalo mimi nalipingakwa nguvu zote kwani huyu naye anaendelea kufanya mambo ya aibu na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya umma nchini.

Ni mimi mwanachama mtiifu na mpenda maendeleo ya chama chetu kitukufu. Mwanachama


mkapanovemba 18, 1995: siku moja kabla hatujamwapisha mh. benjamin mkapa kuwa rais wa awamu ya tatu uwanja wa taaifa wa neshno. kulia ni moshy kiyungi wa the guardian, kabendera shinani wa bbc (marehemu) na mie mbangaizaji. siku kama hii lazima mje siku moja kabla kula tizi na kuangalia namna ya kukaa kupata snepu nzuri


emmily adolph


miss tz 1995 emmily adolph akivishwa taji na miss tz 1994 aina maeda baada ya kushinda. kesho huko china miss tz 2007 richa adhia anapanda jukwaani kutuwakilisha katika miss world. tumuombee heri ashinde na kuletea taifa sifa


mijadala

mijadala kibao imefunguliwa www.dailynews-tsn.com kwa wenye kutaka kuchangia katika 'discussion pot'.
1. kuchelewa kufunguliwa kwa wanja jipya la taifa
2. uraia wa nchi mbili
3. aina mpya ya leseni za udereva
4. wizi wa haki miliki
5. tatizo la foleni dar


kp leo


miss zanzibarjanuari 13, 1968: miss zanzibar wa kwanza hediye khamis mussa (kati) akipozi na wenzie baada ya kutwaa taji. mashindano hayo yaloandaliwa na chama cha hockey, kama ilivyokuwa kwa bara baada ya shindano la kwanza mwaka 1967, yalipigwa marufuku na hadi hii leo hayajafanyika tena huko visiwani


treni lakwama


habari toka mwisho wa reli zinasema treni la abiria toka kigoma limekwama sehemu za kaliua siku ya nne leo na wadau wanasota ile mbaya. hii ni mara ya tatu kwa usafiri huu kuleta noma toka ulipoanza upya tokea stesheni ya dar kwenda bara siku ya novemba 1, 2007


salaaam toka cesena


Nakupa Hi sana tena sana Mr.Michuzi!!!!!

Habari za huko kwetu Bongo, ninapenda kutoa shuikrani zangu nyingi kwako Michuzi kwa kutupatia habari na picha mbalimbali zinazo tukumbusha nyumbani. Mimi nipo hapa Italy mji wa Cesena, mtanzania ni mimi peke yangu hapa mji wa Cesena, ni mpweke sana. Lakini kwa blog yako Michuzi inanifariji sana tena sana, yaani ninafuraha sana kwa hii blog. Hongera sana tena sana, ninakutakia mafanikio mema mengi, nikija Bongo nitakuja kukutembelea. Salamu nyingi sanaaaaaaa......!!!!!!!!

- Mdau Baraka Franco Chibiliti


leon sullivan dinner in washington DC

We are welcoming Tanzanians to our event, but they MUST register online or call us. They cannot just show up at the dinner because the room will be full!!! And we don’t want to turn anyone away!
they must either register online at
call us at 202.736.2239.

Nichet Smith Director,
Public Relations
Leon H. Sullivan Foundation
1800 K. Street NW Suite 1021 Washington,
DC 20006 202.736.2239 202.736.2226
Sullivan Summit VIII "The Summit of A Lifetime"
June 2-6, 2008
Arusha,
Tanzania
REGISTER NOW ONLINE!!


maoni

KAKA MICHUZI SAMAHANI SANA MIMI KAMA MDAU WA BLOG YAKO NA MPENZI MKUBWA WA SOKA NAOMBA UWE UNATUEKEA MATOKEO YA BIG FOUR KILA WIKI ILI WADAU WAKO TUWEZE KUTOA MAONI YETU.
NIMECHOKA KUONA UNAJIPENDELEA MWENYEWE TU MATOKEO YA TIMU YAKO LIVERPOOL WAKATI UMESEMA BLOG YETU WOTE. MATOKEO YA ARSENAL,LIVERPOOL,MAN UNITED NA CHELSEA YAWEKWE NADHANI SIO KAZI NGUMU SANA.

asante sana muheshimiwa michuzi nitashukuru wazo langu ukilitekeleza.


chumvi

wadau kunradhi. eti mtu kuomba chumvi usiku ni mwiko?


mnuso


Dear Friends and Colleagues

Music Mayday Tanzania is happily inviting you for a film launching on Thursday 13th December 2007 at Alliance Francaise

These are 4 films of 3 minutes each made by 4 young Tanzanians after a 6 weeks training

The function will start from 06:00 pm – 09:00pm.

This is under a Show Me Your World Project which is funded by Vipaji Project

This email is to alert you in making this time of your day free and come and support young Tanzanians creative work!

Invitation cards would be sent to you!


Many Thanks


Fatma Mussa
Program Assistant


Music Mayday Tanzania
P.O.Box 34747
Kijitonyama, Dar es Salaam
Tanzania
T. + 255 2771156
F. + 255 2771156
C. + 255 754 592643

www.musicmayday.org
www.b-connected.to


hongera


waziri mkuu mh. el akiwa na mkuu wa mkoa wa kagera na waheshimiwa wengine wa meza kuu wakiwapongeza wanakamati wa kagera dei kwa kazi nzuri. jumla ya milioni 100 keshi zilichangwa hapo hapo na pamoja na ahadi jumla ya shilingi bilioni 1.4 zilipatikana


kombo


kombo ya wadau mbalimbali waliohudhuria kagera dei usiku wa kuamkia leo diamond jubilei


afande achangia


kamanda wa polisi mkoa maalumu wa dar afande tibaigana akitangaza mchango wake huku mc mavunde akisisitiza wakati wa hafla ya kagera dei


kumbukumbu


infwakti vijana hawa walijitahidi sana katika kuweka kumbukumbu ya kagera dei katika mtandao moja kwa moja usiku wa kuamkia leo pale diamond jubilei


kashasha


mh. kashasha akiongoza zoezi la kuhesabu michango ya kagera dei usiku kuamkia leo ambapo milioni 100 keshi zilichangwa hapo hapo