wadau wengi wanaujua ukumbi wa diamond jubilee hall ila ni wachache wanaofahamu asili yake ambayo ni kwamba ulijengwa na jumuiya ya ismailia nchini kama kumbukumbu ya siku waliposherehekea miaka 50 ya uongozi wa kiongozi wa jumuiya hiyo Sir Sultan Mahomed Shah, Aga Khan III, mwaka 1946 sherehe ambayo iliongozwa na kiongozi wa jumuiya hiyo wa sasa Mtukufu Aga Khan ambaye alisimikwa uongozi mnamo july 11, 1957 akiwa na umri wa miaka 20

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. michuzi unatukumbusha kweli, huu ukumbi uko nyuma ya shaaban robert, imetulia.

    ReplyDelete
  2. Asante sana kwa picha hiyo ya kihistoria. Je unaweza kutuwekea mara kwa mara picha kama hizo?

    ReplyDelete
  3. ingekua poa michuzi utafute picha ya lile hall la shaaban robert pia, maana ile shule nayo ilikuwa bomba sana sana, wanafunziw alikua wanafanya maconcerts za party za shule pale pale, tafuta ya srss pia kwa ufupi, utawafurahisha wadau wa srss ulimwenguni.

    ReplyDelete
  4. Ina maana idadi ya wahindi Bongo umepungua? Cheki wahindi walivyokuwa wengi kwenye hiyo picha!

    ReplyDelete
  5. Michuzi

    1. Toa hiyo picha kulia imepitwa na wakati mimi nakumbuka hiyo picha ulipiga wapi

    2. Sio lazima kila comment uziweke humu ndani kwani nyingine zinatupotezea muda huwezi ukamridhisha kila mtu wapumbafu waache wakae na upumbafu wao, hawajui kuwa ukiweka kitu ambacho hakina hakika kinaweza kukuletea taabu au wanataka yakukute yaliyolikuta gazeti la kenya? kuwa makini ndugu yangu kumbuka kuna mafisadi wa blog

    3 Hii ni picha nzuri ya historia Baba alikuwa ananiambia ukimuona mtu mweusi wakati huo huko Upanga basi ujue ni mtumishi wa ndani wa Muhindi na anakitambulisho cha kazi ilikuwa ni marufuku kwa mtu mweusi kupita huko bila kibali kwani eneo lote la Upanga wahindi walilinunua kutoka utawala wa kikoloni Mungu amrehemu Mwalimu Nyerere kwa kufuta hati hizo na kutokea kwamba watu weusi wengi walipata viwanja vya kujenga huko Upanga mmojawapo akiwa baba yangu hii ni historiawatu wanapaswa kuifahamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...