mdau bachalla wa holland akiwa na bobby farell wa kundi lililotamba miaka ya 80 la boney m wakiwa jijini amsterdam leo. bachalla anatwambia kwamba hivi sasa bobby si supa staa tena na anaishi maisha ya kawaida tu akifanya kazi kama mtu mwingine, kuashiria kwamba usupa staa una mwisho hivyo masupa staa, hasa wa bongo, wajiandae na maisha ya umri mkubwa na mapema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Huyo Bobby enzi zake alikuwa Handsome kweli kweli. Wanawake wengi walimtaka na kutamani waolewa naye! Miaka inaenda mtu mzima sasa. Na hao Boney M walivuma sana. Nashangaa hapa Marekani watu hawawajui zaidi ya ule wimbo wa Mary's Boy Child ambayo wanaipiga kila Krismasi kwenye redio.

    ReplyDelete
  2. Duh yani with all those hit records bado wanaishi maisha ya kawaida, nilidhani kwa kuwa ni stars ,atleast kwa kila mwaka hawawezi kukosa kufanya small tours kwa nchi mbali mbali duniani, haswa ukizingatia fans wao ni watu wazima na ni wanahela ya kwenda kwa shows zao.
    Nadhani tuna wahitaji hao jamaa huku hasa sisi vijana tulio kulia enzi za 80's pamoja na wazee wetu walio kuw awamejaza alums zao, na uhakika show itakuwa bomba.
    Nilidhani huyu jamaa naitwa Frank Farrian!

    ReplyDelete
  3. Mimi nilikuwa kipenzi sana wa BoneyM. Hasa nyimbo zao kama trip to venus(night flight to venus),mabberker, bononous,I shall sing, sing a song ti- ti taaa-titi ta, I shall sing, sing a song, shalla la la la laaa! ah aha ha bononous, bononous, ! ( wanakijiji hakuna kunicheka hapa nimejitahidi mwenzenu),chumbani kwangu kulikuwa na picha zao wote.Lakini je bobby hana pesa kabisa? mbona gold zao bado zina uzika.je wanawake zake wako wapi? this is good memory to share!

    ReplyDelete
  4. Duh..jamani !!! nashindwa kuamini macho na masikio yangu!! sasa hawa vijana wetu wa bongo flava ambao nyimbo zao zinasikika hapahapa ilala na magomeni wakifikia umri huo na hali hiyo itakuwaje???? pole mkongwe wetu bobby..hayo ndiyo maisha!Nilikuwa na mpango wa kuwa supa staa sasa sitaki tena!!

    ReplyDelete
  5. Bachalla! Huu ndio ukweli kuhusu maisha iwe ya kisupa staa au ya kawaida ni lazima tujiandae kwani uzee haukwepeki!Nakutakia maisha mema huko uliko na mpe hai mzee mzima Bobby , je wale warembo wake bado wapo muulize tafadhali.

    ReplyDelete
  6. Tatizo ni Mkataba waliokuwa wameingia na Meneja wao aliyejulikana kwa jina la Frank Farian. Jamaa aliwakusanya wakiwa si chochote si lolote, akwapa jina la Boney M, akawatumikisha na kuwakamua vilivyo huku yeye akivuna Masimbi. mwisho wa siku akawaacha akina Bob Farrel, Maizie Williams, Marcia Barret na Liz Mitchell. Mikataba ya kitapeli haiko Bongo tu, ndugu zanguni!!

    ReplyDelete
  7. Jamani Bobby, hapo huwezi kumjua kama hujaelezwa.bachalla asante kutuletea kumbukumbu hii ya msanii huyo maarufu na aliiweza fani yake hiyo kipindi hicho sina hakika ila nahisi hakuna asiyukua akiwapenda group hiyo anapowasikia wanaimba kwa jinsi ya umahiri wao, juzi tu niliukumbuka huo wimbo wa bononous nikawa naimba nikawa nnapicha kua wako vilevile ila ukimuona hapo huamini kama ni yule Bobby M wa miaka ile mpaka uambiwe, jamani uzee huu mhhhm,hapo nakumbuka ule usemi kua ukitaka kujua uzuri wa mkeo mwangalie makweo, na ukitaka kujua uzuri wa mumeo mwangalie bamkweo. Mh! kazi kwelikweli baada ya miaka kumi na kumi na tano ijayo akifika shinyanga tuu ile pyeeee wanamponda mawe eti kizee kichawi hiki. kaaazi kwelikweli

    ReplyDelete
  8. we kobelo umempata wapi kibabu huyo????jamani huyo ajachoka njaa mr bobby,sema vitaa vyekundu vya amsterdam ukiviendekeza lazima uzito upungue na mvi unazo...kwako sekulu.mawaya.

    ReplyDelete
  9. Hamna cha Dar, Bongo flava, Uk, Usa au hata sijui wapi....Maisha ni mpangilio...uwe unalipwa billions au unalipwa a penny ...maisha ni jinsi unavyoyapangilia...Ule wimbo unaosema final uzeeni hawakukosea

    Ni wangapi hata USA walivuma sana lakini sasa hivi hata ukikutana nao mjini huamini ni wao...Tembelea Atlanta. Sijui ni kwanini macelebrities wengi wakichacha wanakimbilia ule mji....Utawaona wengi tu wanakatiza mitaani kama watu wa kawaida. Nilikua napapatika sana nilivyotembelea huo mji kwa mara ya kwanza. Kila nimwonae ninapiga naye picha...mara ikawa kila kwenye kijikona unamuona mtu ..ukikumbushwa ni nani macho yanakutoka..

    Lakini kila mahali pana faida yake..uzuri wa USA ..unaweza kuishiwa ukaanza mwanzo ukarudi juu tena ukijitahidi... na uzuri wa bongo ukiishiwa unakimbilia kwa shangazi na binamu kujisitiri....Ila asiye na shangazi bongo na USA asiye na bahati tena ndio hivyo unawakuta wanafanya kazi za ukorokoroni.

    Wako wengi sana tu kama huyo baba sasa hivi wanaishi maisha ya kawaida tu. Huwa hawawezi kudowngrade lifestyle yao mpaka penny ya mwisho bank....

    ReplyDelete
  10. Huyo Bobby sio uzee tu,alijiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya,yaani ni mteja, mimi mwenyewe ninaishi hapa hapa Holland, na nimewahi kumuona, na sio kazi kumuona, anaonekana sana Amsterdam mjini pale karibu na stesheni ya treni.
    Kwa kweli huyu jamaa amechacha sana, sababu ya uteja, hakuna kingine chochota naomba mnielewe hivyo.
    Kuna kipindi cha mwaka juzi,hapa holland walimpatia tangazo moja katika TV, ili wamsaidie kipato cha kusukumia maisha.
    Hakuna wa kumlaumu ni yeye mwenyewe amejitakia,unajua hapa Holland serikari imealalisha mambo mengi haramu, ndio maana ni rahisi kuwapoteza watu kama hawa.
    wasanii wa bongo kazeni buti tu, mtafanikiwa.

    ReplyDelete
  11. Amsterdam kila tajili lazima achoke kama ukiamua kuishi,kwani ni sehemu pekee kila kinachopigwa marufuku duniani hapa kimeruhusiwa,huyu bobby nazani mtumiaji wa mambo fulani na unyamwezi hawezi kuyapata ndio maana kaja kulikita hapa...bobby kijugu.hata kama hunapesa holland na unatumia madawa ya kulevya unapewa kanisani na padri,bule.bange unanunua kama sigala, vitaa vyekundu sehemu za wanawake unaona kwenye vioo,je uwe na pesa kiasi gani uishi amsterdam,,,lazima uchoke.michuzi umenibania moja nasema kobelo hii usinibanie au nawe ajax kama challa.ajax mnakuja kupigwa bao na fayenoord leo.longa mkude.

    ReplyDelete
  12. Sasa nafikiri mnanikubali,niliwaelezeni kua huyo Bobby ni kijugu, na hakuna mtu yeyote anaekaa hapa Holland na kunjua Bobby, na hasifahamu kua ni kijugu " mtumiaji wa mdawa ya kulevya.
    Nakubaliana na mdau Mkude hapo juu, yeye anaifahamu Holland vizuri sana,na amejaribu kuwaelewesha vizuri wale wasio ijua.
    Holland ni nchi ya kwanza duniani, kuhalalisha mambo yote haramu, Bangi inauzwa dukani "kofieshop"
    Wanawake kwenye vioo "red light"
    unataka wa taifa gani? utapata.
    Masuper star wa dunia nzima wanakuja kufanya starehe hapa,
    Kwa mfano SNUPPY DOG DOG, hapa ndia kwake,kila kukicha anakujakuvuta bangi,kwa sababu imealalishwa, Mwanamuziki maarufu wa muziki wa reggae "CULTURE"JOSEFH HILL, hapa ndio palikua kwake kwa sababu ya uteja wa bangi, na mpaka ikamto roho,Alipomaliza kupiga concet vizuri hapa Holland,Alivuta sana bangi ikawa over Dozzzzzzzzzzzz,
    matokeo yake amekufa ndani ya basi, akiwa amelala, kuelekea Ujerumaini,kuendelea na kazi za kimuziki, iyo ni mifano miwili tu,
    Kwahiyo Mdau wetu Bachala, alipata bahati ya kukutana na Kijigu Bobby,lakini sio mtu muhimu kwa kipindi hiki "kizazi kipya"
    Kuna masuper star wengi sana hapa Holland, mbona hatuwaoni? ni kwa sababu wanajiheshimu na kufuata taratibu za maisha.
    Mbona usimuone wakati ule alipo kua kweli Boney M? unamuona leo wakati amekwisha kua kijugu, msipotoshe watu waelezeni watu ukweli ili nao waweze kujifunza, sio kutaka kuleta ubishoo, kwamba umekutana na mtu maarufu,kumbe yuko juu ya mawe, kachoka kwa upumbavu wake mwenyewe,uko ni kujizalilisha wewe mwenye, eleweni hivyo ndugu zangu mnataka msitake huo ndio ukweli.

    ReplyDelete
  13. Anayeuliza atlanta kuna nini?? Ni cheap std of living...mansion wanazoshindwa kuzilipia east coast au west coast wanazinunua hapa kwa bei rahisi sana....Nyumba ya laki 5 hapa ni mansion hiyo hiyo NY City ni one bedroon

    Huyo babu apewe pole bangi nibangue

    ReplyDelete
  14. HIVI NINYI MNAOMUONGELEA HUYU MTU MNAKUA KAMA HAMJUI KWAMBA AMEESHAFARIKI DUNIA WIKI HII. SOMENI HABARI VIZURI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...