WADAU KUNRADHI, MSIONE KIMYA HAPA NILIPO KUNA EMAIL KAMA 3,000 ZIMEINGIA KWA MKUPUO, NYINGINE KUTOKA SAYARI YA PLUTO NYINGINE KUTOKA SAYARI YA MARS NA NYINGINE HUMU HUMU DUNIANI ZIKIDAI ZAWADI.
INGEKUWA RAHA SANA WOTE WANGEKUWA KAMA HAO WADAU WAWILI WENYE HIZO PICHA AMBAO KAMA NI MPIRA UMEGONGA BESELA NA KUTOKA NJE KABISA YA UWANJA. ILA KWA USTAARABU WAO WAMEKUBALI MATOKEO BILA KELELE WALA MIKWARUZO.
ILA MSIKONDE WALA NINI MSHINDI HALALI KESHAPATIKANA NA ATATANGAZWA SASA HIVI. ILA NAOMBA MUDA NIHAKIKI EMAIL ZOTE NA PIA WATAALAMU WA GLOBU HII YA JAMII WALIOKUBUHU WATHIBITISHE KWAMBA HUYO MSHINDI NI WA HALALI KWA KUWA MDAU WA MILIONI 3 NA SI VINGINEVYO.
KUMBUKA: UAMUZI WA MAJAJI WA GLOBU HII YA JAMII NDIO WA MWISHO...


yaani counter iliacha kuonyesha mpaka ikapita 2, anyway Good Job
Mazembe Nyerere,


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

 1. I hope is a real winner kwa vile mimi niliingia kwenye blog ilikua imebakiza watu kama 100 mara na check tena inaonyesha error #10. Sasa sijui wakati huo ilikuaje kwa sehemu zingine hiyo counter iwe inafanya kazi na kwa wengine isifanye kazi

  ReplyDelete
 2. Itaanza hivyo hivyo, hadi ifikie kama zawadi ya mtabiri wa mechi za Man na Arsenal...Imani inaanza kupungua sasa misupu.

  ReplyDelete
 3. Katika walioumia na hii ngoma ya bahati nasibu na kukosa mimi ni mmoja wapo! NIna hakika kabisa kabisa. Number 2,999,999 nilikuwa nayo, then ikaja 3,000,001 baada ya 3,000,000 kudai # error! That was very strange and never ever seen it before! Picha ninazo. Hongera mshindi. Nadhani kama siyo UFISADI wa ISSA basi ni internte speed imenua hapa!

  ReplyDelete
 4. justineustace@yahoo.com
  woisoje@gmail.com
  hustidoit@hotmail.com

  ReplyDelete
 5. Hongera kwa kumpata mshindi wa milioni tatu, na huyu nae nategemea hatotoka bongo kama yule aliepita, ila kitu kimoja kila shindano lina mshindi wa kwanza mpaka wa 3 kwa nini na huyo jamaa msizawadie hata kalaini ka tigo? nae alonge kama sie?
  mdau mr C.T
  DSM

  ReplyDelete
 6. hilo zoezi kwa mtazamo wangu naona lina kasoro, maana hiyo 3000001 naona kila mtu kaipata, hadi sasa huyo ni mtu wa tano ukijumlisha na watu nilionao karibu, inakuwaje watu watano wakawa na no moja. hata hao wanaosema wamekuwa wa mil.3 kuna uwezekano ikawa kweli maana kwa watu niliowaona hapa karibu no zilikuwa zinagongana, yaani no moja watu watatu.

  mdau....

  ReplyDelete
 7. MICHUZI MIE NIMEKUTUMIA E-MAIL LEO KUSEMA NA NIMETUMA PICHA INAONYESHA MILLIONI TATU NA 2 (3000002) MBONA HUJAIWEKA PIA HUMU UMECHAGUA YA MWINGINE UNADHANI MIE MUONGO??????????????

  INAONEKANA KUWA COUNTER YAKO INAWEZA PATA WATU ZAIDI YA MMOJA KWENYE NAMBA MOJA.

  PLEASE POST THIS AS NAONA UNAWEZA KUWA NA WASHINDI GENUINE WA 3 MILLION NA UKAZANI WENGINE WAONGO

  ITASAIDIA WEYE KUONEKANA KUWA UNAJUA MAMBO NA BILA KUTAPELI

  ReplyDelete
 8. ...hata mimi nilipata error kibao kabla ya kupata namba 3000009 ambayo naamini ina watu wengine kibao. iwapo hata hio milioni 3 ilikuwa na watu zaidi ya mmoja itabidi michu na wataalamu wake wabukue kucheki nani alianza kulog kwenye hiyo namba. natumaini, ndimi...!!!!

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...