Mhariri wa Mtanzania, Deodatus Balile, akiwa ameshika cheti chake cha Shahada ya Uzamili bada ya kula nondozz za Uongozi wa Biashara (MSc Business Management) nje ya Ukumbi wa Middleton katika Chuo Kikuu cha Hull nchini Uingereza. Sherehe za kuhitimu zilifanyika Alhamis ya Januari 24, 2008. asante mdau Ansbert Ngurumo kwa picha na hongera balile kwa nondozzz hizo. karibu homu uendeleze libeneke...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. mambo ya nondozz hayooo.. hongera kaka, rudi home haraka ukibaki huku utaanza pata ugonjwa wa ulaya ulaya .. mabox kwa sanaaa

    ReplyDelete
  2. We Balile wewe!! Si juzi tuulikuwa unachukua Dploma pale Chuo cha Diplomasia haya huyo Masters umemkatishia denge gani? nipe na mi hako kamchong0 n'shachoka kuikala mu Klasi mweeeee!!!
    Enewei kongratulesheni.

    ReplyDelete
  3. Huyo sio mhariri wa Mtanzania,Ni mhariri wa Tanzania Daima.Hongera Balile'
    Felix-USA

    ReplyDelete
  4. Hongera sana mkubwa! God bless you to enjoy the fruits of your hard earned digree.

    Kila lakheri katika majukumu yako.

    ReplyDelete
  5. We Felix,usijifanye mkosoaji wakati huna data.Balile alikuwa mhariri wa TZ Daima lakini baada ya kurejea bongo kutoka masomoni UK,alirudi gazeti la Mtanzania.Mhariri wa TZ Daima sasa ni Absalom Kibanda (kama sijakosea).By the way,Michuzi ni mwanahabari,so anajua alichoandika.

    ReplyDelete
  6. Balile kaniudhi. Kwa nini akasomee digrii ya uongozi na biashara uingereza wakati hata hapa Tanzania zipo zinapatikana kwenye vyuo vyetu?.

    Kwa nini awape mapesa yote hayo waingereza asilipe vyuo vikuu vyetu vya hapa Tanzania ambavyo vinatoa hiyo digrii pia?

    Hata kama wamemlipia wafadhili kwa nini wasimlipie vyuo vyetu hapa walipie kwenye vya kwao?

    ReplyDelete
  7. Huyu Bwana nilikuwa nakula nae box hapo Tesco kwa sana tu !!

    ReplyDelete
  8. Omushaija Balile, mbona kacheti kenyewe kanafanana na kale kwa Lyatonga, ka kweli haka!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...