hu haaaa! wadau, baada ya benki kuu panga la jk lielekezwe wapi sasa na kwa sababu gani?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 51 mpaka sasa

 1. litaelekea daily news.

  ReplyDelete
 2. Naona baada ya benki kuu hilo mashete lielekezwe kwenye mabuzwagi...namaanisha mikataba yoote ambayo haijatulia na kwa kuanzia ni ile ya madini na hasahasa Buzwagi yenyewe

  ReplyDelete
 3. Sasa lielekezwe kwa bodi ya mikopo ya wanafunzi HESLB kwa kutoa mikopo kwa watu wasiokuwepo.mimi nimeshuhudia mtu akipewa check ya sh. milioni mbili bila kupiga sahihi.hizo ni zile nilizoshuhudia mimi,je mangapi yanatokea behind closed doors?????

  ReplyDelete
 4. Tiscan yaani naona wanakula pesa za wananchi tuu kwani kazi wanayofanya ndiyo hiyohiyo TRA wanayoifanya na kusababisha kero kubwa kwa wananchi
  Michuzi fikiria mwenyewe unaleta mzigo kutoka ng'ambo kuja kusaidia hapo nyumbani inabidi uanzie Tiscan uwalipe kisha unaendelea na clearance kisha unawakuta TRA wanaverufy tena sasa huo ni usumbufu mkubwa sana
  Michuzi tuambie ni kilaji cha nani hicho ?

  ReplyDelete
 5. Mbona jambo lipo wazi kabisaaaaaaa! Panga lazima lielekezwe Nishati na MADINI. Richmond mbona kimyaaaaa!! IPTL!!! Mererani!! etc.

  ReplyDelete
 6. Michuzi inaelekea huyo anon wa kwanza hapo juu ni mmoja wa wale walionufaika na buzwagi ya Bot. Akina Changanyikeni Guest House Ltd! Sasa ulivyouliza umemuudhi.

  ReplyDelete
 7. Kikwete hube be serious, hivi waona hii report watz watadanganyika? kama hauhusiki taja taja watu taja... blv me watz wako nyuma yako lkn nahisi kama utaendelea na report zanamna hii jiuzulu tuu baba....

  CHANGA HILI.....

  ReplyDelete
 8. Na kweli lielekee hukohuko kwenye system zenye mkono wa serikali. Tanesco, mahospitalini...Huko ndiko jamaa zetu walikojisahau na kufanya vitu vyao, ukiuliza unaambiwa `tukale wapi..' Lakini Daily news sijui, manake hilo shirika silinamilikiwa na wenyewe...kidumu!

  ReplyDelete
 9. alielekeze ikulu ajikate mwenyewe, ni hela za BOT ndiyo zilimsaidia campaign 2005...kushirikiana na rostam na lowassa.
  Hata kamatwa mtu katika bot, kama atakamatwa mtu, kesi itayeyuka.
  -mwana CCM

  ReplyDelete
 10. Lielekezwe TRA na baadae NBC Holding kwa sababu ya rushwa na kujilimbikizia mali kinyume cha sheria. Ilinganishwe mishahara ya wahusika na mali walizojilimbikizia. Lakini kwanza tunataka tuone hatua zinazochukuliwa dhidi ya mafisadi wa BOT (Benki Kuu) Siyo tu kuishia kutoa taarifa, halafu baadae tuambiwe hakuna ushahidi wa kutosha kuwachukulia hatua. Serikali pia iwe macho kwa watu walioficha mali kwa kutumia majina ya ndugu zao, rafiki zao au watoto wao.

  ReplyDelete
 11. JK hakuna kitu, huyo Balali alikuwa hatakiwa na wahindi walio upande wa JK ili awekwe Gavana wanaomtaka wao ili nao wachote hazina ya fedha zetu!

  Ni yale yale tu hakuna jipya, wahindi wa serikali ya Mkapa walikula chao kupitia kwa Balali, sasa wahindi wa JK ni zamu yao kula kupitia kwa Gavana Mpya

  Hii nchi na wananchi wake ni ya kuhurumiwa tu! NOTHING IS REALLY HAPPENING.....imejaa mafisadi wa karne!

  ReplyDelete
 12. Sote tunajua kuwa anachofanya JK hivi sasa ni usanii tu. Balali alishatema mzigo tangu zamani, leo JK anajifnaya eti kamfukuza kazi. Kama JK anasema kamfukuza kazi Balali basi kwa namna moja au nyingine anakiri kuwa amehusika katika ubadhirifu wa pesa hapo BOT na kama ni hivyo kwanini asimuru hatua zichukuliwa ili Balali arejeshwe nchini kuja kujibu tuhuma? Hii miezi site aliyotoa uchunguzi zaid ufanyike zitaisha bila ya lolote la maana kufanyika. Eti bodi ya BOT ikae na kuwachukulia hatua wahusika!!! Uliona wapi muhusika akijuchukulia hatua mwenyewe? Kama bodi ilishindwa kusimamia pesa zetu unadhani watafanya nini hivi sasa? Inabidi tufike mahali tuache mambo ya ngonjera tuwe makini na mambo tunayofanya kwa faida yetu na vizi vijavyo. BAADA YA MIEZI SITA UTASIKIA KUWA BAADA YA UCHUNGUZI WA MUDA MREFU TUMEKOSA USHAHIDI WA KUWEZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WAHUSIKA WA UPOTEVU HUU WA PESA.

  ReplyDelete
 13. Misupu kama kweli JK ana panga basi panga hilo ni butu kwani halina uwezo wa kukata hata vijiti kwani mi naona mpaka sasa hivi halijakata kitu. BOT yule jamaa kajiengua wala si JK aliyemtoa, mi nakumbuka ule wimbo wa kusuku ulioimbwa na bendi moja ya kutoka kwa watani wa jadi naanza kumfananisha JK na kawimbo hako kwani kazidi kuongea lakini hakuna matokeo wala hatua zinazochukuliwa kilichobaki wanatuletea mahesabu ya safari zake za nje kwa kulinganyisha na wengine hama kweli TZ porojo kweli kweli inapokuwa kitu kibaya wamefanya wanajaribu kuhalalisha kwa kulinganisha na mwengine. Jamani viongozi wetu sisi tunalalamika kama watanzania siyo kama afrika jaribuni kuliona hilo

  ReplyDelete
 14. HAKUNA KITU UMASIKINI WA WATANZANIA UNAZIDI NA UTAZIDI,JK HANA JIPYA TUNACHOONA JINSI ANAVYOLINDA WANAOMZUNGUKA BARAZA KUBWA,SHILINGI INAZIDI KWENDA CHINI,RUSHWA KILA MAHALI,NAFIKIRI HICHO NI KIASI KIDOGO SANA TUNATAKIWA KUANGALIA MIKATABA MINGI KAMA YA UKODISHAJI BANDARI KITENGO CHA MAKONTENA,MIKATABA ILITOLEWA NA PSRC NK

  ReplyDelete
 15. Panga lielekee PSRC. ni sooo!

  ReplyDelete
 16. hamna lolote panga lenyewe baada ya miaka miwili bora nchi iuzwe tu kila mtu ale chake tu

  ReplyDelete
 17. panga liende kwa wawekezaji pamoja na kuchota utajiri wetu bado haki ya mishahara kwa wazawa haipo, serikali iliposema mfano kima cha chini ni 200,000.00 haimaanishi wengine wa juu kidogo kama mfano mhasibu msaidiz alipwe 250,000.00 wakati mhasibu msaidizi wa serikali analipwa laki 323,390.00.

  ReplyDelete
 18. Hakuna Kitu, hakuna panga lolote lililotembea. Balali amejiuzulu toka Dec. 2 2007. Barua ipo. Wewe Raisi leo unakuja kutuambia kuwa umemfukuza kazi.Acha usanii sema umekubali kujiuzulu kwake. Mbona naibu Gavana wakati wa Balali hukumfukuza kazi? Juma Reli, yeye si alikuwa msaidizi wa karibu wa Balali? Acha usanii fanya kazi...HUJAMFUKUZA KAZI BALALI..AMEJIUZULU TOKA DEC. 02 2007 BARUA UNAYO MKONONI KWANINI UNAONGOPA? KAMA KWELI UMEMFUKUZA KAZI BALALI JE MSAIDIZI WAKE MBONA HUJAMFUKUZA?? ACHA USANII, UNAONA MTU AMEJIUZULU UNATAKA KUCHUKULIA POINT KUWA UMEMFUKUZA

  ReplyDelete
 19. Michuzi, samahani kaka. Ila mi naona tunazidi kusanihiwa. Hakuna lolote hapa, huu ni usanii tu.

  Kwani best man kafanywaje mpaka sasa ingawa aliua mbele ya umati wa watu? Iko siku atakuja mtu makini kutuongoza, na wasanii wote watakuwa accountable. Tusijisahau sana na kufikiria tutaongoza milele hata kama tunajichimbia mizizi ya utawala hivi sasa kwa kuhakikisha vizazi vyetu vyote vinaingia NEC. Tuangalie mifano live kutoka kwa majirani wetu.. na sisi tujiandae kwa yajayo. Lets be serious.. angalau once!!!

  ReplyDelete
 20. Ndugu yangu Misupu hii nondo inaukweli mwingi ndani yake!

  Sote tunajua ya kuwa:

  1: Bila ya kele za akina Zito na Slaa, huu uchunguzi usingefanyika
  2: Watawala wetu walitumia nguvu zote mpaka wakazunguka mikoani kukanusha shutuma za akina Zito na Slaa
  3: Pamoja na kelele zilizokuwa zinapigwa na wapinzani, na watawala kujua kuwa ni za kweli bado walikataa kufanya lolote mpaka pale waliposhinikizwa na wafadhili wa nje
  4: Wahusika wa kashfa hii bado wapo kwenye nafasi zao na wanaendelea kufaidi matunda ya ufisadi wao
  5: Balali katolewa kama sadaka tu. Haingii akilini ati pesa zote hizo zinapotea halafu all you can do ni kumfukuza mtu kazi.
  6: MWISHO WA HII SINEMA ITAKUWA KAMA ZINGINE ZOTE. MAFISADI WATAENDELEA KUPETA WAKATI WANANCHI NDIO WANAZIDI KUWA NA MAISHA MABAYA

  ReplyDelete
 21. immigration, hasa mikoani, ni hela ndogo ndogo wanazokula kabla kukupa huduma lakini haba na haba hujaza kibaba!! wanachanga na baada ya miezi kadhaa wanajenga kwa migongo yetu!!!

  ReplyDelete
 22. ndugu zangu watz, kwa kweli sisi tumerogwa eti mpaka ndugu zetu wadosi wanyimwe hela baadaye warushe ile mail basi tuanze kufuatilia!!hela zilizo tajwa ni ndogo na hizi zilizo tajwa zinamfuatilia(lengaz) kigogo mmojaz bale twin tower!kisa totoz!! mchanga huu kwa jumla! Mshikaji wake vipii???

  ReplyDelete
 23. JK haja fanya chochote. Huyu jamaa alisha achia ngazi tangia mwaka jana. Hana ugonjwa wowote ule. Yuko hapa US na mke na watoto wake akila hela za wanachi bila aibu. Ana nyumba hapa US, wala siyo moja. Hana ugonjwa wowote, amejificha. Hakuna mtu ana lazwa hosipitali hapa US kwa muda wa miezi mitatu.

  ReplyDelete
 24. mimi nashauri twende taratibu.hebu tumalize hii saga ya bot kwanza maana nayo kuishughulikia si masikhara,if successfull then....

  ReplyDelete
 25. kaka michuzi,kuna fisadi wa dizaini iyo hapa south korea ,alifilisi kampuni kubwa ya BBK,alikimbilia marekani ivoivo,lakini nbaada ya uchunguzi wa selikali na kugundulika,alifuatwa na kuletwa mbele ya sheria,jee serikali yetu itashindwa kufanya hivyo!!!MDAU SEOUL

  ReplyDelete
 26. PANGA LA MUNGU(SIO LA JK) LIELEKEZWE KWANGU MIMI NYAKATAKULE NIMEKUWA NA TABIA YA KULALAMIKA TU, KUKOSOA TU, KUANGALIA TU NA KUTEGEMEA MIUJIZA YA KUINUA MAISHA YA MTANZANIA TOKA KWA RAIS NA MAWAZIRI NA VIONGOZI WAKUU WA SERIKALI BILA KUJUA KUWA BILA MIMI KUZALISHA NA KUTOA USHIRIKIANO KUWAUMBUA MAFISADI BASI HATA GAVANA WA BOT ANGEKUWA MALAIKA GABRIELI MWENYE PHD ZOTE ZA UCHUMI NA UTAWALA WA FEDHA, TUTAENDELEA KUWA NCHI YENYE UMASKINI ULIOKITHIRI.

  NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO

  ReplyDelete
 27. Panga? Balali yupo kizimbani?

  ReplyDelete
 28. Jamani watanzania mbona mmelala namna hiyo?? Hivi kweli Jk anaweza akamtimua kazi Gavana ambaye aliidhinisha kutoa mamilioni ya pesa kwa ajili ya kampeni zake wakati anawania uraisi??

  Sasa ngoja niwaambieni.... Ukweli ni huu hapa....

  Balali alishafariki siku mbili zilizopita kabla ya Jk hajatangaza kumtimua kazi, na kama mnabisha basi subirini si muda mrefu sana mtasikia Balali amekufa,, JK alichofanya ni kiini macho tu kwa WADANGANYIKA an samahani WATANGANYIKA kwa kutaka kurejesha imani kwa WATANGANYIKA maana asilimia kubwa ya watu wameshachoka na mwendendo mzima wa serikari yake.

  Ninasema hivi kwa uhakika kabisa na kama mnabisha hebu niambieni Balali yupo hospital gani, na ugonjwa wake ni upi, na kwa nini taarifa za ugonjwa wake zinafichwa sana?

  Michuzi usiibanie hii

  ReplyDelete
 29. Kwanza JK alinoe hilo panga na alielekeze kwa Richard L... wa Richmod. Hapo nitampa tano na kura yangu 2010.

  ReplyDelete
 30. HILI NI PANGA GANI LINALOFYEKA MSITU NA KUACHA MITI MINGINE IMESIMAMA? HIVI NI KWA NINI HUYO NAIBU GAVANA AMEACHWA WAKATI WALIKUWA WAKIPIKIKA CHUNGU KIMOJA NA HUYO GAVANA ALIYEFYEKWA? KUSEMA KWELI MIMI SIONI KWA NINI AMEACHWA APETE WAKATI YEYE NDIYE ALIYEKUWA MSHAURI WAKO WA KARIBU!

  HATA HIVYO PANGA LIELEKEZWE NSSF NA WASHIRIKA WAKE KWA SABABU ZIFUATAZO:
  Mnamo tarehe 7/7/2007 Mkurugenzi Mkuu wa Shirirka la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Ramathan Dau alitiliana saini na Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia Rushwa (TAKURU), kujenga magorofa kwa ajili ya wafanyakazi wao, mradi ambao utagharimu mabilioni ya shilingi. Hilo tukio lilifanyika huku baadhi ya wastaafu wakilidai shirika hilo mafao yao bila mafanikio. Wapo baadhi ya wastaafu ambao wamezungushwa hadi mauti yamewakuta kabla hawajalipwa stahili zao za mafao.

  Mbali na hilo tukio shirika hilo, pamoja na mashirika mwenza ya PPF na NPF yamekuwa yakitumia pesa za wanachama kujenga vitega uchumi mbalimbali hasa kuporomosha majengo makubwa ya kupangisha. Ni dhahiri kwamba wapangishaji wa majengo haya hulipa kodi si haba, pesa ambazo huyaingizia mashirika haya mapato makubwa sana.
  Binafsi sina ugomvi na hilo kwa sababu huo ni mojawapo ya ujasiriamali tunaoimbiwa kila uchao. Dukuduku yangu ni kwamba; je, pesa zipatikanazo kutokana na upangishwaji wa haya mahekalu zinawanufaishaje wastaafu ambao wengi wao husota sana kabla ya kulipwa mafao yao? Kuna kiasi chochote cha faida ambacho hugawiwa kwa wanachama wa Mashirika haya?

  Nasema hivyo kwa sababu hii ni biashara ambayo hutumia pesa za wastaafu na hivyo basi ni busara kwamba faida inayopatikana iwanufaishe wenye pesa zao na si vinginevyo. Tuchukulie kwa mfano mtu anapotunza fedha benki tunategemera kwamba hizi fedha zitakopeshwa kwa wafanyabiashara kwa riba na hiyo riba hugawanywa sawia kwa wateja wote wa benki husika. Kwa NSSF, PPF na NPF na mashirika mengine ya hifadhi ya jamii kinyume chake ndio ukweli.Wanachama hukamuliwa pesa kila mwezi kisha pesa hizo hutumiwa kujenga magorofa ya kupangisha ambayo hayana faida yoyote kwao bila ridhaa yao.Je, wahusika hamuoni kwamba huu ni ufujaji na utumiaji wa pesa za wanachama kwa manufaa yenu binafsi.

  Imefikia hatua hadi hizi pesa zinakopeshwa kwa wajasiriamali uchwara ambao hatufahamishwi kiasi cha riba wanachotozwa. Ndio. Kama ni wajasiriamali halisi kwa nini wasiende kukopa benki ambapo riba zake ziko wazi kuliko kukimbilia kwenye hizi benki bubu sizisokuwa na mwenyewe wala usajiri? Ni bora wanachama wakawa na kauli juu ya matumizi ya pesa zao ikiwa ni pamoja na kufaidi faida itokanayo na ukopeshwaji wa pesa zao kwa “wajasiriamali” pamoja na kodi ya upangishaji wa haya mahekalu yayojengwa kutokana na michango yao. Pili, ningependa kufahamu kama faida itokanayo na biashara hizi huwanufaishaje wanachama wa mifuko hii, yaani NSSF, PPF na NPF.Labda faida ipo ila kutokana na kutokujua kwangu siifahamu barabara. Naomba kama kuna mdau ajuaye namna wastaafu (au wachangiaji wa hii michango kwa ujumla wao) wanavyonufaika na faida itokanayo na upangishaji wa haya mahekalu anifahamishe nipate kuelewa.

  Mdau.

  ReplyDelete
 31. WADAU, MIMI NAMSHAURI JK KUJISAFISHA MWENYEWE KUTOKANA NA KAULI NYINGI ALIZOZITOWA KWAWANANCHI NA ZINAZOGUSA WENGI. KWA KUANZIA AANZE KUZIFANYIA KAZI KAULI NA MAAGIZO YAKE YOTE ALIYOYATOWA WAKATI WA KUZITEMBELEA WIZARA ALIPOINGIA MADARAKANI. KULE KUNA MAAGIZO MUHIMU MENGI ALIYATOWA KWA MAWAZIRI NA WATENDAJI WAKE AMBAYO BADO HAYAJATEKELEZEKA. SIHITAJI KUYATAJA KWANI MENGINE HATA YEYE MWENYEWE ALISEMA YANAMKERA SANA. KUNA SIKU PIA ALITAMKA ANAWAFAHAMU WALA RUSHWA WAKUBWA NA ANAWATAKA WAJISAHIHISHE. SASA AWE MU WAZI KWETU JE, WAMESHAJISAHIHISHA? NI VYEMA MH JK AKATAMBUWA KUWA MTU MWIZI NI MWIZI TU NA HAWEZI KUBADILIKA KAMWE. NINGEMUOMBA SANA MH JK AANZE KUZIFANYIA KAZI KWANZA KAULI ZAKE ZOTE ALIZOZITOWA HADHARANI AMBAZO NI NGUZO MUHIMU KWAKE KUJIJENGEA HESHIMA KWA WANANCHI NA SI KUACHA HALI KAMA ILIVYO AMBAPO WACHACHE WANAMKEBEI KWA KUMWAMBIA ANA POROJO NYINGI KULIKO MATENDO. ASINGOJE MPAKA WAPINZANI WALIPUWE NA KUSHINIKIZA KUFANYA KAZI WAKATI HATA NAYE ANAFAHAMU KASORO HIZO.JK TAMANI KUFA KISHUJAA KWA AJILI YA WATANZANIA MASIKINI WALIO WENGI NYUMA YAKO. MDAU TOKA CANADA.

  ReplyDelete
 32. HAPO TUMEDANGANYWA NA HIO ISSUE YA BILALI KUFUKUZWA.HIZO HELA ZILIZOIBWA ZOTE BILALI SIO MPUMBAVU KUCHEZA DILI PEKE YAKE.WOTE HAO MPAKA WAKINA JK KUNDI MOJA BILALI KATUMIKA KAMA CHAMBO ANAENDA KUPELEKWA KUFANYA KAZI UBALOZI WOWOTE NJE YA NCHI MAISHA YANAENDELEA.KUMFUKUZA KAZI WAKATI TAIFA LIMESHAKULA HASARA HAINA MAANA,TUNACHOTAKA KUJUA NU HATUA GANI ZITACHUKULIA.WANGE ANZA KWA KUFREEZE ACCOUNT ZAKE ZOTE KWANZA ZA NJE NA NDANI YA NCHI.HELA ZA WALALA HOI ZIRUDISHWE ZITUMIKE KUJENGEA VISIMA VYA MAJI NA KUBVORESHA MAISHA YA RAIA.MNATAKA KUCHOTA KIASI GANI CHA FEDHA AMBACHO MTARIZIKA NAZO HILI MUWEZA KUANZA KUWASAIDIA RAIA? HAYO NDIO YANGU SIJUI KAMA MICHUZI ATAWEKA.NA MICHUZI UWAAMBIE HIO SERIKALI WAWE WANAKUJA HUMU KUSOMA MAONI YA WATU.

  ReplyDelete
 33. Panga lielekezwe IKULU na BUNGENI.
  Sababu.
  1:Aliyesema Wapinzani/watu wasijifanye Polisi,wapelelezi,mawakili na mahakimu inaonekana ana uhusiano wa karibu sana na Balali.Panga limkate.

  2:Waziri Mkuu yeye alitoa matusi kabisa dhidi ya Dr.Slaa bungeni akimuita mwongo na anaghusi nyaraka toka mtandaoni.Nae Panga limpitie.Inaonekana hajui lolote na anawaonea wapinzani.

  3:Spika Sita nae panga limpite.Huyu yeye kwa jeuri alimtishia Slaa wa watu akitaka kumfikisha mahakamani eti kisa kafoji nyaraka.Slaa wa watu akaamua kuja kushtaki kwa sisi wananchi wake.Sasa kama Spika hawezi kusikiliza mashtaka ya mbunge wake anafanya nini hapo na lijijoho lake.Eti Speed and Standard hahahahahahaha LoL
  Dr.Slaa 2010 gombea URAIS una kura yangu.
  © Majita

  ReplyDelete
 34. MI NADHANI JK ANA MAADUI WENGI CCM..HILO ANAJUA WALE WALIOKOSA HICHO KING'ANG'ANYIRO NA SASA WANATOA MABOMU YOTE NA UOZO WA CCM..ATA HIVYO WANGEPATA MCHEZO UNGEKUWA ULEULE..TZ IS MESSED UP..TOO MUCH CORRUPTION..SASA BADO WATU MIL 40 TUNAIMBA WIMBO WA POVERTY MPAKA LINI?TUNA WASOMI WENGI LAKINI HAWAJUI JINSI YA KUTUMIA ELIMU YAO MPAKA WAWE EMPLOYED ..WALIOPO MADARAKANI HAWATAKI KUTOKA AU KUKUBALI INNOVATIVE IDEAS(HILI TATIZO LA AFRICA)....!!!

  ReplyDelete
 35. michuzi nadhani sasa raisi, aanze kufanya uchunguzi kwa baadhi ya balozi za nchi za ulaya. Kwani wanajinufaisha uko ulaya.

  ReplyDelete
 36. michuzi na comment usiibane, nadhani pia huyo mpiga picha wake, ambadili maana baadhi ya watu wanashangaa na mambo mengine, aajiri mpiga picha mpya. Wewe michuzi ni kiboko sana, hongera sana michuzi, unastahili pongezi toka kwa watanzania wote duniani.

  ReplyDelete
 37. Hivi mithupu...rais JK anaweza akaacess hizi comment zetu....well atazipuuza ila zinatoa picha halisi na zinaonyesha kabisa kuwa watu wamemstukia hamna cha panga wala machete hapo ni viini macho tuu...!!

  Mdau albuquerque

  ReplyDelete
 38. Panga butu hilo...halina ukali,ni maneno tuu yaani 'debe kali hulia zaidi'!

  ReplyDelete
 39. Asante sana Michuzi kwa kuleta hoja hii. Mimi binafsi nadhani JK aelekee kwenye shirika la ndege la tanzania- ATC. Kama itakumbukwa, tayari bodi ya ATC ishatoa taarifa yake juu ya kile kilichopelekea taifa kukumbwa na aibu baada ya mahujaji kushindwa kwenda kuhiji. Sasa JK, anasubiri nini kumwadhibu mheshimiwa balozi wa zamani Saudi Arabia- Mstafa Nyang'anyi?!!

  ReplyDelete
 40. Nawashangaa wanaodai Kikwete hajafanya kitu. Mimi nampongeza sana rais wetu kwani kwa mahali alipo na cheo chake si rahisi kumfatilia kila mwananchi personally, hata nyie mnaoongelea rushwa na mengineyo mkiingia madarakani hamtaweza kucontrol hizo rushwa kwani wote tuna asili ya umasikini na mtataka kwanza mnufaishe familia zetu. Kinachotakiwa ni kwa watanzania wote kila mmoja kwa wakati wake kuzuia hayo matendo maovu yanayohatarisha utendaji bora ila nina uhakika rais hawezi kujigawa kila kona asimamie kila jambo kwani ana majukumu kibao.
  HONGERA JK

  ReplyDelete
 41. pia aangalie sana maamuzi yote anayoyafanya, kwa umuhimu awa taifa, ajadili matatizo yanaowasibu watu anaowafahamu kwa kina, na kutafuta ufumbuzi.

  ReplyDelete
 42. KWANINI HATUWAPONGEZI WAONGO AKINA SLAA? HAWA NI WAONGO MASHUJAA NDIO WANAOOKOWA HAYO MAPESA KWA UONGO WAO DHIDI YA CCM WAKWELI WA UONGO.

  ReplyDelete
 43. Anon January 11, 9:14
  Bravo...haya yote yasingejulikana kama sio wabunge waongo akina Dr. Slaa.
  Hivi mnafikiri vile vitenge na kofia na t-shirts na MINUSO iliyoweza kumfanya Mh. JK ashinde kwa kishondo mwaka 2005 zilitoka wapi??

  ReplyDelete
 44. HAAA HAAAA SUBIRINI MTASIKIA BALALI KAFA, HUYU MTU YUPO HOSPITAL GANI JAMANI!! CHANGA LA MACHO HILO JAMAA KESHAVUTA LONGTIME SUBIRINI MTAAMBIWA SAA HIVI! HAKUNA KESI HAPO WATANZANIA WENZANGU!!

  ReplyDelete
 45. Wewe anony wa 7:42:00AM EAT unaposema kwamba Rais hawezi kufanya kila kitu peke yake na hao wasaidizi wabovu anaowateua kumwakilisha ni wewe unayemtuma? Na wanapofanya ufisadi wewe ndiye unayemtuma kwamba amfukuze mtu mmoja na kuwaacha wengine wakipeta (hasa huyu naibu waziri aliyepandishwa cheo)?

  Sasa kama wanafuja pesa na kuwaacha wewe unategemea nani amuamrishe kuwafukuza? Wacha usingizi wewe au we ni mtoto wa balali nini? Usituletee wenzie tushachoka na hili li-nchi la kizezeta, ebo!

  ReplyDelete
 46. Michuzi vipi umeogopa kuweka maoni yangu? nini maana ya demokrasia?au unaogopa tindikali,mjumbe hauwawi wewe post watanzania wasome.kama vipi funga blog, au ndio walewale?
  Dj.Sukali,USA.

  ReplyDelete
 47. They say u can lead horse to the water but you cant get them to drink it, he sure has shown resilience to the ungrateful Tanzanians, I will remember his reign by the history on our economic growth which has never been as high before since independence but disgustingly we let the real Wafisadi sit on it, and blame to the dignified and hardworking one? But hey time will soon tell how down hill our economy will go and then we can have a real thing to blame on , to not even be able to afford a little maharage, and fuel prices keeps on souring high with no rain in sight , then will think about how unfair to Ballali people have been. To be honest that’s not even an office to worth his time, it’s like a market – you worth more, enjoy your retirement, I dare to say a proper office, and I salute you!!!

  ReplyDelete
 48. Bw. Michuzi hili panga likitoka hapa lielekezwe kwa wale WAONGO yaani WAPINZANI hasa Dr. SLAA kwa kuwa UONGO wao ndio uliosababisha hizi siri zote zikafichuka na hatimaye kumkosesha kazi BALALI. Hivi huyu Dr. Slaa hajua kuwa Balali ana mke na watoto wanaomtegemea? Asa alivomkosesha kazi anategemea mke na watoto wake Balali watakula nini?

  Huyu MUONGO ni lazima awajibishwe ikibidi hata kwa kumwagiwa tindikali mwili mzima ili liwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya kusema uongo!

  ReplyDelete
 49. Daah, JK kwa usanii ndio mwenyewe, hamna panga wala nini...huu ni usanii wa kisiasa tu!

  ReplyDelete
 50. Bw.masupu hii ni kati yangu mimi na wewe,najua hutochapisha hii,lakini naomba kuuliza unamaanisha aelekeze wapi PANGA au JANDO??
  manake huyo bwana twamjua sisi(temeke,kinondoni)

  ReplyDelete
 51. mimi naona yote hayo mashtaka yote tupeleke kwa yesu yeye ndiye anayeona yote hayo yalio mwangani na gizani yote atayadhihirisha damu ya yesu haikumwagika bure ni ili tuokolewe hivyo tuzidi kulia na yesu atashuka na kutembea na nyayo zao kila watakayotua ,watakapokanyaga mafisadi, damu ya yesu itawaunguza tu malaika gabriel na michael watawashukia na kutuonyesha miracles kwa hiyo jakaya kikwete wala hatubabaishi naye tumeshamtumia yesu akazungumze naye hivyo asubirie mishale ya damu ya yesu manake kama anatudanganya ajue sisi tuko na yesu
  amina

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...