THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

picha ya punda


wadau mna habari hii picha yetu ya punda aliyebeba mzigo wa magogo na mtu juu imeamsha hisia za wanaharakati wa haki za wanyama na wamenikontakt kutaka kujua zaidi? basi ndo hivyo, kaeni mkao wa kula na mnaopenda wanyama tuombe hali hii itashughulikiwa ipaswavyo. hebu cheki mzigo aliobebeshwa huyu punda kwa tripu mbili tu...


Kuna Maoni 37 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Hao wanaharakati wachukue taimu huko! haki za binadamu zimewashinda watu wanakufa huko dafua na Kenya sasa wanaingilia haki za wanyama. Wantu wangine bana.

 2. Anonymous Anasema:

  Yap, huyo mchizan aliepanda hapo juu ajue anoyo hoja ya kujibu. Its gonna be agaist the animal abusers and for animals rights. Word. Katty

 3. Anonymous Anasema:

  masikini punda wa watu, yaani watu wala hawana huruma!!!

 4. Mr Paul Anasema:

  Hala hala kaka, hao jamaa wananza na haki za punda ukiwaendekeza wataingia katika haki za kuku na mbuzi na ndio utakuwa mwisho wa rose garden na break point. mr Paul,Sydney,Australia.

 5. Anonymous Anasema:

  Nafikiri haki za wanyama hawawezi kufua dafu, unguja hakuna sheria ya haki za binadamu, sembuse wanyama! Pia punda ni moja ya wanyama kazi, ambao hata serikali inasisitiza kuwatumia ili kuondokana na umasikini.
  LMG

 6. Anonymous Anasema:

  haki za wanyama my foot! ujinga mtupu hao haki za wanyama kama wana ubavu wawashughulie mafisadi basi!!!!

 7. Anonymous Anasema:

  Usifikirie hivyo na wala usikate tamaa haki za binaadamu zipo na haki za wanyama zipo ingawa za wanyama hazijapigiwa kelele sana huko unguja kama ulivyosema.

  Hatukatai kuwa punda tuwatumie ili kutusaidia kazi zetu ili kuondoa umaskini ila cha muhimu tuwatumiaje? kwa mapenzi au ukatili? Pamoja kuwa amegundulika punda anaweza kubebe mizigo ila ni kwa kiasi sio tripu nzima ya mawe au ya matofali ya kubebwa na lori umpagaze punda unakua hapo hujamtendea haki.

  Kuku na mbuzi pia wana haki zao ndipo tuwale(tuchinje), wengi tunawanyanyasa bado wadudu hao hasa kuku tunapowatoa sehemu moja kuwapeleka nyengine mf kuwabeba kwa wingi ikiwa kwenye maboksi au matenga wanabanana mpaka wengine wanakufa kwa kukanyagana na kukosa hewa, au kuwaning'iniza upside down kwa mwendo mrefu kiasi ukiwashusha chini wanakuwa hoi kwa kizunguzungu,au kumchelewesha mbuzi kumfungulia kwenda malishoni au kumsahau zizini bila kumpa majani au maji,au kumsokotasokota na kamba bila uangalizi, kwa kifupi pale tunapowaweka wanyama wakawa uncomfortable. Au kumpiga mbwa unapomkuta kwa kumsingizia mwanga huyooooo naakirudi huku anakutana na jiwe jengine mwangaaa akikimbilia kule huyooo mwisho maskini anaingia barabarani na kukutana na tairi ndo mwisho wake umeshamnyima haki ya kuendelea kuishi.
  anyway polepole mimi wewe na yule tukilielewa hilo tutawapa wepesi wa kuishi kwa amani wanyama wetu wazuri wapendezao,

 8. Agent Anasema:

  Wewe Mr. paul na anony wa kwanza hapo juu hamjui kwamba wanyama nao wanayo haki ya kutonyanyaswa? Ina maana kwamba nyie mnachofahamu tu ni kwamba ukiwa na myama basi unayo haki na uhuru wa kumtumia kipuuzi kama utakavyo au mna maaana gani? Mie siwaelewi.

  Wanaharakati wa haki za wanyama kazeni buti hao wanahizaya waliohusika katika hilo tukio washikizwe adabu zao. Uzuri ni kwamba ushahidi wa kwanza umeishapatikana kutoka kwa huyo mwanahizaya alipepanda juu. Huyo ndie atayekamatwa kwanza kisha akawataje na wapuuzi wwenzake waloshirikiana naye kufanya huo upuuzi! Bw. Mchuzi naomba utoe ushirikiano chanya ili kufanikisha kunanwa kwa hao magaidi waliofanya huo ufirauni ili washikishwe adabu haraka iwezekanavyo.

 9. Dr. Confusion Anasema:

  Hii picha inanikumbusha nilipotembelea kijijini kwetu,siku moja mjomba alinipa historia ya punda mmoja aliyeokolewa kwa kuuwawa:kifo ndiyo kilikuwa salama yake,

  Kuna bwana mmoja alikuwa na punda wake,sehemu za vijihi vya wilaya ya same:Kihurio,Ndungu,gonja,Mpirani na Kisiwani.Nimeweka vijiji vingi kwa maana kamili lakini ni kati ya kijiji kimoja wapo.
  Yule Punda alikuwa ni pumda kwelikwleli,maana alikuwa anapigishwa kazi nzito kuanzia saa 11.00 ya asubuhi hadi majira ya saa tatu,maana kule kuna kilimo cha mpunga,usomaji wa kuni,mbolea na umeme ni bwelele.Mbali ya kazi zile zote na kutumikishwa viboko vilikuwa vinaporomoshewa punda huyo kama mvua ya masika.Kiboko ndiyo kilikuwa chakula na maji yake kwa siku nzima na mizigo zaidi ya uwezo wake.Mwenendo huu ulifadhaisha sana watu na jamii iliyokuwa inamzunguka mzee yule.Kuna muungwana mmoja siku isiyokuwa na jina akajibanza kwenye bonde ambalo punda yule hupitishwa kila asubuhi kwenda kusulibishwa.Alichokifanya mara punda baada ya kujitokeza akaachia mshale wa sumu kutoka kenye upinde na ukamchoma na kifo paepale.Yule bwana alitumua na hakujulikana hadi leo,Kijiji kizima walifurahi na kuafiki hatua ya yule bwana kwani yule Punda aliteseka sana.

  Guys this story is based on truly tale, it is not a fabricated story. So the very first day to see this photo it immensely reminded me about that story. However, others seemed to be against the animal protection activist, the think much about human rights. To be sincerely I don’t compromise with them because they have brain and ability to present or demonstrate, but who is willing to talk on behalf of animals.

  Therefore, I am vigorously support the initiative taken by the Royal Society for the Prevention of Cruelty to Animals (RSPCA) in the campaigning to improve the welfare of these creatures.

  I remain
  Dr.Confusion

 10. Anonymous Anasema:

  Michuzi,

  I think you have chosen a wrong subject here.

  We all understand that, animal should not be abused under any circumstances, either being due to poverty or just as simple as sports.

  But one thing for sure, animal right activists, should start by human right at their door step, my guess is everyone guess, they are pretty much hypocrites.

  Majority of them, looking for attention and media hypes, nothing short of that.

  We have human abuse, people are being short in Kenya, starvation in Ethiopia, Darfur and other corners of the world, this is just a minor thing.

  They should start lecturing the government, by getting more vets to look after these animals and teaching when is the limit in relation with the work load as seen on the picture.

  Animal rights, can pretty much start with their backyard before stepping on other territories.

  Did you know that Skin Exports has gained Tanzania 16Billion as reported by IPPmedia.com

 11. Anonymous Anasema:

  Kwa kweli nimesikitishwa sana na wadau wengine hapo juu, kwa maoni yao ya kupinga haki za wanyama.
  kila kiumbe hapa duniani kina haki zake.Wasichanganye mambo yao ya siasa na haki za wanyama,sasa ukisema Unguja hakuna sheria na haki za binadamu, ndio unataka ukamalizie hasira zako zote kwa wanyama, hii inaonyesha ni kiasi gani watu wanaupeo mdogo wa kufikiri.
  Kumbebesha Punda mizigo kama hiyo ni utesaji wa wanyama"abusers", na anaefanya ivyo anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria za ukiukaji wa haki za wanyama, haraka iwezekanavyo.
  Ni upungufu wa upeo wa kuwaza, uwezi ukambebesha mnyama mzigo ambao unatakiwa ubebwe na isuzu tani kumi na mbili.
  Nchi yetu imepata sifa kubwa sana duniani kote,na pesa za kigeni kwa ajili ya hao hao wanyama mnao watesa,mbuga za wanyama ndio zimeiweka nchi yetu katika ramani ya dunia, wacheni kasumba zenu zilizopitwa na wakati,haki za wanyama zinahusiana nini? na haki za binadamu? hayo ni mambo mawili tofauti, sasa wadau mnaosema hakuna haki za binadamu je wataweza haki za wanyama? huo ni upungufu wa IQ.
  Nafikiri pia hawajatembea kuiona dunia, na kuona wanyama wanavyothaminiwa katika hii dunia ya leo,watu wanalipa maelfu ya pesa, kuja kuwaona hao wanyama, sasa mnafikiri hao ni wajinga? hii ni kuonyesha kiasi gani wanyama walivyo na thamani, na wapewe haki zao zinazostahili.
  Ningekua na uwezo ningewakamata wote wanaotesa wanyama na kuwanyima haki zao,na kuwapeleka kwenye vyombo husika, na sheria zichukuliwe.
  Nawaomba manao usika muajibike haraka, kabla mambo haya hayajakithiri.
  Nafikiri mnamkumbuka yule mganga wa jadi kule kunduchi, aliekua anakunywa damu ya paka, kwa imani zake za kichawi, kua anaondoa mizimu, naomba michuzi umuonyeshe tena huyo mnywa damu ya paka, watu wajionee wenyewe, hatuwezi tukalifumbia macho jambo hili please naomba vyombo husika vifanye kazi yake,hawa wafanyao hivi hawatakiwi kabisa kuishi katika jamii hii ya binadamu.
  Mwisho namaliza kwa kusema acheni kutesa wanyama wapeni haki zao zinazostahili, msichanganye siasa na haki za wanyama, jaribu kuwaza kabla ya kutoa neno mdomoni au kuandika,usijiingize katika mambo usio yaweza.bye Mdau HOLLAND

 12. Anonymous Anasema:

  MICHUZI PLEASE, ONYESHA TENA YULE MGANGA WA JADI KULE KUNDUCHI, WADAU WAWEZE KUJIONEA TENA NA WATOE MAONI YAO,KATI YA MNYWA DAMU ZA PAKA NA MTESA PUNDA. MDAU HOLLAND

 13. Cxgpr Anasema:

  "Punda afe mzigo ufike", Mi nilijua msemo huu hauna ukweli kumbe ni kweli, wangenga kweli walikuwa na akili sana. Ukiona hivi ujue staili hii ni ya siku nyingi sana. Ila hao jamaa kweli ni "MABANDIDU", hawana hata huruma

 14. Anonymous Anasema:

  PAMOJA PUNDA NI MOJA YA WANYAMA KAZI,ANGALIA SIZE YA MNYAMA NA MZIGO ALIOBEBESHWA.INA MAANA MUDA SI MREFU HUYU MNYAMA ATAKUA HAWEZI KUSAIDIA KUONDOA HUO UMASIKINI,HII INAONYESHA TAMAA YA WATU BEBA MZIGO MKUBWA KWA WAKATI MMOJA ATENGENEZE PESA KWA HARAKA.I THINK PEOPLE SHOULD WISE UP,OK HATUNA HAKI ZA BINADAMU SIFIKIRI KUTAKUA NA HAKI ZA WANYAMA BUT THE PICTURE CLEARLY SHOWS ANIMAL ABUSE,AND IT'S ABOUT TIME SOMEONE SHOULD STAND FOR THE ANIMALS,THOSE ANIMAL RIGHTS PEOPLE SHOULD PROVIDE SOME KIND OF EDUCATION.

 15. Anonymous Anasema:

  Hii ndio miundo mbinu ya sehemu za vijijini ambapo watu wengi walikua hawana uwezo wa kumiliki magari au matrekta. Mifugo kama punda na ng'ombe wamekua wakitumika kama njia mbadala ya kurahisisha shughuli za kilimo,usafirishwaji wa mazao n.k. Na si wanyama wote wanaoweza kufanya hizi kazi,ni wale tu waliopata mafunzo wakahitimu.Kijijini kwetu hutumia ng'ombe maalum walifunzwa na kuhasiwa,kwa kulima mashama hasa kuandaa mashamba kabla ya msimu wa kilimo. Hii picha sio ngeni kwa kina sie,au hata wale wadau waliopo India.

 16. MMasanja Anasema:

  Anon WA 12:57PM SIJUI KAMA UNAISHI UK OR NOT IF NOT THEN COMMENT YAKO INA RELATE NA MPISHI MMOJA MAARUFU WA HUKU UK ANAITWA JAMIE OLIVER,AMEWEZA KUONYESHA VIPI KUKU WANAVYOFUGWA HATA SISI TUKAWEZA KUNUNUA KUKU WA BEI RAHISI,CAGED CHICKEN WANAJAZWA KWENYE MABANDA YAO HAWANA HATA SEHEMU YA KUWEKA MIGUU YAO YOTE MIWILI ZAIDI YA SHINGO IKO NJE KWA KUPATA CHAKULA MATOKEO MANYOA YAO YANAANGUKA WIRE ZA CAGE ZINASUGUA KWENYE NGOZI KUSABABISHA VIDONDA.NA WENYE KUFUGWA KWENYE MABANDA MAKUBWA HAWANA SEHEMU HATA YA KUKWANGUA KUCHA ZAO WANALISHWA VYAKULA VYA KUWATIA UZITO HARAKA ILI WAKAUZE, MATOKEO KUKU ANAKUA NA MWILI MKUBWA KULIKO UWEZO WA MIGUU YAKE KUBEBA UZITO,KWA KIPINDI CHA UHAI WA HUYO KUKU BADALA YA KUKIMBIA APATE ZOEZI ANAKAA SEHEMU MOJA KWA KUA HAWEZI KUTEMBEA .VILE HAYA MAMBO YANATOKEA NCHI ZA WATU SUPERMARKET ZINAZO HUSIKA KUUZA HIVI VITOWEO VINAANZA KUBADILISHA MUELEKEO WA VIPI KUKU WAO WAFUGWE ILI KUPATA KUKU ALIEPATA MAISHA MAZURI NA MALISHO MAZURI HESHIMA KWA MNYAMA MPAKA WAKATI WA KUCHINJWA.INAWEZEKANA MTU AKAJIULIZA WHY BOTHER SHOW RESPECT TO AN ANIMAL WHO AT THE END OF THE DAY YOU ARE GOING TO SLAUGHTER AND EAT IT?and my answer is WHY US AS HUMAN BEINGS SHOULD BOTHER TO EAT NICE,DRESS NICE AND ENJOY LIFE WHEN AT THE END OF THE DAY WE ARE GOING TO DIE ANYWAY.

 17. Animal lover Anasema:

  Hata wale kuku wanaosafirishwa kichwa chini miguu juu kwenda sokoni kuuzwa Kwenye yale bamboo baskets zao ni animal abuse. I hope watawazuia watu wanaofanya hivyo pia.

 18. Perez Anasema:

  Michuzi ndugu yangu nakuusia, angalia, PEMBA huko! Ohho!
  Jamaa umemuumbua huyo na kumzibia rizki yake atakupiga KIPAPAI huyo, Ohoo!
  Wenzanko huko wanaenda sehemu moja inaitwa KONDE huko! Ngende yako haioni ndani kwa huko!
  Shauri zako. Mi simo!

 19. Anonymous Anasema:

  We Masanja sawa na mkandamizaji na wengine maannnon hapo juu hamna point. Yaani mnyama umpe haki? Huwezi ukaongelea haki ya mnyama wakati ya mtu bado haijapatikana aisee! Augument ya kwamba kwa kuwa sisi tunakufa kwa hiyo mahitaji tunayopata yawe sawa na kuku kabla ya kuchinjwa!??!! Sielewi nyie Watanzania mmeanza kuchanganyikiwa lini?

  Juzi juzi tulikuwa tunaongelea suala MAFISADI, na bado halijaisha, wewe tena unataka kuingiza haki za wanyama kulinganisha na za watu..!??! Mnyama anatakiwa atume 100% bila kujali ili mradi ale na kushiba. Unapotoa mifano ya kuku kulishwa huko Ulaya ili wanenepe, ndo vitu ambavyo sisi vimetushinda huku bongo tunakufa na njaa! Wewe usiangalie kuku kala nini na wapi, angalia kuku ni mnene kiasi gani. Kwisha! Unless huwa unanunua miguu ya kuku, lakini ikipinda au kunyooka wakati wa kulishwa hiyo haituhusu. Issue ni kumla mnene.

  Haya mambo yametushinda huku bongo, mahindi heka moja gunia 2! halafu wewe uko UK huko unajifanya eti kuku anakula mpaka anapinda miguu??!!

  Tatizo la shule ukisoma sana unaweza usiilewe, hasa kama unasoma shule za questionnaires badala ya zile za high quality scientific research. Masters na PhD nyingi sana bongo siku hizi ni za questionnaires, na hizi kwa kweli zinatuvuruga sana Watanzania. Ulaya, China na Japan ziliendelea kwa scientific research na si kwa kuuuliza maswali.

  Ndo maana huyu anaongelea kuku kupinda miguu wakati akila. Haongelei watoto wa Kitanzania kupinda miguu kwa malnutrition! Inawezekana anasoma shule ya questionnaires.......

 20. MMasanja Anasema:

  WEWE anon wa 11:22PM NYIE NDO MNAO ITWA IGNORANT.MTAENDELEA KUWA HIVYO HIVYO.KWA AKILI YAKO NDOGO UNAONA MNYAMA HANA HAKI,NA ABUSE IS THE RIGHT WAY FORWARD.FROM READING YOUR COMMENTS IT SHOWS YOU ARE THE ONE WHO ATTENDED YOUR SO CALLED QUESTIONNAIRE SCHOOLS,I DIDN'T AND I DON'T EVEN KNOW WHAT THEY ARE.WAZUNGU WAKIKWAMBIA WANAKULETEA GM FOOD WEWE NAONA UTAFAKAMIA KWASABABU UNA NJAA,HUJALI VIMETENGENEZWA VIPI WALA MADHARA YAKE WASUDAN UMEWAONA WAJINGA WALIPO AMBIWA WATAPEWA GM FOOD WAKAKATAA.POINT YANGU YA KULETA STORY YA KUKU NI KWASABABU JINSI WENZETU WALIVYO TAYARI KUBADILIKA FOR THE BETTER KAMA KUNA ABUSE AU MADHARA WANATAFUTA JINSI YA KUREKEBISHA NA CHANGE HAIJILETI YENYEWE ILA MTU AJITOKEZE,MICHUZI KA HIGHLIGHT ISSUE YA HUYU PUNDA INAWEZEKANA FIKA HAKUKUSUDIA KUM EXPOSE HUYU MWENYE PUNDA LAKINI KILA MTU AMEITAFSIRI PICHA KIVYAKE KUNA WALIOONA NI JAMBO LA KAWAIDA NA KUNA WALIOONA SIVYO,MIMI HUNIJUI ALL YOU KNOW NIPO ULAYA LAKINI HUJUI BACKGROUND YANGU ,LET ME TELL YOU THIS NI MTOTO WA KISUKUMA NIMEKULIA KWENYE UKULIMA I KNOW WHAT ANIMALS CAN DO AND WHAT THEY CANT DO,NIMEFUGA KUKU NIMEFUGA NG'OMBE NIMEISHI NA PAKA VILEVILE I HAVE A BROAD KNOWLEDGE OF ANIMALS,UKIM OVERWORK MNYAMA INA MAANA UTENDAJI KAZI WAKE UTAKUA MDOGO SIKATAI PUNDA KAZI YAKE KUBEBA MZIGO, NG'OMBE KUVUTA MASHINE YA KULIMIA,MZIGO ALIOBEBESHWA HUYU PUNDA NI ZAIDI YA UZITO WA HUYU PUNDA MWENYEWE SI ROCKET SCIENCE IT'S JUST COMMON SENSE ANGALIA UONE HAKI YA HUYU MNYAMA IKO WAPI USILETE KUCHONGA TU.
  BUT HAVE A GOOD LOOK AT THAT DONKEY AND THE LOAD IT'S CARRYING THEN TELL ME WHAT YOU THINK,OFCOURSE YOU THINK IT'S OK.WHETHER IT'S CHICKEN,CATS OR DONKEY WE HAVE NO RIGHT TO ABUSE THEM JUST BECAUSE THEY'RE ANIMALS.NA WEWE KAA HIVYO HIVYO UKIONA MAISHA ULIYO NAYO TZ NI SAWA TU HUTOENDA MBELE,KAMA KUNA WATOTO WANA MALNUTRITION WEWE KAMA MTANZANIA UMECHUKUA HATUA GANI KU ERADICATE MALNUTRITION KWENYE NCHI YAKO,NOTHING BECAUSE YOU ARE AFRAID OF CHANGE,ANIMAL ABUSERS LAZIMA WAFAHAMISHWE WAJUE WAPI WANAENDA WRONG,SISEMI WAFUNGWE LAKINI ZIWEPO SHERIA ZA KULINDA WANYAMA KAMA HAWA WATENDA KAZI.
  NYIE NDO WALE MMESIKIA KARIAKOO IMEFUNGWA MMEKUJA JUU KAMA MOTO WA KIFUU.

 21. Anonymous Anasema:

  Sasa we Anony wa Saturday Jan 19 unawazimu ama?

  kosa la hao wengine ni nini? haki za binadamu zipi unaongelea wewe? hivi vitu vinaenda sambamba point ni kuwa "CHENYE UHAI/DAMU KINAIHITAJI HAKI" iwe binadamu ama mnyama ama ndege, na ndio maana hata Kuku kumchinja kuna hatua zake, na wapo wanaopinga hata kumchinja na wao hawali chochote chenye uhai(damu).

  Pili unaposema PHD za questionnaires unamaana gani hiyo scientific reseach unayoweza kufanya bila kuuliza watu labda ya kutengeneza dawa nayo ni lazma utamuuliza mgonjwa anajisikiaje au sio questionnaire hiyo? sio mnakurupuka tu kujibu ili mradi uwe mtoa maoni ya 3,000,000. Dola 500 zitakupunguzia uwezo wa kufikiri.

  Kwangu mi naona wote wawili hakuna aliyekosea mtete Punda na mtoa Questionnaire. labda kama unajingine....

  Wabillah Tawfiq

 22. Anonymous Anasema:

  Kwanza we annon January 20: 6:52 mbeba ma-box unaonekana hata shule zero!. Hujui hata classes za shule. Hilo si kosa lako na labda ndo maana uko huko Ulaya kubeba ma-box yako badla ya kuomba kazi hapo TZ. Kwa taarifa yako, kuna namna nyingi za kupata Masters au PhD degrees. Mojawapo ni kuuliza maswali au questionnaire na nyingine ni kufanya scientific researches laboratory au field. Kama ulivyoona mwenzako annon wa Jan 20 6:59 ambaye anaonekana ana shule ya questionnaire ambayo unaweza kuuliza watu kwenye ma-bar, mitaani au ukajifungia ndani wewe na familia yako mkajaza, badala ya ile ya kufanya research, ni kwamba wengi wa questionnaires huwa wapiga mdomo tu na hawana chochote cha maana. Jaribu kufikiria tu; kuuliza maswali watu usiowajua, inahitaji uwezo mkubwa wa kusemasema na kuongea!. Lakini laboratory au field work ni facts tu ndiyo zinaongea. Ndo maana nchi nilizokwambia hapo awali kwamba zimeendelea sana kwa scientifc research na sisi tubakia kusemasema hovyo kwa sababu ya watu kama hawa. Hatuwahitaji sasa hivi Tanzania.

  Pili, tukirudi kwenye maada ya wanyama, kama ni kweli kila mnyama ana haki, iweje tunafanya kampeni ya kumwangamiza mbu au kuua mende mitaani? Au pia kujidunga sindano ili kuondoa parasites wa malaria kwenye damu zetu? hawa si wanyama? Basi tuwaache waishi maana wanastahili haki za wanyama!

  Kwa hiyo suala la haki za wanyama linatakiwa litazamwe holistically, na siyo myopically kama nyie annon hapo juu. Wewe wa kwanza najua issue ni shule, lakini huyu wa pili tatizo ni shule ya questionnaire aliyofanya!.

 23. MMasanja Anasema:

  YAKHE WA 8:58PM SITOENDELEA KUBISHANA NA WEWE MIE SIJASOMA WEWE UMESOMA,IKIWA MABISHANO YANAELEKEA KWENYE PARASITES WA MBU NA MENDE WHAT CAN I SAY GOODLUCK TO YOU,IT DOESN'T MAKE ANY SENSE TO ME TO EVEN COMMENT ON THAT,TATIZO NI UFAHAMU MDOGO.ILA NIMECHEKA KWA COMMENT ZAKO ZA MWISHO.and for your record sibebi ma-box.i have a good life na nyumbani natengeneza.

 24. Anonymous Anasema:

  Wewe annon Jan 21: 12:06 tulikuwa tunajadili kuhusu wanyama na wewe umetetea sana wanyama kwamba wanastahili haki. Sasa hao kama hujui kuwa ni wanyama na wana haki ya kuishi, basi una haki ya kuacha kuongea. Wewe soma tu, si lazima uchangie. Ikifika maada za makaratasi, nadhani unaweza kuwa una ufahamu kunizidi. Ni lazima unapotoa wazo, uwe makini sana. Si kusema kwa sababu unaweza kusema. Unatakiwa usema kwa sababu ni muhimu kusema! Kwa kheri yakhe na maisha yako mazuri. Hata wabeba mabox wanasema wana maisha mazuri mjomba. Si unaona wanavyotetea kazi zao humu kwenye blog!?? Karibu tena kwa points

 25. Mr Paul Anasema:

  kwanza naomba niombe samahani kama comment nilizotoa zimewakwaza baadhi ya watoa maono wengine. Pili, nataka niungane nanyi katika dialoque hii. katika kuungana kwangu kwangu naomba nikueleze ndugu yangu Agent kwamba atambua kwa kusikia tu kwamba wanyama wana haki perhaps im one of the ignorant individuals katika area hii. but nikirudi katika comment niliyoitoa siku chache zilizopita nakumbuka nilitumia neno "HALA HALA" nikiwa na maana kwamba, kama hao wanaharakati wa haki za wanyama wapo na wanataka ku intervene situation iliyopo sasa basi hiyo intervention should be caried out taratibuna sio kwa jazba na kuleta matatizo mengine ambayo hayakutazamiwa. further, naomba niwaambie nyie ma animal's rights enthusist kwamba please do not let your naivety blind your eyes. kwasababu hawa watu ambao wana promote haki za wanyama wameanzia kaitka mataifa yaliyo endelea ikiwemo Australia. na kwa kiasi kikubwa haki hizo zinatekelezwa kwa wanyama wa majumbani, particularly dogs na paka,(at least that is what i have observed here in Australia). lakni ukienda katika zoo unakuta twiga,swala, simba,tembo aliyetoka Africa anafugwa katika banda ambalo halina mti hata mmoja wenye majani wala majani yaliyoota chini katika ardhi.na hakuna kelele yoyote inayopigwa zaidi ya wao wenyewe kupeleka watoto wao kufurrahia hali hiyo. Now mnadhani hawa jamaa wana qualify kuja kutuambia nini cha kufanya na punda wetu kule vijijini ambako hata njia maalumu ya kupita nagari hakuna? na mnategemea mkulima asafirishe vipi mazao yake, mnataka arudie round ngapi kupeleka tani tatu za mahindi gulioni? naomba nimnukuu mmoja kati wachangiaji ambaye ameandika "animal rights can pretty much start with their backyard before stepping on other territories" Mr Paul, Sydney.

 26. Anonymous Anasema:

  SIPISHANI SANA NA MMASANJA KWANI HUYU BWANA ANATAKA LIGI PAMOJA NA KUWA SHULE YANGU NI YA QUESTIONNAIRE ILA HOJA YA MSINGI UNAIKWEPA EITHER MAKUSUDI AMA BILA KUJIJUA KWANI WAPO WALIOSOMA NA WAKASHINDWA KUITUMIA ELIMU WALIOIPATA KWENYE REAL LIFE!!

 27. Anonymous Anasema:

  Hoja ya msingi ipi tena ndugu annon Jan 21 3:42? Mimi nilikuwa kwenye hoja za watu, kwamba kila mnyama anastahili kuishi. By the way wewe wa questionnaires, unafahamu kuwambu ni mnyama? Na wengine wote mnaotoa comments mnafahamu kuwa mbu ni mnyama? Pia nyie wenyewe nina hakika wengi wenu mmeshiriki kuua nyoka wanapokuja too close to uouir homes. Lakini hawa ni wanyama.

  Mimi ndo maana nashauri kuwa, unapoongelea kitu, lazima uwe unakijua vizuri na si kuosha vinywa. Huyu jamaa kasema ninataka ligi, na yule mwingine kasema haniwezi! Sababu najua wazi hawawajui wanyama kwa maana ya wanyama. Ndo maana kwenye message yangu ya mwanzo nilisema wazi, huwezi kutetea haki za wanyama wakati ya binadamu haipo. Ni kwa sababu wanyama ni wengine mno, mnawafahamu ni hao kuku, punda, na ambao wako kwenye zoo. In facts, ambao siyo kuku, punda, tembo, na hao wa kwenye zoo ni wengie mara 100 ya hao mnawafahamu.

  Wewe wa questionnaire unadhani mimi narukia mambo au nakwepa maada. Niko sawa sawa kabisa. Ila wewe unajadili maana ambayo uilewi. Ni tatizo kubwa.
  annon wa Sydney ameweka facts wazi kabisa. kwamba je wanyama pori wanaokaa kwneye fence ni sawa sawa? Sijui kama mnfahamu kuwa hizo ni moja ya kuwakosesha haki kabisa. Mbwa wanaofugwa huko Ulaya na watu wanatembea nao kama pets wananyimwa raha kabisa. Kwa sababu wanyama hawana hawana uhuru wa ngono, kutembea wenyewe na kuji-stretch.

  Tuwe makini tunapotia mada kwani kuna watoto wadogo wanjifunza pia humu. Wanaweza waelewe tofauti kama Rajabu na mwenzako ambao wamekuwa stranded kule Norway. NI kwa sababu ya wabeba ma-box kama mmojawapo hapo huu, ambao wamewadanyanga hapa kwenye blogu.

 28. Anonymous Anasema:

  MMasaja mianon wa 12:57pm niko mza mtz sie JAMIE OLIVER wa UK.Mi ambae napenda sana wanyama miti ya matunda na maua pia nagundua haraka mambo yanayohitaji huruma hata kwa wanyama hasa wenye mimba, nilijifunza hayo nilipoanza kufuga kuku wa kienyeji MMOJA tu ambae nililetewa zawadi na shem wangu alipokua kwenye safari za kazi HUKO TBR akirudisha gari akaleta kama mboga alipomfunga kamba vibaya akaumia mguu, alipomleta nikawaambia wasimchinje wamuache nikampeleka shamba ambako alikaa huko akapoma kumbe alikua jogoo baadae nikamuona mpweke nikamtafutia makoo ma2 yakae huko nikawapatia chakula kizuri kama mchezo walitaga watoto, nikawachukua watoto nikawalea pembeni na kuwapa chanjo wakataga tena kwa kipindi kifupi nilipata kuku wengi walifika 50 na walikua wazuri, kwa ajili ya matunzo na chakula, kiasi majirani wakawa wanaleta makoo yao wapate ile mbegu, wakishatotoa wanawachukua wenyewe,bado baadae wanauliza mbona wako wanakua haraka tena wazuri?. huwa naona raha siku nikienda shamba nikishuka kwenyegari kama wametolewa nje jioni wananifata nyuma nyuma hadi ninapoenda kukaa kwani wanajua lazima nitawapa kitu kizuri kipya mf karanga dagaa mbegu za papai au papai mtama mzima nk. kuku wa kienyeji watamu sana hasa ukiwapatia chakula kizuri na majani wanakua na mafuta sio vuingwendu tunouziwa sokoni mpaka umbahatishe anotaga ndo utapata ladha ya kuvutia. huwa nawatumia kwa mboga ya nyumbani tu na kuwapatia marafiki zangu kama zawadi bado sijaanza kuwauza ingawa ninawazo hilo nikishakamilisha mipango yangu. asante kwa kuniunga mkono juu ya hilo.

 29. MMasanja Anasema:

  the words never argue with a fool come clear to me now,just by your comments.ni kweli unapenda ligi and there is nothing wrong with wabeba mabox.siajabu una tuma comments kwenye internet cafe,mbeba mabox yupo kwenye pc yake ya jasho lake.ukitaka kuleta comparison leta comparison za maana.i understand what mr paul is saying,placing those animals in the zoo it doesn't mean it's right,i'm with you on that,lakini wewe habari za mbwa kunyimwa ngono ndio sababu nilikwambia wewe msomi mimi mjinga ni bora nibaki na ujinga wangu kuliko elimu yako.ulipata shahada ya kuandika utumbo.hongera sana.ushauri wangu ni kwamba chukua ushauri wako uliotoa kuwa makini na unacho kiandika kuna watoto pia wanasoma hii blog.maana ni pumba tupu.

 30. Anonymous Anasema:

  Mmasanja pole sana sana. Issues zinajadiliwa kwa wanaojua. Pole sana, sina namna ya kukusaidia. Ndiyo maana nikasema ikija issue ya makaratsi, mimi siiwezi. Sitasema hata kidogo.

  Wewe kwa kuwa na PC ya mtumba chumbani kwako kwenye nyumba ya kupanga watu kumi inakufanya unatambe sana huko na mabox yako?! Mimi nawashangaa sana wabeba mabox kama Mmasanja. wote mko hivyo hivyo!

  Kwa hakika mtu mwenye akili timamu hawezi kukimbia nchi akadai kuwa eti imemshinda na anakwenda nchi nyingine! Unadhani wenzako huko nchi yao ilishushwa kutoka mbinguni?! Waliifanyia kazi katika mazingira magumu kuliko wewe uliyoyakimbia huku na sasa hivi unadai eti una PC ndani unajusikia bora kuliko Mtanzania halisi hapa Bongo anayeenjoy kukaa kwake na nchi yake!

  Issue ya wanyama ulikuwa uijui kabisa na ndiyo maana unashangaa ninapoongelea ngono ya mbwa! Wewe unadhani ni mzaha huo?! Ni haki ya mnyama kufanya sex kama wewe unavyofanya. Huwa uonagii hao mbwa huko Ulaya wakikutana issue ya kwanza ni kunusana nyuma??!. Unadhania ni mchezo wa kuigiza huo? Wako starved na wanahitaji haki! Sasa wewe unatoa mifano yako ya kuku kuwa na miguu minene, mimi niliishangaa sana! In short, huna idea yoyote kuhusu wanyama, na hivyo haikuwa sahihi kujadili haki za wanyama kwa mtu kama wewe! Kwa augument zako wewe, sana sana shue yako ni form four failure.

  Bora umeenda huko, labda na wewe ungekuwa kimeo huku kutuletea majanga yasiyo na maana.

  We are Tanzanians, proud of it and we Enjoy being Tanzanians and living in Tanzania! Wewe kaa na PC zako na internet ndani, wakati bibi na babu zako huku wanakushangaa!

  By the way, umesoma kanga ya yule mzungu kwenye post aliyoweka Michuzi hapo juu kuhusu Limbukeni......?! Alikuwa anawaletea nyinyi huko milio na internet ndani na mmekimbilia hilo huko Ulaya na kutuacha sisi kwenye cafee!

 31. Pope Anasema:

  WALLAH MIJADALA MINGINE INGEKUWA USO KWA USO WATU WANGETOANA NGEO
  KAAZI KWELI KWELI

 32. MMasanja Anasema:

  pope nakubaliana na wewe angekua karibu yangu huyo asiekua na jina ningemkata mapanga kwa ubishi usio kua na maaana.inavyo onyesha issue si wanyama ila huyu mtu asiekua na jina ndio ana sex starvation.anataka kuimalizia kwangu mie si gay.

 33. Anonymous Anasema:

  Hili ndio linaloitwa libeneke,naliendelee.

 34. Anonymous Anasema:

  Kijana acha wivu na choyo wewe kula vumbi lako na wabeba ma-box waache wabebe ma-box yao,kutokuishi Tanzania haimaanishi hujivuni kuwa Mtanzania watu wanatafuta maisha.

 35. Anonymous Anasema:

  MMasanja achana na huyu mpumbavu hapo juu ashakua hana mpya.

 36. MMasanja Anasema:

  anon wa 5:36pm asante kwa kufahamu nini makusudio yangu.Mtu yoyote aliepitia kwenye ufugaji wa wanyama aina yoyote atafahamu lengo langu na kwanini nimesema niliyo sema sio wenye kubwabwaja bila point eti amesoma.Huyo kisebengo anaeleta ubishi ana dalili zote za jobless with little education,ukianzia na kiingereza chake kibovu sijui nani alie maliza form iv failure,halafu ukiangalia jinsi anavyo andika anaenda nje ya point zote ni dalili za ku feli mtihani.Inaonyesha ulipewa essay ya THINGS FALL APART ukaandika za MINE BOY yote kutokufahamu.
  Nakupa chambo endeleza ubishi mwanangu.

 37. Anonymous Anasema:

  We Masanja unafunga wanyama kwenye PC uko uliko?! Acha miyeyesho yako na ushamba wako!? Wenzako wenye akili huwa wananyamaza wakikosa points! Hata maana ya form four failure hujui! Una matatizo makubwa wewe na sijui uliingiaje airport za watu huko!?

  Hawa wengine wabeba mabox nao wanakutetea!!??? Mnamtetea Masanja kwa upuuzi wake?! Mshamba sana huyo, Yeye nadhani kufuga wanyama ni kuwajua. Sisi tunampatia facts. Kama nanyi mnamtetea, basi huko mliko kazi kubwa sana!

  Naamini hata kama amekasirika au mmekasirika, ujumbe wangu umefika. Siyo kwake tu, ila kwa wasiosoma walio nje ya nchi na wa-beba mabox wanaodhania kuwa na PC ndani na ku-access internet kwenye chumba mnachokaa watu lukuki ni raha sana kuliko kuwa bongo!

  La msingi, Masanja, wanyama siyo ngo'ombe, Mbuzi na kondoo. Ila hao ni baadhi ya wanyama!

  Pili achana na ulimbukeni. Kumbuka bibi na babu zako, na dada zako , wengine huko Shinyanga. Usije ukajisahau kwenye ka-screen ka kuokota hapo majuu ukadhania life ndo imefika na mwisho. Wenzako walisotea hivyo. Nakumkumbuasha tena kuwa havikushuka kutoka mbinguni!

  Remain myopic, I pray for you!