Hello Mr. Michuzi,
Hongera kwa kazi yako nzuri unayoifanya. Naomba u-posti, swali langu kwenye blog yako tukufu; kama utaliona lina maana.
Swali"Ni kawaida kwa Watanzania hasa wa nyumbani kuona kwamba binti wa ki-Tanzania akiolewa na mzungu ameula. Inakuwaje USA, mabinti Wamarekani weusi hawapendelei ku-date au kuolewa na wazungu; hivyo kuwaachia waafrica kama 'possible dates' inayohusisha mzungu wa kiume na mdada mweusi?? Hapa Marekani ni rahisi kuona samaki anatembea mchangani kuliko Mmarekani mweusi wa kike ana-date mzungu wa kiume.
Nini kinaleta tofauti wakati wote ni weusi (I mean Waafrica na Wamarekani weusi)? "
Mdau Marekani
Naomba usitoe e-mail yangu.
Once again Hongera kwa kazi yako safi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 53 mpaka sasa

  1. watanzania wana shida zao kule nyumbani, hali ngumu, so binti yao akichukuliwa na mzungu wanaona ameula kinamna...mana anaingia kwenye chama cha Makaratasi,,,wamarekani weusi, maisha magumu, lakini kwa wengi huwezi yalinganisha na ya wale walioko bongo wenye kipato cha chini au hata masikini kabisa,,kwa hiyo wamarekani weusi hawawamind wazungu, hapohapo usisahau wamarekani weusi wako sensitive sana na ubaguzi,,,watanzania hatujabaguliwa sana kwetu, hivyo mtu yuko tayari, SABABU YA SHIDA ZAKE, bora akanyanyaswe na kubaguliwa ndani ya nyumba na mzungu, aibuke na makaratasi,,,AT THE END OF THE DAY, MI NAONA NI NJAA NDIO INAPELEKEA MTU KUKUBALI KUWA/KUISHI NA MZUNGU...mkubali mkatae hivi ni vitu viwili tofauti, so ndugu zangu angalieni, kuna swala linaitwa WYT (Wasting Your Time),,kwa kitu ambacho ni obvious, at the end of the day, mweusi ndio looser......kama hamuamini, basi angalieni kule bongo, kuna watanzania wenye uwezo wao au wenye maadili yao, huwa HAWATAKI KUSIKIA, mtoto wao kafunga pingu za maisha na mzungu,,na ukifanya hivyo wanaweza wakakutenga, cause mwisho wake wanaujua , AT THE MIDDLE AND END OF THIS BUSINESS, THE BLACK A*S WILL BE THE LOOSER.

    ReplyDelete
  2. watanzania wanataka makaratasi wamarekani weusi hawahitaji,,kwani what is the definition of mzungu?? Mzungu means source of Makaratasi and a reason to convince the authorities to stamp the most crazy thing in your passport..THATS IT..nafunga mjadala.

    ReplyDelete
  3. Swali zuri.

    Ni kutokana na ukweli kwamba Watanzania wengi kuanzia viongozi, wasomi na watu wa kada mbali mbali bado wako brainwashed kuwa Wazungu ni superior.

    Ukitaka kuelewa zaidi BOFYA HAPA

    ReplyDelete
  4. wamarekani weusi hawakubali kunyanyaswa na kubaguliwa, watanzania hawaelewi hii kitu kwa undani, sisi tunanyanyaswa, ila kwa ufinyu wa ubongo, mtu anakuwa anaona kama ni mambo ya kawaida tu, sio ubaguzi huo,,,ni sababu kwetu hatuyajui haya vizuri, angalia wa south africa walioko huku nje, hemu hesabu wangapi walioamua kudeal na hawa watu weupe,,,ndo utajua,sababu wa south wanaelewa sana hili swala la ubaguzi, na kwa kifupi, sitaki ubishi, wazungu woote, wana kielement cha ubaguzi(ukoloni mamboleo) ndani mwao awe mnene, mwembamba, mrefu, mfupi, ameshatembea nje sana au hajatembea, UKIMCHUKUA UKAMLOWEKA KWENYE SABUNI YA OMO USIKU KUCHA, MKIAMKA ASUBUHI AKIWA BADO NI MZUNGU, BASI UJUE HUYO NI MBAGUZI TU HATA UFANYEJE....ila kama kwa makaratasi mtu unaweza jitosa ukavumilia, ila beyond that kwa kweli i got no comment,,get smart black people,,this is for real.

    ReplyDelete
  5. Hapa nafikiri wadada wengi wa nyumbani wametawaliwa na ile kasumba kwamba ukiolewana mzungu basi mambo yanakuwa swadata. Hao wenzetu wa Marekani wamekaa na wazungu na wanajua vilivyo, kitu ambacho hawa dada zetu hawawajui wazungu kiundani. Na ndiyo maana wanaona fahari kuolewa na mzungu

    ReplyDelete
  6. Huyu jamaa alichosema kina ukweli kbs.Tena si madada wetu walio bongo tu hata walio huku ughaibuni wana hiyo kasumba.

    Hapa nilipo nilibahatika kutana na madada fulani kwenye mitandao yetu hii,good enough we're living in the same city.Lakini wote wanajidai bab-kubwa na hawataki hata sikia mbongo mwenzao au ngozi nyeusi,ilhali hata sikuwatongoza. Mmoja nakumbuka she e-mailed saying i'll end up kumtongoza,na hata hivyo she is not interested ku-date na mweusi achilia mbali "mmatumbi" kama Michuzi uitavyo.

    Lakini pia,madada wetu wabongo hususani ma-miss wote wanakimbilia kuolewa na foreigners,kama si mzungu basi ilimradi ni foreigner.Ni kweli ni shida bongo au ni kasumba?

    ReplyDelete
  7. KUTOKANA NA HISTORIA YA UTUMWA WAKINA MAMA NA KINA BABA WEUSI WAIKUWA NAUMOJA WA AINA YAKE. UMOJA HUO UIKUWA WA KIROHO WA HALI YA JUU. UIWAPA BUSARA AMBAZO ZINA URITHI WA HEKIMA ULIOKITHIRI. UTASIKIA KILA WAKATI KATIKA SALAMU ZAO WANASE KUWA MZURI YAAN BE GOOD WANAMAANISHA WANACHOKISEMA NA WANAKISEMA WANACHO MAANISHA.UKIJARIBU KUPIMA KWA ASIIMIA SAUTI,MANENO NA MAUMBIE YAO WAKATI WA KUONGEA UTAGUNDUA. UPENDO KWWAO NI KUWA HURU NAKAMA MAREKANI NI BIG DEAL HAWAITAJI KWENDA HUKO MAANA NDIO WAMEZALIWA. AKINI DADA AU KAKA ZETU AKIOLEWA AU AKIOA MZUNGU ANAONA ATAPATA NAFASI YA KWENDA ULAYA NA ATAFANIKIWA KIMAISHA KWA HIYO MSHIKA DAU UNAWEZA KUMPOTEZA MWENZA KWA MPAPATIKO HUO WA WAZUNGU

    ReplyDelete
  8. Tatizo ni kwamba madada wa kiswahili hasusani wa hapa bongo ni kama kuku wa kienyeji. Ukimchukua kuku wa kienyeji ukamuweka bandani ukawa unamnywesha maji tu atakushukuru sana. Hata ukumyima chakula( yaani manyanyaso)yeye ataona ni sawa tu ilimradi umpe access ya kuchakura chini na kuokota mchanga ataona ni sawa tu.

    Huo ndio ukweli kuhusu wale madada wa kiswahili wanaowashobokea wazungu. Hata kama wakinyanyaswa au kubaguliwa alimradi wameolewa na wazungu kwao ni poa tu.

    Lakini kwa kuwa wao wanaona ni poa waache waendelee tu kuolewa na hao mafirauni moto wake watausikilizia.

    ReplyDelete
  9. wewe mwenyewe kwanza umeolewa? Na nani, mswahili au mzungu!? Ulifikaje huko Marekani?

    Tunaweza tukawa na sehemu nzuri ya kuanznia kujibu swali lako vema.

    ReplyDelete
  10. Swala si makaratasi kwa akina dada zetu.Swala muhimu ni Identity,who are you? Akina dada zetu wa bongo hawajijui wao ni akina nani! ni wazungu au weusi hilo hawalijui bado! wana-sruggle kutafuta Identity yao.Wengi wamekuwa wanahangaika kutafuta nafasi yao miongoni mwa wazungu kwakujaribu kujifananisha na wazungu kwa njia mbalimbali chini ya kivuli cha beuty,Asilimia kubwa ya akina dada wa bongo wanajaribu kujikoroga rangi zao na kuweka nywele zao katika mtazamo unaofanana na wazungu kwa kudhani kipimo cha utu ni kuonekana kama mzungu huku wakisahau asili yao.Inapotokea anapata bwana wa kizungu basi hapo hupigia mahesabu ya mtoto au watoto watakaozaliwa "mhh!mbona nimeula mwenzenu nitazaa watoto warembo weupe wazungu".Wamarekani weusi waliishapitia hayo yote kwanza waliteswa utumwani wakapuuzwa,wakapoteza Identity yao,Ingawa nao walijitahidi kufanana nao kama wanavyofanya akina dada wa bongo lakini haikusaidia bado hawakukubalika,waliendelea kupigania Identity yao hatimae wameipata na kujikubali kuwa wao ni waafrika tu hata wafanyeje.Kwahiyo kilichobakia ni kuilinda Identity yao kitu ambacho ndicho wanachofanya hadi sasa na ndiyo maana hawataki kudet na wazungu kwa kuhofia kurudia makosa ya mwanzo.Nami nawapongeza kwa hilo.

    ReplyDelete
  11. swali gumu.

    ReplyDelete
  12. lets face up the facts,racism haiko konfaided kwa mtu mweupe,racism ni hulka ya binadamu WOTE duniani.hakuna makundi ya binadamu yasiyobaguana duniani,iwe ni kwa kabila,dini,rangi,ideology......just mention it,binadamu kubaguana ndo zetu.why so....hiyo tumuulize subhana wataaal.tatizo wakalamba tumekuwa wepesi kuwanyooshea kidole ngozi nyeupe kumbe na kwetu binti mhaya akileta mchumba mchaga tunamfukuza,kijana muislam akileta mchumba mkristu tunamtoa baruti....yote hiyo ni discrimination kwa taarifa yenu wadau.tuache longo longo tukubali ukweli wa maumbile.

    ReplyDelete
  13. Mi nimeolewa na mzungu, sio sababu ya dhiki, makaratasi wala nini. Ila wanamme wakibongo sometimes mnabore!
    Suala la kubaguliwa hata bongo lipo japo kwa bongo sio la rangi ila duh, upande wa wakwe wanakuonaje sijui, kama vile umeolewa kimakosa, yaani kero kero kero pu!Bora huku tunabaguliwa kwa rangi inajulikana kweli mimi mweusi, sio tena weusi wenzangu wanibague, nou way I am out of that!

    ReplyDelete
  14. naam maanon wa hapo juu mmenena yote niliyotaka kuyasema, natilia tu mkazo point ya anon wa 12.02 kitu ni kuwa, mtu mweusi anayeoa/kuolewa na mzungu ujue huyo, HAMJUI MZUNGU VIZURI,, hamuwezi niambia otherwise , i am talking from my own experience,nimekaa na mzungu miaka 9 ndo nikaja kujua.
    Nilijua nimepata kumbe nilipatikana

    ReplyDelete
  15. jamani kuona ufahari kuolewa na mzungu hiyo ilikuwa zamani, sikuhizi mbona watu kibao wameowa na kuolewa uzunguni, mbona ni jambo la kawaida, na asilimia kubwa walioa/olewa na wazungu, maisha yao ni ya kawaida kabisa..acheni uongo, sidhani kama kuna mtu leo hii anaona ufahari kufunga ndoa na mzungu, kama ni hivyo, huyo ni mshamba sana.....mi nimeoa mzungu,sioni ufahari, kwanza kwa ufupi KARAHA TUPU, msitake nitoe siri zangu nyingi hapa, aaaakkhhhh kwaherini...i wish i knew that in this kind of business, future is equal to ZERO.

    ReplyDelete
  16. JICOMMIT KWA MZUNGU, UTAKUFA MASIKINI..its very simple, kampuni ya mzungu na mweusi zinaungana kufanya biashara,,mweusi anapata faida 5% na 95% anapata mzungu...mzungu ndio always anakuwa winner hapa especially kama mnaishi kwao, mkiishi bongo mweusi anaweza pata 30% mzungu akachukua 70%.Its always like this, and NOT VICECERSA....

    ReplyDelete
  17. JICOMMIT KWA MZUNGU, UTAKUFA MASIKINI..its very simple, kampuni ya mzungu na mweusi zinaungana kufanya biashara,,mweusi anapata faida 5% na 95% anapata mzungu...mzungu ndio always anakuwa winner hapa especially kama mnaishi kwao, mkiishi bongo mweusi anaweza pata 30% mzungu akachukua 70%.Its always like this, and NOT VICECERSA....

    ReplyDelete
  18. nakaa marekani mwaka wa 20 almost, kwa ufupi nasema, wamarekani weusi hawawapendi wazungu kutokana na lile swala la RACISM, weusi tumebaguliwa saana hapa marekani na duniani kwa ujumla, so a black american, cannot imagine him/herself in the same house with mzungu....by the way, hata watoto watakaotoka hapo wa mchanganyiko, bado wanawabagua, kisa wana damu ya mtu mweusi

    ReplyDelete
  19. black americans hawataki ubaguzi/unywanywasaji, na wao si wapumbavu...watanzania sababu ya ile homa ya makaratasi, basi mtu anaweza akajitahidi kuyavumilia mengi mpaka afanikiwe....
    zaidi ya hapo sina explanation ingine, na ninaweza kuthubutu kusema,hakuna usalama wowote katika jumuiko la watu wawili wenye asili na zaidi rangi tofauti..

    ReplyDelete
  20. wanaolewa na wazungu ndio na sio kama hawaoni ubaguzi au hawajui kuwa watabaguliwa la hasha ni ile tu kasumba iliyojengeka miongoni mwa Waafrika kuwa Mzungu ni kila kitu na mwisho wa matatizo. Kitu kingine ni kuwatambia wasichana/wadada wenzie kuwa ameula lakini zaidi ya majigambo ni matatizo matupu. Jamani nyie wasichana wenzenu waliolewa na wazungu wana shida ya ajabu, tena hivyo walivyofikiri watavipata huwa hawavipati labda aliyeamua kuolewa na kibabu manake kwanza kishajichokea anasubiri kufa na hapo unaweka matumaini eti utaambulia urithi unakuta mwenzio mali yake yote kamrithisha mbwa wake mpendwa, yaani huyo mbwa ana thamani kuliko hata we mkewe.

    ReplyDelete
  21. njia ya mkato kwa papers tu! case closed.

    ReplyDelete
  22. Mi nazani labda madada zetu wamechoka kushindwana na wabongo wenzao walio kiwanja, kwa mfano wengi wabongo wakiingia hapa marekani tunajiona/ kujidai wanugu na ninii! tena hii ni kwa pande zote mbili madada na makaka. Kwa hiyo basi kama mtu hawezi kupata kijana mwafrika halisi, anaona bora apate mzungu mwenye heshima zake. Suala sio ulimbukeni wala nini...mara elfu bora uolewe/oa na mzungu kuliko hawa wanugu...au wabongo wanaojidai wanugu. Wanugu (wengi wao) hawana manners, BAD ATTITUDE, hawaheshimu wanawake, hawako family oriented, tabia mbovu kwa ujumla, wavivu. Utabahatika sana kupata mnugu kama Obama...(see, he's actually African, too). Wazungu kama sio racist hawana noma.

    ReplyDelete
  23. Nimejaribu kusoma comment za walio wengi nikagundua ya kwamba jinsi moja ya kike ndo imevamiwa na kulalamikiwa zaidi ya jinsia nyingine ya kiume. Embu tujaribu kujiuliza maswali machache tu, je ni wasichana wa aina gani huolewa na wazungu hususani watalii ama wataalam wajao nchini mwetu hasa Tanzania? Na je hukutana wapi na hawa wapenzi wao? Na huwakuta katika hali ya namna gani? Tuangalie kundi la pili la wanawake wasomi, je ni wangapi wameolewa na wazungu kwa hesabu zetu za haraka haraka? Kwa watu wanaoishi ughaibuni embu tujiulize ni wanaume wa aina gani wanaooa wazungu? Na wakiwa huku ughaibuni wanafanya kazi gani na katika hali gani? Tukichukua dakika kama tano hivi na kutafakari haya, tutajua kwa undani zaidi ni nini kiini cha haya yote. Hapa sitatoa majibu kufuatana na uzoefu na uchunguzi wangu juu ya hili ila ninawaachia ninyi wenyewe. Na wale ambao tayari mmeowa ama kuolewa na wazungu mwaweza kuwa na majibu mazuri zaidi ya kuwawezesha wasomaji wetu kufahamu undani wake. Nawashukuru wote walitangualia kwa mchango wao mwanana. Imani.

    ReplyDelete
  24. mapenzi hayachagui kabila, siku hizi muzungu muafrika huoana, japanese muafrika vilevile,mbilia a bel kaimba. shida ipo wapi hadi muanzishe mjadala!! one mans meat, is always another mans poison, kwa hio sioni iwe ishu kuolewa na mzungu hadi iwe mada.
    nana

    ReplyDelete
  25. Jamani mbona hii mada imewaandama akina dada tuuu?Mbona kuna mijianaume nayo inaona ujiko kuwa na mwanamke wa kizungu?Au nayo inaolewa?Au ni makaratasi pia?Basi angalieni pande zote za shilingi au vipi?Angalieni na akina baba wanaopenda rangirangi(wazungu).
    Nawakilisha hoja.

    ReplyDelete
  26. TUKIAMUA KUTOA HOJA EBU TUZICHAMBUE.
    1.KAMA MTU YOYOTE KAOA AU KAOLEWA KWA AJILI YA MAKARATASI NA UPANDE WA HUYO MTU AJUI SIO KWELI KWAMBA WANANYANYASWA NA WAZUNGU KWANI MZUNGU HUWA HAWAJUI KAMA WEWE UKISHAPATA KARATASI UTAMKIMBIA.HUWA WANA MAPENZI YA DHATI NA YA UKWELI KWAKO NA HAWAKUBAGUI WALA NINI .SEMA WEWE AMBAYE UNAJUA UNACHOTAKA NDIO NAFSI YAKO INATESEKA KWA VILE HUNA MAPENZI YA KWELI.
    2.SWALA LA PILI KWA WALE WALIOA WAZUNGU NA KUOLEWA KWA MAPENZI YA KWELI HUWA HAWAPATI MATATIZO YOYTE NA KUNDI LAO WENGI HUWA WANAKUTANA MASHULENI NA KUIENDELEZA.HAMNA MTU ANAENDA KUOLEWA AU KUOA MZUNGU KUTEGEMEA MAISHA YAKE YATAKUWA MAZURI .KILA MTU ANA NAFASI YA KUWA NA MAISHA MAZURI MAREKANI INATOKANA NA JUHUDI ZAKO TU.
    3.NAKUJA KWENYE HOJA YA YA KINA DADA WAMAREKANI WEUSI.CHUKI KWA WAZUNGU HIKO KWENYE DAMU KWAHIO UBAGUZI WAO WANASEMA KUTOKANA NA SLAVERY NA IMEENDELEA KUWA HIVYO NA ITAENDELEA KUWA HIVYO.WAPO WAMAREKANI WEUSI WALIO FUNGA NDOA NA WAZUNGU JAPOKUWA NI WACHACHE NA WANAISHI KWA FURAHA NA PIA KUNDI HILI HUWA LINAKUTANA MASHULENI BAADA YA KUWA EDUCATED VYA KUTOSHA NA KUTOA TOFAUTI.WAMAREKANI WEUSI WANA WALAUMU KILA KITU WATU WEUPE KWENYE MAISHA YAO.NA PIA KUNDI LINGINE LA WEUSI WAMAREKANI HUOGOPA KUJIUSISHA KIMAPENZI WATU WEUPE KWA VILE INAOGPA JAMII YAO ITAWAANGALIAJE.
    4. WAZUNGU NA WAAFRIKA NI WATU AMBAO KIDOGO WANAELEWANA KULIKO MZUNGU NA MMAREKANI MWEUSI AU MMAREKANI MWEUSI NA MUAFRIKA.WAMAREKANI WEUSI WANATUCHUKIA NA PIA WANA TUDHARAU SISI WAAFRIKA KULIKO HAO WAZUNGU KAMA UJAGUNDUA MPAKA LEO.
    5.SWALA ZIMA LA KUNYANYASWA.DADA ZETU AU KAKA ZETU HUWA WANANYANYASIKA SANA WAKIWA KATIKA MAPENZI NA WAMAREKANI WEUSI SANA KULIKO WAZUNGU.NA TUELEWA MAKUNDI HAYA YAKO MACHACHE SANA NA PIA TAMADUNI ZETU TOFAUT.
    KWAHIO MDAU ULIOTOA HOJA HII KAMA NI MGENI MAREKANI BASI UTAKUJA KUJIONEA BAADAE JINSI WAMAREKANI WEUSI WANAVYOTUCHUKIA SISI WAAFRIKA.NA KAMA HUKO MDA MREFU UNATAKIWA HUJUE JINSI SYSTEM INAVYOKWENDA.

    ReplyDelete
  27. Ze Makaratasizzz nukta!

    ReplyDelete
  28. Sababu ambayo African Americans (sio black Americans, ndugu zangu) hawapendi wazungu ni kwamba wazungu wa kiume hawajui kuwalidhisha wanawake kimapenzi. Goli huja mapema na stamina hamna. Niliolewa na mzungu, na nili-date mwingine. Ndo maana wacheza kikapu wengi ni weusi (kumbuka msemo; white people can't jump?!). Wanawake wa kizungu wanakimbilia sana weusi ndio maana kila mtoto 0.5 (bongo mnaita half cast) anakuwa mama mzungu baba mweusi. Wazungu wanapenda utaalamu wa weusi wanakwambia "Once you go black you cant come back (to date a fellow white)"

    ReplyDelete
  29. Mimi nataka mzungu sababu nataka mtoto mzuri, yani ile vi biracial kids unavyo viona na beautiful hair and eyes, sio kingine!

    ReplyDelete
  30. WEWE ELIYEULIZA HILI SWALI ACHA KUWA BIAS. MBONA PIA WANAUME WAKIBONGO WAKIOA WANAWAKE WAKIZUNGU WANAJIONA WAMEWIN? mIMI HAPA NINAPOISHI JIMJUI MSICHANA ALIYEOLEWA NA MZUNGU LAKINI KUNA WANAUME WATATU WAMEOA AU KUZAA NA WAZUNGU.. iT GOES BOTH SIDE....WATU WANAJISIKIA SANA WOTE WAKIOA HAWA WAZUNGU

    ReplyDelete
  31. Jamani mapenzi hayana rangi kabila wala cheo.

    Mimi kwa upande wangu ni kuwa watu hao waliooa au kuolewa na wazungu hawajisikii kabisa ila watu walio nje ya mapenzi yao ndio wanafikiria hivyo. Na pia watatafuta kila sababu ya kukufanya hivyo.

    Ni kama sasa hivi jazba la watu wa bongo na watu wanaoishi nje ya nchi. Je mnaoishi nje ya nchi mnajisikia kuwa nyie ni superior kuliko wengine? Laaa...Mimi naona watu tunaoishi nje ya nchi wala hatujisikii ila walio TZ wanafikiria hivyo.

    Kwa hiyo sioni sababu ya kufikiria watu wanajisikia kwa vile wameolewa na mzungu. Ni nyie mnafikiri hivyo.

    ReplyDelete
  32. We annon Jan 27: 6:30 nadhani una dalili mbaya sana za ugonjwa uitwao UJINGA KUBUHU! Unasema unataka half caste? Watoto wote sawa sawa. Huyo wako anaweza azaliwe half caste na asiwe unavyotaka. Usirudishe tena pumba zako kwenye blog

    ReplyDelete
  33. mie mtanzania lakini hata kwa fimbo sijamdate au kuolewa mzungu. they are not fun, yaani mie naonaga kichefuchefu tu. hivi mnawaweza vipi hao watu ambao hawaogi?

    ReplyDelete
  34. Ni Kawaida Dunia nzima vitu kama hivi. Hapa nina rafiki yangu Mjerumani juzi juzi kaenda Indonesia ananiambia licha ya Dini kule, wanawake wakimwona walikuwa wanajitahidi kwa namna zote kumfikia! In fact anasema alikuwa kila siku ana date zaidi ya kumi, wakiwemo wafanyakazi wa ofisi kubwa kubwa. Huyu mzungu alifikia wakati akasema kama akitaka mwanamke anaweza pata popote isipokuwa Ulaya! Lakini mwanamke wa Africa hawezi kwa kuwa ana-risk magonjwa kwa hiyo wazungu wachovu ndo huwa wanakuja na kuoa Waafrica wa Africa!

    Ukitazama maneno yake ni dharau na racims kubwa sana, lakini facts remains: wazungu wachovu ndo wanaoa wanawake wa Kitanzania. rarely utakuta mzungu mwenye uzungu halisi ana mke wa Kitanzania. Fikiria maneno ya huyu Mjerumani hapo juu.

    Kwa hiyo ndugu zangu tusiponde sana. time will tell. Mimi mwenyewe wanawake wa Kizungu siwapendi. Sababu ni wachovu sana na hawawezi ma-issue kama dada zetu wa kibongo!. Pili ukilazimisha sana huchelewi kushitakiwa au kuvunja ndoa! Isitoshe, formulas kibao na zinabadilika kila siku. Ya nini kupangiwa mida ya kurudi matembezi bwana?!


    Dada zetu wametulia sana. Wanaelewa. Nasi tunawaelewa sana. Ndo maana ukiwa na mbongo mnaisha safi sana, mambo ya wakwe au mawifi ni sehemu ya utamaduni. Kama uhuwezi una genes za huko huko!

    ReplyDelete
  35. Nadhani watu wengi wamekuwa very bias hapa. Na kwa mtazamo wangu 95% ya wachangiaji wengi ni wanaume ambao wanatoa maoni yao yakiwa yamejaa FITINA na CHUKI, For no reasons at all.

    Kama alivyosema MZAWA hapo juu, issue kama hii ni vizuri kuifanyia uchunguzi wa kina. Je kwa wale wanaodai kuwa watu wanaolewa na wako tayari kunyanyasika kwa ajili ya makaratasi ni wangapi? Je ni wangapi wanafeel kubaguliwa katika familia waliyooa/kuolewa? Mimi nadhani hayo ni makubaliano ya watu wawili who they feel right about each other.

    Pili, anayeolewa na mzungu na kudhani kaula huyu lazima atakuwa kakutania na huyu bwana wake katika anga mbovu hivyo kuwa na high hopes.

    Tatu, kwa watu waliokutana kwenye mazingira ya kazi, shule nk. it is obvious kuwa hawa wameanza urafiki na mazingira yamepelekea wao kuoana just out of love and no reservations, kama ambavyo tunafanya hapa tz.

    Watu wamefikia kuongelea uwezo kitandani.. mimi nadhani huu ni utoto wa hali ya juu manake siwezi enda olewa/owa na msenge just because ninataka makaratasi au nataka nionekane nimeula.. hivyo mpaka mtu uamue kuolewa/kuowa (hapa awe mweusi kwa mweusi au la) lazima pia hiyo department muhimu na nyingine ziwe zimekuridhisha kama sio kukufurahisha.

    Kwa kifupi ubaguzi upo kona zote za dunia, hivyo kama wewe uliyetoa maoni kuwa umenyanyasika kwa kuoa au kuolewa na mzungu pole zako nyingi... wanawake wangapi wameolewa na wabongo they regret so much... mara hanijali mara anatembea nje mara hivi mara vile.. mara wakwe wako hivi mara mawifi mara mashangazi...so nothing is better. while here we dont have shangazi wala wifi..it is life of two people and nothing else!! hahhaaa patamu hapo

    Na ndio maana wazazi wenye busara wanawaruhusu watoto wao waoane na mtu yoyote ilimradi kuwe na mapenzi ya dhati tuu. na sio kubabaishana. Watu tumeolewa/kuowa wazungu na tupo na very down to earth life.. simuoni mke wangu mzungu as far as am concern she is just mwanamke mrembo, mother of my beautiful kids and i love her very much and promise to live with her for as long as we can!!

    So guyz whatever you are thinking about crossculture...it cant be any better!!!
    Hata michuzi anaoa Uganda sio foreign country hiyo hahhahhaaa


    ciaoooo

    ReplyDelete
  36. hello wewe uliotoa hiyo hoja na watakaosoma
    Kusema kweli kwanza sielewi ni nini ambacho kimekulead wewe kutoa hiyo hoja ila naiheshimu na nitatoa hoja yangu.....

    Siamini kuwa watu wote wanaooa wazungu awe mwanamke au mwanamme wanaoa kwa ajili ya kupata makaratasi kwani mapenzi ni kwa mtu yeyote haimaanishi kuwa basi wewe ukiolewa na mzungu ni makaratasi tu unatafuta.... na hii biashara ya watu kunyanyaswa ukishaolewa na wazungu umetoa wapi mimi ni mtanzania niliyezaliwa australia nimesoma na sasa nafanya kazi katika benki ya marejkani australia nimeolewa na mzungu mwaustralia mbona kunyanyaswa sijanyanyaswa na kuhusu makaratasi ninayo tayari kwani ni mraia hapa so sielewi unasema nini...

    sijui kwa huko marekani kwani swali liligeziwa huko lakini naamini kuna & fulani ya wadada wamarekani weusi ambao hawapendelei na kunanyingine inapendelea kwani huwezi ukaniambia kuwa hakuna wamarekani weusi waliooa wazungu hata masupa staa wanawaoa wazungu........

    ReplyDelete
  37. Mimi ngoja niwape mfano hai ambao umenitokea mwenyewe, ubaguzi sio kwa wazungu tu hata tz ubaguzi upo.
    Wakati nilipokuwa bongo miaka hiyo nilichumbiwa na mwanaume wa kihaya lakini ndugu zake wakanikataa sababu sio muhaya.
    Mwanaume wa pili alikuwa mchaga pia nilikataliwa na ndugu zake, ilinitia uchungu sana, nikaamua kutafuta njia ya kuja ulaya nikafanikiwa.
    Nilipofika huku Mungu akanisaidia kupata makaratasi yangu, nikabahatika kupata mbongo mwenzangu tukaamua kufunga ndoa, baada ya miaka miwili kupita mambo ndani ya nyumba yakabadilika vurugu kila siku mwanaume mlevi, mvivu mimi ndio nikawa mfanyaji kazi yeye ni cha pombe na kila siku ni kipigo kwangu.

    Nilishindwa kuvumilia mateso tukaachana, sasa nimeolewa ma mzungu namshukuru Mungu naishi kwa furaha sana, maisha yanasonga mbele, na amenikubali mimi na watoto wangu

    Kwa hiyo suala la wasichana wa bongo kuolewa na wageni ni kutokana na matatizo tuliyoyapata tunakotoka, ndio maana tunaamua kubadilika na kuachana na wabogo wenzetu.
    Kubaguliwa itategemea na wewe mwenyewe unaishi vipi na mwenzako ndani ya ndoa kama umeolewa kwa ajili ya kumtumia mzungu wa watu upate makaratasi hata mungu anakuona ndio maana anakupa adhabu hiyo ya kunyanyasika, lakini sio wote ambao wameolewa na wazungu wanabaguliwa.
    Naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  38. anon wa 1:55 unayesema umeolewa na mzungu si kwa dhiki, makaratasi wala nini, na kuwa eti bora huko uliko ubaguzi ni wa rangi tu...hahahaaa, usinichekeshe...ubaguzi ninaoujua mimi, ni ule mume ama mke wako mwenyewe tabia zake towards you zinainvolve kiubaguzi flani,,,yaani jamani asidanganywe mtu hapa, mimi niliolewa na mzungu nimekaa miaka zaidi ya kumi, nikaja kugundua kuwa ni upotezaji wa muda tu..labda kama uwe na pesa ya kutosha, (ya kwako mwenyewe si ya mwenzio) na uwe na akili sana kuyafanya malengo yako kwenye maisha, hata ukiwa uko naye huyo( kwa uzoefu nilionao, 99.9% ya mambo ni hakuna cha maana kitakachofanyika), akina dada wenzangu jamani kaeni macho, mtaishia kupigana mabusu weee, cha maana hakuna, naungana na huyo aliyesema mwisho wa siku mweusi ndo anakuwa looser....
    wazungu wajanja sana,ukiona anakuchekea chekea nakupenda nakupenda nyingiii, ujue ameshakuweka chini sana na anafurahia jinsi yeye anavyowin na unavyomfuatisha anayoyataka, ok, then life goes on, lakini ukianza tu kuwa mjanja, ukaanza kuonyesha kuwa na mie maisha ninayaelewa,na nataka tuwe level moja katika kila hali, basi huyo lazima mgombane kila leo, na ukishaona hivyo mwenzangu,,ujue.....akili kwenye kichwa chako....wanadidimiza sana hawa, haswa wanaume wakizungu, wanadidimiza sana sisi akina dada,mpaka unapoteza identity yako, unakuwa kivuli tu katika life,, asinidanganye mtu yoyote kitu chochote hapa tena kuhusu wamarekani wazungu,msiniambie kitu chochote, kaeni kimya kwanza niacheni niende nikalie mie, niulilie muda wangu nilioupoteza na hawa mbweha,,,

    ReplyDelete
  39. pole zetu wote tuliooa ama kuolewa na hawa wadudu waitwao wazungu hawa, anyway,,its never too late kuangalia mbele...namshangaa huyo aliyesifia yeye hakuolewa kwa shida, sawa mama, lakini nani kakuuliza hayo? maneno uliyoandika tu yanaonesha kuwa una ugonjwa wa ulaya ulaya, ambao ukali wake huzidi kama unaishi na hawa wazungu hawa...

    ReplyDelete
  40. we anon wa 7:57 unasema waliobongo ndo wanadhania kuwa mlio nje mnajisikia na walioolewa/kuoa weupez hawajisikii.....sikatai, sio wote wanaojisikiaga, wengine wametulia saana, na wala si wa kupenda kujishowshow,,,ila mi naona wewe umeoa ama umeolewa na mzungu,,,(mawazo yangu ya chapchap), na wewe uliyoyaandika yanaonekana kabisa unaumwa haka kaugonjwa haka ka Ughaibuni,,pole mama, tafuta tiba haraka...mi nakubali wengine wako na wazungush ila wamejituliza sana, ila kuna wenzangu na mie mmh akiwa na hiki anataka aje mbele aonyeshe, akipata kile anataka mjue, tena sikuhizi kila kitu mnavianika kwenye Hi5, ooh my crib, my car, my sijui nini... vichekesho kweli, HALI YENYEWE INAJIELEZA, mtu mwenyewe anayejigamba CHOKA MBAYA,,ooh darling kanijengea, kama kakujengea mbona sura imejaa wasiwasi hivyo...kamdanganye mtoto wa darasa la tatu..nayeye awe kijijini wa Dar es salaam sikuhizi nawao hawadanganyiki.

    ReplyDelete
  41. Napenda utaratibu wa maisha ya wahindi kwa jinsi wanavyolinda utamadudi wao kwenye swala la kuoa

    ReplyDelete
  42. Acha ushankupe hapa mwenye kuleta mada.Mpaka ulinganishe na wamarekani weusi!!! Haya kofi Annan nae ana mzungu anatafuta ujikona makaratasi.Mbona husemi mkristo na muislam au mgabacholi na mmbongo mpaka uruke mabara!!!!
    Mafisadi nao huwa wanatafuta nini wanapowaibia!!! Acheni kusakama watu na maisha yao.Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe so long
    hajafika kwako kukulilia shida acha kuleta kejeli.Watanzania wenzetu kibao wananyanyasika nchini kwetu kwenye majumba ya wahindi na viwanda vya wahindi na hilo wala hulioni kwa kugaganga njaa kwa kufanyishwa kazi km watumwa.Hebu kawasaidie kwa kuwatafutia wazungu wa kuwaoa au kuoa.

    ReplyDelete
  43. mimi naungana na annon wa hapo juu yangu kwamba mapenzi hayana rangi wala cheo. sidhani kama ni busara kwa mtu yoyote kunyimwa au kuinyima nafsi yake furaha ya kuwa na mtu anayempenda kwa kigezo cha rangi au uhalisi wake.eti tu kwa kuogopa watu wa jamii yake watasemaje ndoa sio rangi kuna mambo makubwa yanaendelea vyumbani jamani. Afterall, hao watu weusi wanaongoza kwa devorce hapo marekani na hii ni dalili kwamba wenyewe kwa wenyewe wanaonana kenge.nadhani wangeanza kwanza ku deal na matatizo yao kabla ya kuwa concerned na ndoa za mchanganyiko. la pili, mimi nakataa hawa maswala ya hawa jamaa kufananishwa na waafrica, kwa sababu hapa tutakauwa tunahusisha context context mbili tofauti sana.kufananisha jamii hizi mbili ni sawa na kuota kuwa size moja ya viatu inaweza kuwatosha watu wote.wao harusi ni optional while kwa wengi wetu kule Africa harusi ni compursory hasa katika jambo la kutunza heshima yako na ile ya wazazi. kwa hiyo sisi hatuna muda wa kuangalia rangi wala ngozi kwa sababu tafsiri yetu ya harusi ni tofauti sana na ile ya kwao. Asanteni sana. Sydney, Australia.

    ReplyDelete
  44. Ukitaka kula nguruwe, chagua aliyenona. If you want to eat pig, choose one which is fat. Lakini kumbuka Mzungu Wa kula hafundishwi mwana. The process of eating is not taught to a child.
    Kila mtu mweusi huota ndoto za mzungu wa kike na hii ni hakika...sawa na jike leusi pia lipende dume zungustop kidding la sivyo msingenyemelea kila kitu zunguzungu!!!

    ReplyDelete
  45. VIDETI CHAPTER 1:1

    Kwanza nampa nne mzawa maana kwa kiasi fulani (sio kila alichosema) nakubaliana sana na uchambuzi wake.
    Binafsi napenda kuchangia kama ifuatavyo.

    A.Suala la kujiunga katika TAASISI NDOA linapaswa kufanyika chini ya misingi mikuu miwili nayo ni HIYARI NA UPENDO WA DHATI. Ukimisi kimoja au vyote basi andaa dawa za kutuliza maumivu mazito ya kisaikolojia katika kujitambua na hata kutofuraia matunda ya hiyo taasisi aliyoianziasha Rabuka pale Edeni.

    B.Ubaguzi ni ugonjwa mpana kuliko wengi tunavyoufikiri. Aidha pia ni vema kumtofatisha Mbaguzi na Mtaifa au na Mpenda Kabila au utamaduni wake au Mzalendo n.k . Mfano , nchi kuweka sera za namna ya kuwapendelea Wananchi wake katika huduma fulani kuliko wageni mfano mikopo ya elimu , pembejeo, masoko n.k huo si ubaguzi (pengine wengine wangeuita ubaguzi chanya) bali ni utekelezaji wa Serikali katika kuwalinda na kuwawezesha wananchi wake kwa mujibu wa majukumu ya viongozi kama tulivyokubaliana ndani ya Katiba yetu ya nchi. Lakini Kiongozi mmoja anapoamua mfano kumpa mkopo wa elimu mwanafunzi mwombaji kwa mningínio wa kuwa anatoka katika kabila au dini yake huo ni ubaguzi maana hatuchakubaliana na vigezo hivyo katika utoaji wa huduma hiyo.


    C.Ni kweli USA kuna Ubaguzi (hasi) na wabaguzi, lakini pia ni kweli kuwa hata Tanzania kuna wabaguzi na ubaguzi. Nachelea ku- generalize’ kuwa Wazungu wote au wengi wa USA ni Wabaguzi maana nitakuwa siwatendei haki wale wengi ambao si Wabaguzi. Nitoe mfano wa kabila la Mama yangu; Ni uchovu wa kufikiri kuhara kauli hafifu kwamba , kwa sababu Mwanamke Mhaya au kundi fulani la Wanawake Wahaya 10 waliwahi kufanya (kazi ya) ukahaba wakati fulani katika mtaa maarufu wa Lutiginga basi leo Wahaya WOTE, POPOTE, KILA WAKATI , VYOVYOTE ni Malaya.

    Tasnifu hiyo haikatizi miongoni mwa mchambuzi yeyote makini kwa sababu:-

    i.Hao Wahaya 10 hata ingekuwa zaidi wanabeba uwakilishi gani kati ya wengine wote waliobaki (sijui) labda milioni mbili.
    ii.Nani kamwambia kuwa mpaka leo ukienda Lutiginga utawakuwa wanaendelea. Mbona siku hizi Mtaa umefurika wenyeji Abhagangaji . Na mbona sasa tunawafahamu Abhagangaji zaidi ya 15 katika shughuli hiyo lakini bado hatujasajiri kabila hilo kuwa ni Malaya?

    Je hii ni mojawapo ya zile korasi za kilevi zenye ghani ifuatayo?
    “Wachaga wote ni Wajasiriamali fisadi, Wakurya wote ni maafande wa LY, Wakinga wote ni wabishi wa ukoo, Wajita wote wana malingo yasiyona kitu, Wazaramo wote ni wababaishaji , Wamasai wote ni washamba wa kila kitu, Wafipa wote ni washirikina, Wakristo wote ni wanafiki; Waislamu wote ni waongo, Wahindi wote ni wakwepa kodi; Viongozi wa Afrika wote wanawahi Ikulu kwa nguvu, Wajerumani wote ni wakatiri, Wanawake wote wa Kiafrika hutongozeka (nje ya ndoa), wanaume wote wa kiafrika hutongoza (nje ya ndoa), Wahudumu wote wa vyumba vya maiti ni mateja wa kutupwa wakati Wataalamu wazuri bingwa wa upasuaji wote ni walevi, Wanaume wote wanaopenda upishi ni mashoga, watoto wote wa mapolisi hutembea wakitema sumu toka kamusi za matusi, na hata hii ya Wazungu wote wana maisha ya hali ya juu!! n.k”

    iii.Ok, hata kama hao uliowaona enzi hizo bado wapo wanafanya biashara hiyo, je ni nani aliyekuloga kufikiri kuwa Umalaya ni mpaka uishi huo mtaa au uwe katika kazi hiyo tu. Je hakuna Malaya huko mahofisini, viwandani, vyuoni n.k na pia je unawaitaje wale wanaume wa makabila yote wanaonunua ‘bidhaa’ kwa hao akina mama? Mbona makabila yao hujayatendewa haki kutuzwa ukahaba pia?

    D. Ndiyo ni kweli kuwa kundi fulani la Wazungu na Waarabu wakati fulani wa mababu waliwabaguwa Waafrika na kuwachukuwa utumwani. Je ni haki leo hii kuwaita Wazungu na Waarabu WOTE , VYOVYOTE , KILA MAHALI kuwa ni Wabaguzi? Kwanza napenda kuwakumbusheni kuwa hata wakati huo wa historia chafu kuna wazungu na Waarabu kibao walioathirika vibaya na siasa na biashara hizo na walipinga vikali japo walikuwa wanashindwa kutokana na nguvu za dola za enzi hizo.

    E. Ni kweli kuwa wapo wanaooa na Wanaoolewa na watu wa mataifa mengine kwa mahesabu rahisi ya yamkini za upatu fulani (Convenience Marriage ties) wa kimaisha japo hata kama hajampenda mwenziwe kwa dhati; kama ambavyo wapo Watanzania wanaojitahidi kuoa kuolewa na Mtanzania anayedhaniwa kuwa tajiri hata kama upendo wa dhati haupo. Kwa hiyo ni kosa kubwa sana kuwavika hao watu (WACHACHE) uwakilishi wa WOTE walioolewa au kuoa watu wa mataifa mengine. Kuna watu humu wanazuka tu na kusema oh wote ni wahangaikaji wa kutafuta makaratasi na utajiri na kwamba walio katika ndoa za kimataifa wanajisikia sana; Kamwe siwezi kuacha tungo tete na za ki-kashifa kama hizo zikatize kunichafulia mimi na wengine wote tunaofuraia Taasisi hii na matunda yake chini ya misingi miwili tajwa hapo juu.

    Mimi nimeoa mwingereza (mzungu). Wakati tumeonana, tukawasiliana na kupendana nikiwa TZ, mimi nilikuwa na mali kuliko hata yeye. Sasa tunaishi hapa kwao UK kwa muda kimasomo . Siku moja mama mkwe aliniuliza kuwa kwa nini nisiapply kabisa sasa kuwa na Uraia wa Uingereza maana nimekuwa nikipewa Resident Permits za miaka mitatu na mitano mara mbili na nina sifa zote za kuomba uraia wao. Nilimwambia kuwa mpaka hapo Tz labda itakapokubali kuwa na uraia wa nchi mbili, sitaweza kuukana Utanzania wangu eti kwa sababu nafikiri kwamba kuwa Mwingereza ni bora zaidi ya kuwa Mtanzania.

    Jamani kama alivyosema mchangiaji mwingine, si kila mtu aoaye au olewaye na mzungu eti anatafuta unafuu fulani wa kimaisha kwa njia ya mkato. Na wala mimi utambulisho wake wa uzungu au Uingereza hauniongezei wala kunipunguzia pendo langu kwake. Kwa hiyari yetu tulioana kwa sababu tunapendana kwa dhati. Na mara baada ya kumaliza nondo yangu tutateremka wote kama tulivyokubaliana tulipwe madafu na tutoe huduma nyeti kwa umma wa ndugu zangu Watanzania na wakweze bibi Nyakatakule.

    Mara kadhaa nikionacho ni ukinzani wa kifikra dhidi ya watu wenye mtindio wa kujitambulisha (identity problems) na kutojiamini au ni wale wabaguzi wanaodhani kuwa ‘international marriages’ ni kitu kisichowezekana au ni usaliti wa aina fulani au ni chukizo kwa Mungu.
    Hao ndio binadamu tukutanao, kisha unasikia wanawambia wenzao eti ‘du! kaoa mtasha huyo! ‘, Kitu ambacho kamwe mimi sitawahi kujitambulisha na ulimbukeni wa jinsi hiyo . Au mtu anakuona na mkeo mnatembea sokoni anaanza kusema jamaa anajisikia sana au sijui ametawaliwa sana na mkewe huyo; Nyoka mkubwa we! unataka asiwe karibu nami ili wewe uchukuwe nasafi??
    Mara mbili nilisimamisha gari kununua kitu fulani kwa vijana wajasiriamali wanaotembeza bidhaa Dar, hao vijana wenzangu walikataa kuongea na mimi bei wakisema kuwa wao wenyewe wanataka kukubaliana eti na ‘Mtasha Mtalii’ niliyekuwa nimembeba. Kwa sauti ya upole na unyenyekevu nilijitahidi kuwaelewesha sana Watanzania wenzangu kuwa huyo alikuwa mke wangu na mimi ndiye nilikuwa mnunuzi na mlipaji wakakataa mpaka walipoona ninaondoa gari ndipo wanakuja sasa mbio kufukuzana na gari wakisema ‘eti haya mzee tuongee biashara kumbe ulishafanya kweli!’

    Hakuna hapa kitu chochote cha ajabu! Kuna Waafrika maskini, kuna Wazungu maskini na kinyumeche; kuna Waafrika vilaza, kuna Wazungu vilaza na kinyumeche; kuna Waafrika wasiojua kupenda, kuna Wazungu wasiojua kupenda na kinyumeche; kuna kuachika / kuachwa Afrika, kuna kuachika / kuachwa Ulaya, Marekani n.k na kinyumeche .
    Tumia uhuru wako kuchagua yule umpendaye anayekupenda! Kumbuka pia kuwa mapenzi huanza katika kuwasiliana kwa namna moja au nyingine.

    Mleta hoja anasema; nanukuu.
    “Hapa Marekani ni rahisi kuona samaki anatembea mchangani kuliko Mmarekani mweusi wa kike ana-date mzungu wa kiume.”

    Mdau ya nini kujaribu kutaasisisha msawazo wa rangi ya ngozi katika suala la ndoa?
    Kama kweli unatafuta kumalilisha mahesabu hayo basi endelea na kazi hii uliyoianza kwa kubalansi kwanza idadi ya wanawake Wamarekani weusi iwe sawa na idadi sawa ya wanaume wazungu na uondoe utakavyojua toka uso wa dunia ya marekani, Wanawake wote Wazungu na Wanaume wote Wamarekani Weusi na Wamarekani wengineo wote waishio Marekani na kisha uwasiliane na Mungu akupe kibali cha kuongeza maandiko yafuatayo.

    ENENDENDENI NYOTE SI NJE YA MAREKANI, MKAOANE NA WATU WA NGOZI TOFAUTI TU HATA KAMA HAMPENDANI!

    Videti sura 1:1 inayofuta maandiko mengine yote ya uhuru wa kuchagua mwenza.

    NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO

    ReplyDelete
  46. KUNA HATARI KWAMBA SISI WEUSI NI WABAGUZI, TUNAWABAGUA WEUPE HATUTAKI KUWAOA KWASABABU NI WEUPE, AU LABDA TUNAJISIKIA WADOGO, INFIRIORITY COMPLEX....SIJUI UTUMWA NA UKOLONI ULITUFANYA NINI!

    ReplyDelete
  47. HAYUKI HAYUKI HAPO JUU UNASEMA NJIA MKATO KWA PAPERS, CASE CLOSED!!!UNA MAWAZO MAFINYU SANA!! HIVI HUJUI KWAMBA NCHI ZINAZOKUWA KAMA AFRICA SIKU HIZI NDIO ZINA DEAL ZAIDI KULIKO ULAYA? WATU TUKO HUKU, TUNA WAZUNGU NA HATUNA URAIA WA HUKU, NA TUNARUI BONGO KUFANYA VITUZZ, SASA UTASEMAJE?

    ReplyDelete
  48. Dada zetu wa kitanzania ni wa-roho sana wa pesa na mali. na fikira zao mzungu kwao ni mwisho wa matatizo yote. ndoto ya mwanamke wa kibongo ni kuolewa na mzungu.

    ReplyDelete
  49. YAANI MOST PEOPLE HAPA ARE VERY STUPID AND HAVE SIMPLE MINDS!! HIVI KWA WALIOSEMA MAKARATASI... DO YOU THINK IS A NIGHT THING KUYAPATA NA JEE WOULD YOU MARRY SOMEONE BILA MAPENZI ALAFU USOTE HAPO MIAKA NENDA MIAKA RUDI KISA MAKARATASI..NO WAY!!

    KWA WALIO UK WANAELEWEWA FIKA..IT IS A THING OF PAST KUWA UNAPATA PAPER THAT EASY..THE TRUTH IS.. IT CAN TAKE MORE THAN EVEN FIVE YEARS KABLA HUJAYAPATA HAYO MAKARATASI KWAKUWA UTAKUWA UNACHUNGUZWA FIKA KUWA ARE YOU LIVING TOGETHER AS A WIFE AND HUBBY, AND LOADS OF OTHER STUFF (KWA KUWA KUNA A LOT OF BOGUS MARRIAGES HAPA) SO PEOPLE TRY TO BE A BIT REALISTIC SIO KURUKIA RUKIA VITU MSIVYOVIJUA. WATU WANAOANA KWA SABABU NYINGI - MAPENZI, ETC...AFTERAL WAZUNGU WENGINE WANAOA ILI WAPATE MAKARATASI YA KUISHI AFRICA..SO WHAT ABOUT THAT????

    HAO MNAESEMA WANANYANYASIKA.. NA KUBAGULIWA NANI ASIYEJUA NDOA ZA KIBONGO, NANI ASIYEJUA AMBAVYO UNAWEZA KUONWA KAMA TAKATAKA NA HUKO WALIKOOLEWA AU KUOWA... SO SOMETIMES THIS KUNYANYASANA IS A UNIVERSAL THING!! NI BINADAMU AND NOT COLOURS!!! ANGALIAA MDADA ALIYELETEWA MWANAMKE NDANI YA NDOA YAKE NA WATOTO WA ZIADA ,..THAT IS WORSE THAT UBAGUZI TO ME!!

    NA WALIOSEMA KUULA... NDO WAJINGA WA MWISHO ESPECIALLY WEWE ULIYETOA MAONI YAKO HAPA. NI LAZIMA UWE VERY PRIMITIVE KUFIKIRIA HIVYO. AU LA UMETOLEWA MOJA KWA MOJA KIJIJINI NO EXPOSURE NO WHAT?? LAKINI KAMA YOU HAVE ENOUGH EXPOSURE THEN YOU WONT TAKE IT THAT WAY. THIS MEANS KWA WALE WALIOOANA KWA KUKUTANA VYUONI, MAKAZINI NK HUWA WANAELEWA FIKA WHAT TO EXPECT. ILA KWA CHANGU ALIYEOKOTWA PALE KINONDONI MAKABURINI OFCOURSE ATAFIKIRIA KAMA WENGI WALIVYOCOMMENT HAOA NA SIMPLE MINDS ZAO ZILIZOJAA USHAKUNAKU HAPA !!

    ReplyDelete
  50. NGOJA NIONGEZE MY 5CENTS...NIMEDATE MMBONGO,MWARABU NA MZUNGU! (WASHINGTON) KATI YAO WOTE WANASIFA TOFAUTI.
    MBONGO:TULIANZA VERY GOOD FOR THE 6MONTHS.NIKAMUAMINI KIASI NIKAAMUA KUMOVE-IN NAYE. KAMA KAWAIDA WOTE TUNAPIGA MZIGO BUT SIJAWAHI KUACHA VYOMBO VICHAFU KWENYE SINK/KUONDOKA ASUBUHI BILA KUTANDIKA KITANDA. MWANZONI ALIPRETEND KUWA NAYE NDIO ALIVYO. BAADAE IKAWA NI MYRESPONSIBILTY ANA IKAFIKIA POINT KUWA ANALALMIKA ASIPOKUTA KITANDA HAKIJATANDIKWA (guess who was the last prsn)BAADAE AKAANZA KUSEMA HANA HELA ZA RENT NYUMBANI WANAMATATIZO. BUT KILA SIKU ANARUDI NA NEW KAPELO,NEW TIMBS,BELT ETC... LAST STRAW AKAWA ANATONGOZA WANAWAKE WENGINE MBELE YANGU. NIKIWA KAZINI NAPIGA MZIGO ANALETA WANAWAKE NDANI YA NYUMBA AMBAYO TUNALIPA RENT WOTE.YAKANISHINDA.
    to be continued.......

    ReplyDelete
  51. Anon hapo juu inabidi hii story uimalizie,maana ilikua imeanza kunoga.Yalikuaje ulipo date mwarabu na mzungu.Mimi nasubiri.

    ReplyDelete
  52. Continued from Wensday Jan 30,2008 1:04am....
    BASI WANDUGU NIKAPATA MWARABU (OMAN)HUYU NAYE AKATAKA NIMOVE IN NAYE...NIKAMTOLEA NJE COZ UKISHAUMWA NA NYOKA UKIONA UNYASI UNASHTUKA (trust me!) KWAHIYO RELATIONSHIP YETU IKAWA YA KUSLEEP OVER ON THE WKD. JAMAA ALIKUWA POA KISHENZI CRIB YAKE ILIKUWA SAFI,KUPIKA NDIO USISEME ALIKUWA ANANITOA KNOCKOUT VIBAYA MNOO.
    IN SHORT I WAS HAPPY!
    NIKAUMWA FLU....EVRYTNG CHANGES!!!!HABIBI AKAWA KAMA JIBRIL MTOA ROHO ANAKUJA KWANGU MIE NDIO FEVER IMEPANDA KISHENZI HATA KUJICHEMSHIA CHAI SIWEZI, KUSIMAMA BAFUNI KUOGA SIWEZI NAONA KIZUNGUZUNGU KISHENZI NIKAMWAMBIA NAOMBA MSAADA (BAADA YA KUMUONA HAJITUMI)ALIPOKUJA ANANIPELEKA BAFUNI KUOGA NATETEMEKA NA BARIDI JAMAA ANATAKA ALE TUNDA LA MTI WA KATIKATI????(TRUE)NIKAMWAMBIA CWEZI KABISAA KWANI ALINISIKILIZA?? AKAJIPINDA...MIMINALIA KWA MADONGE NA MAHASIRA NA SHOCK JUU YA KUTOAMINI KINACHOTOKEA ALIPOMALIZA AKAJIDAI NISIFANYE BG DILI YEYE MWANAMME KASHINDWA KUJIZUIA KUONA UTUPU WANGU (wakati keshauzoea..ovyo)HAKUISHIA HAPO TUMEMALIZA KUOGA NIKAMUOMBA ANISAIDIE KUBADILISHA SHUKA MAANA UNAJUA UKIWA NA FEVER UNAVYOSWEAT UCKU NA NILIKUWA CJAOGA 3DYS KULALIA TENA SHUKA ZA MADASO IKAWA NGUMU! MBONA NILIKOMA MWANAMME AKANIONYESHA MAKUCHA YAKE ALINISEMA NA MATUSI JUU ETI NAMFANYA YEYE NDIO DEM ANAJUTA KUTOKA NA MIMI WANAWAKE WA KWAO WANADRIP MKONONI WANAPIKA,WANAOSHA VYOMBO NA AMRI YA SITA WANAIBANJUA...
    to be continued........

    ReplyDelete
  53. aah dada story tamu japo inasikitisha, huyo muarabu amakweli firauni, enhee endelea, ulipokuwa na mzungu ikawaje....aakhh umeniburudiasha story tamu sana...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...