THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

kulikoni jambo forums?

wadau kunradhi. katika kupitia mitandao ya wadau wengine jioni hii, nilipofika jambo forums nimepata kitu hicho. nimejaribu tena sasa hivi mambo ni yale yale. je kuna anayejua kimetokea nini ama ni mimi tu mwenye kuikosa?


Kuna Maoni 46 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Wawili washikiliwa na Polisi kwa sababu ya Jambo Forums. Kwa maelezo zaidi visit www.klhnews.com

 2. Anonymous Anasema:

  Even mi nimeanza kuitafuta muda mrefu sana kuanzia kwenye saa kumi na moja mpaka saa nne hii haipatikani, Lakini kwa data nilizonazo ni kwamba kuna mdau mmoja wa JF emechukuliwa na watu waliojiita ni maafisa usalama na wamemwambia wanamchukua kwa ajili ya mahojiano naye lakini wadau wengine wa JF wanaendelea kumtafuta baada ya kumtafuta katika vituo maarufu vya polisi bila mafanikio, sasa yawezekana kuwa haya ndo matunda yake baada ya huyo mdau mmoja kukamatwa....

  Inasadikika kuwa wanausalama wanahangaika kujua ninani haswa anayehost hii JF na ni nani haswa anayelikisha habari nyeti kwenye wanja la JF.

  Hope itakuwa sawa ngoja tuone maana pale ndo sehemu ya kujua mauozo ya mafisadi wa nchi hii.

 3. Anonymous Anasema:

  Duh wameshafanyiza huko tayari! Yaani wamebenewa! Dalili zilionekana tangu jana! Tutakoma nchi hii!

 4. Anonymous Anasema:

  Jamboforums imefungwa sasa hivi kwa vile polisi Tanzania wameanza kuwakamata memba wa JF walioko TZ wakidhani kuwa ndio Invisible au robot yule anayerekebisha mambo ya JF

 5. Anonymous Anasema:

  Si wewe tu kaka,naona kuna tatizo kubwa. Nahisi hii site imeshafanyiwa ufisadi. Mapema kulikuwa na taarifa kwamba muendeshaji mkuu wa site hiyo na jamaa wengine wawili wamekatwa na watu wa usalama wa Taifa, mwenye taarifa zaidi atumegee humu pse.

 6. Anonymous Anasema:

  Mimi nilianza lushindwa kusikiliza misiki jumapili jioni....Lakini labda wanafanya upgarade na hawatumii log na ndio inakua hii shida site inakua down...
  Natumaini watarudi soon kwa vile na miss nyimbo zao

 7. Anonymous Anasema:

  Soma KLH news ya Mwanakijiji, wanadia wameifunga sijui kuna watu wamekamatwa na polisi ndio wameifunga. Nayo hiyo JF na KLH news nafikiri ni mali ya Chadema.

 8. Anonymous Anasema:

  Nahisi hii ngoma JK ameomba msaada wa FBI wakaipiga chini kama wanazima kibatari vile, hili litakuwa bonge la zawadi kwake kwani ilikua inamnyima usingizi na ilikua inakua kwa kasi.

 9. Anonymous Anasema:

  Leo Michu utapata maoni yenye akili sana kwa kuwa 'vipanga' wote wa JF hawana pa kwenda! LOL!

 10. Anonymous Anasema:

  kaka michuzi,huu ufisadi sasa umezidi,naona sasa umeingia kwenye blog,hivyo wamiliki wa blog kaeni chonjo!

 11. Anonymous Anasema:

  Hawajalipa subscription hao. Naona hawalipi mpaka wakatiwe!

 12. Anonymous Anasema:

  Michuzi,

  Hiyo ndio demokrasia ya Kiafrika! Ukisema ukweli wewe mwongo na mzushi, yanayoandikwa Jambo forum yanawafichua mafisadi sasa imefikia wakati mafisadi kuchukua hatua kali.
  Navyosikia kuna wahusika wachangiaji wametiwa ndani na wengine wanatafutwa.
  Uhuru na Kadi?.... kazi ya chama!

 13. Anonymous Anasema:

  Nimekutana na kitu kama hiyo.....

  Mafisadi oyeeee!!!!

 14. Anonymous Anasema:

  Michuzi usishangae
  WanaHARAMU wametenda walichoamua kutenda. Kwani wewe hujui kilichoikumba JF?
  Wewe una bahati maana bado waoga kijani kijani ati! Najua unaweza kuamua kuuza IP zetu sie wadau wako. Hakuna neno itakuwa kheri tu ila naamini kwa moyo wako wa dhati hutafanya hivyo

 15. Anonymous Anasema:

  kuna soo....jamaa wawili waku ndani..

 16. Anonymous Anasema:

  Inawezekana wametumia "bandwidth" yao kwa siku, kwahiyo hosting account yao imesitishwa kwa muda au hawajalipia hosting kwahiyo wameisitishwa kwa muda...

  Ila sidhani tatizo ni pesa kwasababu wanatengeneza pesa nyingi kutoka adsense.

  Sitashangaa kama wanatengeneza zaidi ya $5000 kwa siku hasa ukiangalia wana matangazo mengi ya obama na clinton ambanyo yanawagarimu "adwords advertisers" zaidi ya $1 per click. Wacha bwana hawa jamboforum wana traffic isiyo yakawaida

  Michuzi weka adsense nawewe ili utengeze hiyo mihela. Kama unahitaji ushauri wa ku-monetize website yako nitakusaidi.

  Hata kama hatu nunui kitu tuta click hizo ads ili kaka yetu upate hiyo mihela.


  Ukiweka ads utaweza kutengeneza mpaka $10,000 per day and i'm not kiddin kwasababu traffic unayo tena FREE kutoka kwa loyal WADAUZ.

  I been running businesses online for more than five years... trust me I know what I'm talking about.

  Intrapreneur (internet entrepreneur) kutoka duniani-papaliko19@yahoo.com

 17. Anonymous Anasema:

  Nenda http://www.klhnews.com/ utapata full information.

 18. Anonymous Anasema:

  Michuzi kwa taarifa kuhusu Jambo Forums BOFYA HAPA

  Inaelekea kuna watu hawapendi uhuru wa habari. Lakini hawajui kuwa harakati za kwenye internet huwa haziwezi kuzimwa.

  Kama hawajui wakamuulize Mugabe ambaye ameonja joto wanaharakati wa internet.

 19. Nungunungu Anasema:

  Huko JamboForum moderator muhimu kasababisha hiyo suspension.Lakini kumbe wewe Michuzi na ujanja wako wote unatumia Internet Explorer?

  Mambo ni Firefox bwana, halafu naona unatesa na Vista yako mwenyewe - anyway wabongo wengi ni Windows sababu Mac ni gharama wakati Linux wengi hawaijui.

  Jambo itarudi, na ikishindikana itaundwa forum mpya.Kama ni njama za mafisadi basi watakwama.

 20. Anonymous Anasema:

  mimi nawapata poa tu labda wewe na kilaptop chako kimeo

 21. Anonymous Anasema:

  Wewe hapo juu labda unawapata jambo network...jambo forum hawapo hewani

  Yaani mafisadi walikua wanasubiri tu Bush aondoke nchini

 22. Anonymous Anasema:

  HII SHUGHULI YA JACK PEMBA KAINGIA MITAMBONI KATIKA MAHAKAMA KUU YA UINGEREZA KAOMBA IFUNGWE KWA SABABU IMEMWARIA JINA, HIVYO MAHAKAMA YA UINGEREZA IMEWEKA INJUCTION IFUNGWE. FOR MORE INFORMATION GO TO GSB WEB SITE.

 23. 255Texter Anasema:

  Duh, hata siamini. Yaani jamaa chupi zimewabana mpaka wameamua kifungia forum yetu yenye akili ya JAMBO FORUMS? Sasa hii ni kwa sababu jamaa wa JF ndio walioleta taarifa za kupigwa kwa wapinzani kule Kiteto?? Nadhani CCM sasa imeanza kutapatapa.

  Anyway, tutafika tu.

 24. Anonymous Anasema:

  SIDHANI KAMA JAMBO FORUMS INAWEZA KUFUNGWA KWA SABABU YA KUTOKULIPA SUBSCRIPTIONS, NINAVYOJUA MIMI KUWA CHADEMA INASAIDIA KWA HALI NA MALI KUIWEZESHA JF IWEPO. NA CHADEMA HAIJASHINDWA KWA HILI.
  HUENDA LABDA KUNA TATIZO JINGINE.

 25. wazalendo Anasema:

  Wakimbizi wa JAMBO FORUMS tushapata kambi nyingine ya kujistiri...hapa:

  http://wazalendo.wordpress.com/

  Brother michuzi tunashukuru kwa msaada unatupatia

 26. Anonymous Anasema:

  HII INANIKUMBUSHA SOO LA BCSTIMES.COM ENZI HIZO NDIO FORUM ZA KWANZA KWANZA JAMAA YANGU POPE ALIPATA MATATIZO KAMA HAYA ALIWEKWA NDANI NA KUHOJIWA NA ILE FORUM ILIFUNGWA, NAWAKUMBUKA WATU KAMA
  POPE
  MWANAKIJIJI
  DUME
  LAPTTP
  MKANDARA NA WENGINEO NILIPATA KUJUANA NAO PALE NA LEO NAWAONA HADI HUMU.
  SO KWETU HAYA MAMBO BADO WANATAKA YAWE NA MIPAKA.

  MDAU MPONJIKA

 27. Anonymous Anasema:

  Wana Jamboforums, inawezekana wameturn against us kwa sababu kadha wa kadha. So far, tutapatikana kwenye wwww.klhnews.com, at this particular moment watu watajadili njia mbadala kwenye hiyo website.

  Brother Michuzi thanks kwa kutupa hifadhi kwa muda hapa.
  Mtanganyika

 28. Anonymous Anasema:

  forum haina matatizo ya kifedha,na wala hakuna chama chochote kile cha siasa kinalipia forum. Ni propaganda tu za serikali ya TZ na wale wezi wa fedha za serikali ndio maana imekuwa imekuwa blocked, lakini itarudishwa tu, msijali.

 29. Anonymous Anasema:

  Jambo Forum is not affiliated to any political party in Tanzania. It is an independent institution that welcomes all Tanzanians who are pushing for changes for betterment of Taifa.

  Yes we are critical of malaise and poor governance by Serikali, that is why you will brand us Anti-Government.

  We are going to stay strong and keep up the fight.

  JF Premium members and Senior expert members please email me kishoka70@yahoo.com

  Rev. Kishoka

 30. Anonymous Anasema:

  Finally the chickens have come home to roost!! Bora wameifunga na ningefurahi sana kama yule bishoo aliyekuwa anajiita "Invisible" wangemtia lupango pia.

  La ajabu ni kwamba kulikuwa hakuna uhuru wa kutoa maoni kwenye ile forum wakati wao walikuwa mstari wa mbele kudai uhuru huohuo wa kutoa maoni. Ile slogan yao ya "Where we dare to talk openy ilkuwa ni gimmicks tu

  Halafu kuna baadhi ya wachangiaji walikuwa wakijiona wao ni elite mle na ukiwapinga au kuwashutumu basi wanakutishia kukufuta uanachama (haswa yule primadonna aliyejipachika jina la "mwafrika wa kike"). Yote kwa vile wanajuana wakati wao hapohapo walikuwa wakilaani usiku na mchana dhana za cronyism, favoritism, nepotism etc.

  Na ule msemo wao wa eti walikuwa pale "kumkoma nyani giladi" naona sasa kibao wamegeuziwa wao ... bwahahaa! :-)

  Kidumu Chama Cha Mapinduzi!!

  Mzee Avenue Mavuzi

 31. Anonymous Anasema:

  hapo wanachemsha tu wabarikiwe kwa muda ,,,,,,,,,,mambo zenu tetehhhhh mnachekesha wanapoteza muda wao,,,bugup mwanakijiji invisible,,tupo pamoja jamani
  jamani haloooooooooooooooooo

 32. Anonymous Anasema:

  kwa upande wangu mimi jambo forum naiona kama genge la wahuni tu! Ukisoma mawazo ya watu kwenye ile forum kwa hakika utaondoka siku hiyo hiyo ya kwanza.

  Mawazo mengi ya watu yamejikita kwenye vitu vya kufikirika tu! Uchochezi na uwongo! Dini, na upuuzi mwingine mwingi sana. Mtu anaweza kusoma section ya bible au Quran akaamua iwe thread! Waht is that?! Kwa kweli, kwa mtu ambaye ni intellectual, kwa hakika jambo forum atasikiliza music tu. Maana huo hauna shida. The rest ni garbage. Na dhani na watu wanaochangia huko ni GARBAGE pia.

  Laiti kama wangeweka majina yao, sina shaka ingedhihirisha ninayosema. Ndo maana wanaficha majina. Lakini ndo mambo ya DEMOCRARY

 33. Anonymous Anasema:

  Ooh Kumbe JF na KLH news ni mali ya Wachaga oops sorry CHADEMA, sikujua hilo. Haya na nyie CCM tafuteni forum yenu sio kufungia forums za vyama vya upinzani ala!

 34. Anonymous Anasema:

  Nyie vilaza mnaoponda na kukandia JF mna walakini katika uelewa wenu. Kumbukeni kwamba yale ni mawazo ya watu, na kamwe huwezi kumzuia mtu kuwaza! Huwezi kuzuia mvua ama jua! Kama mnadhani JF ndio imekufa poleni sana, kwani hamjui mtendalo, bado inaendelea huko kwingine kama kawaida. Kile sio chama cha kisiasa, ni vyama vya kisiasa, ni taifa huru, ni serikali huru, ni mawazo huru nk, kwa kifupi inatisha!
  We Avenue ******** ulifungiwa kwa sababu wewe ni mwendawazimu, kwani kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kutumia jina ambalo huwezi kulitamka hadharani.
  Michuzi usibane maoni yangu, kwa sababu bado tunaendelea na juhudi za kuiweka JF hewani very soon!

 35. Anonymous Anasema:

  Wana JF nimecreate blog itakayo tuhost kwa muda huu.
  www.jamboforums.blogspot.com , vile vile kwa wale premium members unaweza kuwasiliana na Rev kishoka, au fika pale klhnews.com.
  unaweza kuni email kupitia mtanganyika01@yahoo.com
  Thanks kaka michuzi

 36. Anonymous Anasema:

  Acheni propaganda zenu, mmetumwa sasa kuja kuichafua JF? Hamtafanikiwa, JF ina mizizi iliyokomaa na itarudi kwa nguvu zote.

  JF sio CHADEMA wala hailipiwi na CHADEMA. Inaendeshwa na Watanzania wenye moyo na mapenzi kwa nchi yao.

  Haya ni mapambano, njiani kunaweza kuwa na miiba na visiki, lakini tutavuka tu.

  Kama tulivyowaumbua Richmond na vibaraka wao, BOT na mafisadi wakiongozwa na Rostam. JF itaendelea kudumu na kutetea maslahi na maliasili ya Watanzania.

  Msiyumbishwe na hao wanaoleta siasa za mafisadi hata kwenye mambo ya maana.

  JF inakuja kwa nguvu zote, tunaomba muwe wavumilivu. Muda sio mrefu tutakuwa na nguvu zaidi ya hii tuliyokuwa nayo sasa.

  Kama kuna mtu ana visa na Mwanakijiji au Mwafrika wa Kike basi akapambane naye kwa hoja, at JF we dare to speak openly.

  Mwambie Lowassa kwamba JF ni garbage, mwambie JK, kwamba JF ni garbage, Mwambie Hosea kwamba JF ni garbage. JF imewakuna pasipokunika na ndio maana mnaanza kuleta propaganda.

  Hatutawaachieni mwaka huu mpaka kieleweke.

 37. Gembe Anasema:

  we will be back soon.i know it so sad for Tanzania,

  it is my hope Mungu atalipa kwa hili?kwanini iwe hivi.

  Mzee Pinda unaanza Vibaya,Naomba sana utusaide kwa hili!

  tatzi o ni lipi?

  Jf on Fire soon,I need the archives only.

 38. Anonymous Anasema:

  Huyu mwanakijiji mnafki nambari wani anajifanya amesikitika kufungwa JF kumbe anafurahia watu wajae kwenye website yake ambayo siku zote imekuwa imezorota. Wadau wote wa JF njooni hapa kwa Michuzi tuendeleze libeneke. lakini tuache ushabiki wa Chadema ambao wameshindwa kulipia fee ya forum

 39. Anonymous Anasema:

  Ebwanajamaa walikamatwa na polisi mmjo toka DAR TECK na mwingine akitokea ARUSHA.MDINGI wao ndo alitoa mchongo wakamatwe.

 40. Anonymous Anasema:

  KWA KWELI IWE TU HAWAJALIPA FEE.ILA KAMA NDIO WAMESHIKILIWA NA POLISI TUTAANDAMANA HADI IKULU JK ATUELEZE KULIKONI AMA LA TUTACHUKUA SHERIA MKONONI.TUMECHOKA NA MAFISADI.WAISHI VIZURI KWA JASHO LA WENGINE.

 41. Anonymous Anasema:

  Wanamjamvi, naomba niweke bayana JF na KLHnews vyote si mali ya CHADEMA. CHADEMA kwa sasa haina chombo chochote cha habari zaidi ya tovuti yake www.chadema.net. Ingawa baadhi yetu wanaCHADEMA tumeshikiriki mijadala JF na kwingineko kama watanzania wengine wanavyoshiriki. Tuelewe kuwa mabadiliko hayana chama, wapenda mabadiliko wanaweza kufananishwa kwa dhamira zao za kutaka mabadiliko. Hivyo, kupotea kwa mitandao ya namna hii ni hasara kwa wote bila kujali itikadi. Ni pigo kwa wapenda ukweli na fikra mbadala. Leo nilikuwa mambo ya ndani asubuhi na nimeonana na Mac na Mike pamoja na Wakili Tundu Lissu. Kwa kweli tumeelezwa mengi na wao na hata polisi waliokuwepo. Sitapenda kusema chochote kati ya yale tuliyoyazungumza. Furaha yangu ni kuwa vijana wenzetu wameshatoka polisi na sasa wako mtaani. Kama kuna mwenye kutaka chochote awasiliane nao. Na nimejikusuru kwenda huko leo kwa kuwa mimi ni mwanachama wa JF, na muumini mkubwa wa hizi jumuia za TEKNOHAMA. Lakini kwa upande mwingine, Mac ni rafiki yangu wa siku nyingi. Nawaombeni tuwaunge mkono vijana wenzetu katika harakati zao hizi bila kujali itikadi kwa kuwa faida yake ni kwa taifa letu. Lakini pia, waswahili wanamsemo kwamba 'mwenzio akinyolewa nawe tia maji'. Tukiruhusu JF ikazama, wakimalize JF jiulize, ni kijiwe gani kitafuata? Kwa maelezo zaidi wasiliana nami kupitia mnyika@yahoo.com au 0754694553. Nawatakieni heri. Pamoja tutashinda.

  JJ

 42. John Mnyika Anasema:

  Tamko langu kuhusu suala hili linapatikana hapa: http://www.chadema.net/blogu/mnyika/2008/02/kwa-niaba-ya-baraza-la-vijana-wa.html

  Kijua ndio hiki, tusipouanika- tutautwanga mbichi.

  Mnaweza pia kutembelea www.klhnews.com naona Mwanakijiji na wengine wanaweka updates za mara kwa mara kuhusu suala hili.

  Bujiku Ngw'aka(kwa wale walio nyumbani)

  JJ

 43. Anonymous Anasema:

  WE ANON FEB 20,2008 4:16:00 UNAAKILI KWELI WEWE?/ AU NA WE NDO WALE WALE??

  UHURU WA KUTOA MAONI AMBAO TUNAUPATA KLH NA TULIOKUWA TUNAUPATA JAMBOFORUMS KWA MICHUZI HUWEZI KUUPATA DAIMA.

  MICHUZI ANAOGOPE ASIJE AKABANIWA NA YEYE NA NDO MAANA UKIPOST COMMENTS ZENYE KUFICHUA MAOVU YA SERIKALI AU VIONGOZI WA SERIKALI HAWEZI KUYAPOST KABISA SASA WE UNAWAAMBIA WATU KUWA MWANAKIJIJI NI MNAFIKI WAPI NA WAPI BWANA??

  GROW UP MZEE AMKA SHITUKA PIGANIA NCHI YAKO.

 44. Anonymous Anasema:

  sasa kanga zilizokua zimeandikwa we cherish democrasy alivyokuja Bush zilikua zina maana gani? Au ilikua kebehi tu....Where is the freedom of speech in our mother land...Sijawahi kusoma hiyo blog( I wasn't aware of it) Lakini kama ni kweli watu waliyoandika humu ...basi we have a long way to go....

 45. Anonymous Anasema:

  Hakuna Demokrasia ya kweli Tanzania. Leo wanaanzia kwa Jambo Forums kesho watakuja mpaka kwa Michuzi au Mjengwa na kuwaambia wazifunge blog zao. Mambo mengi kuanzia Kashfa ya Richmond, Benki Kuu na nyingine nyingi zilianzia Jambo Forums.

 46. Anonymous Anasema:

  jamani mimi niko bongo niko form one pale makongo cjui hiyo jambo forum inamaanisha nini naombeni mnisaidie kunielekeza ni kitu gani?