jk na mama salma wakiagana na wageni wao leo
jk akiongea na rais bush muda mfupi kabla rais huyo wa marekani kuondoka leo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewashukuru wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani nchini, kwa kufanikisha ziara ya Rais George Bush katika Tanzania.

Rais Kikwete alitoa pongezi hizo leo (Jumanne, Februari 10, 2008) asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Es salaam, baada ya kuwa amemuaga kiongozi huyo wa Marekani.

Mara baada ya ndege hiyo kuwa imepaa kutoka uwanja huo kuelekea Kigali, Rwanda, ambako Rais Bush ameendelea na ziara yake, Rais Kikwete aliwaendelea wafanyakazi hao na kuwashukuru.

Kwanza alimshukuru Balozi wa Marekani katika Tanzania, Bw. Mark Green, kabla ya kupeana mikono na wafanyakazi wengine waliokuwa wamekusanyika karibu na balozi huyo.

“Asanteni sana,” Rais Kikwete aliwaambia wafanyakazi hao waliokuwa wamefika uwanja wa ndege kumuaga Rais Bush.

Rais Bush aliwasili nchini Jumamosi iliyopita kwa ziara ya siku nne katika Tanzania, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku sita katika Bara la Afrika.

Kati ya siku hizo sita, Rais Bush amekaa Tanzania kwa muda wa siku nne. Alianzia ziara yake katika nchi ya Benin, Afrika Magharibi, ambako alikaa kwa saa chache tu kabla ya kuwasili Tanzania.



Kiongozi huyo wa taifa lenye nguvu zaidi kuliko taifa jingine lolote duniani, alitarajiwa kukaa saa chache katika Rwanda kabla ya kuendelea na safari yake kwenda Ghana. Atamalizia ziara yake katika Liberia.

Akiwa nchini, Rais Bush alitia saini mkataba wa msaada wa mabilioni ya fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Pia kiongozi huyo alitembelea miradi inayosaidiwa na Marekani chini ya mipango yake mahsusi kwa ajili ya kupambana na magonjwa ya malaria na ukimwi.

Rais Bush ameamua kupambana na ugonjwa wa malaria kupitia mpango wake wa President’s Malaria Initiative (PIM), na ule wa ukimwi kupitia mpango wa Presidential Emergency Fund Plan for Aids Relief (PEPFAR).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Haya sasa mgawane fungu alafu mseme oh naachia ngazi tutafunga mtu this time.

    ReplyDelete
  2. Michu, mimi sijaona sababu ya mke wa JK kuvaa nguo za kumsifia mume wa mtu na nchi yake. Was it compulsory kwamba avae hivyo? Mbona hakumshonea na mwenzake avae za kibongo-bongo? Designer wa mama JK inabidi ajieleze, kulikoni?

    ReplyDelete
  3. Hawa mabwana wanaagana kuvaa suti zinazofanana kila wakati?

    ReplyDelete
  4. asante Michuzi kwa kufuatilia kwa karibu safari ya Bush, ....sasa hii vipi. una news zozote au hutaki wadaku wako wasome!!!!!
    http://www.klhnews.com/index.php/headlines/wawili-washikiliwa-na-polisi-kwa-sababu-ya-intaneti.php


    Mungu yupo!!

    ReplyDelete
  5. Michuzi mwandishi mkuu ...leo ni february 19,

    Hivi mlipata bahati kuchat na waandishi wa habari wa marekani. Did you see them ....what did you find out ....???? They are very pro right??? I hope mlilearn something.

    I still love you though

    ReplyDelete
  6. Michu... Vipi tena, hawa ndio wametuachia pesa na wameondoka na Jamboforums yetu?.. Uko Richabo or not richabo?

    ReplyDelete
  7. Michuzi samahani leo ni tar 19,feb na sio tar 10 bwana mbona unaturudisha nyuma?Sasa Bush kaondoka sijui kitakachofuatia ni nini?mana ya BALALI TUSHASAHAU YA LOWASSA NA BARAZA YA LAKE TUSHASAHAU,SASA YA BUSH NAYO TUTASAHAU SOON,MMH SIJUI LITALIPUKA BOMU GANI TENA??UWIIIIII

    ReplyDelete
  8. Haya tunasubiri lini wataweka Military base..ndo kinachowaleta hao huku.

    ReplyDelete
  9. jamani!kunong,ona mda wote kikwete na bush kulikoni?mmmmmmmh!maongezi hayaishi mpaka uwanjani au majadiliano ya nje ya mkataba?mmegawana wewe na mama wa kwanza,hahahaaaaaaa.

    ReplyDelete
  10. something wrong leo...Jambo Forums is not reachable lazima kuna kamkono ka mtu (either fisadi ama Polisi) we will see.

    ReplyDelete
  11. Mimi pamoja na umbumbumbu wangu nimefikiria kidogo juu ya ujaji wa Bush, kwanza nikawaza ziara za JK za mara kwa mara nje zimezaa matunda, lakini nilipokumbuka kuwa tunavijifununu vya kuwa na mafuta, nikawaza samaki mkubwa hunasa kwa mdogo,hizi ML 700 za Bush ni chambo au ni roho nzuri yake? sijapata jibu. lakini hata iweje bado ninamshuru kwa msaada mkubwa alio utowa, kama zikitumika vizuri zitaokoa watu wengi. MBUMBUMBU

    ReplyDelete
  12. Kuna mtu kauliza kuhusu nguo za mama wa kwanza, watanzania tatizo ni kutothamini vya kwenu hiyo kanga ina ubaya gani jamani au mlitaka avae masuti ya kizungu. Halafu hapo mwenzenu kapanda chati kaonekana yuko simple hana makuu amevaa nguo ambazo mji mzima wamevaa hana tofauti na raia wengine, maana hizo kanga na vitenge vimezagaa mji mzima.

    Kwanza kumvalia mzungu suti ni kujidhalilisha unaonekana kama huna asili yako. Waoneni wanaigeria wanavyothamini nguo za kwao na sie ni hayo hayo makanga na vitenge.

    Haya tena kuhusu JF siku moja nilisema mimi haya mambo ya udaku kuna siku watu wataenda kuisaidia polisi, tena kwenye internet mbona ni rahisi sana kudakwa maana ushahidi wote uko wazi wazi. Kutakuwa tu kuna uzushi wamezua tu huko. Jamani mtu ukilisema neno uwe na uhakika nalo ni la kweli na unalijua vilivyo ili siku ukiitwa kutoa msaada polisi bali usaidie kikweli kweli sio kupata kibano cha bure.

    Ndio maana mie huwa nasema mambo ya ngoswe muachie ngoswe mwenyewe uhuru wa habari una mipaka yake jamani sio kupitiliza! Ehe shauri yenu!

    ReplyDelete
  13. Huyu tandoori vipi? Amewashukuru kufanikisha ziara kabla haijatokea? Feb 10 ni jumapili iliyopita Bwana Misupu!!

    ReplyDelete
  14. Mtu aliyefaidika na ziara hii ya KICHAKA ndani ya BONGO si mwingine yeyote isipokuwa LOWASSA.Kuanzia sasa hakuna GAMUTU yeyote atakayediriki kupanua domo lake juu ya lowassa.Kila inshu itakuwa jinsi ya kusunda hivyo vijipesa vya YUECHIEI

    ReplyDelete
  15. Michuzi unajua habari zenu msipokua makini basi na historia itakua potofu hivyo hivyo...Hizi habari zitaingia kwenye kukifadhiwa...Sasa kama waandishi wa habari hampo makini si ndio mtandanganya vijuuu vyenu....Wakiingia kwenye kumbukumbu za kihistoria wengine wataona raisi wa US alivisi bongo sijui tarehe gani mpaka 10 february ...........huoni kuwa utawakuwa muwajibikaji kweli....kama hata tareheh ni shida kuandika za kweli ...je hayo mengine tusio na uwezo wakujua fact zake?????

    ReplyDelete
  16. bY BaNguSiLO


    BUSH NDIYO MWANAMUME WA DUNIA BWANA,HAKUNA FYOKOO WALA NINI.NINGEKUWA NAUWEZO NIWA CONVINCE WAMAREKANI WABADILI KATIBA ILI BUSH AWE RAIS WA MILELE ILI TUFAIDI VIZURI ILE INAITWA UGAIDI POLICY.
    nani anabisha hapa?

    ReplyDelete
  17. Wabongo nao kahela kenyewe hata uwanja wa wembley (£757mil) hakajengi. Kelele kibao. Hiyo ni pre paid. There is no free lunch in this planet earth!

    ReplyDelete
  18. Sir ISSA HABARI ZA KAZI MAALIM..NAONA MGENI AJE "..MEWNYEJI AFAIDI.."..LAKINI KUNRADHI JAMANI.."..KULA NA KULIPA NDIO MTINDO WA KISASA.."

    ReplyDelete
  19. wewe unayesema wabingo bwana hata kaela!!wewe mwenyewe hata dola 300 huna,,,acha wabongo wajirushe na walichopata wewe inakuuma nini?hivi kwanza umejenga choo kwenu wewe?unalinganisha eti na uwanja wa wembley!!acha nyodo wewe
    mdau norway

    ReplyDelete
  20. bush hana shida a mafuta YA TZ . Bill G naye anapenda kusaidia Tz. Jay Z naye kaja Tz hivyo ni kiutu cha kujivunia kuwa maskini sis tunatambulika kwa umaskini wetu na uzuri wetu wa asili, utaona msururu wa watu kutoka Hollwood waakuja kucheza movie Tz, unatona B. gates anaongeza misaada hasa kwenye malaria na HiV. Thanks God, acheni majungu chapeni kazi alichofanya bush ni voluntourism and cultrural tourism and safari tourism. tz is one of the top destination in Africa,

    ReplyDelete
  21. watu wengine wana akili za paka.Eti Bush ni mwanamme wa dunia.Hivi hujui haya mambo yanafanywa na kila mtu anayekuwa rais wa marekani na si Bushit pekee?Hata hapo mwakani kama Obama,H.Clinton nk mmoja wao atakuwa Rais wa marekani anaweza kufanya mambo kama haya?

    ReplyDelete
  22. According to the American Ambassador, Mr. Mark Green, President Bush’s visit to Tanzania will stimulate investment because for four days the world media would focus on Tanzania. Of course, Mr. Green dismissed claims about Bush’s keen interest to station AFRICOM in Tanzania. Instead, Bush’s noble intentions include intensifying the fight against malaria and Aids. To this end, Tanzania will receive $818.4 million to fight Aids. During the visit, Bush would also highlight his country’s commitment to improving health in Africa. In summary, the iron spine of the argument justifying Bush’s trip is economic gain, both, actual and prospective.
    Unless if Tanzanians wish to fall prey to racist reasoning, Mr. Green’s story is nothing but an attempt to disguise ignoble motives beneath a glittering façade of altruism. Why should Mr. Bush be so concerned about improving the health condition of Tanzanians and at the same time use the most sophisticated weapons to kill and maim, with zest and ruthlessness, the Iraqis and Afghans and now the Somalis? Why? Is it because we are black and they are Arab? In his recent State of the Union Address, Mr. Bush, amid cheers from his sycophants, vowed to heighten his hawkish policies world wide. And yet, Mr. Bush is so kind and altruistic to Tanzanians. Why? Of course we know from history that even the sordid intentions of tyrants are always dressed up in glowing principles. Hitler occupied Czechoslovakia because he wanted to promote peace and social welfare for all; Mussolini invaded Ethiopia because he wanted to liberate the savages; Japan invaded China to create an earthly paradise; the US and UK invaded Iraq because Saddam Hussein had Weapons of Mass Destruction; and so on and so forth.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...