kila kukicha ujasiriamali mpya unaibuka bongo. safari hii ni suti maalumu za harusi ama hafla yoyote maalumu aina ya tuxedo na vikorokoro vyake na nguo za bibi harusi na wapambe toka marekani zipo za kukodi. unachukua alhamisi unarudisha jumatatu kwa bei poa. jamaa wapo duka la winwin (zamani supamaketi ya imalaseko mbezi bichi, tangi bovu. namba zao zipo kwenye kadi hiyo hapo juu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Huu ndio mwanzo wa kuambukizana ukurutu..!
    LOL

    ReplyDelete
  2. hapo kwa wabongo tunavyopenda mtelezo. Unadhani hao jamaa wanaokodisha ukirudisha hujaifua na haina doa watafua, sasa ugonjwa wa ngozi.

    ReplyDelete
  3. Safi sana vijana we have to be creative in this world to remain relevant....

    ReplyDelete
  4. mimi dungayembe ndo itakuaje sasa ??? mbona wana ni diskriminet hivyo aaaiiii

    ReplyDelete
  5. Nawaona Mr & Mrs Mshana (Devotha Nyambo na Rogart Mshana)Hongereni kwa kufunga pingu za maisha.

    ReplyDelete
  6. Anonymous 1&2,

    Wala hakuna wasiwasi wa usafi. Kwanza waazimaji wala hawatakiwi kuzifua. Wajibu wa kuzifua ni wetu sisi. Ni wajibu wa Signature FormalWear kuhakikisha Suti hizi zinatunzwa katika usafi wa hali ya juu. Sasa hivi tunashirikiana na the best DryCleaning Service in Dar kuhakikisha usafi ni priority yetu ya kwanza.

    Karibuni wote!!

    Signature FormalWear (SF) Mgmt
    Tel-0786948360; 0753048151

    ReplyDelete
  7. Anonymous 1&2,

    Wala hakuna wasiwasi wa usafi. Kwanza waazimaji wala hawatakiwi kuzifua. Wajibu wa kuzifua ni wetu sisi. Ni wajibu wa Signature FormalWear kuhakikisha Suti hizi zinatunzwa katika usafi wa hali ya juu. Sasa hivi tunashirikiana na the best DryCleaning Service in Dar kuhakikisha usafi ni priority yetu ya kwanza.

    Karibuni wote!!

    Signature FormalWear (SF) Mgmt
    Tel-0786948360; 0753048151

    ReplyDelete
  8. Huu sasa ubahiri, yaani siku yako muhimu ya maisha ukakodishe suti!!? Suti yangu niliivaa mpaka ikachakaa na mke wangu nguo za harusi mpaka sasa hivi ziko kwenye kabati kama kumbukumbu, miaka kumi imepita sasa na tuna watoto.

    ReplyDelete
  9. Wabongo tuache ushamba ......
    huwa vitu kama hivi vina mikataba unarudisha vinafuliwa au vinapelekwa dry cleaner kwa ajili ya matumizi ya baadaya .
    Mimi binafsi nawafagilia hawa coz mtu unaweza kusave hela nyingi ktk harusi hasa ukizingatia hizi extended family zetu .
    Mko kumi ndani ya nyumba ..kla mtu umshonee suti ..roughly 50,000 pear head ...you end up with 500,000 wakati ukikodisha hiyo suti within couples of days hata moja ya tano ya gharama haifikii ..
    Umefika wakati kwa wabongo kuwa creative on business ..
    keep it our brothers ..
    Mdau , Okinawa

    ReplyDelete
  10. That was my idea...lakini wameniwahi...si mbaya tukiwa na vitu kama hivi..imefika muda wa kusave gharama zisizo na mpango...nguo ya harusi mtu anavaa siku moja....it is a shame wanaokandia hii biashara...

    My sister gauni lake walikua wanaazima majirani na marafiki mpaka sasa hivi limechakaa na lilikua likirudishwa wala sio kuwa wameliharibika ...sasa kama kuna kitu kama hiki steady ...why not....it is about time

    hayo magauni yalivyo makubwa ...kuna ubaya gani wa kurent na kulirudisha....Watu wengi vijana wanaoa wanaishi kwenye vyumba au nyumba ya kupanga...Kuhamisha hilo gauni kila mnapohama it is not a joke kama unataka kulikeep vizuri linachukua nafasi saaana tu...na kam hulihifadhi professinal baada ya miaka kadhaa kitambaa kinabadilika rangi na lina katika...so why waste your money on a thing that eventually utaishia kulitupa..Kuna heirlooms nyingi tu kama unataka kupass kwa generetion yako....?

    Good job guy ....I am following your steps soon I hope mta frinchise...hahahahah....

    ReplyDelete
  11. Hongereni sana kwa ubunifu wa hali ya juu mliouonyesha. Tanzania, tunahitaji mambo kama haya. Labda tu niwape changamoto, itakuwa vyema endapo mtaweza kuwa na tovuti yenu ambayo itaonyesha "designers" ambao tuxedos zao mnazo. Kwa sisi tulioko ughaibuni itakuwa imetupunguzia adha za kusafiri na tuxedos na kurudi nazo tena huko. Hongereni sana!!

    ReplyDelete
  12. Huu Utamaduni wa kukodisha nguo unatoka wapi??

    Hii ni siku muhimu, inabid uwe na kitu cha kumbukumbu,

    Tukiendekeza haya mambo itafikia siku tutaanza kua na;
    BIBI HARUSI WA KUAZIMA,

    VIATU VYA KUAZIMA,

    KEKI YA KUAZIMA,

    WAPAMBE WA KUAZIMA,

    WAHUDHURIAJI WA KUAZIMA,

    PADRI/SHEKHE MFUNGISHA NDOA WA KUAZIMA,

    VYAKULA VYA KUAZIMA,

    VINYWAJI VYA KUAZIMA,

    NA KILA KITU CHA KUAZIMA,

    Baada ya harusi, wanandoa hawana hata kitu cha kwo wenyewecha kujivunia,

    TUACHE UBAHILI

    ReplyDelete
  13. Jamaa

    Asante kwa changamoto yako mzuri.

    Pengine labda inabidi tuelimishane vizuri zaidi. Kama baadhi ya wachangiaji walivyosema, siku ya harusi ni siku ambayo utokea mara moja katika life time. Sasa basi, kutokana na kuwa such a special day, vitu vingi tunavyojihusisha navyo siku hiyo huwa hatuwezi kuvirudia tena katika siku za kawaida. Mfano halisi wa vitu hivyo ni mavazi.

    Pia naomba ukumbuke kwamba utamaduni wa kukodisha nguo za harusi haujaanza leo katika jamii yetu. For decades, mabibi harusi wamekuwa wakiazimana magauni ya harusi na mashela. Kilichokuwa kinatokea ni uazimishaji usiokuwa rasmi...mabibi harusi walio bahatika kununua magauni ya harusi, walikuwa wanajiingiza katika biashara ya kuyakodisha magauni yao mara harusi zao zinapopita. Mpaka leo hii kuna maduka yanayouza nguo za harusi ambayo yanatoa option ya kuzikodisha. Kwa hiyo hili sio jambo geni. Tulichofanya SF ni kutanua biashara hii na kuwakidhi mabwana harusi pia...kwa kusupply suti zao.

    Kwa kumalizia tu, naomba tujulishane kuwa option ya kununua ipo pia. Kwa hiyo kama kuna mteja ambaye angependa kununua badala ya kukodisha, anakaribishwa pia.

    Tusonge mbele na nyakati wandugu..

    Karibuni wote!!

    SF Mgmt
    0786948360; 0753048151

    ReplyDelete
  14. Anonymous wa 11:41,

    Asante sana kwa support..

    Utengenezaji wa tovuti ni mmoja wa mipango yetu ya karibuni.

    Asante.

    SF Mgmt

    ReplyDelete
  15. Jamani, vikwapa vya Bongo halafu mnashea suti! Utakuwa unanuka jasho la mtu mwingine! PWEEE!

    ReplyDelete
  16. Ukweli kwa hali halisi ya Bongo baaaado sana kuanza ku-rent nguo tena za harusi. uSAFI NI KITU CHA KUZINGATIA SANA NA SIJAONA KAMA MNAWEZA KUZINGATIA HILO.

    ReplyDelete
  17. Jamani, wahusiika wameshasema wao ndio wenye jukumu la kupeleka nguo hizo kwa dry cleaners, sasa huyo mtoa maoni vipi aulize hana uhakika wataweza kuzingatia hilo.

    Jamani, swala la kukodisha nguo liko kila mahali. Si Marekani, si Uingereza si nchi yeyote ambako watu wana mapesa yao ya uhakika tu kununua nguo mpya. Bottom line, kwa nini uingie gharama wakati unaweza kusevu kwa kukodisha na kutumia pesa yako kufanya mambo mengi ya maana. Pia inasaidia kuwasakama watu na michango. Besides, unapata nguo za uhakika na pia hutabakia na swala la utunzaji baada ya sherehe.

    Mtao maoni aliyepita amenifurahisha kwa kusema kuwa kwanza ni tabu kama mtu wahama toka nyumba moja ya kupanga hadi nyingine. Ni kasheshe tupu kubeba nguo hizi za harusi kwa namna ambayo hazitaharibika.

    Na kama tuxedo, ni nguo unavaa mara moja moja tu, sasa kwa nini zikae zinaota ukungu wakati kuna watu wanaweza kukukodishia nguo za uhakika, zilizo on fashion na safi wakati wote? Wake up people!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...