simba akiwa amejichokea kwa upweke wa muda mrefu
watalii wa ndani wakiambulia kuona majabali na nyasi
watalii wakijiuliza cha kufanya
mtalii akilalamikia uchafu wa jaketi la usalama ambalo linaonesha halijafuliwa mwaka sasa
sehemu za kisiwa hicho ambacho kikitunzwa na kushughulikiwa ipaswavyo ni kivutio kikuu kwa watalii wa ndani na nje

swala wawaili ambao ni kati ya wanyama watatu tu waliosalia kisiwani humo, ukiongeza na simba. haijulikani wahusika wanawaza nini kukiendeleza kisiwa hiki ambacho zamani kilisheheni wanyama na ndege kibao kiasi cha kuvutia watalii kibao wa nje na ndani ya nchi. maoni ya wengi ni kwamba endapo wameshindwa wampe mwekezaji apaendeleze kuliko kupaacha panadoda...



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. michuzi naomba unichekie dili mi nataka kukinunua hiki kisiwa, nimetunza vihela fulani vya box naona hii itakuwa investment nzuri

    ReplyDelete
  2. We anony wa 11:24 mjinga au nini?hata ukijiuza mnadani mara millioni mia huta weza kununua hicho kisiwa kwa sababu...'every inch belongs to the the people of Sovereign Tanzania'.

    ReplyDelete
  3. Nasikia kulikuwa na mbuni hapo,je wametoroka kwa sababu ya njaa?ah siwalaumu kwani si hata wabeba maboksi wametoroka kunyemelea ughaibuni!!!

    ReplyDelete
  4. MIMI NI SHAHIDI WA HILI. MWAKA JUZI NILITEMBELEA HII HIFADHI.

    WAKATI NAFIKA KATIKA OFISI ZAO KUFANYA TARATIBU ZA KWENDA MBUGANI MAELEZO NILIYOPEWA NA NILIYOYAONA HUKO YALIKUWA MAMBO MAWILI TOFAUTI.

    NILIPEWA TAARIFA KWAMBA NITAPATA FURSA YA KUMWONA SIMBA, TEMBO, SOKWE, NA BAADHI YA WANYAMA WENGINE KAMA VILE FISI, TUMBILI NA SWALA.

    SIMBA:
    NILIPEWA TAARIFA KUWA SIMBA AMEPELEKWA DAR KATIKA MAONYESHO YA SABASABA. TAARIFA NILIZOPEWA NI KUWA SIMBA YULE NI MMOJA TU NA NI DUME NA HATA HIVYO AMEKUWA MPWEKE KIASI KWAMBA KITAALAMU ANAWEZA KUISHI KWA KIPINDI KIFUPI TU...

    HUYU SIMBA ALILETWA AKIWA NA UKUBWA WA PAKA MDOGO, NA ALILELEWA NJE YA BANDA MPAKA PALE ALIPOANZA KUKIMBIZA WATOTO NA KUWAANGUSHA NDIPO WALIPO MFUNGIA NDANI, JAMANI KWA KIFUPI SIMBA HUYU HAJAWAHI KUISHI NA JIKE, JE HUU NI UNGWANA NA NI SAHIHI KWA HAKI ZA WANYAMA?

    WADAU MKIONA BANDA LA SIMBA UTAOMBA MUNGU ASIWEPO, KWANI WAVU UMECHAKAA NA YULE SIMBA IPO SIKU ATAMRARUA MTU TU!

    WAFANYAKAZI PALE WANATUMIA VIFAA DUNI SANA KWANI NILIMKUTA KIJANA MMOJA AKITUMIA JEMBE LA MKONO KUZOA UCHAFU KATIKA LILE BANDA LA SIMBA, NILIKAA PALE KWA MASAA NANE NA MPAKA NAONDOKA HAKUWA AMEMALIZA!

    SOKWE:
    KULIKUWA NA SOKWE MTU AMBAYE ALIKUWA NI KIVUTIO KIKUBWA SANA KWA WATALII LAKINI KWA BAHATI MBAYA SANA SOKWE YULE ALIPOTEZA MAISHA NI HABARI YA KUSIKITISHA KIDOGO LAKINI KWA UFUPI ILIKUWA HIVI.

    SOKWE YULE ALIKWA MJAMZITO ILA KUTOKANA NA KUTOKUWA NA HUDUMA NZURI KUTOKA KWA WATAALAMU WALE WASIMAMIZI HAWAKUGUNDUA KUWA NI MJA MZITO.

    MPAKA ALIPOKARIBIA KUJIFUNGUA NDIPO WALIPOGUNDUA, WALIPOTOA TAARIFA KWA WATAALAMU MJINI MPAKA KUFIKA KUTOA MSAADA ILIKUWA TOO LATE...KWANI ALIKOSA MSAADA KATIKA KUJIFUNGUA NA MTOTO ALIPOTEZA MAISHA PAMOJA NA YEYE MWENYEWE.

    KWA KWELI INATIA HUZUNI KWANI SOKWE YULE ALIKUWA KIPENZI CHA WENGI NA ALIKUWA ANAPENDA SANA KUCHEZA MZIKI NA KUNYWA BIA ANAPOFURAHI.

    WITO WANGU KWA WAHUSIKA NI KUWA TUTHAMINI NA KUENZI VYANZO VYA MAPATO YA UTALII NA TISITHUBUTU KUVITELEKEZA.

    INAVYOONEKANA TUNAJISAHAU KATIKA HILI, EMBU NENDA BAGAMOYO NA UTASIKIA HUZUNI JINSI VIVUTIO VILIVYOGEUKA KUWA MAGOFU NA MAGENGE YA WAHUNI, ANGALIA MAKABURI YA WAJERUMANI, ANGALIA NGOME YA KWANZA YA WAJERUMANI, ANGALIA BANDARI YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA NCHI HII KABLA YA BANDARI YA DAR ES SALAAM, ANGALIA SEHEMU WALIYOKUWA WANANYONGEA MASHUJAA WALIO PINGA UTAWALA WA WAJERUMANI, ANGALIA GEREZA LA WANAWAKE, ANGALIA GEREZA LA WANAUME, ANGALIA PALE WATUMWA WALIPOKUWA WANAWEKWA KUSUBIRI MASHUA, NA KAMA HIYO HAITOSHI ANGALIA MJI WENYEWE!!!!

    ReplyDelete
  5. Hebu Viongozi wa Mwanza oneni AIBU katika hili!Hizi kelele za kuendeleza Utalii nchini,ni danganya toto au?Kisiwa hiki ni kizuri na kingeweza kuwa kivutio kikubwa sana kwa watalii wa nje na hususan wa hapa nyumbani.'Dont forget,Pleeeeeeeeeeeeeaaase,The role of our Government is to create an enabling investment environment!Serikali hatutakiwi kujiingiza katika Biashara.Kazi hiyo tumewaachia sekta Binfsi.Sisi tumesha weka mazingira safi ya uwekezaji.SAFI YA WAPI?Mbuzi hawa!Ila katika Vijimikataba vya uwekezaji mtatusamehe,serikali bado itaendeleza libeneke.Kama unavyo jua sekta binafsi bado iko changa sana,hawawezi negotiations!Ama kweli tutafika.Vision 2025!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...