Haya wadau,

nimejaribu kutafakari niliyoyasikia kwenye vyombo vya habari hapa kwetu lakini bado nadhani moyo wangu haujapata jibu kamili…naomba na nyinyi wadau wangu mniambie vipi kuhusu hawa wasanii matajiri hapa kwetu Tanzania?


WASANII HAO NI HAWA HAPA NA THAMANI ZA RASILIMALI ZAO

1; LADY JAY DEE - MILLION 500

2; JUMA NATURE – MILLION 300

3; BANANA ZORRO – MILLION 280

4; MATONYA - MILLION 180

5; FEROOZ - MILLION 140

6; PROFESA JAY - MILLION 130

7; STARA THOMAS -MILLION 80

8; AY -MILLON 60

9; KLYNN -MILLION 45

10; MWANA FA - MILLION 30

HAYA KAZI KWENU


Mdau Ngwega (pichani,mbele)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 77 mpaka sasa

  1. kulalalalalalalalalalalalambegeze michuzi unapenda ligi kweeeeeli kweeeli, unataka tuache box sasa tuje kuimba bongo flava si ndio???

    ReplyDelete
  2. Jamani,ufisadi hata kwenye habari?

    ReplyDelete
  3. lady jd ana worth 500 tsh millions??? kesho naenda kumtukana supervisor tena na beef nae ananibebesha box ka mtumwa, halafu naacha box najiunga na bongo flava
    michuzi nihakikishie usilostishe maisha yangu babu nisije kikauvaa mkenge

    ReplyDelete
  4. Hiyo habari nahisi sio sahihi. Kama ni sahihi, je wametumia vigezo gani? Na kama wanazo kumbukumbu zao za mapato na matumizi, je wanalipa kodi? Pia kama kuna ukweli katika hilo basi nahisi watakuwa wanafanya na biashara nyingine zaidi ya usanii.

    ReplyDelete
  5. Hakuna milionea hapo, wote tunawaona mbona wamechoka? lady jaydee angalau, naye si milionea bali anajiweza kimaisha

    ReplyDelete
  6. sasa hiyo mil 500 ya jide kutokana na ile hiace ya kuchorwa au vipi lakini hiace si $4000 tuu dubai kama angekuwa na hizo si Gadne angekuwa na redio yake

    ReplyDelete
  7. Hiyo Nature labda ni vipisi vya bangi vilivyoingia mwilini mwake

    ReplyDelete
  8. Samahani wadau!! hizo milioni zilizotajwa hapo juu zipo benki kwenye akaunti zao au ndiyo thamani za hiace, magitaa, computer zao, gari zao za kutemb elea, majeans yao pamoja na nyumba zao au kuna project kubwa ambao hawa wasanii wamawekeza? Niambieni vigezo vilivyotumika kupata hizo milioni walizo nazo.

    ReplyDelete
  9. Huyo Klyn labda kama wamethaminisha private assets zake alizopewa na mungu atafikia 45Million. Mbona hana kitu jamani? Hana gari wala nyumba na anakaa kwa baba na mama mpaka leo. Hizo 45 Mil zimetokana na nini?

    Mauzo ya album yake ni kama milioni 16 hivi na distributor alichukua mmilioni 9 na studio iliyotengeneza ilikula milioni 4.
    Embu tuambiane kama hili ni changa za macho?

    ReplyDelete
  10. Hizo millioni ziko kwenye account zao au? maana bado sijaelewa, kwasababu kuna wasanii wengine hapo bado wanaishi nyumba za kota na ukiwaangalia wengine hayo mabenzi wanayoendesha ni ya mwaka 47. Naomba Ufafanuzi TASAVALI.

    ReplyDelete
  11. wamepata hizi hela kwa kuuza cd au wameiba wapi, kama masoko ya cd yangekuwa kam huku ughaibuni basi ningalikubali lakini mimi naangali kwa makini siyakatai lakini pia sikubaliani nayo

    all the best

    ReplyDelete
  12. wewe unaishi zimbabwe? unachanganya

    ReplyDelete
  13. million 500 za kusifiwa na sio za kweli msitishike jamani wala kuacha box,na ukiuliza ana invest vp pesa yake hakuna ni kuimba tu,poa sana naona ray c wamemuacha kisa anakatika sana na ananata sana eti ana 5m tu,sio kweli mgongo wake tu una bima ya 10m na mwili wake ni kama 100m sasa hatakosa vp si ndio shakira wa bongo na ana boutique,saloon,table dance club,na kama una 1m unapata one night stand,tz shwari jamani

    ReplyDelete
  14. Wametumia vigezo gani kupata hizo thamani za hela?Watu kama Forbes magazine wana criteria zao zisizo na kwere... Huchelewi kukuta wamepiga evaluation ya hata magari. Anyway, looks muziki unaanza kulipa Bongo...

    ReplyDelete
  15. Ha,ha,ha Basi kachemsha maana box haachi mtu. Ila nimashaka na Ferooz maana nilisikia kuna siku za karibu alikosa hata Nauli ya kurudi bongo akitokea Uganda baada ya kutiwa mchanga wa macho na Promoter wa Onyesho aliloenda kutumbuiza huko. WASANII WENGI- NO COMMENT

    ReplyDelete
  16. mmmmmmmmmmm ni kweli sikubali basi kesho naanza kuimba,Inabidi niache kazi ya kulea wazee.
    Rose Norway

    ReplyDelete
  17. Ni kigezo gani mmetumia kujua wana kiasi gani kwenye bank?

    ReplyDelete
  18. First of all nawapongeza hawa wanamuziki kwa kazi yao.Lakini these figures are so unreal,I mean how do they value their wealth,based on what:Album sales,Copy rights,Tour/Concert sales,Ringtones,Shares ama kitu gani?

    ReplyDelete
  19. Hiyo sio kweli next hiyo hela ni ndogo sana.Mi namjua mtoto mwenye tsh 3bis anauza mawe na yuko 24yrs old

    ReplyDelete
  20. hizo data umepata wapi? michu sometime post kama hizi unazipotezea, hao washkaji wengi wao life zao tunazijua, kutuambia mtu kama ferooz anautajiri wa 140m wakati anakaa kwa washua wake ni vichekesho istoshe jeep yenyewe kaiuza, data mnatoa wapi? na haya mambo ya kuitana matajiri wakati hata hamlipi kodi ni kuzinguana...2pac alisema i wanna pay rent when rent is due, lkn hao washkaji kazi kuombana biere tu club..siyo issue..haimake sense ferooz sijui kuhusu matonya awe juu zaidi wakati watu kama dady, ay na fa wapo juu sasa esp ay ambaye ana clothing line ambayo nasikia inafanya vema sokoni, vp kuhusu ray c, tid wenye mashow kibao mbele wapitwe na stara ambaye kitambo hatujasikia tungo zake??? ni mtizamo wazee lkn tuache kuzinguana, mkatutia mdadi wa kurudi huko na kuacha bata huku kwa joji kichaka teteteteeee

    ReplyDelete
  21. Doh!!,yaani T.I.D mbwembwe zote alizo nazo hata ktk top 10 ya wasanii matajiri hayumo!!!yaani stara yupo juu ya T.I.D,kweli noma.

    ReplyDelete
  22. 500m?????? MICHUZI HAUKO SERIUOS

    MAISHA YAO MBONA TUNAYAONA HAWANA HATA VITEGA UCHUMI MFANO KUNUNUA SHARES(HISA) KUFUNGUA MIRADI MBALI MBALI KICHA WAKO BAAA HWANA HATA WANASHERIA,DOC,WASHAURI,HIYO 500M SI MCHEZO KWA BONGO

    ReplyDelete
  23. Issa Michuzi mie yangu macho. kama kweli vizuri kwao ila lady jaydee kidogo naweza kukubali yuko makini na market zake, Tanzania mauzo wanaibiwa na wahindi kama wanahesabu nyumba zao nam agari yao sawa. lakini unambie kwenye bank wanazo hizo ni uongo mtupu. T.I.D vipi hayupo na Ray-C mie naona wengine wanatumiwa kupitisha UNGA tu Airport zetu wanakatiwa mshiko na baazi ya ma MP jamani tuweni makini kabla kusifu uongo. anayeingiza pesa Producer na muuzaji CD's Tanzania.

    ReplyDelete
  24. wabongo kwa chuki binafsi na wivu tunaweza kubeba kombe duniani kwani cha ajabu ni kipi mtu kuwa na 500m wenye wivu wajinyoke na kila mtu na bahati yake ala?
    we kama huna umiza kichwa ufanye nini sio majungu na kama hutaki basi kaa hivyohivyo na mdomo wako

    ReplyDelete
  25. HIYO LIST MBONA R C HAYUMO???

    ReplyDelete
  26. JAMANI SIJAELEWA SASA KAMA UNATHAMANI YA HELA HIYO MBONA WANAISHI KWENYE UNFINISHED HOUSES MATOFALI YANACHUNGULIA NJE.MIMI NI WAZAZI WANGU WANAFIXED ASSETS ZA THAMINI KUBWA SANA NIKIPIGA HESABU NDIO LABDA KUKARIBIA HUKO HUKO NA SASA NASHINDWA KUELEWA HUYO JAYDEE ILE NYUMBA NA AU MLINZI AU GARI NDIO THAMANI YAKE AU

    ReplyDelete
  27. Ah! Lakini tusishangae sana maana bongo ukivaa dhahabu ni tajiri, ukinunua gari ni tajiri, ukijenga nyumba ya kawaida ya kuishi ni tajiri hata nguo unazovaa ni pia ni utajiri. Hii ni ajabu sana. Inawezekana ndivyo walivyoviangalia. Halafu wanamziki wetu wanapenda sana kujilinganisha na na wanamuziki wa marekani. Hapa bongo musiki bado kabisa hayo tunayoimba ingekuwa kanisani ningesema mapambio. Hata zaire hatuwafikii, south ndo kabisa. Anyway kama tumeamua kupakana mafuta kwa migongo ya chupa ndo hapo sasa. Wacheni wavimbe mibichwa lakini mi naangalia hivi akina temba nao hawana kitu? Craz GK naye je?

    ReplyDelete
  28. data hizo si kweli kwani hata kwa data za prime time promotions ambao ndio humega sehemu kubwa ya mgao huu , bushoke aliuza kuliko jd.na hakuna mtu atakupa data za kweli kwa ajili ya ufisadi wa all the players, primetime wasambazaji ka GMC wote ni wa kwepa kodi wakubwa.Kama wanabisha wajitokeze watuambia true statistics

    ReplyDelete
  29. THAMANI YA RASILIMALI ZAO = ardhi, nyumba, magari, fedha nk. Kwa Tz nadhani hata nguo na vipodozi wamehesabu.

    ReplyDelete
  30. Waaungwana huyu michuzi anawachongea hawa watu jamani si balaa hiii?

    ReplyDelete
  31. Hongera zao hao wasanii mamilionea.
    Haya na nyie ndugu zangu wabeba mabox wala msitishike sana na kutaka kukimbilia bongo. Kumbukeni hizo pesa za wasanii hapo juu ni madafu, sio US dollars au Pound Sterling. Kwa mfano hiyo million 30 ya Mwana Fa ni sawa na pound elfu kumi na mbili (12,000) za UK. Haswa nyie mlioko Uingereza endelezeni sana libeneke maana ukija na mshahara wako wa mwezi mmoja hapa bongo wewe ni milionea. Kitu nachowashauri ni kuwa bebeni sana hayo maboksi na ku-save kila mwezi huku mkikumbuka kujenga/kununua nyumba nyingi muwezavyo huku bongo. Si mnajua tena huku nyumba ni bei nyanya tofauti na UK. Na siku hizi nyumba Dar zinalipa kichizi, unavuta pesa kiulaini. Na nyie mlionunua nyumba za mortage miaka iliyopita huko mkiamua kuziuza sasa uongo maana hiyo profit ndogo mtayopata na kuamua kuileta bongo hata huyo Lady Jay Dee haoni ndani.

    Asante sana kaka Michuzi, nakutakia weekend njema.

    Mbeba maboksi mstaafu

    ReplyDelete
  32. Huo ndo uzushi haswa. ingekuwa baadhi ya hao madogo siwajui sawa. hapo naona ni mtu kaamua kutafuta attention tu. Yani kijana wa kiswazi awe na tuseme 300m halafu kuwe na amani uswahili,Haiwezekani. Hapo naona ni changa la macho hapo. Nafikiri huyo lady J walikuwa wanamaanisha 500K

    wenger

    ReplyDelete
  33. kiukweli hapa bongo ukiwa na njenge basi ww ni mkali na tunaamini tayari uchumi wako ni mzuri nimebatika kuona nyumba ya JD ambayo value yake inaweza kuwa 150 milioni Professor J 100 milion Banana zoro 80 milion kwahiyo ukiwa na nyumba ni heshima kubwa lakini ukweli awajaweza kuingia katika sector ya investment ambayo wao inaweza kuwatoa na wakafika mbali kwani pesa zao huwa kama za msimu lakini dada judith Wambura anakwenda vizuri na wengine wanafuatia lkn walio wengine wamewekeza kwenye pombe, mademu,na kubadili magari kwahiyo hizo juu data sio sahihi kabisa

    ReplyDelete
  34. TWAAAAAT!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  35. mh, hamna kitu kam hicho labda biashara haramu pia

    ReplyDelete
  36. BOLA MIMI SIJASEMA

    ReplyDelete
  37. Habari za masiku wana blog! Hongera Lady JD kwa kuweza kuwa na hiyo fortune ya 5oom.Lakini kwa upande wa pili bado na hoji kuhusu Gadna,NAELEWA NI SUALA BINAFSI ZAIDI, inakuwa aje anaendelea kuwajibishwa kwa kazi ya 80,000/=pm.Kwanini asijikite na mke wake wakafanya mambo yao zaidi hasa ktk fani hiyo ya Music.kwani hata Gadna ana knowledge kubwa sana ktk masuala ya music kwani hata huko nyuma alisha wahi kumiliki KIBANDA CHA KUUZA CDs.Au Marriage Contract terms haziruhusu FINANCIAL ENGAGEMENT.

    ReplyDelete
  38. Sasa kama na $ laki tano mbona ana nyumba ya $30,000? ...mtu mwenye hela kama hiyo bongo angetakiwa awe na vitega uchumi vingi tu na nyumba i we na vitu vya maana...makochi tuliyaona ya $2000...na ile nyumba kama yangu nimejenga bongo na mimi ni mbeba boz nimetoka shule mika minne na nusu iliyopita....sasa kama kweli ana hizo hela something is wrong with her....bongo hela kama yake angekua hata na usafiri mzuri....Maybe I am wrong lakini it sound a little fishy...

    ReplyDelete
  39. Michuzi baab kubwa,

    Hii taarifa imetulia sana,

    Please tupatie list zingine kama za wanamuziki wa 'jazz band' matajiri.

    pia utuletee na list ya wachezaji mpira matajiri.

    Mbona kwenye hiyo list Fresh Jumbe hayumo?

    Michuzi na wewe pia ni milionea kwani hata kule kwa Mugabe kila mtu ni milionea.

    ReplyDelete
  40. Weeeeeeeeeeee haiwezekani...Kylnn worth more than Ray C na T.ID na AY??...PLZ gimme a break. Michuzi fanya utatisi mzuri kisha tuletee data manake siamini hata moja hapa..

    ReplyDelete
  41. sasa wanalipa kodi hizo

    ReplyDelete
  42. wabongo utawajua tu! always negative mind, sina hakika na hiyo statistic ya kiwango cha fedha cha wasanii waliotajwa hapo juu...lkn napenda tu tujue jamani kuwa sio kwamba kwa kuwa wao ni wanamuziki basi wabweteke na hela ya mauzo ya music bila ku invest na kufikiria activities nyingine. naweza kuona jinsi jitihada za AY katika kujijasilia mali na sitashangaa kusikia kama ana worth ya that amount.....Hlf kitu kingine cha kushangaza, mbona wabongo hamuhoji wanamuziki wa mamtoni wanaothaminishwa utajiri wao kwa kuangalia assets walizo nazo plus hela ya bank? tufikie wakati sasa tukienda ulaya tusome na utafute kazi za maana, hizi za kupiga BOX zinatufanya tuwe na negative minds kwa kila kitu kwa sababu ya Inferiority complex..tunakuwa wazembe wa kufikiri mpaka tunaona kila kitu hakiwezekaniki....bongo ya sasa sio ile ya kukusanya vijipaund kwa miaka miwili baada ya box la ASDA na kuja kutesa bongo kwa wiki mbili..muamke otherwise kila siku mtakuwa mnakuja bongo hlf mnakimbia baada ya siku 2...bongo ya sasa si ya kumuogopa mtu anaeongea kizungu..tunavalishwa na wachina sawa lkn at least tunaishi maisha yenye dignit..sitaki kuwalaumu sana maana wengi wenu kutokana na knowledge ndogo hamuwezi kupambana bongo...niwapongeze wote walio mamtoni na wanaojua maana ya shule na wale wanaofanya kazi intelectual na professional....muwaamshe watanzania wenzenu waliolala huko na kuamka kila siku kwenye blog ku critisize

    ReplyDelete
  43. Nyumba ya Lady Jay Dee tumeonyeshwa na sasa twaambiwa ana hizo pesa. Ama kweli pesa za madafu....

    ReplyDelete
  44. kwanza kabisa napenda kusema kuwa sina imani kuwa habari hii ina usahihu wa 100%. Lakini pamoja na hayo kuna vitu vichache nataka kusema.
    1. Unapozungumzia kipimo cha utajiri iwe Bongo au mtoni, huzungumizii hela katika akaunti. hela iliyokaa tu katika akaunti haina maana, faida ya utajiri ni kuwekeza utakapokuwa na kuongezeka. Hivyo suala la mtu kuponda eti wamehesabia nyumba/magari, n.k. ni upuuzi, kwani hizo mali zote ni sehemu ya utajiri.
    Mtu kama Nature najua kuna kipindi alipoibuka akapata hela zake aliwekeza katika viwanja/nyumba kadhaa na thamani ya viwanja sehemu nyingi Bongo imepanda sana katika miaka michache iliyopita.

    2. Wasanii wa Bongo utajiri hawapati katika mauzo ya CD maana wanaibiwa sio na wahindi tu, hata na sisi wengine tunaoendeleza libeneke ya kunakili CD na kuweka MP3 zao katika mtandao bila ridhaa yao na kulipia. Hivyo wengi wanategemea kupata mapato kutokana na show. Jide najua kuwa anakamata bingo ndefu kwa gig yake Peacock hotel.

    3. Umaarufu wa msanii haumaanishi utajiri. Inategemea mauzo yako ya CD na show,, n.k. Inategemea hela zako ulizopata umetunza au umetanulia zote. Na inategemea una vitega uchumi gani nje ya kuimba. Mfano P-Didy, Jay Z na Master P Marekani amabao wamewekeza hela zao katika biashara nyingine nje ya muziki. Hivyo suala la fulani mbona hayupo katika list hii wakati ni maarufu sio hoja, inawezekana anazidiwa ujanja na hao walio juu yake.

    4. Inanisikitisha sana kuona tabia ya kuchukiana na kupondana tuliyo nayo wabongo. Wanamuziki waliotajwa hapo hawajiandika wao, habari kaandika mtu mwingine. Kama una mashaka na usahihi wa habari hiyo mkosoe mwandishi sio unaanza kuwaponda hao wanamuziki kuwa fulani yuko hivi, fulani yuko vile.

    5. Bongo flava imepiga hatua kubwa katika miaka ya karibuni na wasanii wengi (lakini sio wote) ambao uongo mbaya kwa maisha yetu ya Kibongobongo wanajiweza angalau. Sisemi kuwa wana mamilioni ya hela zilizotajwa hapo juu; ila angalau mtu ana kibanda somewhere, maybe kausafiri kidogo na hela ya pamba, n.k.

    6. Sidhani kama takwimu zilizotolewa hapo juu ni sahihi (angalau kwa baadhi ya wanamuziki), lakini sina ushahidi wa kubisha. Lakini sidhani kama ni busara kuanza kupondana na kuiponda Bongo yetu na umaskini, n.k.

    Mwisho nawatakia mema wasanii waliotajwa na kama bado hawajafikisha thamani ya fedha zilizotajwa hapo juu, basi wafanye itihada inshallah siku 1 labda watafika. Kama sauti ndio kipaji chako kwanini kisikutoe basi

    ReplyDelete
  45. wewe wa pili kutoka chini acha kuwa na akili finyu km unakula funza wa kuwa na mil 300 kwa hapa bongo hasa hawa wasanii wetu nani?unafanya masihara nn na huyo muhindi?katoa hela ningi kwenye album yako mil 30 ss hiyo 500 mbali na asset zako unafanya mchezo

    ReplyDelete
  46. jamani hiyo taarifa si kutoka kwa michuzi kuna gazeti moja hapa bongo linaitwa BAB KUBWA ni la udaku ndio wamefanya research yao wameona hao ndio wasanii wao.vigezo vilivyotumika ni kujuana kwa hiyo sishangai,limetawaliwa na masifa kwanza gazeti lenyewe so don believe everything u read in the papers

    ReplyDelete
  47. M500? Kwa hile nyumba ya bati na ambayo iko ka Xmas tree ama? Usitutanie Michuzi! Angekua na hizo m500 asingekimbilia Kimara kwenye viwanja vya bei rahisi.

    ReplyDelete
  48. Watanzania bwana sijui tupo vipi sasa kama ww huna pesa na huna deal ya kupata pesa hiyo basi kaa kimya kwa sababu hayo mambo ni yanawezekana kabisa. Halafu na hili swala la kubeba mabox jamani kazi ni kazi kwa hao wenzetu huku ndio maana walipata maendeleo angalia wenzetu China, Singapore, Korea, Japan nk watu huku hawachagui kazi ndio maana wanapata maendeleo. Mimi nimeshuhudia kwa macho yangu nilipokuwa Singapore jamaa ana degree ya utawala lakini anafanya training ya kuwa konda wa train na ana part job ya kufanya usafi katika hiyo station. nilipo muuliza aliniambia hawezi kukaa kusubiri kazi aliyosemea life hamsubiri kazi ikipatika poa. Nchi hizo zote nimefanya kazi kwa hiyo najua na nimebeba sana mabox nilipokuwa Wiingereza, nilikwa sichagui kazi labda ndio maana leo hii nipo hapa nilipo. Tufanye kazi kwa bidii Watanzania wanzangu tuache majungu.

    Mdau kwa sasa nipo Cameroon

    ReplyDelete
  49. ahahah samahanini sana kwa watu ambao hamjanielewa swala langu bado lipo palepale mimi nimepata habari hizi kwenye kituo kimoja cha radio ambacho ni maharufu sana hapa bongo...ndio maana nikaamua kuwajulisha na kupata maoni yenu..ila kwa imani yangu inaweza ikawa kweli..kwani hao wasanii kwa kwa mfano matonya ni msanii ambaye anafanya shoo nyingi sana ndani na baadhi ya nnchi za hapa afrika mara nyingi na vilevile nimeona maendeleo yake binafsi ambayo ameyapata kwenye kwenye music na anamiliki baadhi ya nyumba na magari na hata vitega uchumi....huyu tid kwa kweli huku nyumbani mi bado sijaona kitega uchumi chake chochote zaidi ya kung'aa tu na kuzulula huko ughaibuni.....kwa upande mwingine bongo kwa sasa ipo juu angalau baadhi yenu mnasema hata kama wanazo lakini sio ela ahahah kibongobongo sisi tunaona ni ela....kwa upande mwingine nashangaa sana kuona nyie baadhi ya watu wa uko ughaibuni kujiona mshayapatia....kumbukeni uku ni nyumbani na mnahitaji kupaheshimu....nadhani tumeelewana ....ni mimi mtoa maada ngwega

    ReplyDelete
  50. Watanzania kweli sie watu wa michapo yaani mtu na akili yako unaweza kuamini habari kama hizi...wanamuziki mashuhuri dunia ndiyo wenye thamani za 500m kama P.Diddy , JAY-Z , 50cent,Phatfarm ,JLO ....e.t.c hao watu wahapati hizo hela kwa kuuza album au concept... wana blend siyo chini ya tatu...sasa hao wabongo hizi milioni wamezipata wapi kwa kupiga muziki kwenye ukumbi wa ukonga bar halafu utegemea kukusanya milioni nyie watu mnacheza na hizo namba..
    in general income ya wanamuziki inategemea pato la wananchi sasa Tanzania ambayo mtu anaishi kwa dollar moja kwa siku hizi ni details za world bank leo hii huyu mtu akalipe kiingilio cha dollar 50 haya mahesabu sijuhi mmeyapigaji..mtu unaweza ukawa na dolar 500m ukajenga kimara uswahilini...kwanza ukiwa na hela hiyo uwezi kukaa Africa... ndiyo maana bara zima hakuna milionia hata mmoja mwafrica ikifanikiwa anahamia overseas.. hacheni michapo jadili vitu vinavyoendana na maisha ya kwetu andikeni habari kama ...ongezeko la vifo vya watoto wachanga au kupungua kwa uwezo wa kununua(purchasing power)kwa watanzania walio wengi for last two years hizo ndiyo thesis zilizo karibu na jamii kulikoni haya mambo ya michapo......
    Doctor..

    ReplyDelete
  51. ISSA ACHA UFISADI

    ReplyDelete
  52. Inavyoonekana wanaokandia ni wale waliondoka nyumbani sikunyingi wakiwa na mategemeo ya kufanikiwa majuu ilahadisasa hata shule hawawezikulipia na hela zote za mabox wanalipia bills.Jamani Tz imebadilika,mtakalia kupiga makalele ya ufisadi wakati wengine wanaendelea kula!nawatakia mafanikio vijana wote wahangaikaji!msiwasikilize wapiga domo

    ReplyDelete
  53. Jamani huyo aliyetoa habari hii hawatakii mema hao wasanii. Anataka hao vijana watafutwe roho zao na majambawazi buree!!!.

    ReplyDelete
  54. anony wa Mar 9, 10:56, haijatajwa kuwa currency inayozungumziwa hapo ni USD. Kilichoandikwa ni thamani ya mali tu, inaweza ikawa ni TZS

    ReplyDelete
  55. TANZANIA REVENUE AUTHORITY TUTHIBITISHIENI KUHUSU MADAI YA UTAJIRI WA WASANII HAWA, KAMA HAWALIPI KODI KAMA INAVYOTAKIWA BASI WAWEKENI KATIKA ORODHA YA UFISADI.

    ReplyDelete
  56. maharufu (badala ya "maarufu")
    Wiingereza (badala ya "Uingereza")
    hile (badala ya "ile")
    hacheni (badala ya "acheni")
    blend (badala ya "brand")

    ---
    Makosa ya kiuchapaji yanayotokana na vidole (na sio "vidore") kuteleza mfano "wahapati" badala ya "hawapati" nimeyachunia.

    ReplyDelete
  57. Tuangalie lugha pia. Michapio hii nimeiona kwenye baadhi ya comments hapo juu:

    (1) maharufu (badala ya "maarufu")
    (2) Wiingereza (badala ya "Uingereza")
    (3) hile (badala ya "ile")
    (4) hacheni (badala ya "acheni")
    (5) blend (badala ya "brand")

    ---
    Makosa ya kiuchapaji yanayotokana na vidole (na sio "vidore") kuteleza mfano "wahapati" badala ya "hawapati" nimeyachunia.

    ReplyDelete
  58. wabongo tuache dharau.
    Tutafanye utafiti wa kitaalamu na kuweza kujua ukweli, ili nasisi tuwe angalau kama wao.
    Kuna maajabu gani kwa hao kuwa na fedha hizo, na tukumbuke kuwa sio kama wanazo chini ya mto au ziko benki, maana yake wanafikia hapo kwa hesabu za vitabu.

    Robert B. Mujuni

    ReplyDelete
  59. HEBU FIKIRIENI, WASANII HUPATA KATI YA SILIMIA 5 NA 7 YA MAUZO HAPA TANZANIA, SWALI LA KIZUSHI....HAWA WADOSI WANAOBAKIA NA ASILIMIA 80, WANALIPA KODI?

    ReplyDelete
  60. we ngwega funga domo lako kwanza umetuma hii na lipicha lako kutafta umaarufu tu...uongo mtupu wewe na huko uliposkia

    ReplyDelete
  61. Hapo imetajwa tu 500Mil,

    fedha inawezwa kuwakilishwa kwa njia nyingi.

    Yaweza ikawa katika makumi, mamia, maelfu, malaki n.k

    Sasa inawezekana hizo figure ziko katika Zimbabwean Money au pia Zambian Kwacha.

    Pia kuna vigezo vingi vya kupata data,
    Inawezekana alieleta hizo data hapo juu kajumuisha nyumba, magari na mali zote ambazo ye kaziona wasanii wakiigiza nazo kwenye video.

    Yaan kama JD katumia nyumba flani basi inawekwa kwenye mahesabu.

    Kama ndivyo basi hakunaga msanii maskin

    ReplyDelete
  62. Inawezekana hizo takwimu zinajumuisha mali (magari, nyumba etc) ambazo wasanii hao wametumia kwnye video zao kama mdau alivyopendekeza.

    Habari kama hizi zitawaweka baadhi ya vijana hapo juu katika mazingira magumu. Imagine mtu unaishi kwa wazee halafu wanasoma magazetini eti una wealth ya 500M! Hapatatosha.

    ReplyDelete
  63. Bado tuna safari ndefu. Mwaka 1990 Michael Jackson alikuwa ana worth Millioni 350 US dollars...hizo ni sawa na Billioni 35 za Tanzania..he he he....tuna safari ndefu....!!

    ReplyDelete
  64. doctor sunday 10 56 si dollar hiyo baba ni madafu (Tshs). halafu mamilionea wapo africa na wanaishi africa angalia fobes tajiri wa 336 ulimwenguni anatokea wake na anishi wapi (Nigeria) wa mia moja na sabini na mbili au tatu antokea africa ila sina uhakika ni wapi. na wengine wengi tu waakina SSB LTD Salim Said Bakhresa tunao bongo na wengine wengi tu siwezi kuwataja hapa wote. ninachokushauri usitoe comment kama huna uhakika nazo

    ReplyDelete
  65. ahaahaa! i like that, nadhani wengi wetu tulio Nje ya nchi ni mamilionea basi Bongo. duuh hii kali ok.

    ReplyDelete
  66. Is that TZ currency or Mugabe's currency?????kama ni Mugabe then i believe but if its TZ currency, i m NOT convinced. Mdau T-Dot

    ReplyDelete
  67. Unajua nini??? watu hawashangai kuwa kapataje hizo hela. Ila kama ana hizo hela basi angeishi vizuri zaidi...

    Wengi tuko huku kama mini nimemaliza shule sio mda mrefu na nimejenga nyumba. Na nyumba kaka Michuzi aliyotuonyesha honesty sio najisifia lakini yangu iko much better. Na mimi sina hata hela za kutanua na nimejenga hiyo nyumba yeye mwenye laki tano basi angekua na nyumba nzuri zaidi.

    Msianze kusema ana malengo yake au ana save...Bwana hata vitu ulivyonavyo ndani kama una laki tano hutaenda na vile alivyonavyo

    Hela alizonazo ni zake na mimi nampongeza sana kwa kupata hela kupitia usanii mgumu wa africa usio na copyright ila waliotoa habari ndio wawe makini na data zao.

    You can fool some all the time but you can't fool all the people all the time. Hata kama hatuishi bongo value ya dollar tunaijua.


    ReplyDelete
  68. I have only one big question: Assume the numbers are true, are these guys TAXED (I mean TRA friendly)?????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????

    Jafar

    ReplyDelete
  69. KAKA MICHUZI
    MIMI NAOMBA SOURCE(CHANZO CHA HIZI TAKWIMU)HILI TUWEZE KUZIFUATILIA,KUZIHAKIKI KUWASHAURI NA KUWAPONGEZA!
    KAMA HUNA
    I HAVE NO COMMENT.

    ReplyDelete
  70. mimi nasema kama watoto wana Wealth those amount ni safiiiii sana it shows how Tz arts inavyo kubalika lakini to be honest I doubt with that dataz kwa kuwa nazani kama kweli muziki wa bongo ungekuwa unauza hivyo master J na P. Funky wasinge pumzika na wangekuwa mbali sana labda wange kuwa na ela kama mengi kwa kuwa hao wote hakuna mwenye Track 10 ambazo amerikodi nje ya MJ na Bongo record .....lakini kama kweli mzuka

    ReplyDelete
  71. Jamani hivyo ni vijisenti tu, hao mabwana wadogo hawna kitu bado na ndio wanajitafutia rizki, kwahiyo msiwaghasi na kuwaongelea saana. Tuna mambo mengi ya kuongelea zaidi ya hivyo vijisenti vya hao mabwana wadogo, lakini wanajitahidi,wanaonesha juhudi. Ni mwanzo mzuri tu

    ReplyDelete
  72. Haw wasaani wote ni choka mbaya tuu, 500m za jay dee ni ile nyumba ya rangi rangi nyekundu au nini. na mbona Ray c hayupo, TID naye hao wote si wasanii wa bongo?? hizo infor niza udaku na masifu ya buree, mamilionea wenyewe wametulia hapo hapo bongo hawaitaji kujulikana habari zao.

    ReplyDelete
  73. inawezekana ikawa ukweli ila mdau atuiambie amatumia njia ipi kupata hizo data

    ReplyDelete
  74. kwa kweli hakuna msanii bongo mwenye utajiri huo hata kidogo wote hao wanajitahidi kufika katika maisha mazuri zaidi.

    ReplyDelete
  75. WOTE HAO CHOKA MBAYA HAMNA MWENYE HIZO THAMANI..........BABU ACHA KUTUYEYUSHA HATUPENDI HIZOOOO....EBOOOOOOH!!

    ReplyDelete
  76. KAMA WANA THAMANI HIYO AU WANA FEDHA HIZO MBONA WAMECHOKA SANA! MAANA WAKO CHOKA MBAYAAAAAAAAAAA.
    DUUUH KWELI KAMA KUPEANA MAUJIKO BASI HAPA BABU UMEZIDISHA. HATAAAAA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...