Wadau,

kuna mzungu ameandika kuhusu Tanzania, ipo sentensi moja katika blogu yake imenichefua mno. Tafadhali naomba walioguswa nao wakemee hii tabia ya kulinganisha vitu visivyolingana, ni kebehi na dharau! Sentensi iliyoniudhi ni hii:


"a female traffic officer in a tight blue skirt and with legs as thick as small tree trunks" .


Walaumu anavyofanya kazi yake na si kumwingilia mtu maungoni! Mambo kama haya hayasemwi hadharani hivi, labda uwe na ugomvi binafsi na si kumnyumbulisha mtu kwa mfano wa kitu.


This is what the traffic looked like this morning at 7. Incoming and out-going, switching between fast and slow lanes, evidently obeying new rules every day.


Sometimes you drive according to the traffic light: On occasion it doesn't work (but you still drive as if it sort of did): Most mornings a female traffic officer in a tight blue skirt and with legs as thick as small tree trunks is orchestrating the traffic.


Many mornings it feels sort of like a mental preparation of my mind for attacking the heaps of work in my office.
Inapatikana:
bofya hapa
Subi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Huyu mama wa MS Tanzania anatakiwa kupewa onyo kali au kushtakiwa kwa kumuita mtu mwenye mguu kama shina la mti. Ama kweli hii ni dharau ya hali ya juu sana. Anaweza kushitakiwa huyu kwa matamshi ya kibaguzi

    Mdau

    ReplyDelete
  2. wengine kwao wametokea prison sasa adabu yao iko kisogoni..shenzy zake. alifikiri sie tunatembelea mikono. Naona wao hawajui mbongo na mguu wa bia

    Mdau

    ReplyDelete
  3. Huyu mama lazima aombe msamaha manayake naona ata feel kama vile kavamiwa kwenye site yake. Anaenda kujua ni jinsi gani issa michuzi iko popular.

    ReplyDelete
  4. kwa sababu kaandika mzungu,basi imekuwa issue, you lot get a life

    ReplyDelete
  5. Sasa acheni hayo mambo.Mimi nilifikiri katukana mambo ya ajabu.Hiyo comment ni ya kawaida kama mtu akiwa"frustrated".Kuna mambo mengi ya maana ya ku"discuss" siyo mambo ya kitoto kama haya.Mzee Michuzi hii Blog ni Blog kali sana,so please maintain your standard dont let people put it down.

    ReplyDelete
  6. Inabidi tumwombe huyu mama kiuungwana a post picha yake inayoonyesha mwili mzima ili na sisi watanzania tumtolee comment.

    ReplyDelete
  7. we subi usituyeyushe kwenye blog yetu ya wananchi. hayo ni maandiko ya kawaida. hata mimi nawatukana humu..nyamayao

    dogo

    ReplyDelete
  8. Michuzi,
    Mbona mie naona hapa Dada yetu ana sifiwa kwa kuvaa sketi iliyomkaa na ionyeshayo umbo alojaaliwa na maanani!, na pia kujaliwa usafiri(miguu) ilojaa kama chupa ya bia!! maana hajasema 'ana miguu minene kama ya mti wa mbuyu. Maana dada zetu wa sehemu mbalimbali za Bongo wamejaliwa 'usafiri' na maumbo yaliyonawiri. Kweli dada zetu wa kitanzania wazuri kweli kweli na wanaenda na wakati kimavazi.
    Mdau Na.1
    London.

    ReplyDelete
  9. Hebu tokeni zenu hapa hatakiwi kuomba msamaha wala nini, si amesema ukweli bwana, kuna ma-traffic police vibonge kama wacheza sumo vile. Hongera sana Mzungu kwa kutoa dukuduku lako kudadadeki.

    ReplyDelete
  10. Kweli lakini hakuna aliloongea ambalo ni uongo yote kweli tu.Badala ya kumlosoa mi naona tujikosoe wenyewe kwanza ili apate mazuri ya kuandika

    ReplyDelete
  11. Kuna wanawake wazungu wengine ni malaya tu wanaokuja kujiuza nchini kwa wanaume wa kizungu.

    Si kila zungu jike mnaloliona mjini au kwenye blogs ni jitu la maana mingine ni michangudoa tu.

    Mingine huletwa na mahawara wa kizungu badaye ikitelekezwa inabaki nchini kazi yao ikiwa kufanya umalaya na kupiga umbeya kwenye mablogs.

    ReplyDelete
  12. Sioni tatizo zaidi ya kwamba Michuzi ame-prempt liwe tatizo. Huyo mama ameufananisha ukimbaumbau wake wa kizungu na guu la mama wa kibantu.
    Sisi wote ni mashahidi wa jinsi baadhi ya dada zetu wa trafiki walivyo vibonge huko barabarani. Je
    angemuongelea trafiki wa kiume na kusema 'tumbo lake kubwa kama pakacha' tungesemaje? si sisi wenyewe tunayasema haya kila siku?????

    ReplyDelete
  13. Wewe Subi usimlalamikie huyu mzungu. Sisi wenyewe kwa wenyewe tunafanyiana mambo kama haya mbona ujaongelea msamaa? Kila siku watu kama Pinda, Flaviana, Lady Jay n.k wanakashifiwa kila siku.

    Ina maana kwamba kitendo cha watanzania kuwakashifu watanzania wenzao ni sawa wakati mila zetu tumefundishwa kuwaheshimu watu? Inabidi kwanza sisi wenyewe tujirekebishe kabla hatuawarekebisha wengine.

    ReplyDelete
  14. "kulinganisha vitu visivyolingana". Kwa mfano "simba wa afrika". Sitiari, bwana.

    Nadhani nimemwona huyo trafik. pernille hajasema uongo.

    ReplyDelete
  15. na kweli watanzania wengine wamejaa chuki, wivu, kuonea wenzao wivu wengine kama umefanikiwa basi mpaka wanakukatisha tamaa, watanzania ndio maaa hatuendelei. nawajua baadhi mimi kupenda kusema wenzao, ya kwao yamewashinda.

    ReplyDelete
  16. WABONGO TUKUBALI KUKOSOLEWA.
    HAYO MANENO ALIYOONGEA HAKUNA HATA MOJA LINALOONYESHA UBAGUZI ILA NI UHURU WA VYOMBO VYA HABARI.WAACHENI WAANDISHI WETU WAANDIKE UKWELI.
    IF U DONT WANNA LOOK FAT GET A SLIM PILL

    ReplyDelete
  17. Aisee kweli kazi ya kufanya hatuna...Ingekua mimi, I would left my comments ont he big fat legs of the traffic police.... vitambi vya hao matraffic tell another story.. corruption, extortion of money from small people etc... Pernille keep it up girl!

    ReplyDelete
  18. Nadhani watu mumemwelewa vibaya huyu dada, hiyo ni ametumia descriptive language ili uweze kupata picha akilini mwako sio tusi wala nini. hakuna anything negative about tree trunks, anamaanisha tu kuwa mama amejazia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...