Mzee anayetuhumiwa kumfungia kwenye chumba bintiye na kisha kuzaa naye watoto saba anatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo huko Austria.

Mzee huyo Josef Fritz mwenye umri wa miaka 73 hapo jana alikiri kuwa alimfungia mwanaye huyo wa kike aitwaye Elizabeth kwa kipindi cha miaka 24 ambapo alizaa naye watoto saba.

Mkuu wa upepelezi wa makosa ya Jinai nchini Austria Franz Polzer alisema mmoja wa watoto hao saba aliyozaa na mwanaye alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa na kwamba aliutelekeza mwili wa kichanga hicho kwenye tanuri la nyumba yao.

Mdau Malumbo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Tusishangae sana kwani wazungu wanamafatasi mengi na sisi ni wepesi wakuiga kila wanacho kifanya kuna mengi katika jamii zao hawa watu hata kuliko sisi wafrika Tanznaia tuwe macho na kupenda kuiga kila anachokileta au kukifanya mzugu na ndio utakuta katika miaka 20 ijayo bongo itapoteza mila na tamaduni zake

    ReplyDelete
  2. Anatia kichefuchefu hata ukimwangalia, HAsid Allah.

    ReplyDelete
  3. shame on u babu kizee.una mapepo wewe sio bure

    ReplyDelete
  4. Imenisikitisha mno hii habari nilipoiiona kwenye BBC NEWS yaani hawa wazungu tunawaonaga watu wa maana kumbe ni watu wakatili yaani wanaweza kufanya kitu ambacho hata mnyama awezi kufanya kitu kama hicho washenzi sana na awafai

    ReplyDelete
  5. kweli wanaume hawazeeki,mtu atazeeka uso lkn kiwandani production kama kawa.teh teh

    ReplyDelete
  6. anacheka au ndivyo alivyo? mmm mkatili sana anazaa na binti yake makubwa!!!!!!!!!!!!!
    alafu kichanga kakiteketeza jamani muhukumuni na hilo!!
    sweet
    Arusha

    ReplyDelete
  7. MMh! Pepo huyo apite mbali. Ingawa nasikia wapo wazee wengi tu wamezaa na binti zao huku Tanzania lakini wengi wao ni "USHIRIKINA" na hata hao mabinti wanadiriki kuwa dharau mama zao. Na vile akina mama wa Afrika wamefundwa wanapiga kimyaaa!!
    Naomba Mungu wapitishe mbali pepo huyu kwa vijana wetu maana mama mdau hapo juu alivyosema, kasoro yetu watu weusi ni kuiga tu!! Ipo siku utasikia yametokea huku. Eeh! Mola tuepushie!!!

    ReplyDelete
  8. Michuzi naomba habari nzima ya huyu mzee kwa kiswahili toka mwanzo hadi mahakamani, ninatatizo na english please!! Au mdau yeyote nayeijua hii story vizuri, kweli inasikitisha lakini ni vizuri nikawanajua hasa nini kilifanya mama mtu asijue binti yu wapi?

    ReplyDelete
  9. hakika ni kitu cha kusikitisha sana toka duniani hadi akhera ni kupita unyama.

    kitu cha kunisikitisha sisi watanzania pia ni wanyama wengi wetu kwanini tulaumu wazungu wote maana kuna wazungu wengi sana ambao wazuri na kuna watanzania wengi wazuri na wabaya pia.

    chukulia majambazi yanayoteka mabasi na kuwavua nguo abriria bila kujali kama kuna wazazi au madada haya sijui pia mzungu.

    haya jingine kuwachinja maalbino kwa ushirikina hii nayo sijui wazungu.

    haya mtoto salome juzi tu kauwawa kwa kuchinjwa kama mbuzi hebu waulizeni wazazi wake sijui nayo ni mzungu.

    watanzania wangapi wamezini na mama zao, dada zao na watoto zao tena wengine watoto wa kiume wamiziniwa na baba zao.

    watanzania ni muhimu sana tusilaumu taifa bali tumlaumu na ikiwezekana kumlani mtendaji kosa maana hamna taifa lisilokuwa na wabaya na wazuri.

    mafisadi siyo wanyama kuibia mali za wanyonge wengine hata chakula kwa shida jamani na hapa pia wazungu.

    basi hatari kila kitu sisi watanzania hatuana kosa bali warabu, wazangu na wahindi.

    burundi mtu ulikuwa ukiulizwa unataka kufa vipi kwa panga na mkuki bure ama risasi inabidi ulipie kosa ni kuwa mhutu au mtusi hii nayo mzungu.

    basi watanzania wote tutaenda peponi maana makosa yote ni ya wazungu.

    MUNGU IBARIKI HAKI AMEN

    ReplyDelete
  10. yaani wewe anony wa April 30,10:48 unathubutu kufanya joke kwenye hii habari ?? Kiwandani production ndio nini hicho kiwanda akamfanyie production MWANAKE WA KUMZAA kwa MIAKA 24 ?
    Sasa mimi nataka kujua watoto huwa wanamuita nani ? na mama yao wanamuita nani ? hii si laana ya kuangamiza Ulimwengu woote jamani !!!! Mambo kama haya ndio maana siku hizi tunapata maafa makubwa sana ulimwenguni maana tunashindana na Sodoma na Gomora kwa mpango huu.
    Mimi naamini kama huko kwa Mwenyezi Mungu kesho huo moto jamani watu wote hatuwezi kuwa sawa sawa lazima kuwe na steji maana dudu kama hili hata kukaa nalo motoni bora unipe muuaji na jambazi , hili dudu ni linatisha kwa unyama wake hata ibilisi mwenyewe nambari wani hapa atatoka mbio sana.
    Jamani tusifanye kuleta joke hapa this is not a joke tusali tuombee Ulimwengu wote na vizazi vyetu Mwenyezi Mungu atupe mwisho mwema.Anaweza akatuangamiza na dunia yetu hii kama vizazi vilivyopita kwa matendo kama haya.Mimi naogopa sana.

    ReplyDelete
  11. Wazungu wana mambo mengi ya kutisha na unyama lakini huyatafutia sababu uyapooza ili yaonekane kama special case. Tayari wameshaanza kumjengea hoja ya kuwa na matatizo ya kisaikolojia. Lakini miaka 24? Tena alikuwa mjuzi hadi kumlazimisha bintiye kuandika barua za kuwasalimia na yeye kuzipost. Alisingizia binti yake kutoroka nyumbani na kujiunga na makundi ya siasa kali za kidini (cult).
    Sijui sisi kwa nini tulikiachia kile kibabu kilichokuwa kikipiga picha za ngono Mwanza. Huku asingeona jua.

    ReplyDelete
  12. anon wa kwanza ni kweli unayosema lkn hizo mila na tamaduni kwani bado zipo? mimi sizioni zimeshatoweka! hasa hao kina dada wenzangu na viblauzi vyao wanavyoviita nguo au gauni kuwatia wanaume majaribuni wakiwamo wapita njia na wazazi wao pia! ndio wazazi nakusudia wajomba na baba zao si wanaume nao? halafu wakibakwa tutamlaumu nani aliyebaka? sisemi aliyebaka hana kosa lakini wakina dada wengine wanajibakisha na wao wachukuliwe hatua na yote sababu ya kuiga kwao, wazungu wenyewe wana sehemu za kuvaa nguo hizo. Mwisho huyo babu Mungu ameshamlani ni bora anyongwe tu jela atakuwa anapelekwa picnic tu kwa kosa kama hilo! Kiranga huyo haliliwi wala haekewi matanga.

    ReplyDelete
  13. yeeees. tena kichefuchefu chenyewe hana tofauti na yule mtoto mla watu! ghhh ptuuh! laanakum!

    ReplyDelete
  14. Huyu itakuwa anatumia viagra tu hana lolote!

    ReplyDelete
  15. Lakini Brother Michuzi, mi kwa kweli bado najiuliza maswali yafuatayo naomba wadau tusaidiane kubadilishana mawazo.
    1. Hivi kweli miaka yote hiyo mke wa huyu Babu alikuwa hajui? Au hana mke? Na kama alikuwa anajua kwa nini hakutoa taarifa kwa vyombo husika? Au walishirikiana na mkewe?

    2. Yaani hawana watoto wengine ambao wangeweza kustukia kuwa dada yao kafungiwa huko chini?

    3. Kama kuna watu wengine kwenye hiyo nyumba walikuwa hawatembelei huko vyumba vya chini?

    3. Na huyu Binti Mwenyewe, miaka yoke hiyo definately alishakuwa mtu mzima-hivi hakuweza kustukia kwamba ameshikiliwa bila ridhaa yake na kujaribu mbinu zozote za kujiokoa hata kama ni kupiga kelele?
    Au na mwenyewe aliridhia?
    Au alimpumbumbaza kwa madawa fulani?
    Au alimfanya Msukule?

    Kwe kweli nakosa majibu.
    Wadau hebu nisaidieni

    ReplyDelete
  16. Anony hapo juu ina maana kwa sababu huyo aliyefanya hayo mambo ya ajbu ni mzungu basi wazungu ni wa ajabu na washenzi?!!Juzi juzi kuna mtu bongo alikula kichwa cha mtoto, sasa tusemeje kuhusu waafrika? That's stereotyping!Watu wanaofanya mambo ya ajabu wako katika kila aina ya race.Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  17. Nani anayebisha au kukataa kuwa bongo hamna tabia hii, ya wababa kulala na watoto wao wa kike, tena kuna makabila fulani amabyo ni kawaida sana, HAPAHAPA TANZANIA.

    Hakuna kuiga shetani yuleyule ndiyo yuko na huku TZ ni kwa kuwa vyombo vya habari havijagundua hili.

    watoto wengi wa kike wa matajiri nchi hii wanalala na baba zao!

    LA MUHIMU NI KUOMBA JAMANI, DUNIA IMEISHA, WANGAPI HUWA MNASEMA UONGO?? PALE UNAPODHANIA UONGO NI KITU CHA KAWAIDA NDIPO NA MWINGINE ANADHANIA KUUA NI KAWAIDA(kama Ramadhani) mwingine anadhania kulala na mtoto wake ni kawaida kila MTU ANA TBS YAKE YA DHAMBI.

    TUMWOMBEA YESU ATUSAIDIE, tupige vita hali hii na nyingine yoyote ya dhambi huku na sisi tusiiingie kwenye mtego wa kuchagua dhambi hii ni sawa na hii sio sawa!!!!!!

    kuna kisa nitakileta kinachofanana na hiki, give me 4 days.

    stay blessed
    mdau canada-

    ReplyDelete
  18. Huyo anayeuliza hii habari kwa Kiswahili na wenye mwaswali yao mimi nitajaribu kuyaweka sawa.

    Kwanza mjue huku maisha ni tofauti sana na bongo. Sisi kwetu tunajuana mtaa mzima na wakihama watu mnajua. Mimi hapa naishi neigbors zangu siwajui hawanijui. Ni hey hey imetoka.

    Usipokua na wakukumiss huku utakufa au kupotea na wala watu wasijue chochote. Kila siku kuna habari mtu kafa zaidi ya mwaka au hata miaka miwili kwenye nyumba yake na hamna hata jirani aliye notice au mailman kujiuliza kwanini barua zinapile up na hamna anayezichukua? Maisha ya huku ni very confidential, lonely, troublesome na yakutoaminiana. Unaweza ukamtrust next door neighbor kumbe ni serial killer. Huku unatakiwa kuwa so careful kuchoose marafiki na sio kila mtu umwonaye au unayeongea naye ni rafiki yako.

    Okay back to the story

    Huu baba ana mke wake na wamezaa pamoja watoto saba. Huyo mtoto mmoja sijui order yake ya kuzaliwa lakini mara alipotea. Baba akasema huyo mtoto ni mapepe kwa hiyo amekimbilia kwa wanaume. Hadithi ndio ikawa hiyo na police wasema kwa vile yupo 18 na wazazi wamethibitisha kuwa kakimbilia kwa wanaume basi tena.

    Ati hata kuna siku aliwaletea barua kuwa mimi sijambo na msinitafute. Kumbe anamwambia huko kwenye basement andika hivi na hivi masikini mtoto wa watu.

    Mara siku moja watoto watatu ati wakawekwa mbele ya mlango wao na note ni kutoka kwa mtoto wao kuwa ameshindwa kuwatunza hivyo wamsaidie. Walikua bado wadogo kwa hiyo huyo baba na mke wake wakawa adopt. Na wale watoto hawakuwa na kumbukumbu yeyote ya huko chini.

    Mtoto mmoja huyo mwanamke alimzaa kakafa huyo baba akakatupa kwenye sewage drainer.

    Hao watoto watatu walikua hawajui nje kukoje na wala walikua hawajamwona doctor hata siku moja.

    Hii issue imefunguka baada ya mtoto wake mmoja huko kwenye basement ambaye ana miaka 19 kuugua na ikabidi apelekwe hospital. Na doctor wakawa wanamuuliza maswali ndio hiyo siri ikafichuka baada ya kuona hadithi haziendani na hazieleweki.

    Huyu baba aliandaa haya mambo kabla hajamuweka huyo bintie huko kwa uangalifu sana. Kwasababu wamekuta huko alikowaweka aliweka sound proof nzuri sana.

    Na pia mtu ukiwa captive baadaye akili inabadilika na unakuwa unamsikiliza huyo aliyekuteka kwa vile ndio anakuwa kama Mungu wako. Wako wengi tu waliotekwa ukisikiliza hadithi zao unajiuliza kwanini asifanye hivi au vile lakini ni kwavile hujawahi kuwa hapo kwenye hiyo situation na huyuji psychological brain imeshakua vipi.

    Yule mtoto Utah (Elizabeth Smart) alichukuliwa na yule mzee wa dini usiku alivyokua amelala. Yeye alikua anatembea njiani na huyo baba na wake zake na wanapita hata mitaa yao kabisa na kuona nyumba yao hiyo hapo lakini hakuwaza hata kukimbia.Anawaona police na wala hakuwaza kuwaambia mimi ndio ninayetafutwa. Na alikua ana miaka 14.

    Mimi ninachojiuliza ni kuwa kama huyu baba angekufa si na hao huko kwenye basement wangekufa kwa kukosa supplies? Manake choo, bafu walikua nacho ila chakula sijui walikua wanapelekwewaje. Kwenye picha zilizoonyweshwa sijaona jiko. Hivyo nadhani mlo ulikua take out tu kila siku.

    Na huyo mke wake hakuona hata dalili zozote kabisa kuwa mume wangu something is not wright? Ila naona pressure ilikua mwaka wa kwanza alipomweka huyo msichana huko baada ya hapo labda routines zake zikawa kawaida. Na sidhani kuwa lipanga angemweka miaka yote hii ila kama wanavyosema alikua ana msexual abuse toka miaka 11 basi alijua ameshafikisha umri wa kuhama nyumbani na akihama atamreport kwa police. Who knows alikua namwambia ukisema nitakuua?

    Hawa watu sio wakuchechea wana mambo mengine unashindwa kuelewa ni kwanini, ilikuaje na ubongo wake unawaza vipi?

    Ila hawa wao kuna ya kwetu ambayo wanatushangaa sana tu kama hayo ya voodoo nao hawaelewi.

    But he is a very sick guy. Atakua mkaa wa kuchoma watu wengine jehanamu.

    ReplyDelete
  19. Mungu ndio Muhukumu ila watu kama hawa moto wanauona hapahapa duniani, Kuna mtu kauliza kama kwanini mke wake hajui?

    1. Mke wake anaweza asijue sababu kuna wake kama hao tanzania, anakuwa mwanaume ana power yakusema lolote asitoke au usiingie chumba hiko na asiingie kweli.

    2. sawa na wale wazee ambao wanawatisha watoto zao mpaka wanakosa raha hata ukubwani wapo tanzania pia.

    3. MWanamke naye inaonesha alifikia mwisho moyo wake ukapenda kimapenzi na huyu mzee mpaka kuogopa asije kumwaribia mzee huyo, kwa kuogopa.

    4. tujaribu kufundisha sana wenetu kuhusu hizi tabia mbovu hasa nyumba za watoto yatima, wanaolelewa, na watoto wengi wa kike hata wakiume.

    Huyo mzee laana tupu ndio wachawi wenyewe hao wazungu uchawi wao pia wanyama sana. anamtoto mwengine anamiaka 19 wakike ndio hao wanapanda mgomba ndizi wanataka waanze kula wao, tukitoka nje ya mada. mie naona huyu mwanamke wa 42 atakuja kuuuza story yake ya kitabu mapesa mengi sana. hata mie nipo tayari kukisoma.

    ReplyDelete
  20. Wewe unayesema huyu ana matatizo ya akili, sikubaliani na wewe. Huyu anaonekana ni MASTER PLAN wa hatari sana. Na osama wanatoka droo.

    hayo mazingira tu alivyoyaandaa, hadi akawahidhi binadamu kwa miaka yote hiyo? MM nasema huyu jamaa ni inteligent sana. Alitakiwa afanye kazi na CIA.

    Isipokuwa in otherside, huyu ni SHETANI HASA tena kati ya wale waliokabidhiwa funguo za kuzimu. Yaani hana tofauti na hao wachawi wa bongo. tofauti ni kuwa tu hawa wameendelea na wanafanya mambo yao ki sayansi.

    Dada T

    ReplyDelete
  21. To add on what Perez asked:

    4. Hao watoto waliozaliwa hawakuwa wakilia au kutoa sauti ya aina yoyote hata kuwafanya majirani kujiuliza kulikoni ndani ya nyumba ya huyo mzee, au alikuwa na rach?

    5. Huyo binti alikuwa akizalishwa na nani wakati wa kujifungua?

    ReplyDelete
  22. Hii habari inanifanya kukubaliana na ma-comedian wa kimarekani(weusi)kwamba wazungu ni mazoba/mazuzu kiszhenzi.
    Nimeona CNN kuwa hiki kibabu kilikuwa kinakwenda likizo(vacation) nchini thailand.Sasa cha ajabu ni kuwa hawa wafungwa(vyovyote utakavyowaita) hawakuweza kukimbia,kuomba msaada toka polisi,kupiga kelele kwa majirani zao.Ndiyo tunajuwa huku majuu kila mtu ni kivyake hakuna cha jirani ,lakini najuwa mtu ukipiga kelele mtaani kwa vyovyote vile watu wataita polisi.Sasa kwa nini hawa watu hawakufanya chochote kile cha kuweza kutaarifu majirani.Pili mtu anasafiri masafa hadi thailand watu wako basement tu hawajui kama mtu kaondoka ama yupo?Ni ajabu siku ya kwanza inapita humuoni mtu,ya pili inapita kimya ina maana hawa watu walikuwa wamefungwa midomo ama.Hapa wangekuwa watu weusi isingechukuwa hata miezi sita wangekuwa huru.
    Kuna mtoto(mweusi) mmoja kuna mtoto wa kike(wa miaka 10 hivi) walim-kidnapu(nimeshindwa kupata jina la kiswahili) hapa Philadelphia sababu baba yake alishindwa kulipa deni la madawa ya kulevya,akafichwa basement ya jumba bovu ndani ya jiji hili.Lakini ilimchukuwa mtoto siku moja kutoroka na kurudi kwa wazazi wake.Sasa fikiria mtoto mdogo aliweza kutoroka iliwashindwaje hawa wajinga kutoroka kama si ujinga.

    ReplyDelete
  23. Duh jamani huyo ndie mswahili haswa...amefanya mambo ya kinyaturu kweli kweli...mambo kama hayo yapo kwetu kule vijijini yapo kila siku...sasa mnashangaa nini???

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 01, 2008

    MIMI SIONI KOSA LA KULA KUKU NA MAYAI YAKE. WATU WANAMSAKAMA BULE AMEJITAHIDI SANA HAKUNA HATA MTU MMOJA ALIYE JUA USHUJAA WAKE NI VIZURI WAM ENZI NA KUOMBA USHAURI JINSI YA KUONA ALIVYO FANYA HUYU SHUJAA WA AUSTRIA.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 05, 2008

    Wewe anon wa April 30, 200811:16 huna akili hata kidogo! Wewe uliona wapi Wanyaturu wanafanya uchafu kama huo? Naamini wewe si mnyaturu hivyo hujui mila za kinyaturu! Shika adabu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...