KUNDI la mwanamuziki Bozi Boziana kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo linatarajia kusindikiza uzinduzi wa albamu ya Impact ya bendi ya Akudo Impact.


Msemaji wa Akudo amesema leo kuwa kundi la Bozi Boziana linatarajia kuwasili Mei 13 likiwa na wasanii takribani 17.


Uzinduzi wa albamu hiyo umepangwa kufanyika Mei 16 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee ambao utafanyika kwa ushirikiano wa Kampuni za Qssp Group Ltd na NY Production.


Mratibu wa tamasha hilo Bahati Singh alisema : " Akudo wao wako kwa ajili ya vijana, lakini tukaona ni heri tuwape burudani ya watu wa aina mbalimbali na ndio maana tukaamua kuwaleta Bozi Boziana kwa ajili ya watu wazima na Jahazi Modern Taarabu kwa wapenzi wa muziki wa mwambao," alisema.


Habari zaidi na picha nenda: lukwangule.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Duu!!! mmmm!!!wazairwa wanatumaindisha.Abiria chunga mzigo wako,wazaire on a mission to take our women.Jamani mawindo haya,mimi akifika tu jamaa mke wangu nafungia kwenye clozeti nishachoka mara wazambia,wasouth,Koffi,khah!!! Bozi naye

    ReplyDelete
  2. Okey!Mzee Aboubakar Bozi Boziana,
    ni vema kuwa umeguata mila na desturi za blog ya jamii kuwa Fulanaziiiiii!uliyovaa ni ya aina ya MKUU WA TAGETA mheshimiwa Kaka
    Michuzi hapa hakuna cha Usupa staa
    bali ni kufuata mila na desturi za baraza la jamii

    ReplyDelete
  3. Hana lolote huyo kuwashinda wazee wa kutwanga na kupepeta.
    Vena , arusha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...