'MCHAWI' MWINGINE ABAMBABWA TABATA
Siku tatu tu baada ya kijana kukamatwa na kichwa cha mtoto, kijana mwingine, safari hii msichana, amekamatwa katika hospitali ya Tabata iliyopo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar kwa tuhuma za kutaka kuiba mtoto wodini.
Rehema Kefa(18) Mkazi wa Mkuranga alikutwa akitaka kumtorosha mtoto huyo jana aliyekuwa katika wodi ya mateniti hospitalini hapo jana.

Inasemekana Rehema alibambwa na nesi wa zamu katika wodi hiyo ambaye ni mlokole, ambaye baada ya kuona mauzauza ya huyo msichana inasemekana alifanya maombi, na mtuhumiwa huyo akaanza kutambaa kama nyoka wodini hapo.

Polisi waliitwa na kumpeleka Rehema kituo kidogo kilichopo karibu na hospitali hiyo ambako alikiri kwamba yeye ni mtu wa juju, na kudai kwamba shughuli hiyo kafundishwa na bibi yake kwa jina la Salome Nganame.
Aliwaambia askari kwamba hakuwa peke yake katika skuli hiyo, kwani mafunzo hayo ya undondocha kafunzwa yeye na kinadada wengine aliowataja kama Asha Said(29), Fatuma Saleh(23) na Khadija Mpogolo.
Alisema yeye na hao aliowataja ilikuwa waibe pamoja mtoto pele hospitali na kwenda kumnyonya damu.
aliwaambia askari kwamba walipomkamata bibi huyo na wenzie walikuwa wanawacheki tu kwenye 'TV' yao huko waliko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Jamani hivi haya mambo ni ya kweli? nafikiri Sodoma na Gomora is here now.wachawi siku hizi uchawi wao haufanyi kazi. mungu anafichua kila aina ya ukora. mwacheni Mungu aitwe Mungu

    ReplyDelete
  2. jamani ni bora tufe huku tukiwa tunabeba dox lkn bongo hakurudiki
    kwa hali hiyo

    ReplyDelete
  3. Yaani hii ni noma balaa kubwa sana nimeamini kuwa watoto na watu wazima kibao waliopotea ilikuwa hawa jamaa wanawachukua inaonekana hii ndio shughuli yao ya kila siku, mambo tuliyozoea kuyaona kwenye sinema za kichawi bongo yapo live kabisa sasa ukweli ndio unaanza kujiachia, Naomba kuuliza wadau kama serikali haiamini uchawi sasa nini kitafanyika kwa hawa watuumiwa, yaani afadhari ukutane na kibaka kwenye uchochoro akachukua simu na kula kona kuliko ukutane na mchawi anatamani kukunyonya damu, pia nikiangalia ajali nyingi sana zinazotokea hapa bongo ni mikono ya kichawi tu sio kila kitu uzembe wa madereva kani tukumbuke yule kijana aliyetoa uhai wa malaika wa watu alisema yeye pamoja na wenzie walikuwa wameusika na ajali mbaya iliyokuwa imetokea pale maeneo ya magomeni siku alipokamatwa, sasa hapo ndugu zangu ajali ngapi zimetokea kwenye mazingira yasioeleweka na nyingi kwa kweli, nyingi sana hapa bongo, nakumbuka kuna mwaka flani nilipokuwa naishi Iringa kuna bibi mmoja alikuwa anasifika sana kwa uchawi lakini mimi nilikuwa mgumu sana kuamini mpaka siku moja jamaa mmoja alipogonga paka wake baada ya tukio lile yamaa akapata ajali na kufa pale pale yaani kama dk 10 baada ya tukio lapaka kugongwa, sasa najiuliza tuna idadi kubwa sana ya wachawi bongo kwa nini wasitumie huo uchawi kuleta maendeleo badala ya kunyonya damu za watu na kukaba watu usiku, starehe gani wanaipata hawa jamaa, najua katika wasomaji na wachangiaji wa blog yetu hii ya jamii wapo wachawi pls naomba watusaidie kutueleza ni faida gani wanazipata kwa machafu wanayoyafanya, mwisho napenda kuwaeleza wanablog wote kwamba wachawi wapo kila kona kwenye office za serikali, office binafsi, makanisani misikitini kila kona hapa bongo wajaribu kuacha huo uchawi.
    Mchangiaji mwenye machungu na wachawi

    ReplyDelete
  4. Nawe acha kushabikia ushirikina. Ndo maana kila mmoja huko bongo anahaha kufungulia yulekijana kesi ya mauaji. Sasa si muende kwa waganga wawape tunguli kisha mumpeleke mahakamani kama ndio mnanywea.

    Achane kuusmbazana kuupamba ushirikina kwan kwa njia hiyo badala y akuumaliza ndo mnaukuza. Naamini hata vijana ambao walikuwa hawaamini ushirikina sasa ndo wanaenda kutafuta tunguri.

    mmeturudisha nyma kw amiaka zaidi ya 100 kwa namna ninyi waandishi mnavyoushabikia ushirikina. au nanyi mautumia? Bora chenge kuliko ninni mnao kumbatia ushirikina.

    kwa kuwa hii nimeituma kwako mh. mkku wa nanhii ya tegeta ( amayo naamini hujaenda bagamoyo ili itangazwe rasmoi) basi hata usipoibadika nitaridhika tu kwani ujumbe umefika. Hofu yangu inaweza kuishia kwa hao waidizi wako. tafadhali nnyi wasaidizi mpeni bossi enu hii hata kama ni privately.

    TAFUTA HABARI ZA MAANA ACHANA NA USHIRIKINA WA KUTUNGA NA USANII.

    ReplyDelete
  5. nashindwa kuelewa hizi story kabisa sasa zinanichanganya kichwa hapa duniani mara kichwa mara kuiba mtoto mara mzee amezalisha mtoto wake austria du kweli duniani kuna drama

    ReplyDelete
  6. kazi kweli kweli!!

    ReplyDelete
  7. Hizo ni frustration za maisha kwa sababu ya umaskini tuu. Our government should do more to help its people! Mi ni kati ya wale ambao siuamini uchawi......Ni dhahama tuu za maisha...

    ReplyDelete
  8. Mwaka huu mafisadi na wanga watakoma mbona! walokole ongezeni spidi kupambana na wanga sisi tunmaendelea kupambana na mafisadi.

    Aluta continua

    ReplyDelete
  9. Tougher sentences and hard labor, should be sanctioned against these individuals, and DEATH sentences should be given to those who perpetuate these kinds of crimes. The worst thing, they are starting to teach young people and children to do the crimes for them.

    It must be a PUBLIC trial, to send a clear message to those are engaging/interested in these devious shameful ACTS.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  10. Wewe usiyeamini uchawi upo basi na Mungu humuamini.Coz ukiamini Mungu, his opposite ni Shetani and all his satanic acts ikiwa ni pamoja na hayo mauzauza. Unakua kama serikali yetu inayosema haitambui uchawi huku wote wakati wa kampeni wanahamia Bagamoyo! Wewe hufikirii kwa nini barabara ya Bagamoyo inameremeta mpaka mwisho? Utalii sio kigezo! Unless if u prove that all infrastructures to touristic area are bomba! I respect your freedom of belief, but you should open your eyes further, usiku ukimkuta yule dogo wa Tabata kitandani kwako ndo utajua! Uchawi upo ndugu yangu na kwa stile hii only those protected by the pure blood of Jesus will stay safe. Tuzidi kuomba jamani maovu yamezidi!

    ReplyDelete
  11. HII INATISHA SANA.WAKINA PROFESA MAJI MAREFU WAKO WAPI NA MASHEIKH NA MAPADRI WAUNGANE WAENDE NYUMBA BAADA YA NYUMBA WAWATOE WACHAWI?
    Inatisha sana tena sana.

    ReplyDelete
  12. yaani nimependa comment ya anon april 30, 5:05 wa pili, Nimecheka ingawa ni habari ya huzunii, yaani ni kweli walokole wapambane na wachawi, wengine mafisadii. TRUE TRUE kabisa

    ReplyDelete
  13. Wewe Anon. Wa pili aliyekuambia kubeba box afadhali nani. Tena wazungu ni wabaya kupita kiasi, na wana maovu mengi sana wanayafanya. MM huwa siwaamini hawa jamaa kabisa.

    Unaweza mkuta yupo decent kkumbe mambo anayoyafanya ni ufirauni mtupu. just recent issue, huyo jamaa wa Austria,huyo si ni kama mchawi tu na mara sijui mtu anawateka wasichana wadogo anawaua nakuwazika ndani kwake, wewe unasema Africa noma au kwakuwa waafrika wanasafiri na nyungo? Acha upuuzi wewe, dunia imeharibika sasa, hakuna palipo na afadhali kote balaa tu.Mwanadamu ameshindikana kwa uovu popote pale. Wewe endelea kubeba box kwa raha zako. Nadhani tumuombe tu Mungu.

    mimi kusema la ukweli japo nipo huku nje ya nchi, lakini naogopa sana hata hawa wazungu tena ni hatari.

    Life is crazy every where

    ReplyDelete
  14. sasa ufisadi wa kisiasa na kiuchumi umepamba moto, wachawi naona na wao wameshindwa kujizuia.

    Hii sasa hatari DUuuuu!

    Dunia inatisha kila pahali,

    Tuzidishe maombi ili wachawi wazidi kuanguka na nyungo zao, na kina mkapa wazibitike.

    Kweli unaambiwa malipo ni hapa duniani mahesabu ahera, sasa nimeamini full. Ukifanya maovu, ipo siku penda usipopenda, Mungu lazima atakuumbua tu.

    God bless Tanzania.

    Dada T

    Dada T

    ReplyDelete
  15. ALL I can say is.
    MUNGU BABA TUANGALIE WAJA WAKO, TUNAKUHITAJI BABA,IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE,AMEN.

    ReplyDelete
  16. Michuzi mimi naomba nitofautiane na hao ambao wanasema eti hawaamini uchawi, ni vizuri lakini sijui wanataka ushahidi gani zaidi kuwaonesha kuwa uchawi upo...
    labda niwaulize mtoto wa miaka 15 kula nyama ya binadamu tena aliyoiua mwenyewe tena mbele za wtu tena bila uoga wowote tena amekiri kwa kinywa chake mwenyewe kuwa hiyo ndio kazi yake na tayari anavyo 5o vingine, hiii yote ha watu ambao eti hawaamini uchawi wanaiitaje???? jamani tufungue macho yetu tuone nini kinazungumzwa hapa, na pia samahanini sana wale wote ambao eti wanasema michuzi atafute habari za msingi na sio kung'ang'ania ushirikia, nawaambia waombe sana yasiwakute.
    chamsingi anapoleta habari yoyote na kwa ajili ya kujifunza na kuchukua tahadhari, sasa nyie kama mnataka yawakute ndio muamini, shauri lenu. ila kama mtakuwa na busara, mngekaa na kufikiria hili jambo mara mbili.
    kaa sawasawa na Mungu wako. that is the only thing we can use to fight against ushirikina, uchawi na mambo ya giza kwa ujumla!

    ReplyDelete
  17. NI UFISADI NA UCHAWI TANZANIA

    ReplyDelete
  18. Mimi sikubaliani na mtoa hoja kwa jina la ",mshirikina" hapo juu.

    Unamtuhumu nani kuwa anashabikia ushirikina? Michuzi? Waandishi wa habari, au wewe mwenyewe? Mimi naona kama kuna shabiki wa ushirikina basi ni wewe maana hata jina lako linaonyesha. Michuzi au waandishi wa habari huwezi waita mashabiki pale wanapotoa hizo habari. Kwa mfano, ona jinsi waandishi walivyotoa habari na kusaidia kuwaumbua mafisadi, je hapo utawaita kuwa ni mashabiki wa ufisadi?

    Mimi sijaona ushabiki wa Michuzi, na hata pia nashangaa kwanini ameruhusu hii comment yako ije. Kutoa habari kwake, na hata kama habari kama hii imejuridia mara nyingi ni ili sisi tunaosoma tuone jinsi gani ushirikina ulivyokithiri huko nyumbani, tena si ushirikina mdogo ila ni ule wa kinyama. Hii habari inatoa fundisho, onyo na hata mwito wa kuchukua tahadhari juu ya wizi wa watoto.

    Naomba umtake radhi Michuzi kwa tuhuma hizo. Sisi tunahitaji habari za nyumbani, chonde chonde ndugu "mshirikina" usiwakatishe tamaa waandishi wetu. Mchango wao nchini tumeuona na bado tunawahitaji katika vita ya kujenga nchi yetu.

    Mdau- Amsterdam!

    ReplyDelete
  19. I'm gutted n speechless! it's a shame.

    ReplyDelete
  20. KUTOKANA NA TAARIFA ZA MAJUZI WATU MJIHADHARI NA MATAPELI WATAKAOANZA KUJA KWA STYLE YA KUTOA HADITHI ZA KUTISHA NA KUTEKWA ILI KUPATA PUBLIC ATTENTION/SYMPATHY! INATOKEAGA, NA HABARI NDO HIZO ZIMEANZA KUMIMINIKA.

    ReplyDelete
  21. hata wezi wa ugoni watakuwa wanakuja asubuhi wanajidai nilitekwa mke wangu kwa nguvu za giza nisamehe, shauri yenu! watu wata take advantage of this situation. be aware folks.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 01, 2008

    Kwanza napenda sana kukupongeza mkuu MICHUZI kwa kazi zako jinsi zilivyokuwa nzuri mimi napenda sana tena nafurahi kujua habari za kwetu kila siku na uendelee hivyo hivyo mkuu usijali sisi tupo na wewe.haya nafungua ukurasa mpya kwa huyu anajiita MSHIRIKINA

    Naomba nikupe habari zako wewe mshirikina naomba kwanza ukae ujue unayoyaongea yanatoka kichwani kwako au kuna mtu anakuambia sema hivi na hivi alafu unaandika kwanza mtu mzima na akili zako unasema kwamba etii waandishi wa habari kuwa wanaendeleza kusambasa ushirikina wewe ndio inaonekana katika mazungumzo yako yote ni mshirikina usitake kuleta habari zako za kishamba hapa kama unataka tengeneza website yako alafu weka vitu unavyotaka wewe maana hukumsaidia kutengeneza hii website na hujui kiasi gani katumia kuitengeneza kwa hiyo wacha afanye anavyotaka yeye au unataka kumtafuta ubaya toka lini umeona michuzi anatabia mbaya kama ulivyo wewe basi na wewe ni mshirikina na kama ukiona kitu wewe kaa kimya sio uanze kuongea ujinga wako mbele za watu na unaongea vitu ambavyo havina kichwa wala miguu shika heshima zako na umemkuta mtu mwenyewe anaheshima na ni mpole usiwe unalopoka vitu vya kijinga mbele za watu wewe unawatetea hao wachawi na wewe basi upo kwenye kundi hilo kwanza ni mara ya kwanza hapa kwa michuzi au tanzania kusema kwamba uchawi umetokea sehemu fulani jiheshimu tutakuheshimu maana hii ni website ya jamii sio sehemu ya kuja na kuanza kusema etiii habari za kutunga wewe kinakuuma nini?vitu vitokee tanzania alafu michuzi akae kimya kwasababu kuna watu watakasilika sisi tunakuja hapa kwa ajili ya kupata habari mbali mbali zinazotokea tanzania kwa hiyo kwa ushauri wangu kuwa tengeneza website yako na ufanye unavyotaka wewe sio kumpangia mtu kazi yake umeelewa?

    Ok mkuu michuzi mimi ni ujumbe wangu kwa huyo anayejiita SHIRIKINA.kwa ambao nimewaudhi naomba radhi wandugu mtu akienda vibaya lazima umrekebishe hatuwezi kukaa kimya hata siku moja.

    Mdau
    U.K

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 01, 2008

    Hawa hamna cha uchawi wala nini, ni copycat kila mtu atajifanya mchawi sasa. Mi naona kila anayejifanya kuja na mawewe yake basi ni kunyongwa tu bila kuenda mahakamani. Wakiona hivi wataishia kufanya uchawi wao usiku tu na kuwalimisha mashamba watu wachoke lakini wawaachie watu uhai wao.

    Huo muda wakujifunza uchawi wangefanya mambo ya maana au kwenda shule kusoma. Sasa mtu wa miaka 29 ndio anafundisha uchawi wenzake. Zamani ilikua tunasikia vibibi vya miaka 100 ndio vichawi. Lakini who knows huyo Asha Saidi (29) ana wajukuu tayari.

    ReplyDelete
  24. UJUMBE KWA WASIOAMINI KWAMBA UCHAWI UPO:

    Kitu kama kipo kutokuamini kwamba kipo hakukifanyi hicho kitu kutokuwepo. Wachawi na Waganga wa Kienyeji wote wanaopiga Ramri wanatumia fani hii.

    Kutokuamini kwamba Uchawi upo ni sawa na Kutokuamini kwamba Mungu yupo. Mungu Mwenyewe anatambuwa kwamba Uchawi upo na Wachawi wanatambuwa kwamba Mungu Yupo. Kuamini kwamba uchawi upo si kwamba tayari na wewe ni Mchawi. Tatizo ni pale mtu unapoanza kutegemea Uchawi katika mambo yako yam maisha.

    Wachawi ni watumishi wa Shetani.Na lengo la Shetani ni kuangamiza binaadamu. Wao wenyewe hawana faida yoyote wanayopata kutokana na uchawi huo. Zaidi zaidi wanateseka, yaani wanatumikishwa. Ni watumwa wa Shetani. Wamejazwa fikra potovu ili furaha yao iwe ni kuona binaadamu wenzao wanalia na kuteseka na kuangamia.

    Katika hili wanafanana na Mafisadi. Fisadi yuko tayari kuweka mabilioni ya pesa nchi za Ulaya na Amerika wakati Watanzania wenzake wanazeeka wakiwa vijana kutokana na kazi ngumu wanazofanya na mzigo mkubwa wa umasikini juu yao.

    Tofauti kati ya Mchawi na Fisadi ni kwamba Fisadi anafaidika (yeye mwenyewe labda na familia yake) kwa Ufisadi lakini Mchawi anamfaidisha Shetani.

    Kwa maneno Mengine Wachawi, Mafisadi, Majambazi, Wabakaji (na mtu yeyote anayehusika katika kuondoa amani kwa watu wengine) ni watumishi wa Shetani na Viongozi wa Dini ni watumishi wa Mungu!

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 02, 2008

    Mungu hadhihakiwi hata siku moja.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 02, 2008

    Asante Yesu kwa kuendelea kujidhihirisha kupitia watumishi wako,maana binadamu wamekuwa wagumu kuamini.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 02, 2008

    Nakubaliana na maoni hususani ya anony wa May 02,2008 9:03AM Tumshukuru Mola kwa kujizihirisha kupitia watumishi wake kuwabaini hawa. Tunazidi kuomba wabainike wengi tu wapo mjini hapa ambao huwezi amini ni warembo na mabishoo wa hali ya juu walakini kazi yao ni kufanya mambo haya ya uchawi naweza kutaja wachache ambao mashoga zao wenyewe wametoa USHUHUDA KANISANI, kwa waliyotendewa na waliokuwa karibu nao, wenye tabia hizi, samahani naomba niwataje ili tabia hizi zitokomezwe ni MWANAHANISI JUMA, NA LILIAN MZIRAY. Lakini Mola si Asumani kwani kila wakijijanya kuwapeleka shoga zao kwa waganga ili kuwasaidia wakati wanawageuka na kumlipa mganga awatendee mabaya na kuwapa mikosi. Wamewagundua, na Michuzi fanya utafiti wako mwenyewe utaona uhakika kuwa marafiki wote wa MAANA wamewakimbia.
    Michuzi naomba usiniminyie hii. Ndio njia pekee ya kutokomeza haya mambo duni.
    Shukrani.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 02, 2008

    Bwana ainuliwe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...