NA MGAYA KINGOBA

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE LEO AMEMTEUA NDUGU MUHIDIN ISSA MICHUZI KUWA MKUU MPYA WA WILAYA MPYA YA TEGETA ILIYOPO WILAYA YA ILALA, DAR ES SALAAM.


TAARIFA TOKA IKULU IMESEMA UTEUZI HUO, AMBAO UNAANZA MARA MOJA, UNAKUJA SIKU MOJA TU BAADA YA SERIKALI KURIDHIA OMBI LA WAKAZI WA TEGETA KUIFANYA SEHEMU HIYO KUBWA KUWA WILAYA KAMILI, NA KUFANYA DAR ES SALAAM KUWA NA WILAYA NNE - ZIKIWEMO ILALA, TEMEKE NA KINONDONI.


KABLA YA UTEUZI HUO, NDUGU MICHUZI ALIKUWA NI MPIGA PICHA MWANDAMIZI WA MAGAZETI YA SERIKALI YA DAILY NEWS NA HABARI LEO, KAZI AMBAYO IMEBIDI AIAGE ILI KUSHIKA WADHIFA WAKE HUO MPYA.


"HAKIKA NIMEHEMEWA KWANI KAZI YA UKUU WA WILAYA SI NDOGO UKIZINGATIA KWAMBA NDIYO SHINA LA SERIKALI KUU" NDUGU MICHUZI ALISEMA BAADA YA KUHOJIWA NA GAZETI HILI LEO JIONI.


HII SI MARA YA KWANZA KWA RAIS KIKWETE KUTEUA WANAHABARI KUSHIKA NYADHIFA KAMA HIYO, WENGINE WAKIWA NI MH. BETTY MKWASA AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA KOROGWE, NA MH, HALIMA KIHEMBA, MKUU WA WILAYA YA KILOSA. WOTE HAWA NI WANAHABARI


AKIONGELEA HATMA YA BLOGU YAKE, MH. MICHUZI AMESEMA KWA LUGHA YAKE ANAYOPENDA KUITUMIA KWAMBA ATAENDELEZA LIBENEKE KAMA KAWAIDA HATA KAMA ANGECHAGULIWA KUWA RAIS.


"HII BLOGU NI YA JAMII HIVYO SINTOELEWEKA ENDAPO KAMA NITAAMUA KUIACHA ATI KWA SABABU YA KUPATA WADHIFA SERIKALINI.
"SIONI NI JINSI GANI NITASHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YANGU KAMA MKUU WA WILAYA MPYA YA TEGETA NA WAKATI HUO HUO KUHUDUMIA JAMII KUPITIA BLOGU YAO HII," ALISEMA MH. MICHUZI.
UAMUZI WA KUIFANYA TEGETA KUWA WILAYA KAMILI UMEFIKIWA BAADA YA KUONEKANA KWAMBA ENEO HILO LILILOPO KASKAZINI MWA JIJI LA DAR ES SALAAM LIMEKUA KWA KASI NA KUWA NA WAKAZI WENGI KIASI YA KWAMBA KUENDELEA KUWA CHINI YA WILAYA INGINE KUNGELETA MATATIZO KWA WAKAZI WAKE.
MH. MICHUZI ANATARAJIWA KUAPISHWA LEO ASUBUHI NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, MH ABBAS KANDORO, KATIKA SHEREHE ZILIZOPANGWA KUFANYIKA KWENYE OFISI ZA MKUU HUYO WA MKOA, ILALA BOMANI.
SOURCE: GAZETI LA HABARI LEO
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 213 mpaka sasa

 1. HONGERA SANA. BIDII YAKO INAKUBALIKA NA KILA MTU.

  KILA LA KHERI KATIKA MAJUKUMU MAPYA!

  MDAU UK rdor7819@hotmail.com

  ReplyDelete
 2. Ongera Bro Michuzi kwa wadhifa wako huo mpya lakini kumbuka kuwa leo ni tarehe 01.april siku ya waji...... Duniani humpati mtu na hiyo Fulanaz

  Mdau

  ReplyDelete
 3. Duh siku ya wajinga 1/4. Jamani huyo mwandishi hata hajui namna ya kuifanya habari iwe ya kuaminika. Yaani aseme Tegeta wakati hata Ofisi ya Waziri Mkuu haijawahi kuongelea hiyo wilaya mpya. Alitakiwa ataje wilaya ya kikweli kweli kule swekeni na akasema aliyekuwa huko atapangiwa kazi mpya.

  ReplyDelete
 4. Mshikaji....hata kama tunabeba box..tuna kumbukumbu kuwa leo ni siku ya wajinga...Michuzi ibane kwanza...tuone utawapata wangapi..teh teh teh

  ReplyDelete
 5. Hongera bwana Michuzi, heheee naona kumekucha! Haya bwana enjoy your day!

  ReplyDelete
 6. Happy APRIL FOOL DAY,Bro Michuuzi...!!!
  ENDELEZA LIBENEKA kaka...

  ReplyDelete
 7. ha ha ha ha ha ha ha eti Mkuu wa Wilaya anaapishwa na Mkuu wa Mkoa! kaazi kweli kweli ... siku ya wajinga baba!

  ReplyDelete
 8. Habari kaka Michuzi,
  Hongera kwa kuteuliwa hewa kuwa mkuu wa wilaya. I hope this is a joke, ni siku ya wajinga leo!
  Neema

  ReplyDelete
 9. Hii kweli ni siku ya wajinga, hadi michuzi naye anatufanya sisi wasomaji wake hamnazo!

  ReplyDelete
 10. Isije ikawa SIKUKUU YA WAJINGA.. 01/04

  ReplyDelete
 11. hahaaaaaaaaaaaaa misupuuuuuuu.jk sasa anachemshaaaaaaaaaaaaaaa

  ReplyDelete
 12. hii ni habari mbaya kwa wanablogu-duuu.

  ReplyDelete
 13. HAPPY APRIL FOOLS DAY!!!!! HAHAHAHAAHAHAHAAHHAHAAHAHAAAAAAAA

  ReplyDelete
 14. sasa ze t shirt yako imelipa wamesema sana na sasa imekuwa kweli

  ReplyDelete
 15. Nimecheka sana bro michuzi ila kwa mtaji huo utawazoa wengi,andaa kapu la kuwahifadhi hahahahaaaaa!

  ReplyDelete
 16. NIMECHAKA, SINA MBAVU......

  HONGERA SANA MHESHIMIWA MICHUZI. NAONA MHESHIMIWA RAIS ANAPOKUAPISHA, AMEKUSHIKA MKONO NA ANAONEKANA KIDOGO SANA(MKONO WAKE).

  MIMI NAONA UTEUZI HUU NI SAHIHI KABISA, KAMA NI KWELI, KWA MAANA MCHANGO WAKE NI MKUBWA KWA JAMII KULIKO WA WANA HABARI WALIOWAHI KUTEULIWA KABLA YAKE. MICHUZI ATAKUMBUKWA NA ANAJULIKANA KWA KUWAUNGANISHA WATANZANIA, NA WALIMWENGU WENGI SANA KOTE DUNIANI. WENGI TUMESAFIRI KWA TASWIRA KWENDA TANZANIA BILA NAULI KUPITIA BLOG HII. PIA, MIJADALA YA KIUCHUMI, KISIASA, KIJAMII NK, IMEFANYIKA KUPITIA KIJIJI HIKI.

  SASA SWALI, SIJUI ATAENDELEA KUVAA TISHETI (FULANA) HIYO HIYO KAMA MKUU WA WILAYA YA TEGETA? INGEKUWA WAZO ZURI ILI WATU WASIMSAHAU KABISA.

  BILA SHAKA MAKAO MAKUU YA WILAYA YATAKUWA ENEO LA 'TANGIBOVU', AU BAHARINI KABISA, MAANA MICHUZI ANAPENDA SANA MAENEO KAMA HAYO YANAYOFANANA NA 'NGURDOTO'* HOTEL....

  Hongera sana Michuzi,

  Maisha ni Kupanda na Kushuka; yeye amepanda!


  Msomaji wa BLOG ya Michuzi,

  MARKO MWIPOPO, USA

  ReplyDelete
 17. HAPPY FOOLISH DAYYYYYYYYYYYYYYY
  HONGERA KAKA MICHUZI

  ReplyDelete
 18. kudadadek...mbn siamini amini hivi!!!! haya ni ya kweli au ndo mambo ya kina Manka..ilimradi baraza lichangamke? Sikupi hongera michuzi manake sina uhakika mkuu,,,,,

  ReplyDelete
 19. Babuuuuuuuuuuuuu....Hongera zako mazzeeeeeeeee !!!! Kweli Bongo Tambalale !

  ReplyDelete
 20. Asante kwa siku ya wajinga!!

  ReplyDelete
 21. kwa mtaji huu sasa niko poa maana kijitalu changu kiko tegeta na sasa wewe bwana misupu or mh.mkuu wa malaya or wilaya,basi ututendehe haki tupate maji na barabara nzuri kwa kweli.Hongera sana bwana misupu naona humu sisi tunaendeleza libeneke tu so hongera sana mdau mkuu kwa kazi mpya ila usije tufisadi wananchi wa tegeta tu

  ReplyDelete
 22. happy fools day....

  ReplyDelete
 23. Its a fools day! teh teh teh....

  ReplyDelete
 24. Nilifikiri kuwa Tegeta iko wilayani Kinondoni...mmh, huyu mdau sio kuwa anaendeleza libeneke la watu ambao sikukuu yao ni leo (AF)?

  ReplyDelete
 25. Happy Fools day mithupu! Bado hujanitia hio kamba! Good ambition tho! Mdau Edmonton Canada

  ReplyDelete
 26. Naona mambo ya April 1st,,, WACHA ZENU HIZO ,,kuna jamaa walishawahi kuambiwa siku kama ya leo ..watu kumi wa kwanza kufika ubalozini mapema watapata viza za kuja Marekani basi watu waliamka saa nane usiku kwenda kujipanga ubalozini Ilipofika asubuhi .. kuja kushituka kumbe ni siku ya mambumbu.. Duniani ..
  Any way lakini jifagilie mzee ip[o siku MAMBO YATAKUWA KWELI..

  ReplyDelete
 27. Mmm! uteuzi huu wa tarehe hii, basi mtawapata wengi.

  ReplyDelete
 28. lol let's see if people will look at the date...

  ReplyDelete
 29. kaka michu nimekupataa,hapy fools day too.wee umenifurahisha kweli.wacha nikauze magazeti sasa.Mdau wako norway

  ReplyDelete
 30. MICHUZI,HABARI ZILIZOPATIKANA SASA HIVI RAIS ABEBATIRISHA UTEUZI WAKO NA BADALA YAKE AMEAGIZA UPELEKWE SEGEREA

  ReplyDelete
 31. Ama kweli sikukuu ya werevu imeanza kwa kasi mpya,Michuzi mkuu wa wilaya mpa ya `tegeta'iliyo ktk wilaya ya ilala na ataapishwa na kandoro, makubwa.
  umesomeka michu,subiri salamu za pongezi.
  tawile.

  ReplyDelete
 32. Bwana Michuzi.

  Sijui kama hili ni gumzo la Muchuzi ama ni taarifa za ihakika.

  Kama ni sahihi basi nakutakia kila la heri katika nafasi yako mpya.

  Kwa kweli sijui kama nikupongeze ama hapana kwa sababu naona kama kazi yako ya zamani iliyokupa nafasi ya kupanda mapipa kila siku na kuona ulimwengu huku ukiwa na vi allowance mfukoni kama ilikuwa bora zaidi ukizingatia kwamba sasa itabidi uwe unakabiliwa na fitna za siasa. Ila nakutakia heri.

  Itabidi vekesheni sasa zipungue ama maadui wa siasa na wenye wivu wataleta kelele. Yaani hapo wilayani likitokea kosa dogo hata kama si kosa lako watasema huyu jamaa kwani anafanya kazi? si yuko kwenye blogu 24/7!!

  Mimi nakuonea huruma kaka yangu ila nakutakia kila la heri!!!

  ReplyDelete
 33. HAPPY FOOLS DAY...

  ReplyDelete
 34. Tusisahau kuwa leo ni siku ya Wajinga duniani.

  ReplyDelete
 35. APRIL FOOL!!!

  ReplyDelete
 36. APRIL 01 FOOLS DAY/LEO NI SIKU YA WAJINGA, KWAHIYO HII NI FIX TU.

  ReplyDelete
 37. kaka michuzi hah ha ha ha hahaaaaaaaaaaa
  Acha kutuzingua sie labisaaaaa, kwakuwa leo ni APRIL FOOL.

  Hiyo wilaya umeiunda mwenyewe kwa raha zako?

  Wewe endelea kutuletea picha sisi na habari, ukuu wa wilaya utaupata ukianza kuwa na MMVI na wajukuu,

  Saa hizi mapema sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

  ha ha aaaaaaaaaaaaa

  dada T

  ReplyDelete
 38. Hongera Michuzi na hii April 01 siku ya....

  ReplyDelete
 39. DAH HONERA KAKA MISUPU KWA WADHIFA HUO NA ULAJI PIA KAMA KWELI KUNA HIYO WILAYA MPYA HUKO BONGO SIKU HIZI, LAKINI PIA SIKUMBUKI ILE SIKU YA WAJINGA HUWA NI MWEZI NA TAREHE GANI KILA MWAKA...ILA KAMA KWELI HONGERA SANA KAKA...

  ReplyDelete
 40. Hongera sana katika siku ya Wajinga! Hongera Ndugu Issa Michuzi Kuwa Mkuu wa Wilaya Ya Tegeta ilipo Ilala!
  Bora kuwa na siku za Wajinga duniani kubadilisha akili!

  ReplyDelete
 41. LEO NI SIKU YA WAJINGA DUNIANI!!.SO DONT FREAK OUT!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 42. Yeah, happy fools day to you too mate!

  ReplyDelete
 43. you Almost got me there. april Fools Day, humpati mtu....Rais Jakaya Kikwete amepinduliwa.....

  -BooSt3D.

  ReplyDelete
 44. ...Is this April Fool's Day Report...Bwana Michuzi...wajinga ndo waliwao...ingawatungefurahi kusikia jambo kama hilo hapo baadae...wewe ni muwakilishi mzuri...

  ReplyDelete
 45. Hongera sana mkuu michuzi. Angalia husije ukaenda kuwa fisadi na wewe.
  Hakika ni habari nzuri sana kwa wanablog wote. Tuko pamoja nawe mzee ktk kusherehekea mafanikio yako ata kama tuko mbali na Bongo.

  ReplyDelete
 46. April fools...!!!???

  ReplyDelete
 47. Yani nusu nianze kujigonga kwako, ili nipate tenda za huko Wilayani.

  ReplyDelete
 48. Unajua umebugi wapi?Jiulize na kanya boya lako.Humpati mtu humu,wewe na libeneke la globu tu mshikaji.Ingawa JK anakusikia na kwa vile wote Bwagamoyo iko siku atafumba macho na kuweka jina lako.tehetehtehe.

  ReplyDelete
 49. Kaka hujatupata bado wananchi leo ni April Fools day. Tumekushtukia....

  ReplyDelete
 50. Hongera sana sana Kaka.. Sasa mambo yameshawiva. Tutaendelea kuwa nyuma yako 2010 endapo utachukua fomu ya Ubunge pia..Safi hiyooo!!

  ReplyDelete
 51. Kaka Michuzi acha kudanganya jamii. Leo ni siku ya
  "wajinga duniani"aka April Fools.Eniwei ni good try.

  ReplyDelete
 52. APRIL FOOL!
  GOT CHA! MICHU BOY!

  ReplyDelete
 53. IS THIS APRIL FOOL THING?

  ReplyDelete
 54. Inshaallah dua lako liwe la kheir
  lakini sio leo MMBADOO!

  ReplyDelete
 55. Michudhiiiii! Hamna cha sikukuu ya wajinga wala nini! Hii ni janja yako tu ya kujipigia ndogondogo kwa muungwana! Hakyanani Michuzi nimecheka vibaya sana! Kumbe ndo mnajipigiaga ndogondogo hivi eti? Una akili sana mwanawane!

  Ewe JK uliyeko Ikulu, tunakuomba usikie kilio hiki cha ndugu yetu Michuzi! Tunaomba hayo kwa jina la gulobu yetu hii ya jamii, tukiamini ya kuwa utatenda baba! Aaaaamin!

  ReplyDelete
 56. Naskia JK kaota ndoto hiyo hiyo leo
  sjui akiamka itakuwaje! michu boy we jitayarishe tu! mwambie mama chanja apige pasi ile suti yetu ya ughaibuni na akubakishie chai japo ya mkandaa kwenye thermosi pengine hutowahi mahanjumati yake asubuhi!
  any way 'LOVE IT. Nyimbo mbaya habembelezewi mwana,sku zote nyimbo nzuri tu!

  ReplyDelete
 57. SEMA WEWE KABUNGA MWENYE KIGUGUMIZI NIKISEMA MIMI MSHAMU NTAAMBIWA MWIZIII. APRIL FOOL!!!!!

  ReplyDelete
 58. OHOOOOO! HONGERA BWANA MICHUZI MWENYEEZI MUNGU AKULAZE PEMA PEPONI. AMEEEEN. [APRIL FOOL]

  ReplyDelete
 59. Thank You Mr. Michuzi kwa kutuanzishia April Fool!!!! Ungepiga tai hapo labda tungedanyika lakini ukuu wa wilaya na T-shirt yako hiyo kauka nikuvae:)Badoo, hujanipata. Anyway, Heri kwa sikukuu ya wajinga!! Samahani nimesahau, Marekani imeamua kumpa U-Rais Obama...!!!

  ReplyDelete
 60. Duu, hiyo kali !!! hivi siku ya wajinga ni lini vile ?

  ReplyDelete
 61. HONGERA KAKA MICHU,MAMBO MSWANO!
  UNIKUMBUKE KWENYE UFALME WAKO,HONGERA SANA.
  JK SIO MCHOYO WA MADARAKA

  ReplyDelete
 62. Hongera sana Michuzi, kutoka Canton, OH.

  ReplyDelete
 63. DUUUH MICHUZI UMENISTUSHA KINOMA BRAZA IKABIDI NIANGALIE KALENDA YANGU KIDOGO ,NA MIMI NIMEAMUA KUKUANDALIA PARTY KUBWA SANA YA PONGEZI IJUMAA HII.FUATILIA MAONI KWA MAELEKEZO ZAIDI. TE TE TE TE TE

  ReplyDelete
 64. T shirt imekuwa DC,
  haki ya baba yake mtume ISSA wa MOHAMAD, we jamaa ni shushu na FISADI wa chini chini, Ila hongera sana mkuu, sasa ze mashimoz, handakizzzz!! umepewa rungu, je utarekebisha?? na ule msitima wa Ilala barabarani bado upo, yaani tutakubana mpaka balaa, Hongera sana mtu wa wadau, Yaani wee sio DC wa Tegeta, bali ni DC wa wadau, michuzi tuombe ushauri ili tukufundishe namna ya kuwa mkali kwa watendaji, maana wee mpole mno ndo ubaya wako!!, duh ila nimecheka saaana!!! kweli mhuni ni mhuni tu hata akifika kwa Mungu, Kikwete ni mtoto wa kihuni! hata ukiibana lakinin utakuwa umesoma! kazi njema RC wa tegeta!

  ReplyDelete
 65. michuzi oyeeeeeeeeeee
  ccm oyeeeeeeeeeee

  ReplyDelete
 66. Uskonde wala nini Michu Boy, utafika tu.Kwanza JK watu wamempungukia wote RICHMOND! Hivi unafkiri ukiingia kwenye ulingo wa siasa kwa kura zetu unaingia kiulaiin tu. Hata mpaka white house tutakupeleka we jaribu zali tu na BLOGU letu tunalibeba huko huko!

  ReplyDelete
 67. ...aaah!haya wajinga wote ndo watakamatika hapa!HAPPY FOOLISH DAY!

  ReplyDelete
 68. na wasiwasi hii sio sikuku ya wajinga mmmh, niko Canada lakini machale yananicheza,tegeta kuwa wilaya??sikuwahi kusikia hilo vuguvugu, nitakupa hongera mpaka gazeti la uhuru wathibitishe, au nisikie kupitia BBC! kama sikukuu ya wajinga ebu ibanie kanza hii mail- tuone watakaovagaa mkenge!

  mdau-canada.

  ReplyDelete
 69. HONGERA MICHU BOY WE HONGERA
  NA MIMI MDAU EEH NIHONGERE
  MAMA UCHUNGU MAMA UCHUNGU
  NYAMA LA MWANANGU OYEEH
  NYAMA LA MWANANGU SUNGULAUDELE
  LINAUMA MNO EH OYEEH
  YUWAPI EH YUWAPI JR AJE HAPA TUHANGAIKE NAE!
  LEO NI LEO LEO NI LEOO
  TUTAWAONA WALO WAJINGA KWELI SIUONGO!!!!
  but i'm not one of them!

  ReplyDelete
 70. hongera sana misupu,itabidi hako katishirt ukatupe sasa,mwendo ni suti tu,

  habari nyingine za kuaminika ni kuwa bwana michuzi ameongeza na mke wa 2 baada ya kuukwaa ukuu,mbona hilo husemi

  ReplyDelete
 71. Hahahahahahaaaa!! Yani nimefurahi utadhani mie ndio Michuzi!! Dah! Ongera sana mtu wetu!! Sasa sipati picha Mkuu wa Wilaya na kamera shingoni! dah! Hii kali ya mwaka!! Poa Bro! Michu! Tunakupa hongera ya mwaka lakini endeleza libeneke mwana wane!! hahahahahahahahh hahahahahaha!!

  ReplyDelete
 72. Mkuu Michuzi,
  Hongera sana. Naona mkuu wa kaya ametambua mchango wako kwenye jamii na juhudi zako.
  Usilegeze makalio huko, kaza buti na kuwa karibu na shirikiana na wananchi wa Tegeta kuwaletea maisha bora.
  Mdau wa JP.

  ReplyDelete
 73. WITH ALL DUE RESPECT TO YOU BROTHER MICHUZI KAMA HII INGEKUWA KWELI BASI JK ANGEKUWA AMECHEMSHA KWA MARA NYINGINE. AU SIO WADAU? APRIL 1ST IS A FOOLS' DAY ... HAPPY FOOLS' DAY

  ReplyDelete
 74. HUNA LOLOTE MISUPU
  HAPI FOOOOOOOOOOLS DEI....

  Ila unajitabiria vizuri na we ukajifisadishe kamgodi ka Kokoto kule Tegeta. loooolz

  ReplyDelete
 75. Aaaaaaaaaaaaaaaaah ... wewe Misenti leo kweli umenipata.
  Leo ni siku ya mafala!

  ReplyDelete
 76. APRIL F...

  ReplyDelete
 77. Mimi binafsi ninapenda kumpongeza ndugu muhidin issa michuzi kwa kuwa makini na kufatilia vizuri mambo yanavyoenda duniani ambapo kumbukumbu yake nzuri imemwezesha kukumbuka kuwa leo ni siku ya wajinga duniani(April 1st- fool day) na tunamuombea busara na kazi njema katika kuongoza wilaya ya tegeta mpaka hapo mnamo saa sita alasiri matani haya yatakapokwisha.
  Hongera sana ndugu mheshimiwa michuzi.
  Chibiriti atakuwa anarukaruka huko anajua atapata udiwani angalau ubalozi wa mtaa huko tegeta, hahaha
  Mdau mjuaji,
  devyako@yahoo.com
  michuzi unaweza kuibania hii comment mpaka baadae- later during the day uwapate vichwa maji mi niko mkao wa kula nasubiri komenti zao

  ReplyDelete
 78. April Fools' Day???

  ReplyDelete
 79. LOLOLOLOL...Duh ni april fool nini???????? but kama ni kweli hongera bro..

  ReplyDelete
 80. EHWALLAHHH!! SASA MJOMBA MICHUZI NAOMBA UNICHONGEE MCHONGO WA KUPATA KIWANJA HAPO TEGETA, BEI MAELEWANO AU VIPI,

  ReplyDelete
 81. Asante Kaka, Leo ndio tarehe ngapi vile? Hongera kwa njozi njema, yatatokea tu siku ya siku!NIMEKUKAMATA!

  ReplyDelete
 82. Wilaya ya Tegeta sio?Ok Hongera Misupu..Usisahau kusherekea vyema siku kukuya WAJINGA.....


  Mwanaharakati

  ReplyDelete
 83. E Bana e! Kudadeki! Yaani Mithupu umelamba dume hivihivi tunakukodolea! Da, hii ni kali. Lakini sasa Mithupu ndiyo umelamba dume, hiyo wilaya ni mpya na najua mambo mengi yatakuwa ndiyo yanaanza. Kwa hiyo Bro wewe endeleza libeneke na pia wawashie moto huko Tegeta mpaka wajue kuwa sasa mambo yanakwenda mbele. Isijekuwa siku mbili-tatu ukazoea mambo ya ofisi kuu ya wilaya ukatuacha juani. Hongera Sana Bro!

  ReplyDelete
 84. kaka Michu acha kuota kaka!!!
  LEO NI APRIL MOSI,SIKU YA WAJINGA DUNIANI,na mimi sio MJINGA

  ReplyDelete
 85. Licha ya kwamba ni siku ya wajinga nakuhakikishia kwamba kitu kama hicho kinakuja ndugu yangu.

  ReplyDelete
 86. Ka'Michuzi, umeiwezea kweli April Fool's day!!!! lol


  SteveD.

  ReplyDelete
 87. Issa,
  Ni kweli kabisa unaweza kuitumia siku kuu ya wajinga ukastukia unapata kula hivi hivi. Ngoja tu-check utawapata wangapi!

  ReplyDelete
 88. Weweeeeeeeee hutupati ng'oooooooo, am not among the other fools......

  Debbie

  ReplyDelete
 89. Hongera Muheshimiwa Michuzi,ninakutakia mafanikio mema ktk wadhifa wako huo mpya, kama ulivyo ahidi tunatarajia libeneke litaendelea kama kazi ama siyo!!!

  ReplyDelete
 90. Siwezi kuwa kati ya hao utakao waongoza katika tarehe ya leo.Happy fools day michuzi.

  ReplyDelete
 91. Hongera Mzee Michuzi kwa kuja na bonge la April fool.Kwa Mungu hakuna kubwa.Iko siku habari hii haitatoka kwenye siku ya April fool.

  ReplyDelete
 92. ahahahaha April fool uwezi kutudanganya bwana.

  ReplyDelete
 93. DUH,HONGERA SANA MHESHIMIWA MANAKE TENA WEWE SI MWENZETU TENA TUTAANZA KUTANGULIZA HILO NENO MHESHIMIWA,MUNGU AKUZIDISHIE NA AKUPE NGUVU YA UJASIRI WA KUONGO ZA WATANZANIA WENZAKO NAJUA UTAWEZA JIAMINI TU SAFI SANA MZEE WA MIKONOZIIIIIII,

  ReplyDelete
 94. Hongera umeambulia mlo ndugu yangu.

  ReplyDelete
 95. ALUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU, haijatulia, leo ni siku ya WAJINGA, wengine sisi bado ni tarehe 31 ila kwa TZ ndio sherehe yenyewe. Endeleeni kusherehekea.

  ReplyDelete
 96. Bro Michuzi ni April Fool day.
  Cheers. JMK

  ReplyDelete
 97. hahaa wajinga ndio waliwao

  ReplyDelete
 98. Hongera sana kaka michuzi...sasa lile tour la kuzunguka mabara yote ulilonitonya pale doha airport ukiwa unaelekea frankfurt si ndio yameota mbawa tena! umeshakuwa mheshimiwa kaka..but u deserve mzee mzima.....nadhan Madaga shabaan madaga nae atakuwa kapandisha munkari kweli kweli....let see, labda raisi akianzisha wilaya ya sinza ..jamaa ataunyaka..ila tafadhali, usiache kutembea na camera

  ReplyDelete
 99. Happy April fool Mithupu!!!

  ReplyDelete
 100. 1 april michu..tumekushtukia.mdau Holland

  ReplyDelete
 101. Congrates bro MICHUZI, hopefully u make this region 2b # 1 passing K'ndoni in the near future. As we all know u will help as many people in that area as u help many thru this glob. Again HONGERA bro
  Mdau T-Dot

  ReplyDelete
 102. leo ni siku ya wajinga ! mimi sio mjinga, umenikosa hapo michuzi !

  ReplyDelete
 103. Acha Uongo Wako Mzee Ki T shirt. Duu Kama Hivo Lazima Michuzimond Ianzishwe Fasta .Hihihihi Ila KAMA NI KWELI NAKUPA PONGEZI KUBWA SANA KAKA MISUPU MAANA HIZO ZILIKUA NI DUA ZA WADAU HADI UBARIKIWE KAKA.(MDAUBOX)

  ReplyDelete
 104. Michuzi kamba hizoo april Fool leo.

  ReplyDelete
 105. Heri ya Siku ya Wajinga..!

  ReplyDelete
 106. hongera kaka michuzi kwa kulamba dume utukumbuke katika ufalme wako

  ReplyDelete
 107. Michuzi labda udanganye hicho kitisheti chako ulichovaa ndio kinaweza kukusikiliza...april fools day!

  ReplyDelete
 108. Michuzi nimekuona kwenye Luninga ukila kiapo na suti kubwa..ila wamesema wilaya yako ni Katalamba sio Tegeta..sasa kaza buti kuendeleza libeneke

  ReplyDelete
 109. HONGERA MZEE WA LIBENEKE.
  ILA ITABIDI UONGEZE WASAIDIZI WAKO WA KURATIBU MAONI KWANI SIO RAHISI MKUU WA WILAYA KUPATA MUDA.
  125th ST./HARLEM.

  ReplyDelete
 110. I hope this is not the april fool thing.

  ReplyDelete
 111. Happy April Fool's Day to you too!!! P.

  ReplyDelete
 112. Mithupu!

  Naona umeula sio, safi sana! endeleza libeneke lako huko Tegeta na ukiweza omba ubadilishe jina la hiyo sehemu paitwe Tegetazzz au siyo?

  Hepi fuls dei!!

  Mdau wa Newala.

  ReplyDelete
 113. unakizizi bro hebu tupatiye na sisi, mara tutasikia umekuwa mbunge au waziri au hata rais wa nchi, big up bro na kizizi tupeane.
  mdau kutoka newala

  ReplyDelete
 114. SIKUKUU YA WAJINGA LEO,HAHAHAHAA.HUNA LOLOTE MZEE WA MIKONOZIIIIII,NIMESTUKA KAKA,DUH UNATISHA KWA UONGO,HAHAHAHA,

  ReplyDelete
 115. leo ni sikukuu ya wajinga bila shaka kikwete kakudanganya tu,hahahahaaaaaaaaaaaaaaa,

  ReplyDelete
 116. Kaka sio mbaya kujikuta uko ndotoni. Allah S.W. anazisikia sala zako ipo siku utakuwa mkuu wa mkoa kwelikweli na sio huu mkoa wa April mosi. Aqram Allawi

  ReplyDelete
 117. APRIL 1 IS A FOOLS DAY

  ReplyDelete
 118. Leo ni sikukuu yetu wajinga a.k.a "Wadanganyika" Kila la kheri wajinga wota duniani katika kuadhimisha skukuu yenu.

  ReplyDelete
 119. ACHA KUTUYAYUSHA WEWE. lEO NI SIKUKUU YA WAJINGA DUNIANI.

  ReplyDelete
 120. hongera kwa habari za kutengeneza
  kwani leo si april full au vp?
  inapendeza lkn unaweza kuja kuwa kweli mkuu wa wilaya

  ReplyDelete
 121. Hongera sana!!! and on another note:
  April Fools' Day is observed throughout the Western world. Practices include sending someone on a "fool's errand," looking for things that don't exist; playing pranks; and trying to get people to believe ridiculous things.

  The French call April 1 Poisson d'Avril, or "April Fish." French children sometimes tape a picture of a fish on the back of their schoolmates, crying "Poisson d'Avril" when the prank is discovered.

  ReplyDelete
 122. happy fools day michuzi

  ReplyDelete
 123. Wacha URONGO bwana misupu.leo siku ya wajinga

  ReplyDelete
 124. Mhhh Sikukuu ya wajinga!

  ReplyDelete
 125. Duuuuh sio mchezo! Yaani bwana Michuzi kidogo tu hata mimi unibambe katika hii siku mambumbumbu.Sasa tatizo nimekushtukia kwenye maeneo mawili.Kwanza kusema taarifa ya ikulu kidogo machale yakanicheza.Maana nijuavyo mimi, japo uteuzi wa MaDC unafanywa na Mh.Rais lakini taarifa yake kwa umma hutolewa na ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI.Lakini lingine ni kwamba kwa kawaida wilaya mpya wanakabidhiwa watu wenye uzeofu na kazi za ukuu wa walaya.Ungetaja moja ya wilaya kongwe ingeingia akilini kidogo.Hatahivyo,ni jambo jema sana kujitabiria
  mafanikio iko siku itakuwa hivyo bwana Michuzi, endeleza ukada kwa nguvu zote.
  Kada,Tumsifu-USA

  ReplyDelete
 126. Hongera sana Bwana Michuzi, nimekuwa nafuatilia kwa makini makala yako, nategemea hutaacha kuandika katika hizi blogu. Mimi ni mtanzania pekee hapa Nepal. Wakati nyinyi mko mwaka 2008 sisi hapa kalenda yetu ni mwishoni mwa mwaka 2063. Hapo April 17, 2008 kwa mwaka wenu sisi huku tutasheherekea mwaka mpya 2064. Bwana michizi mimi nina shida. Kuna mtu alinitapeli kiwanja kule tegeta. Vipi ukiwa mkuu wa wilaya unaweza kunisaidia. Niko tayali kukupa asante 10% of the value. ila kama utaweza kutumia madaraka yako kunitafutia kiwanja kingine nitafurahi. Vipi Mbezi beach itakuwa chini ya himalaya yako?

  ReplyDelete
 127. mmh..happy fools day to you too kaka michuzi

  ReplyDelete
 128. Haya Issa let me hope siyo April`s fools! Kama umetudanganya, ole wako Issa..

  Hahahahah..in anyway you deserve, kwani nini bwana?

  Whatever it is, hongera kwa yote.

  ReplyDelete
 129. Wewe michuzi weweeeeee haaaa unaota siyo! Poa ila dont worry ndoto zako siku moja zitajakuwa za kweli! Unaonekana unachapa kazi ile mbaya usikonde one day itakuwa YES on your side!!

  ReplyDelete
 130. Wewe mwandishi unatufanyia siku ya wajinga sisi kumbe unajifanyia mwenyewe kwa mana hata hujui Tegeta ipo ilala au Kinondoni!

  ReplyDelete
 131. HAHAHAAAA! SIKUKUUU YA WAJINGA LEO HUTUPATI HATA KIDOGO NG'OOOOOO.
  mwaki.

  ReplyDelete
 132. Ap.....FO......Day

  ReplyDelete
 133. Bado hujatu-fool bwana, jaribu tena...

  ReplyDelete
 134. mie sio mjinga
  wadanganyikao ni wajinga
  tar 1 leo ati

  ReplyDelete
 135. Michuzi usishangae watu wakaanza kukupa hongera na Happy Belated Bithday bila kutazama tarehe ya post yenyewe hao utawapata wengi tu.

  Mdau wa kwenye sky

  ReplyDelete
 136. Ha ha ha! You didn't get me on this one! I ain't no Fool. A good one though!
  Mdau
  http://drfaustine.blogspot.com/

  ReplyDelete
 137. Nami nakupa hongera sana maana hata tegeta inakaribia kua nchi itakayojitegemea so una wakati mzuri sana wa kua Rais wa eneo hilo ila angalia yasikukute ya Kanali Mohamed Bakati wa Moheli Moroni Comoro. Weeee
  wapi Kanali Bakari wapi mafisadi wa EPA wapi mafisadi wa Richmonduli wapi
  fisadi namba moja mzee mwenyewe aliekuwepo? mbona kimya sana?

  ReplyDelete
 138. happy april fools day!!!
  u got me, that was good

  ReplyDelete
 139. HappY April Fulllllllllllllll.

  michuzi mm nilishtuka..nilidhani tangazo la kifo, nilikua naogopa hata kuscroll down.hehehe


  HappY ApriL FuLl wadau

  ReplyDelete
 140. Kaka Michuzi

  Leo ni siku ya Wajinga Duniani(April Fool's Day). Na kwa hili nimekushtukia.

  Mdau Dommy

  ReplyDelete
 141. HONGERA SANA BRO. MICHUZI KWA KULAMBA HUO UKUU WA WILAYA. NDIO MAANA HICHO KISHATI CHAKO ULIKUWA HUKIACHI NAONA KINA KAMZIZI. USITUBWAGE TU WADAU MAANA HII BLOG YAKO WENGINE TUNAINGIA HATA MARA TANO KWA SIKU TAFADHALI USIJIUNGE NA MAFISADI UKATUSAHAU.HONGERA SANA!!!!

  ReplyDelete
 142. Hongera kaka misoup nilijua jinsi unavyo kula raha kila siku nilihisi tuu kuna mtu anakubeba anyway hongera sana kaka.

  ReplyDelete
 143. Sheeeeeeeeeeeee!!! no comment

  ReplyDelete
 144. Ebwana Michuzi kaka yangu...Mimi ndio niliacha comment kutoka Canton, OH. Ebwana umenipata kabisaaaa...kumbe leo ni April fools! Hahahaha...Hapa najicheka. Ila uzuri nimegundua mimi mwenyewe kabla hata hujaweka comment zangu zilizopita...

  ReplyDelete
 145. Mhh hii kali. lakini ukizingatia leo ni tarehe 1 ya mwezi wa 4 basi jaribu kupost tena siku ingine, leo haikamati (Son of a peasant)

  ReplyDelete
 146. NI SIKUKUU YA WAJINGA LEO. MIMI SI MMOJA WAO.

  ReplyDelete
 147. ACHA NDOTO ZA ALINACHA HIZO!!!!!

  ReplyDelete
 148. happy fools day michuzi

  ReplyDelete
 149. Ndugu Michuzi....I wish you a wonderful April fool's day.

  ReplyDelete
 150. HONGERA KWA KUDANGANYWA HIVI HATA WEWE MICHUZI NI MJINGA?
  UNAADHIMISHA SIKUKUU YAKO?

  ReplyDelete
 151. kaka hongera tena umepata wadhifa katika tarehe 1 may inamaana huko tegeta ni wa... na siku yao ni leo,sina mbavu

  ReplyDelete
 152. yu r just kidding bro Michuzi, tumekushtukia, maana leo ni cku ya wajinga. ciao!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 153. kaka upo kama betty mkwasa umeuchinja je ka tshirt kwenye vikao vipi?

  ReplyDelete
 154. APRIL FULL

  ReplyDelete
 155. Jamani mie sijui hata tufanyeje!!! sijui tumpongeze Michuzi au tusikitikie Blog yetu hii!

  Ukweli ni kwamba Libeneke litakuwa limefifishwa kwa kiwango kikubwa sana.

  "By the way Hongera Bro Michuzi,"
  Umeula ndugu yetu.


  Mdau.
  DRC

  ReplyDelete
 156. jina mheshimiwa au bro michuzi??? Hongera fanya fituzi sasa wakati ndio huu

  ReplyDelete
 157. Mbona hupost maoni hayo?


  wewe mzee wa Roiko Michuzi Mix unatumix

  ReplyDelete
 158. Samahni, haihusiani na Picha wala maelezo,

  Eti hivi leo ni tarehe ngapi vile??

  Maana kidogo kalenda yangu hapa imeloa na mvua zinazoendelea kunyesha

  ReplyDelete
 159. No one is fool,lakini huwezi jua kaka michuzi mbona Mkwasa kaupata jitahidi kupiga picha na ukiwa karibu na Rais unajifanya uko serious

  ReplyDelete
 160. FOOLS' DAY APRIL 1!

  ReplyDelete
 161. Ha ha haaaaa, April fools day. Ahsante kaka Michuzi

  ReplyDelete
 162. HONGERA SANA, KWA KUKUPONGEZA NIMEKUTUMIA ZAWADI YA BAJAJ KWA MATUMIZI YA HOUSE GIRL WAKO.

  ReplyDelete
 163. SIKUKUU YA WAJANJA!!!!!

  ReplyDelete
 164. hii itakuwa tunapigwa mchanga wa macho ukizingatia leo ndo ile wajinga dei.misupu nimeshtukia te te te heeh..

  ReplyDelete
 165. leo hii hii april fool? haya bwana ngoja tukupe tu hongera kwa kuwaza mbali.

  ReplyDelete
 166. WEWE MICHUZI ACHA HIZOO! LEO SI NDIO SIKUKUU YA WAJINGA...HUNIPATI N'GO!

  ReplyDelete
 167. leo siku ya wajinga....hujanikamata bado...ila subiri wabeba maboksi waamke na comments zao za kufurahisha...haya...mimi simo

  ReplyDelete
 168. 1st April, fools day

  ReplyDelete
 169. Hahahahaha, very funny, but Happy April Fool Kaka Michuzi.

  ReplyDelete
 170. aaaaahhh WAPI ,HILI CHANGA LA MACHO JIBABAB,MICHUZI WENGINE BADO SISI HUKU TULIKO HAIJAFIKA TAREHE MOJA MWEZI WA NNE SAAA HIZI SOO .
  BADO SILIKUBALI DOMNGO HILI.
  WEE SEMA UNAONYESHA " FULANAZZZZZZZZZZZZZZZZ"
  MDAU HOUSTON

  ReplyDelete
 171. Ha ha ha haaaaaaaa...Kaka michuzi utawapata wasukuma peke yao!!! me ndo maana nimeamua kuzima siku yangu kwani mwaka jana nilipatikana kwa kupigiwa simu kuwa nimeshinda Rav4 Celtel, nilitimka kutoka ofisini kwangu hadi Celtel nikajikuta natoa macho getini, walinzi wananiuliza nikasema nimeshinda Rav4, wao hawana MBAVU KWA KUCHEKA!! Kumbe walishaenda na wengine kabla yangu.

  Hongera sana kakangu, may be utajapata uheshimiwa siku moja Inshaallah!!! DREAMS COME TRUE!!!!

  ReplyDelete
 172. Congraturation mdau but am worried it might be another fools day.

  ReplyDelete
 173. Hahahahaha!

  April Mosi, siku nne kabla ya siku yangu ya kuzaliwa!
  Safi sana, utawashika wengi tu!

  ReplyDelete
 174. Wajameni hivi leo ni tarehe ngapi? Otherwise Hongera bro michuzi kwa uteuzi huo ambao mwisho wake ni saa 4 asubuhi kwa saa za africa mashariki. Big up sana

  ReplyDelete
 175. fools day

  ReplyDelete
 176. Mich nimeustukia leo ni siku ya wajinga kwahiyo hapa kidogo umeteleza ingawa kwa wengine lazima wangejua ni kweli eheeeeee eheeeeee eheeeeeee eheeeeeeeeeeeee

  ReplyDelete
 177. hilooo leo ni cku ya wajinga hata humpati mtu!
  mdau XXXL

  ReplyDelete
 178. Hii kama siyo April mosi sijui.Unajua leo ni siku ya wajinga.Kama ni kweli Mh.Michuzi kaula, basi nampa pongezi.Kama ni siku ya wajinga duniani,Basi nimemstukia.
  Mdau Ujerumani

  ReplyDelete
 179. Humpati mtu hapa Michuzi na hiyo April fools day yako....

  Overland Park, Ks

  ReplyDelete
 180. Is it because of April's fools day?

  ReplyDelete
 181. "Hongera" ila mimi nilisikia kuna mpango wa Bw. Michuzi kupewa machimbo ya mererani ili ayaendeshe kwa muda hadi hali itakapokuwa salama baada ya janga lililotokea!!

  ReplyDelete
 182. tarehe moja mwezi wa nne.

  ReplyDelete
 183. daaaa michuzi leo sio siku ya wajinga kweli?
  maana hii habari ya wewe kuwa mkuu wa wilaya naiona kwenye blogu yako tuuu.
  hongera sana mkuu kwa kuwa mkuu wa wilaya ila leo siku ya wajinga.
  Amen

  ReplyDelete
 184. Hivi Raisi gani awezaye kuwa Mjinga akachagua Mjinga siku ya sikukuu ya wajinga awe mkuu wa wilaya ilyojaa.........!!!!!

  ReplyDelete
 185. hamna kitu km hiko michuzi,leo ni siku ya wajinga ila fresh 2 jipigie debe,uenda siku moja ikawa kweli ukaukwaa ukuu wa wilaya sumve

  ReplyDelete
 186. Hivi leo ndiyo siku ya wajinga duniani?

  ReplyDelete
 187. We Michuzi usituzingue wala nini-leo ni April 1st kwa hivyo story kama hizi zitakuwa kijiji.

  ReplyDelete
 188. Mkuu hongera saaana!!
  Keep up the good work na huko kwenye wilaya!!

  ReplyDelete
 189. Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Misupu!!!! unaota Mchana Eti eeeh. Unalo hilooooooooooooo, utalinywa Mwenyeweee wadau hatumo.... hakuna MJINGA HAPA!!! UKITAKA UKUU WA WILAYA ANZA KUVAA SUTI MFULULIZO... AFU UKIPATA UKUU WA WILAYA..FAITI UJE MWANZA - NYAMAGANA TUKUPIKIKIE SUPU YA SATO FRESH, UPATE KITAMBI KDG. TEH TEH TEH!!!

  ReplyDelete
 190. UNCLE MICHUZZZZZZ,
  KUMBE BONGO TANZANIA NI TAREHE MOSI APRILI TAYARI! NIMEJUA KWENU TAYARI NI SIKU YA WAJINGA! NIMEANGALIA KALENDA, NIKAPIGA HESABU ZA HUKO NA KUGUNDUA HUKO NI APRILI TAYARI, NDIYO MAANA SIKUNG'AMUA TANGAZO HILO MAPEMA, MAANA HAPA US BADO NI APRILI 31, 2008.

  NAJUA WENGI WATAPATIKANA TU HASA WALIOKO UROPA NA KWINGINEKO. HONGERA LAKINI KWA NDOTO, UNAWEZA KUKUTA UNATEULIWA KIKWELIKWELI, WHO KNOWS MAN!

  M. Mwipopo, USA

  ReplyDelete
 191. Lols, you almost had me there! But then i remembered its April Fools Day!

  ReplyDelete
 192. Wajinga day michu!!!! usituzingue!!!!

  ReplyDelete
 193. April Fool Day, Issa Michuzi has no ambition of being a politician. GOOD try though
  Listen to him talking with Dewsi on Radio BUTIAMA.

  UJUMBE ENDELEZA LIBENEKE

  By Mchangiaji.

  ReplyDelete
 194. Michuzi sasa ni wakati muafaka kufanya hesabu ya wajinga katika globu yako. Katika wote waliotoa comments, hebu tuhesabie ni wangapi walioingia mkenge na ni asilimia ngapi ya wote?

  ReplyDelete
 195. SASA ITABIDI NA WEWE UPATE WASAIDIZI AMBAO NI CHIBILITI BIN CHIBATARI NA MANKA MUSHI KAMA UKIWA UPO KWENYE HOLLIDAY WAO WATALIENDELEZA LIBENEKE WILAYANI.CHIBILITI RUDI BONGO SASA NI TAMBARARE WEWE UMETEULIWA KUWA MAKAMU WA MKUU WA WILAYA.APRIL FULLYYYYYYYYYYYYYYYYY

  ReplyDelete
 196. MICHUZIII kumbuka leo ni sikukuu ya wajinga. Mdau wako Mnamba.

  ReplyDelete
 197. kweli leo umewaokota wengi ambao walikua hawajui kama ni fools day

  HAPPY FOOLS DAY

  ReplyDelete
 198. Michuzi umewadaka kiasi ila siyo kwa sana

  Katochi)

  ReplyDelete
 199. tehe tehe.....
  kaka michu mbona hujamalizia taarifa yako kua utaapishwa viwanja vya jangwani saa 5.30 am.na watakaotoa burudani ni ze comedy.big up.ritha

  ReplyDelete
 200. Michu, ukitoka ukuu wa wilaya mpaka kuwa rais wa tanzania. Ukifikisha miaka 71 kama mc cain

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...