Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akichanganya michanga ya ardhi ya Zanzibar na Tanganyika wakati wa Muungano 1964 huku (kulia) aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Rashid Mfaume Kawawa akiangalia tukio hilo na nyuma (kushoto) aliyekuwa Rais wa Zanzibar Abeid Amani Karume akishuhudia tukio hilo.

Zaidi ya karne tunayoijua sisi nchi yetu ya Tanganyika ilipewa jina hilo, ambalo kwa lafdhi ya baadhi ya wazungumzao lugha ya Kiswahili Afrika Mashariki, maana yake ni "Changanyika". Je, aliyeipa jina hili la Kuchanganyika kabla ya tukio la hapo juu halijatokea, alikuwa na HIKMA yoyote?
Ahsante Kaka


Mhariri - Zenjydar Community Association

-- Zenjydar Community Association

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. kitendo cha karume kutochukua mchanga km nyerere wakachanganya pamoja inaonesha kuwa rais wa muungano ndio mwenye mamlaka hivo nyerere ndio mwenye mamlaka ya huu muungano kwani tuliona namna alivoweza kuiendesha znz mpaka ikafikia mda kumlazimisha aliyekuwa rais wa znz kujiuzulu kwa maslahi ya taifa jeuri hii nyerere alikua nayo kitu ambacho kwa bahati mbaya sana rais kikwete inamshinda tunaona namna anavoiachia znz kuteseka huku akijua ni kwa hali hiyo taifa litataabika ipo haja sasa tukatanguliza maslahi ya taifa mbele wakati huu wa kusheherekea muungano. udumu muungano

    ReplyDelete
  2. wadau naomba kuuliza kijisuali kwanini mwalimu alichanganya michanga peke yake?na wala hakumshirikisha rais kalume

    ReplyDelete
  3. jawabu ni kua nyelele likua mbinafsi ndo mana kachanganya mchanga alone..period!
    na mie hapo hapo nataka kuuliza kajisuali kadoogo tu...
    huu muungano kwa kweli hasa una faida gani ambazo bila kukuwepo muungano zingekosekana??

    ReplyDelete
  4. Nami nauliza karume ni yupi? huy mwanaume karibu na nyerere au yule kule nyuma kulia kwa nyerere ukimuaca kawawa anayepiga makofi.

    kwanini akisimama mbali kiasi kile badal ya kumsaidia rais mwenzake? si nure kuna namna na kuna ujumbe hapo. labda alilazimisha hivyo ilikuwa ni namna y akuprotest. hii imekaaje wanahistoria nassi watoo tujueE

    Kawawa wewe bado upo hai tusaidie kisa cha hiyo itifaki ya kinamna kama unavyoona hata wewe uko mbali lakini karume yupo masafa

    ReplyDelete
  5. Matonya kwenye nyimbo yake ya Anita amekataza mambo haya amesema USICHANGANYE CHANGANYE

    ReplyDelete
  6. Jamani eeee namie nnakajiswali kangu kuhusu huu tunaouita muungano , IVI KWANINI KILA MWAKA SHEREHE ZAKE KITAIFA ZIFANYIKE DARISALAAM TUU ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...