Habari za leo wadau,
Ule wakati tulio usubiria sasa umefika, Website ya pekee itakayo jishughulishaktk kuutangaza muziki wa Tanzania ipo jikoni na ina karibia kuiva.

Unataka kusikiliza muziki wa nyumbani? Basi watembelee wajuzi wa fani hiikupitia
www.mkmusicgalaxy.com kwa miziki mipya na ya kizamani uburudike na roho yako.

Kumbuka, hawa ndio walewale wakiokupaga raha siku za nyuma na mambo ya mahusiano.com. sasa wamekuja upya!!

Nawatakia siku njema.


Kind Regards,

Support Department

MK MUSIC GALAXY - Exploring the Tanzanian Music.

Part of MK GROUP OF COMPANIES (T) LTD - http://www.mkgroupltd.com
Tel: +44 - 752 - 792 - 9234

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Michuzi asante sana, mimi ni yule yule wa Washington DC niliyekuwa nafuatilia na wewe kuhusu Mahusiano.com. Jana tu nilijaribu kuangalia kama wamerudi hewani nikakuta hewa. Anyway, nimefurahi sana, kwakweli hakuna website ya miziki ya TZ kama Mahusiano, wengi wamejaribu lakini mh...

    ReplyDelete
  2. Mimi Mjenga nchi sio mbomoaji:
    1. Wewe mwenye mahusiano dot nini sio mahala pa kutangaza web yako
    2. Nimeicheki ila bado yainesha unastahili kazi sana maana maPOPups kibao na hizo singoz mbona zinaniridairekt katika web nyingine.
    3. Huna Home button so najikuta lazima nirudi mwanzo kwa kukclick back haahahhaha
    4. MK ni wa hapa au wa wapi? maana muziki wa home (japo mmeweka michache hata cd moja haijai) na namba ya Nje uzalendo unanisuta hapo, kimasoko na kudaka mioyo ya watu mngeweka namba ya home kuepuka kuonekana mna vijisent nje ya nchi
    5. haha hahahaah ah

    ReplyDelete
  3. Anony wa Tarehe April 29, 2008 10:01 AM, kweli waenga walisema akili ni nywele kila mtu ana zake,

    1: Kila mtu ana haki ya kufanya lolote, haujui kwamba this is free world. Pia wewe sio michuzi kipi kinacho jifanya kuingilia?.

    2: Umechemsha kwa kwenda ktk website ambayo si yenyewe. Web tunayo ipata na tunakula miziki ni www.mkmusicgalaxy.com. siku nyingine utulie mzee.

    3: Home button ipo, jaribu kuangalia website vizuri.

    4: Namba za Tz nimeiona ktk website yao, ata kama isingekuwapo haujui ya kwamba ktk maswala ya biasha dunia imekuwa kijiji kimoja? Hii haujulishi kuwa na namba yoyote ile.

    5: Watu wanabaki wanakucheka wewe kwa kutokukaa chini na kusoma ujumbe vizuri na kukimbilia mahali si penyewe.

    6: Ushauri:
    Next time, Jaribu kuwaza kitu utakacho kufanya kabla ya kukurupuka.

    Nawakilisha Huston.

    ReplyDelete
  4. Sasa mbona video ziko tatu tu? Ama ongezeni ama mzitoe kabisa hizo tatu tujue kabisa kwamba hakuna video.

    ReplyDelete
  5. Anony wa 10.01 mshamba big time, nadhani hayuko conversant na computer halafu anajidai kuchonga saana. Jifunze computer kwanza weye, alaa! Watu tunajivinjari miziki kibaoo karibu alfu moja wewe unaruka ruka tu sijui kwenye website gani. Ati pop ups, kwani wewe hujui kucontrol popups kwenye computer yako? Ah, sorry probably ulikwenda kwenye internet cafe, si ndio?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...