Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kiongozi wa Chama cha Upinzani nchini Zimbabwe ,The Movement for Democratic Change(MDC)Bwana Morgan Tsvangirai jana jijini Addis Ababa wakati viongozi hao walipokutana kwa mazungumzo ya faragha katika hoteli ya Sheraton.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete awali alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe Bwana Stanley Shimbalasha. Pichani Rais Kikwete akisisitiza jambo wakati akizungumza na waziri huyo wa mambo ya nje wa Zimbabwe katika hoteli ya Sheraton jijini Addis Ababa jana jioni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Shikamoo anko michudhi mimi ni mwanafunzi wa daratha la tatu shule ya mthingi Kithutu.Naomba kuulidha huyo morgan alienda Adith Ababa kama nani?Raith wa Dhimbabwe?Au alipeleka malalamiko yake kwa mwenyekiti wa AU?Athante mjomba michudhi,lakini mbona mwenyekiti wa AU amekaa kimya kuhuthu zimbabwe tofauti na jirani dhetu walipota matatizo karibu ya kufanana na haya ya Dhimbabwe?

    ReplyDelete
  2. kweli tabasamu la jk si kwa kila mtu.ebu ona morgan anamsalimia kwa tabasamu yeye kauchuna.mmh

    ReplyDelete
  3. ...body language ya picha ya chini ni kama vile mwenyekiti anasema 'achaneni na hiyo biashara ya kung'angania madaraka. Mambo yalishaharibika!

    ReplyDelete
  4. Huyu Morgani ni kibaraka wa wazungu na anatumia matatizo ya wananchi wa Zimbabwe yaliyosababishwa na vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi kwa serikali ya Mugabe ambavyo vimeporomosha uchumi wa nchi hiyo ili apate uraisi na kuwatumikia wazungu. Kwa sasa afrika haihitaji kiongozi wa namna hii bali inahitaji kiongozi aina ya Mugabe ambaye ana uwezo wa kuwasema wazungu bila kuuma maneno. Pia viongozi wetu wa kiafrika inabidi sasa waache unafiki na kuwaambia wazungu kwamba afrika ina uwezo kwa kujisemea na kuamua mambo yake kwani ni aibu kuona mambo ya afrika yanapangwa na kusemwa na wazungu na watekelezaji ni waafrika. Viongozi wetu kuweni na confidence kwani nanyi mmepatikana kwa demeokrasia na mnaongoza watu kama viongozi wa nchi za magharibi. Inasikitisha kuona mambo yanayoamuliwa na nchi za magharibi ndiyo yanakuwa msimamo wa nchi za afrika na yanatekelezwa ipasavyo lakini mambo yanayoamuliwa Adis Abas yanaishia kuwa blaa blaa tu na hakuna linalotekelezwa.Why? kwa nini? au kwa sababu ya umasikini wetu? kila jambo zuri kuhusu waafrika lazima kuna mkono wa wazungu!! Hii ni aibu. AFRICA IS MATURE ENOUGH, LET'S BE ONE VOICE. Jamani sasa umefika wakati wakuchambua kipi ni kibaya na kipi kizuri kuhusu afrika na siyo kuwa watu wa kupokea tu kwa visingizio vya umasikini kwani siku hizi kuna NGO'S hata zinadiriki kutoa takwimu za uongo ambazo zinaonyesha matatizo ya afrika ili zipate pesa. Hivi mkionyesha takwimu halisi hamtopata pesa? Tena haya mambo yanafanywa na wasomi na kila siku ndiyo wa kwanza kulalamika kuhusu haki za binadamu huku wao ndiyo wa kwanza kuwadhalilisha waafrika wenzao. Acheni, hii ni aibu kwani mara nyingi kwenye makongamano ya kimataifa utasikia mambo mabaya kuhusu afrika ndiyo yanawasilishwa na mazuri ya wazungu. Tubadilike, tusiwe kama kasuku.

    ReplyDelete
  5. This is a wave of political change spreading across the african continent like a 'democrazia virus' and nobuddy absolutely nobuddy including Kikwete,Museveni,Gadhafi,Biya,& Co. will ever be able to stop it!Katika hili hakuna 'kura ya maoni' wala 'usanii wa kisiasa'.Ole wenu muibe kura tena Zanzibar 2010,itawatokea Puani! Kamuulizeni Mugabe,hajui kagongwa na Dude gani!Dude hilo linaitwa 'MULTI PARTY DEMOCRACY'.Ukiwa Fisadi umeula wa Chuya,njomba Palanchichi(Francis)!Wali kwa Kima bwana Ntaaamu tafikiri Kalima yeye!

    ReplyDelete
  6. Annon hapo juu usuluhishi mwingine si wa kuweka mambo hadharani.we unataka umuone kapanda ndege mpaka harare kisha aongee na waandishi?
    Suala hilo ni nyeti.Atoswe mugabe na mabeberu warudi,kwa mlango wa demokrasia?
    Kinachofanyika sasa kwa maoni yangu ni jinsi gani pande zote zitaridhika.
    Ikumbukwe kua kumtosa mugabe ni rahisi sana lakini kuung'oa ubeberu gharama yake kubwa ikizingatiwa kuwa atakua analindwa na wababe wote wa dunia.
    Sasa picha umeziona kama ulivyotaka subiri kitakachofuata.
    Kwa maoni yangu mchakato umeanza na wote wamealikwa hakuna aliejipeleka,tuwaombee wavuke salama vinginevyo mimi na wewe tujiweke tayari kujiandikisha kwenda kuikomboa tena zimbabwe.

    ReplyDelete
  7. Hizo tumeshazizoea.
    Maalim seif mwenzenu anakula posho na mafao kama mstaafu wa smz.
    hakuna mseto wala dengu nenda kama hutaki rudi oman ukatawale jangwa tupu

    ReplyDelete
  8. unajua michuzi nadhani huyu mugabe ndiye anakuaga agenda kubwa sana kwenye vikao vya sadc, jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa afrika, kikwete anajitahidi.

    ReplyDelete
  9. Mtoa maoni wa 1.16PM wngi wetu hatuelewi kimetusibu nini hasa sie waafrika wenyewe, angalau wazungu wanajua kilichotusibu na wanatuchezea kama mwanasesere watakavyo. Huu ni ujinga wetu wenyewe wakutotaka kujua mambo kwa upana wake na kukalia kula propaganda za magharibi. Ikiwa waafrika wenyewe tutakuwa na msimamo thabiti wakukataa kutawaliwa basi kina mwanasesere kama huyo hapo juu wa Zimbabwe hata pata nafasi ya kutaka madaraka ili awatumikie mabwana wanaompa mapesa kwa kuwarudishia nchi waendelee kutawala na yeye aendelee kuwa mwanasesere. Hivi watu hawajifunzi kwa yaliyomkuta Sadam Hussein, alichezewa kama mwanasesere wa plastici akaviringishwa kila walivyotaka na kutumika kuwaua jirani zake wa Iran. Lakini matumizi yake yalivyoishwa aliyeyushwa kama mwanasesere aliyetiwa kwenye moto wa gesi. Na huyo bwana Tsv naye ajifunze, angekuwa si kibaraka sidhani kama angekosa sapoti ya viongozi wa Afrika. Ukitaka kujua msimamo wa AU kuhusu Zimbabwe ingia kwenye website yao wameshatoa press release nami nawaunga mkono kwa msimamo huo.

    ReplyDelete
  10. Wewe unayesema Morgan Changirai ni kibaraka wa wazungu ukome kabisa na usirudie tena.

    Morgan ni mgombea uraisi halali wa zimbabwe ambaye hata tume ya uchaguzi Zimbabwe inamtambua kama mgombea uraisi halali.Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe ni ya wazimbabwe na wameona anafaa kuwa mgombea uraisi.

    Wewe Unayemwita Morgan Morgan Changirai kibaraka wewe ndiye kibaraka wa Mugabe mshenzi mkubwa wewe.Kibaraka ni kibaraka tu uwe wa mzungu au mwafrika.

    Wewe kibaraka wa Mugabe nenda kamuulize Mugabe nyumba na pesa zake walizotaifisha wazungu Ulaya na Marekani pesa zake alizitoa wapi? Kama siyo kuwaibia wananchi wa Zimbabwe.Wazungu walipomjia juu wakaamua kutaifisha mali na mi-akaunti yake Mugabe Ulaya na Marekani ndio anajitia kuwa mtetezi wa wanyonge ili ajifiche huko.Pesa na mijumba yake ulaya na Marekani imekwenda Mugabe amebaki na kelele tu za danganya toto jinga hata hajui akimbilie wapi sababu ya ulofa hajui ataishije huko atakakokimbilia anabaki kushilia kukataa kuondoka uraisi.

    Morgan Changirai hoyeeeeeeeeeeeee.
    Robert Mugabe na mkewe ziiiiiiiii

    ReplyDelete
  11. TVs sio kibaraka msiwafanye watu waliomchagua kwa kura nyingi kuwas ni wajinga hawajui walichokifanya.Mugabe sasa hivi ameshapitwa na wakati na kinachomponza sasa hivi ni tamaa ya madaraka.Miaka 84 still anataka madaraka.Tusiwalaumu wazungu kwa ujinga wetu wenyewe, angalia mfano mdogo tu jinsi siwe wenyewe tunavyojitafuna, watu wamesoma kuliko kabla ya kupata uhuru lakini hebu angalia ujinga uliopo kwa viongozi hao tunaowategemea mfano wakaribu na mdogo Mh Chenge Mh Mcapa halafu zikija shida mnsema wazungu. tusitafute visingizio visivyo na msingi

    ReplyDelete
  12. Sielewi watu wengine humu,sijui ni ujinga au kutokuelewa,mnawalaumu wazungu kwa swala la Zimbabwe,kwani wazungu ndio wamepiga kura...wananchi wamepiga kura na wapinzani wameshinda ndio maana Mugabe hataki kutoa matokeo,yaani kwa mawazo kama yenu ndio maana tunarudi nyuma kila siku!

    ReplyDelete
  13. Ndugu zangu wachangiaji na watoa maoni, Naamini kila mtu atoapo maoni yake huongozwa na utashi wake na uelewa wake katika upeo mbalimbali wa uelewa wa siasa, uchumi wa kimataifa nk...
    Tatizo kubwa nilionalo katika nchi zetu za Afrika ni kile nikiitacho kujificha katika kichaka cha karanga. Wazungu wanaendelea kutuchezea kama wanasesere kwa sababu moja tu. Hatujakubali kuwa binadamu wote ni sawa. Tunasema hivyo tu lakini najua kuwa watu wengi wanaamini kuwa mzungu ni bunadamu mwenye Quality nyingine. Ndo maana kama muafrika ameoa au ameolewa na mzungu swali linakuwa: Nasikia wewe umeoa/umeolewa na mzungu bwana...Kwanini swali lisiwe nasikia umeoa/umeolewa na ikawa ndio basi...na mifano mingi mingi...Tunahusudisha mambo ya nje kuliko ya hapa nyumbani (exocentrism). Alafu tatizo la pili; We don't mind our own business... hili linatufanya tunakosa "ownership mentality" mfano wake ni ule wa wananchi kuuza nchi yao kwa watu wengine kwa njia za rushwa...kwa mfano immigration workers wanapouza passports kwa watu wasio watanzania, kiongozi kuamua ku invest billions katika foreign countries badala ya kuinvest nyumbani at the same time anasafiri kwenda kutafuta wawekezaji hapo nyumbani....
    Na la mwisho ni short sightedness ya kimawazo. Ukiwaza wizi na unyang'anyi unaofanywa na mafisadi, ni mfano mzuri wa kutowaza mbali. NI mali nyingi ambazo mtumiaji hatazimaliza na hajui kuwa hata watoto wake watazitumiaje maana hawezi kuelezea sources na jinsi ya kuziendeleza. Anyways blablabla... tunahitaji kubadilika all in all na ni kizazi hiki cha watu waliozaliwa kuanzia miaka ya 1970 ndo mnatakiwa kuwaza strategic plans za ku own back our countries and our nations. Kwangu mimi naona tu kuwa mkoloni amebadilika rangi kutoka mzungu na kuingia mkoloni mweusi na looting inakuwa ile ile kama mkoloni mweupe alivyokuwa anafanya... Kibaraka namba moja ni yule anayeiba mali Africa na kupeleka majuu... Ikiwa Tsv anafanya hilo, sawa yeye ni kibaraka na ikiwa mpango wake ni kuwawezesha wazimbabwe wastop hiyo inflation... basi nadhani yeye ni genuine leader aliyeshinda uchaguzi... demokrasia imechukua mkondo wake.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 01, 2008

    Mi naona ni heri Wazungu warudi hata Tanzania, wata-FISADI ila wananchi watapata huduma nzuri, mabarabara, watapata ajira na si hali ya sasa bn inaitwa visenti. INAWEZEKANA HIYO KAULI INAMAANA NZITO Kwamba mbona wafisadi wenzake wanazaidi ya hizo?

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 01, 2008

    Ukweli unabaki palepale ya kwamba Morgan ni kibarka wa wazungu na sera zake zinapangwa na wazungu na hivyo hafai kuitwa mkombozi wa wazimbabwe. Kitendo cha chama chake kupata kura nyingi za ubunge haimanishi kwambwa wananchi wanampenda sana ila inawezekana wananchi walilishwa propaganda mbaya zilizotengenezwa magharibi na pia hali iliyopo ya uchumi. Tatizo kubwa la waafrika ni uwezo wa kuchambua mambo kwa wakati muuafaka na kuchukua maamuzi stahiki ni mdogo na hivyo kufanya wanasiasi matapeli kuwatapeli kiurahisi wakati wa uchaguzi na kuja kustuka baadae. Mifano ni viongozi ambao wanalalamikiwa kwa rushwa lakini wanashinda kila chaguzi. Morgan na vibaraka wenzake wanaoishi kwa misaada ya wazungu ndiyo wanaochangia uchumi wa zimbabwe kudorora kwa kuiongopea dunia kwamba zimbabwe haki za binadamu zinavunjwa sana. Hivi wahahisi hao wazungu kwao hawavunji haki za binadamu na kwamba hizo haki zinavunjwa afrika tu? Acheni ukibaraka, zimbabwe ilishakombolewa na hivyo tusingependa kuona wazungu wachache wanatunyanya ktk ardhi yetu. Huu ni ujinga mkubwa kwani kwao watunyanyase na kwetu pia tuwapigie magoti kwa sababu ya rangi yao. Vibaraka tafuteni njia nyingine ya kuishi

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 01, 2008

    Hii ngozi yetu ina matatizo! Utajiri tunao lakini kutwa kusingizia wazungu! Uchumi mby wa nchi zetu unatokana kwanza na uongozi mbovu uliojaa watu wenye tamaa, mafisadi wasiojali watu wanaowaongoza! Watu wanalipa kodi lakini hakuna hata panadol hospitali, miundombinu mibovu, maji safi na salama issue! Umeme hapa TZ only 10% wanapata na sio wa uhakika, shule kibao hazina walimu wala vifaa vya kufundishia...KODI ZETU ZINAENDA WAPI? JERSEY BANK? KUNUNUA MASHANGINGI NA KULIPA POSHO ZA SAFARI ZA WAKUBWA NA ZILE ZA WABUNGE! HAPA PIA MTASEMA WAZUNGU????

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 02, 2008

    Zimbabwe itakuwa bora mara kumi bila ya Babu Mugabe,sera mbovu zimeharibu Zimbabwe,na uamuzi wa kuchukua mashamba kwa wazungu wachache wa Zimbabwe ilikuwa ni njia ya kujinufaisha kisiasa baada ya kuona amefilisika.Afrika haitaji viongozi kama Mugabe wanaotumia njia zote kubaki madarakani.Suala la kuchelewesha kutoa matokeo ya uchaguzi wa urais ni Wazungu pia?Tusizingie upumbavu wa viongozi wa kiafrika kila kitu wazungu.Hivi kuna maana kumpa ardhi ekari miamoja mtu wakati uwezo wake ni kulima hekari moja?
    Lazima watu wakubali Zimbabwe kuna matatizo makubwa hata wazimbabwe wenyewe wanajua hilo.Mgombea wa MDC ni mgombea halali na wana haki wananchi wa Zimbabwe kujua matokeo,MDc imefanya kampeni za uchaguzi wa hofu kubwa na hawakupewa uhuru sawa wa kunadi sera zao kama chama cha dikteta Mugabe lakini watu wa Zimbabwe wamechagua MDC hakuna propanda wala nini.Mambo ya Zimbabwe ni ya aibu tupu!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 21, 2008

    huyu jamaa mugabe atakumbukwa kwa kumlinganisha na amin,bokassa,mobutu,nguema,dos santos n.k. this mugabe just by himself has run zimbabwe to the ground, mnakumbuka kile kikosi cha fifth brigade amabcho kilimaliza watu wa matabeleland katika miaka ya 1980s kule aliwamaliza kabila ya nkomo kwa sababu walikuwa wapinzani, sasa kawarudia washona wenzake kina morgan wanapigwa hadharani kama vile nini. kitu cha kujiuliza wakati anauwa ndebeles nyerere alisema kitu? sasa mnataka jk amwambie kitu gani huyu haramia mugabe? morgan brother hawa kina jk,mbeki n.k. bure tu hawatakusaidia kitu. watu kazi yao kulaumu wazungu tu hawana wanachoelewa, leo mugabe akiachia madaraka, watu zimbabwe wataanza kufufua makaburi yaliyojaa maiti huko matabeleland, its damn shame

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...