Mwenyekiti wa AU Jk akimpa tano mwenyekiti wa kamisheni ya umoja wa afrika (AU) aliyemaliza muda wake profesa alpha oumar konare ambaye leo kakabidhi madaraka hayo kwa mh. jean ping huko addis ababa ethiopia
JK: Bei hizi za mafuta zinatuua
*Aitaka Afrika kuongeza sauti yake kuhusu bei za mafuta na chakula
Na Freddy Maro
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Mrisho Kikwete amelionya Bara la Afrika kuamka na kuanza kutafuta njia za kukabiliana na tatizo la bei kubwa za chakula na mafuta duniani.
Akizungumza leo katika sherehe ya makabidhiano ya uongozi wa Kamisheni ya AU kwenye makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, Ethiopia, JK amesema kuwa bei hizo ndiyo changamoto mpya na kubwa zaidi kwa wakati huu ya Afrika na uongozi mpya wa Kamisheni ya AU.
Katika makabidhiano hayo, Mwenyekiti wa Kamisheni iliyomaliza muda wake, Alpha Omar Konare wa Mali amekabidhi madaraka kwa Mwenyekiti mpya, Jean Ping wa Gabon.
Kabla ya kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kamisheni ya AU, Konare alikuwa Rais wa Mali wakati Ping alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Gabon.
Rais Kikwete ambaye alikuwa Mwenyekiti na msimamizi mkuu wa sherehe hiyo, amewaambia mamia ya watu waliohudhuria sherehe hizo: “Kamisheni mpya inaingia katika madaraka wakati Afrika inakabiliwa na changamoto mbili kubwa sana na mpya. Changamoto hizo ni bei kubwa vya chakula na bei kubwa ya mafuta.”
Ameongeza: “ Kama changamoto hizo hazikukabiliwa haraka na ipasavyo zitamaliza kabisa chumi nyingi za Afrika, ambazo kwa bahati nzuri zimekua zinakua vizuri katika miaka michache iliyopita.”
JK amesema kuwa iko hatari kubwa kweli kweli kuwa mafanikio yote ya kiuchumi ambayo yamepatikana katika Afrika yatamezwa na bei hizo kubwa za chakula na mafuta.
“Katika hili, sauti ya Afrika inatakiwa kusikika na uongozi katika jambo hili unatakiwa kuonekana dhahiri,” amesema JK.
Mbali na changamoto hiyo ya bei za chakula na mafuta, Rais Kikwete pia aliorodhesha changamoto nyingine zinazolikabili Bara hili kwa kadri uongozi wa Kamisheni unavyotoka mikononi mwa kundi moja kuingia kwa kundi jingine, kwa amani.
Changamoto nyingine ambazo zitaukabili uongozi huo mpya, kwa mujibu wa JK, ni migogoro katika Darfur, Chad, Jamhuri ya Afrika ya Kati, na Somalia.
“Pia hali za DRC, Burundi na Zimbabwe zinahitaji uangalizi wa karibu wa AU.”
JK pia ameutaka uongozi huyo mpya kuongoza mjadala kuhusu utekelezaji wa Azimio la Accra kuhusu mwelekeo wa baadaye wa AU na mapendekezo ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja ya Afrika na pia kuongoza mjadala kuhusu tathmini ambayo imefanywa kuhusu AU yenyewe.
Hata hivyo, JK ameongeza: “Pamoja na kwamba changamoto ni kubwa na ni nyingi, lakini sina shaka kwamba taasisi yetu iko katika mikono yenye uwezo na yenye uzoefu ya Jean Ping, Makamu wake Erastus Mweche na makamishna wengine wapya.”
Ameongeza kuwaambia viongozi hao wapya“ Hili linanifanya niwe na imani. Kwa niaba ya Serikali na Watu wa Afrika nawaombeni kusimama kupambana na changamoto hizi.
"Najua mtaifanya kazi hiyo, kwa ufanisi.” Rais Kikwete pia ameelezea baadhi ya mafanikio ya AU katika kipindi kifupi tokea kuanzishwa kwake kutoka taasisi ya zamani ya Organisation of African Unity (OAU).
“AU sasa imejijenga kama taasisi ya kikanda inayoaminika na inayotegemewa kwenye uwanja wa kimataifa. Matokeo yake ni kwamba AU imejenga ushirikiano wa nguvu na Umoja wa Ulaya, Japan, China, Korea Kusini, Nchi za Marekani Kusini na hivi majuzi na India. Tunatarajia kuwa uongozi mpya utaimarisha mahusiano hayo na kujenga mpya.”
JK pia amemwagia sifa kemkem Konare kwa uongozi wake wa AU. “Profesa Alpha Omar Konare ni mtu wa mawazo mengi na makubwa. Visheni ya AU ya mwaka 2015, kimsingi, ni matunda ya ubongo wake; matokeo ya bongo yake inayochemka na visheni.
"Ndani ya moyo wa Afrika, kuna sehemu maalum ya Afrika, na watu wake. Ni Mwafrika kweli kweli kwenye sifa ambazo ni ngumu kuzielezea kwa ufasaha wa kweli kweli.”
Ameongeza JK: “Profesa Alpha Konare ni mtoto wa kweli kweli wa udongo wa Afrika ambaye ameitumia taasisi yetu vizuri sana na kwa ari, moyo mkubwa wa kujitolea na imani kubwa. Profesa Konare siku hizo amekuwa chanzo cha ari kwetu sote.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jean Ping:
    The son of a Chinese trader and a Gabonese mother,Jean Ping is was one of President Bongo's closest and longest-serving ministers and one of the most powerful figures in Gabon. His half-Chinese parentage is one reason, however, why he is never likely to become Gabonese president after Bongo leaves power,

    Ping was one of the key figures who helped arrange the visit to Gabon in 2004 of Chinese President Hu Jintao, who used the capital Libreville as the platform for making a land-mark speech promising a new era of engagement with Africa, "without political strings."

    Ping was formerly married to Pascaline Bongo Ondimba, President Bongo's daughter who is on the board of directors of several companies including the oil company Total Gabon. Pascaline is now married to Gabonese Oil Minister Paul Toungui.

    ReplyDelete
  2. Kwisha kazi! Hiyo profile tosha kutuambia huyo mteule ni nani.

    60s na 70s baada ya vikao vya OAU ndege zilikuwa almanusura zigongane kwenye maeapoti na angani kwa jinsi walivyokuwa wanawahi kuwa wa kwanza kubreak news kwa De Gaulle, Pompidou, d'Estaing na Mitterrand. Na wengine walikuwa wanawahi London kwa Douglas-Home,Wilson, Heath, Callaghan na Thatcher kuwasemelea wenzao waliokosa heshima kwa dola kuu.

    Sad but it is a fact, that we are still the same as way back to 60s and 70s. Hatukui, tumedumaa.

    ReplyDelete
  3. Kuundwa kwa AU hakujamaanisha kitu chochote zaidi ya kutengeneza "nchi" nyingine masikini itakayoomba misaada na kudhulumu watu wake!
    KUna njia nyingi za kushirikiana bila kuwa na formal union.
    Tuache porojo,tujenge nchi...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...