Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika ikulu ya Entebbe jioni hii.
JK , Museveni wazungumzia Burundi
Rais Kikwete, Museveni wazungumzia Burundi Na Mwandishi Maalum Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo (Aprili 30, 2008) mchana amewasili mjini Entebbe, Uganda, na moja kwa moja kuingia katika mazungumzo ya faragha na Rais Yoweri Museveni wa Uganda katika Ikulu ya Entebbe.
Rais Kikwete amewasili Uganda akitokea Addis Ababa, Ethiopia ambako alikuwa kwa siku tatu kwa shughuli za nafasi yake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
Mazungumzo kati ya marais Kikwete na Museveni kwenye ziara hiyo ya kikazi ya siku mbili, yanahusu hali ilivyo katika Ukanda wa Maziwa Makuu, na hasa katika Burundi.
Rais Museveni ndiye Mwenyekiti wa hali ya Ukanda wa Maziwa Makuu, na Rais Kikwete ndiye Makamu Mwenyekiti.
Pamoja na kujadiliana kuhusu hali ya jumla ya Ukanda wa Maziwa Makuu, viongozi hao wawili walisisitiza hasa hali ya amani na usalama katika nchi ya Burundi.
Katika siku za karibuni, waasi wa kikundi cha PALIPHEHUTU-FNL wameanzisha tena mashambulizi dhidi ya majeshi ya Burundi, na dhidi ya mji mkuu wa nchi hiyo wa Bujumbura, kinyume cha makubaliano ya amani kati ya pande hizo mbili.
Kabla ya kuwasili mjini Entebbe, Rais Kikwete alikuwa Ethiopia ambako alishiriki katika shughuli za AU, ikiwa ni pamoja na kushuhudia mababidhiano ya madaraka kati ya uongozi wa zamani wa Kamisheni ya AU na ule upya.
Kamisheni ya Afrika ndiyo huendesha shughuli za siku kwa siku za AU. Katika makabidhiano hayo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Alpha Omar Konare wa Mali alimkabidhi madaraka ya kuendesha Kamisheni hiyo Mwenyekiti mpya, Jean Ping wa Gabon Jumatatu wiki hii katika sherehe iliyofanyika Makao Makuu ya AU mjini Addis Ababa.
Mbali na kushuhudia na kusimamia mabadhiano hayo, Rais Kikwete pia alihudhuria kikao cha Kamisheni ya Amani na Usalama ya AU ambacho kilizungumzia migogoro ya Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. MMh Ama kweli Mganda ni Mganda tuu ! sasa Mzee Museveni na hiyo Kofia ya jua shambani ndani ya sitingi rumu ya hadhi namna hivyo ni aje ?? Anamletea ubishororo JK hajui kama mwenzie Braza Meni nambari one. Ama nielewesheni labda mimi ndio wa kuja !

    ReplyDelete
  2. Mseveni na hiyo kofia - akiwa ndani haitoi? Pink furniture and white chairs!! May be the colour softens his mood.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2008

    Hi! Mr.Michuzi,nafurahi kuona kilakitu kinaendelea vizuri as planed!

    Mimi ninaushauri mmjatu kwa Watanzania wenzangu.

    Huyo Mseveni, anatakiwa kuangaliwa kwamakini sana, na Hata JK anapo deal nae awe makini sana, Mseven sio tena Mwana mapinduzi kama alivyo inia Madarakani mwaka 1986,sasa hivi ni mtu mwenye uchu na madaraka, na mwenye kutaka kutawala milele.

    Sasahivi anataka kumpush JK ili Africa mashariki ziungane,sasahivi sisi kama Tanzania Hatujawa Tayari kufanya hivyo, ilayeye anataka kama kutumia Ubabe wakidiplomasia,kwamba yeye ndio mzoefu katika marais wote wa Afrika amsahriki,kwahiyo anataka kutumia huo ujanja ili awa convince hawa Marais wengine wakubaliane nae, Kenya walisha kubali ila Tanzania ndio tulikua bado.

    USHAURI;
    Tusidanganyike na Uzoefu wa Mseveni, Napenda Kumkumbusha Rais Na Watanzania wote kwa ujumla, Kwamba Tanzania nichi yenye uzoefu mkubwa sana Kisiasa,kwasababu tuna maofisa wangapi ambao wame staafu ila bado wapo? natuna marais wangapi walio staafu nabado wapo? natuna wakuu wa majeshi wangapi walio staafu na bado wapo?
    Uganda ni nchi changa sana ukilinganisha na tanzania,kwahiyo tuendelee na msimamo wetu wakuto kuji unga mpaka tutakapo kua tayari kufanya hivyo,tusilazimishwe wala tusiwe influenced kwasababu yoyote.

    Namoja ya mapendekezo yangu nikwamba Tusiungane mpka hapo Uganda itakapopata Democrasia ya kweli.
    Kwasababu mpaka sasahivi,Mseveni simtofautishi na Mugabe wote nia madictator.
    Tuliangalie hili swala kwasababu sisi ndio tutakuja kuumia.Rais kikwete atamalizamdawake na ataondoka,huyo Rais Mwingine atakae kuaja pia asije akajikuta anaingia kwenye mitego ya Mseveni.Kwasbabu najua Raisi mwingine atakuja atamkuta Mseveni bado nirais.Mseveni ndio mchochezi wa vita nyingi mpaka sasa zinazo piganwa katika maziwa makuu,kwahiyo Tuwe makini na Mseveni,naninasikia ana push Afrika mashariki iungane ili yeye ndio awe Rais wa Afrika mashariki, kama anaiendesha hivyo nchi yake, je ataiendeshaje Afrika mashariki, kaa,tafakari,chukua hatua.

    Mdau.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2008

    Natamani JK angemwalika IKULU ya TZ aone ma interior decoration!Hizo rangi mmh! Sijui kakumbuka kumwuliza anaachia ngazi lini?? Maana JK anaweza kupiga 10 bora zake na kumwacha jamaa akiendelea kuwa BOB MUGA WA ZIM au 'RAIS WA MAISHA WA UG!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2008

    Naungana na mdau wa 11:56AM kwa 100%

    Museveni ni DIKTETA ambaye kwa sasa anasaidiwa kwa karibu sana na GADAFI wa Libya. Amewapa waganda upofu wa kisaikolojia, na anatumia fedha za nchi kununua pillars of support.

    Kuna haja ya WATANZANIA kuanzisha Non-violence movement kumpinga huyu jamaa kwa nguvu zetu zote. Akija Bongo tumpokee kwa mabango n.k.

    Muda sio mrefu, yaliyojiri Kenya na yanayoendelea Zimbabwe yataikumba Uganda. Tanzania nayo itaathirika!! Hatuwezi kukwepa hili. JK anatakiwa kuwa makini sana. Museveni alifanikiwa 'kumnunua' Mkapa na kati ya mengi aliyofanya kupata support yake ni 1.Kuahidi ujenzi wa shule ya Msingi, na 2. Kujenga HOTELI YA KIFAHARI huko Entebe under partnership (MUSEVENI + MKAPA) ambayo kwa sasa iko finishing.

    Watanzania, Museveni sio mtu wa kuchekea hata kidogo. Ni dikteta; mbaya kwa Afrika! Mgogoro wa DRC yupo! Mgogoro wa Somalia yupo! Mgogoro wa Kenya alikuwa kinara wa Kibaki, hata kumpongeza kwa 'ushindi' dakika za awali. Mgogoro wa Rwanda alikuwepo, na thanks God Kagame amemstukia. Mgogoro wa Burundi ana mkono wake! Jamani... huyu ni dikteta. Shime vijana ... you are the cause of change, non-violently!

    Seve

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 01, 2008

    kaka Michuzi hao manony wawili hapo juu wameongea sawia kuhusu udikteta wa Museveni mimi sina la kuongeza tuu isipokuwa naomba uhakikishe hizi salamu zinamfikia Mheshimiwa Rais JK. Najua kwa umri wake na upeo wake wa kisiasa ana hekima nyingi ya kuwatambua watu kama hawa na Alhamdullilah mwenyezi Mungu katujaalia kipindi hiki Tanzania Kiongozi asiye na uchu wa mali na anaelekea kujali mawazo ya wananchi anaowaongoza hivyo natumai kaka Michuzi sisi sio tunakomment comment humu halafu hufikishii walengwa inakuwa haina maana tunatwanga maji kwenye kinu. Lakini mzee nakuaminia una contacts na networking kila kona so I hope Mheshimiwa Rais huwa unamjulisha na akipata muda katika busy schedule yake anasoma maoni ktkblogu yetu hii tukufu. Wasaalaa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 01, 2008

    jami hivi mume-notisi ya kwamba hiyo kofia ni ina kamba ..........!! duu Baganda noma

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 01, 2008

    Nchi za Afica jamani...yaani pamoja na umasikini halafu tanazidi kuuwana tena? Hivi NGOZI nyeusi ina laana? Watu wengine wanapigana lakini sababu si mtu mmoja au kundi fulani kung'ngania madaraka na Utawala.

    Nchi za Africa sasa ziige mfano wa Angola. Inatosha kuuwana. Mbona zinakuwa kama ni nchi zilizojaa WACHAWI tu?

    Halafu wanaongeleaje Mambo ya Burundi wakati Viongozi wa Burundi hawapo?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 01, 2008

    Naona 'wanamitindo' ni wengi humu naona madongo kwenye kofia ni mengi.

    Wabongo kwa kuvaa tu...ndiyo maana utakuta mtu akiwa mtaani kamechisha lakini ukifika home kwake analala kwenye mkeka!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 02, 2008

    HAPO SIJUI NANI NI MWANAMAPINDUZI KWANI WOTE NCHI ZAO ZINAMIGOGORO YA KISIASA NA HAWATAKI KUITATUA BALI WANAJISHUGHURISHA NA MATATIZO YA NCHI ZINGINE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...