Ndugu Wadau,
Chuo cha LONDON SCHOOL OF COMMERCE (associate college of university of wales) kinatangaza usajili maalumu wa wanafunzi wapya wa mwaka huu wa masomo 2008/9 unaoanza mwezi wa sita (June) 2008.
Kwa taarifa zaidi na kozi mbalimbali wanazotoa tembelea tovuti yake www.lsclondon.co.uk .Kuna punguzo maalumu la Ada kutoka £6450 mpaka £3950 kwa mwaka wa masomo huu kwa wanafunzi wa kitanzania watakaopitia kwangu kuomba na kukubaliwa masomo yao hapa chuoni, punguzo hili maalumu utalipata kwa kuwasiliana nami ili nikuwakilishe hapo chuoni.
Naomba wanafunzi wenye interest na kusoma chuoni hapa kwa kozi zilizotangazwa kwenye tovuti ya chuo tuwasiliane kwa namba yangu hii hapa +447506458289.... au email hii
ally.abdallah@lsclondon.co.uk
Natoa tahadhari kwamba Mimi ni wakala wa wanafunzi wa kitanzania ninayehusika na punguzo la bei tu.. Sihusiki kabisa na upatikanaji wa kibali cha kuingilia Nchini (visa), kwahiyo naomba nisiulizwe maswali kuhusu swala hilo,chuo kitakamilisha kila taratibu za mwanafunzi aliyekubaliwa masomo na kupata nafasi chuoni ili eweze kupata visa..
kwa maelezo zaidi kuhusu upatikanaji wa visa za uingereza bofya hapa http://www.ukvisas.gov.uk/en/
Ni matarajio yangu, kila mwenye kutaka kupata habari zaidi za kusoma chuoni hapa na punguzo hili la bei atapitia tovuti ya chuo (www.lsclondon.co.uk) kwanza na kumaliza mushkeli aliokuwa nao, kisha kuwasiliana na mimi ili kupata punguzo hilo la ada.
NB: unapowasiliana nami tafadhali nukuu jina la chuo kwanza LSC na wai umeona tangazo hili halaf endelea na ujumbe, maswali yako nk.
TAHADHARI: Sitopokea malipo kutoka kwa mwanafunzi yeyote yule,ada na malipo mengine yanafanyika katika kitengo husika chuoni, ili upate punguzo ni kuwasiliana na mimi nikupe taratibu husika (Bure).
Asanteni

,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Thats kind of you man. Keep it up.

    ReplyDelete
  2. Bwana Abdallah,ni jambo zuri unalotaka kulianzisha hapa,lakini tunakuwa na wasiwasi ati!Tunaomba ujitambulishe hapa wewe ni nani na unaishi wapi(street n.k)picha kama huoni hatari,ili watu wakufahamu kama hapo unaposema haupo kuna wadau wengi huko watatueleza.Dunia sasa hivi imekuwa hatari,yanatoka hadi matangazo ya kazi uko Ulaya mtu unaacha kazi bongo unafika ubalozi wanakwambia hilo shirika/kampuni hai/lipo kwao.Ndiyo hatari ya email hiyo.Unaweza kum-rob mtu kwenye email na kumwingiza mjini.Kama kweli uko serious jiweke hadharani.Siku-challenge tunaogopa Wanaigeria!!Asante.Muhidini u need to be a bit careful yasije yakawa yale mambo ya salaam kutoka...........!!!!!

    ReplyDelete
  3. sasa nyie mbona mnaanza uzushi? mshikaji anataka kusaidia wabongo wa huku waweze kuongeza elimu wewe unaanza kuquestion maswali wakati yeye anafanya bure hataki hata sumni, unajuwa ni jinsi gani vigumu kupata £6000?
    hiyo kazi unayoo fanya mzee babu kubwa kwani mimi mwenyewe nishasikia kuwa wewe mzee unatowa msaada kwa wabongo tupate discount, waambie kama wanaona vipi waende holborn college same course same university lakini ada £6950

    ReplyDelete
  4. Mdau Tarehe April 29, 2008 3:05 PM
    Mimi Ndie niliyepost Tangazo hili kwa michuzi.. Nadhani nimeeleweka pale niliposema kuwa mawasiliano yote yawe ni moja kwa moja na chuo, Address ya chuo ndio address yangu ya Ofisi nayo nimeambatanisha hapo kwenye PDF file iliyo pembeni mwa Tangazo.. Nimeweka Wazi kabisa Kwamba ili upate Punguzo Hilo unatakiwa kuwasiliana na Mimi kwanza ili nikuunganishe na chuo.. Malipo na taratibu Nyingine zote utafanya na chuo moja kwa moja bila Mimi kuhusika.. nadhani Mnaelewa maana ya wakala Wadau. Sitoweza kuweka picha kwasababu za kiusalama. Siui lakini Wabongo hatupendiani mema, Who knows what will happen to me then..! Pili Si katika sheria za kazi kutangaza kwa kutumia Picha binafsi kwakuwa mimi Ni wakala tu na Muajiriwa wa chuo, Sio mmoliki wa chuo. Nafahamu kabisa wimbi la wasanii na matapeli Waliopo kwa kulenga wadau wa nchi za dunia Ya tatu kama wanavyoziita, Narudia tena , SITOPOKEA MALIPO YA AINA YOYOTE KUTOKA KWA MDAU YEYOTE.

    nakutakieni Maisha mema na taratibu njema za masomo.. Karibuni LONDON..
    Ally Abdallah.

    ReplyDelete
  5. Ally- Umefanya jambo la maana kabisa. Hilo jambo unalolifanya linaeleweka vizuri kwa watu waliokaa nje ya nchi na wachache waliotoka kidogo japo kuosha macho.
    Kwa wale ambao hawajatoka basi ujue maswali na wasiwasi utazidi kuwepo,kwa kuwa waombaji wengi wako au watatoka Tanzania. Kama ulivyosema waanze kuwasiliana na chuo, then swala la kupata Discount hilo wakufuate wewe baada ya kumalizana na chuo kwa kila kinachowahusu. Mie naona umejiileza kiu-naga baga na sijui kwa nini watu wanaanza kuleta za kuleta. Everything is clear. Ila nakuomba usijibishane na watu hapa katika hii blogu maana kama unavyojua uhuru wa habari na kujieleza mara nyingi huwa sisi tusio waungwana tunautumia kwa kuonyesha ujinga wetu hadharani, na hasa katika vioo visivyotuonyesha sisi ni akina nani.
    Natumai hicho chuo ni accrediated na nashukuru umetupunguzia watu wanaosema kila siku tuwasaidie form za vyuo waje kusoma.

    ReplyDelete
  6. Chuo kiko accredited na body zipi? kuna chuo cha London school of excutives kimewaibia watu wengi hivi karibuni.naomba sana watu wafanye utafiti wa kutosha kuliko kujitosa kwenye vyuo vya mitaani. siku zote bure ghali.hasa kwa vyuo vinavyosema kuwa viko affiliated na chuo kingine.
    Michuzi naomba usiondoe hii post yangu kwa maslahi ya Wa Tanzania.
    Namuamini Abdallah lakini nina watu wamesoma sehemu miaka mitatu na kuchukua cheti kumbe si genuine.

    ReplyDelete
  7. kaka michuzi chuo hiki hakina shaka mimi nasoma hapo na watumishi wa serikali yetu wapo hapa na wengine ni waalimu wa vyuo vikuu nyumbani wamepitia hapo kwa hiyo wadau uwanja ni wenu mwakilishi ally asante sana kwa kazi nzuri wenzetu wakenya wamepiga hatua kwa sababu wanainformation nyingi,information is power,kama wasemavyo wenyewe wadau nawasilisha ughaibuni LSC,MBA-student,nondo itakamilika next year university of wales inshalla nitairusha.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 02, 2008

    Ndugu Abdallah ni pongezi sana kwa habari zako,ila kuna umuhimu gani kama shule wanatoa discounts kwa wanafunzi wa kitanzania wapitie kwako??wakati kila kitu kimejieleza kwenye website yao mimi nimesoma mara kibao hapa sasa hivi,au kama kuna kitu unapata kupitia hao wanafunzi bora ukaweka wazi tuu wadao wakaelewa mambo yote kuliko kuweka mambo under pants ndiyo maana wana wasi wasi,asante kwa habari yako tupo details zaidi kuhusu hawa wanafunzi kupitia kwako unafaidika vipi,maana haingia akilini London ilivyo busiest area akafanya kazi ya bure tuu.

    Asante mdau Canada

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 03, 2008

    hongera ally abdalla,vijana wa kitanzania tunasikitisha sana, eti mtu kaamua kutoa information ya kusaidia wanafunzi anaulizwa kama yeye anafaidika vipi kifedha!!keshakwambieni yeye ni mmoja wa wafanyakazi hapo chuo, na kutoa information ni free yes london ni buzy city lakini information ni free.msimdhanie mambo mabaya kwanza amekwishabainisha kuwa yeye hapokei malipo yoyote.sisi tuliyo london tunajua hii habari ya hichi chuo kutoa discount,this is genuine deal ili vijana wa kitanzania wajiendeleze kielimu.kuna watu wana ugumu kweli kwa kuelewa au labda sio wasomaji basi tuu wamezoea kuzozana bila mpango wowote alimradi na yeye atoe comment!!!si uingie usome habari ya hicho chuo!!?? kama yeye ally analipwa au halipwi inakuhusu nini wewe??? yeye ametoa habari tuu.mbona mkiomba information na vyuo hamuulizi waliotoa information wanalipwa na nani??na kuhusu kama chuo kinafaa au feki , ndio maana akakwambia uingie kwenye link ya chuo ufahamu zaidi kuhusu hicho chuo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...