Mtoto Ramadhani, siku alipokutwa na kichwa, alimpa onyo mwandishi wetu kuwa naye hana muda mrefu wa kuishi)


“Wakati mwanangu anaendelea kucheza nje niliamua kuweka neti kitandani ili aje alale na kabla sijamaliza kutandika akaja baba yake akaniuliza alipo mtoto nilimfahamisha kuwa anacheza nje ambapo alikwenda kumuangalia, baada ya muda alirudi ndani akaniambia hajamuona.


“Hata hivyo, shangazi yangu aitwae Furaha Majani ambaye tulikua naye ndani alitoka nje kumtafuta bila mafanikio hali hiyo ilinipa wasiwasi na kunifanya nitoke nje kumuangalia lakini nami sikumuona.

soma zaidi kwa kubofya hapa





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. michuzi tukitaka kusoma zaidi hiyo habari inasema error, page not found!! please jaribu kuiweka vizuri tuweze soma!! ni habari ya kusikitisha, na tunahamu kujua kinachoendelea, plz plz tusaidie kuiweka page sawa. Mungu aiweke roho ya mtoto huyo mahala pema, na huyo kijana na wenziwe waliofanya hivyo, nawe hukumu yao iwe kama walivyomfanya mwenzao

    ReplyDelete
  2. Inasikitisha kweli maskini, ah Africa mambo ya ajabu tunayapenda! Mimi hata huyo mtoto mchawi nae namuonea huruma tu for God's sake he's just a kid himself, sijui ndio mambo ya kurithishana uchawi?? Jamani halafu haya mambo ya kuwaacha watoto wanazagaa nje kucheza na wenzao inabidi tuyaache mambo mengi yanaweza kutokea kwa mtoto, hili ni mojawapo na kubakwa etc etc. Mimi ni mzazi wa mtoto mdogo tu na nina uchungu sana na kilichomtokea huyu mama wa watu. Mimi mwenyewe nilipokuwa mdogo nilicome close to incidents za kubakwa, so I have learnt from my own experience. Watoto wako kwenye risk all the time.

    ReplyDelete
  3. hivi bwana Michuzi kama angalau angekuwa amechinjwa mtoto wa mdogo wako ungeandika "LIBENEKE LINAENDELEA KIANA" kama kichwa cha habari hiyo ya kusikitisha? binafsi nimesikitishwa sana na hiyo lugha. Unaweza kuacha kwa kuwa blog ni yako na wewe ndo mhariri, mwandishi na kila kitu. lakini nakuomba ufikiri kama wazzazi wa salome wakisoma sidhani kama watafarijika.

    ReplyDelete
  4. Mwenzenu kila nikiona sura ya huyu kijana inanichafua kweli, yaani hafai kupewa publicity namna hii, kilicho baki siku ya kunyongwa ikifika ndio tuonyweshwe umauti wake fisi huyu.

    ReplyDelete
  5. Imenishitua sana, imenisigitisha sana na kunifadhaisha sana kwa tukio hili la kinyama. Mimi kama mzazi nipo pamoja na wazazi wa Marehemu Salome katika majonzi makubwa.Naiomba serikali ifuatilie jambo hili sio kwa kuamini kuwa ni jambo la kishirikina bali kwa kuwa ni mauaji ya kinyama na kubaini kundi zima lilohusika kwani hainingii akilini kama Ramadhani alikuwa pekee ktk tukio hili. Kwa upande wako Bro Michuzi kichwa cha habari sio mahali pake hili ni jambo la kweli na la huzuni ebu jaribu kuweka kichwa kufuata tukio. Mungu aiweka roho ya Marehemu Salome pahali pema peponi.

    ReplyDelete
  6. Michuzi au Anayehariri naona mliposoma shule ya Msingi mliruka kusoma kile kipengele cha "Ufahamu" ambapo kwenye kiinglish kiliitwa 'Comprehension" hicho kichwa cha habari hapo juu hakifanani kabisa na habari. Kama vile unaleta masihara wakati watu tumeumizwa na habari hii mpaka miili inasisimka. Ushauri naomba uwe unandika kichwa cha habari kifananacho na habari yenyewe. Isiwe kama magazeti fulani nisopenda kutaja majina yao. Naomba kuwakilisha. mdau Arusha.

    ReplyDelete
  7. Mimi naweza kukubali kweli huyu mtoto ni mchawi lakini tukio hili la kuchinja mtoto ni la kihalifu na huenda halihusiani na uchawi. Nahisi hivyo kwa sababu huyu mtoto anasema yeye na wenzake anaishi kwa kula nyama za watu lakini hatujawahi kuona vipnade vya miili ya watu kama huu wa salome na pia kama kweli wanakula hizo nyama za watu inamaana kichwa tu ndicho kiliwacho? Mimi naona huyu mtu ni muaji na huenda alikuwa ana sababu zingine za kufanya hili tukio na kitendo chake cha kukipeleka muhimbili inaonyesha alichanganyikiwa baada ya kumchinja huyu mtoto. Polisi inabidi imbane vizuri huyu mtoto na ukweli utajulikana.

    ReplyDelete
  8. Cherry unamawazo kama yangu mi kila nikipita humu sitaki kuangalia hiyo sura ya huyo mlawatu, najisikia kuwaka hasira na kichefuchefu kila nikimuona, hata zile kauli zake, alizokuwa akizitoa wakati wanamnyang'anya kichwa alokuwa nacho, inanisumbua sana.

    Poleni wafiwa, na mimi ni mzazi, najua uchungu mnaoupata mpaka sasa, na hamtazoea itabaki kifuani kila mnapukumbuka. Mungu wa haki atawalipia kwa haki ishallah.

    ReplyDelete
  9. michuzi unawafariji wafiwa au unawazidishia machungu?? mimi nilifikiri sisi watanzania wote tunawajibu wakuwafariji lakini naona kwako wewe ni tofauti sna unaposema libeneke sijui kama unawafariji au unawazidishia machungu badilika kaka


    chelsea

    ReplyDelete
  10. jamani hata mi nikimwangalia huyu mtoto mchawi nasisimka duuu wakuuliwa tu huyu mtoto hafai kabisa. jamani salome mtoto wa Mungu roho yake ilazwe mahali pema AMINA.
    Sweet
    Arusha

    ReplyDelete
  11. Poleni sana wafiwa na mwenyezi Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu. ninachokifikiria mpaka mwili unasisimka ni kuwa maumivu aliyoyapata huyo malaika wakati anafanyiwa ukatili huo, ni siri kubwa ameondoka nayo. Mimi binafsi wala sitaki kuamini kama huyo muuaji ni mgonjwa wa akili. angekuwa ni mwehu mbona hakukibeba kicwha waziwazi kutoka tabata mpaka muhimbili na alikihifadhi vizuri ndani ya mfuko ili watu wasikione, au mbona hakukila hicho kichwa kwenye daladala? enhh yeye si mwehu!! na mbona kiwiliwili alificha vizuri akakizingirisha kwenye kanga na akakidumbukiza kwenye shimo la choo na juu akafunika na kitu ili watu wasione, si angekitupa tu hata nje ya nyumba yao!!! hata sijui huyu kijana wakimsogeza mita mia kutoka nilipo nitamfanya nini, nina uchungu sana naona kama amenichinjia mwanangu. nahisi serikali na mimi ingenifunga. May her soul REST IN ETERNAL PEACE!!!

    ReplyDelete
  12. Kwa huyu muuaji nahisi nahitaji mshauri wa Anger Management, maani hapa kwenye screen nikimuona hasira zinanipanda mpaka nauma meno, nisije nikapigana na computer bure. usimuweke tena hapa huyu baradhuli ananiharibia siku. Wazazi wa mtoto Salome muwe na subira na muombeni sana Mungu kwani hakuna hakimu zaidi yake yeye na damu ya Salome haitopotea bure.
    RIP Salome!!

    ReplyDelete
  13. The baby girl Salome Yohana will once again raise from the dead during the ressurection day!and for that case with no dought she will reach the kingdom of heaven!
    poleni sana wazazi wa huyu binti na mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  14. jamani tuwe tunafikiria kwa undani sana huyu mtoto ramadhani sidhani kama naye alikuwa anajijua alichokuwa anakifanya nadhani inabidi abanwe ili aseme ilikuwaje kwani naye ni wakuonewa huruma kwani ukute alikuwa kama zombie tu hajui chochote pale.

    ReplyDelete
  15. Nendeni Global publishers www.globalpublisherstz.com/

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 02, 2008

    BINAFSI YANI NAJISIKIA UCHUNGU SANA YANI NAFIKIRIA ADHABU INAYOMFAA HUYU MCHINJAJI LAKINI SIONI TUKISEMA APIGWE MAWE HADI KUFA TUTAKUA TUMEKIUKA SHERIA YA HAKI ZA BINADAMU NA KWANZA SHERIA HIYO WATANZANIA SISI JINSI TULIVYOUMBA NA MIOYO YA HURUMA HATUIWEZE HIYO ADHABU,ADHABU YA KIFUNGO GEREZANI NADHANI HAITOSHI KUWAKOMESHA NA WENGINE. SIJUI APEWE ADHABU GANI INAYOMFAA HUYU FISADI KIWEMBE.
    WATANZANIA NI JUKUMU LETU KUMLILIA MUNGU KWA BIDII AINUSURU TANZANIA YETU MAANA KILA KUKICHA USHIRIKINA UNAZIDI KUCHUKUA SURA MPYA KATIKA JAMII YA WATANZANIA.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 03, 2008

    pole na kazi kaka michuzi! mimi nipo huku ukerewe mwezi june mwaka huu nataka kuja bongo na wanangu lakini nimeanza kupata woga kama hali yenyewe ndio hii watu wameanza kuchinjana na kulana wenyewe kwa wenyewe kama congo ya zamani zaire naogopa kweli kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...