KAKA MICHUZI,
TWAREJEA KATIKA SWALI LAKO KWA WATU WAISHIO UGHAIBUNI.TUNASHINDWA KUJIANDIKISHA KTK BALOZI ZETU KWA MAMBO MENGI NA MENGINEYO NI KAMA IFUATAYO;-
1)KATIKA SHEREHE ZA MUUNGANO 26/04/08,TUMEALIKWA KWA KISHINDO KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU HIYO NAKUJULISHWA KWAMBA MGENI RASMI ATAKUWA BALOZI WETU KUTOKA SWEDEN.
KWA SISI TUISHIO MBALI NA OSLO,TULISAFIRI TOKA MAKWETU KWENDA JAPO KUMUONA HUYO BALOZI WETU AMBAYE ANGETUPA MACHACHE KUHUSU NCHI YETU,LAKINI KILICHOTOKEA HUKO NI KWAMBA BALOZI HAJAONEKANA VIONGOZI WA CHAMA CHA WATANZANIA WAMESHINDWA KUTUPA JIBU KAMILI KUHUSU KUTOKUONEKANA KWA BALOZI WETU AMBAYE NDIYE ALIYEKUWA MGENI RASMI.WALA MTU YOYOTE KUTOKA UBALOZINI HAKUONEKANA.
KWA HAYO MACHACHE KAKA MICHUZI TUNAKUOMBA UWAFIKISHIE UJUMBE HUU HAO WAHUSIKA WA UBALOZI.
NA MPAKA HAPO UTATAMBUA NI KWANINI WATANZANIA WAISHIO UGAIBUNI HAWAJISIKII KWENDA KUJIANDIKISHA KWA MAUDHI KAMA HAYA AMBAYO YANATUKOSTI MUDA WETU NA FEZA ZETU.
2)SHUKRANI KWA CHAMA CHA WATANZANIA OSLO KWA PART NZURI NA CHAKULA KIZURI.NI MATUMAINI YETU UJUMBE HUU UTAUWEKA HEWANI KWANI MJUMBE HAUWAWI.
WAKEREKETWA NORWAY,
Ă…LESUND

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Sasa mbona hueleweki, suala la kujiandikisha ubalozini na hiyo party vina uhusiano gani? Mimi ninavyojua kujiandikisha ni jambo la kiofisi, na wala sioni kwanini kuto kuja kwa balozi kwenye hiyo party kunakukwamisha nini wewe kwenda kujiandikisha

    ReplyDelete
  2. Yeap, Anonymous said umenena points tupu.Anachokisema hakina uhusiano na kujiandikisha au anataka tufahamu kama yupo Norway.Muhidin sometimes you have go through the article b4 you post it.This is too nonsonse to post.Huwezikumfurahisha kila mtu.Kwa sasa tunahitaji Blog ya kiwango cha juu.
    By Kajicho,Hungary.

    ReplyDelete
  3. wewe maisha yamekushinda,umechacha naomba urudi nyumbani kwenu.Kha!! tafuta demu akukeep busy.sasa unataka sisi tufanyeje,labda balozi alikuwa anaumwa tumbo,ulitaka akujulishe ili iweje.Tuelezee mabo ya maana,shule umemaliza au ndio unaoslooslo huko.tutakutumia twanga pepeta wakupooze ok usilie duuu!!!

    ReplyDelete
  4. Samahani ila naona better tujaribu kwanza kumwelewa mtu anaongelea nini ndo tuanze kumsagia.
    Mie nafikiri anazungumzia uhusiano wa Ubalozi kwa wa Tz huko aliko. Nilivyo elewa ni kuwa Oslo waliandaa get together ya Sherehe ya Muungano na balozi aliahidi kufika. Siku ya siku wabongo walikutana (wakafahamiana, wakala misosi,party ikaiva vizuri) ila balozi hakutokea. Huo ndo uchungu wa jamaa. Yaani mgeni wa heshima hakutokea. Hiyo inamaana kuwa mwakilishi wa TZ gov aliwaacha kwenye mataa. Iwapo balozi hatuthamini ktk mambo ya raha na shwari , Je? kuna umuhumu gani wa sisi kujuregister ubalozini? Hilo ndo swala lake.
    Nyie mnao mkandia na kuficha majina yenu naona jua kali tu na mvua nyingi zinawasumbua....
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  5. Mimi nadhani jamaa lengo lange si kulalamika tu...lengo ni kuwa mheshimiwa Balozi alialikwa kwenye sherehe, akaahidi kuwa angekuja. Kama sikosei viongozi wa Chama Cha Watanzania Oslo, waliwaalika mawaziri wawili wa Norway. Hao mawaziri hawakuweza kutokea na waliotoa sababu kitambo kuwa wasingeweza kuja kwa kutingwa na kazi, walituma wawakilishi wao. Sasa waalikwa wa Norway wamekuja, Balozi haonekani!!! Picha gani wameipata kwa mwakilishi wetu nchi za Skandanivaia na za Baltics?

    ReplyDelete
  6. Bw Malima, mzee wa Ă…lesund tumekusikia. Ila kama walivyosema wadau jitahidi kuhusianisha mambo!

    ReplyDelete
  7. Kutofika kwa Mheshimiwa Balozi katika sherehe hizi + kutotoa taarifa za kutofika kwake + kutomtuma muwakilishi wa aina yoyote katika sherehe hizo + Kufika kwa wawakilishi wa Uongozi wa Norway haifai kuwa sababu maalumu ya kutojiandikisha ubalozini kwako. Kujiandikisha ubalozini hutusaidia katika kutunza takwimu, kuwezesha mamlaka za serikali zetu kujua ni nani yuko wapi (in case of any unforeseen events kama majanga yoyote yawezayo kutupata sisi huku ugenini nk)
    Hata hivyo ninakubaliana (to a certain extent) kwamba wawakilishi wa nchi zetu katika maeneo mbalimbali hawajaweza kukidhi haja zetu kufikia katika viwango tunavyotarajia. Katika hilo, mimi kama researcher nisingependa kutoa sababu za kuhisihisi... hapa kuna potential ya mtu kufanya hata Masters au PhD ya research hii.... Kwanini watanzania hawapendi kujiandikisha wanapokuwa nchi za nje? By the way, angalia passport zetu katika ukurasa karibu wa mwisho kule nyuma utaona kuwa unapaswa kujiandikisha kwa balozi wako au kwa bibi Eliza ikiwa huna balozi hapo kwako! utakuwa hujafanya kosa lolote naamini!
    Ni maoni yangu binafsi tu!

    ReplyDelete
  8. michuzi usibane huyu balozi ni mzembe sana, kwa wanaomfahamuw atakubaliana na mimi, naomba usinibanie amejinyanyua sana, ndio tabia yake hapendi watanzania wafanikiwe ana tabia ya wivu michuzi usinibanie, kutokuonekana kwake amefanya maksudi, na watanzania tusichukulie hili kama jambo la kawaida, lazima tulalamike, hali hii mpaka lini.

    ReplyDelete
  9. The only balozi ambaye nimeona anagive a damn about her people ni huyo wa England ambaye nae pia anachemsha na mashina yake ya CCM, the rest don't give a damn about Tanzanians. Utazungushwa kupatiwa passport tu kama unaomba nauli vile. People are tired of their bullshit, bora watu waanze kivyao. Hata tukipatwa na maafa, since when have they done anything tukipatwa na maafa utasikia wanafuatlia then kimya, tell me what happened with Walter and his fiance's death, si walisema wanafuatilia, how far did they get. If it was turned around American Embassy wangehakikisha kinaeleweka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...