KAKA MICHUZI POLE NA KAZI YA KUTUELIMISHA SISI JAMII, NAOMBA KUWEKA HII MADA YA USAFIRI HEWANI ILI IWEZE KUJADILIWA NA WADAU KAMA INAWEZEKANA, HAPA MJINI MOSHI KUNA MATANGAZO YAMETAPAKAA KILA MAHALI KUWA IFIKAPO TAREHE MOJA MWEZI MEI NAULI YA DALADALA ITAPANDA KUTOKA SHILINGI 300/= YA SASA HADI KUFIKIA SHILINGI 450/= KITUO HADI KITUO.
JE ITAKUWAJE KWA WALE WAFANYAKAZI WA SERIKALI WANAOLIPWA KIMA CHA CHINI CHA SHILINGI 84,000/= BILA MAKATO (KODI NA KADHALIKA), NA ANA FAMILIA INAYOMTEGEMEA (CHAKULA,MALAZI, SHULE N.K),MWENYE NYUMBA ANASUBIRI KODI YAKE, KUFIKA KIBARUANI KWAKE INABIDI APANDE DALADALA MBILI, KWENDA NA KURUDI NI NNE, JE KWA MWENENDO HUU SERIKALI INAWAJALI RAIA WAKE MASKINI KWELI? HII KUPANDA KWA NAULI NI UAMUZI WA WAMILIKI WA DALADALA AU NI SERIKALI NA MAMLAKA HUSIKA? NINI KIFANYIKE ILI ANGALAU WANANCHI WAONE FAIDA YA SERIKALI YAO?

MDAU KCMC


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. tatizo haliko kwa wamiliki wa gari wao hawana jinsi hawawezi kuendesha biashara kwa hasara mafuta yamepanda lita ni 1800 hadi 2500 kwa sehemu zengine daladala inachukua watu 18 piga mara hiyo 300 halafu piga 1800 mara lita 5 kwa tripu? bado spea hela ya trafiki na posho zengine. si bora gari uipaki tu. laana iwaendee hao wenye mamlaka zinazohusika kwa kutuongezea ugumu wa maisha

    ReplyDelete
  2. Mi nasema ngoja kwanza wananchi tuumie ndo tutajua kwamba serikali ya CCM ni usanii. Sisi si ndo tunaipigia kura kila baada ya miaka mitano? Ngoja kwanza tuendelee kuumia, naamini iko siku itafika tutagundua kwamba tunahitaji kuwa serious na kura zetu.

    Mdau wa KCMC pole sana, ila ukae unajua wote tuko humo humo, maisha magumu na serikali ni ya usanii tuu!

    Hope tutaelewa siku moja. Kwa sasa ngoja tuendelee kuumia.

    Mdau

    ReplyDelete
  3. Wazungumza matatito ya fisenti tuu
    Kama hamwezi kulipa daladala amka asubuhi zaidi na vaa viatu vyako vya recycled dunlop,tia milage, if you cant pay for water kaoge njoro
    Naomba samahani in advance
    Mdau

    ReplyDelete
  4. WADAU HUU NDIO WAKATI MUAFAKA WA KUTAFUTA MKOPO HATA NINUNUE KIHICE NIJIUNGE NA SCHOOLMATE WANGU AUBREY AU MR PRICE . MAANA BIASHARA ITALIPA SANA. HILI DILILI INABIDI UJASIRIAMALI UFANYE KAZI.

    ACADEMIA TUMAINI GEOFREY TEMU
    MARANGU MOSHI

    ReplyDelete
  5. Mwenye daladala hana kosa hata moja, yeye anafanya hivyo ili kucover gas cost. Sasa kama serikali inataka kuzuia wananchi wasiumie inabidi watafute kampuni itakayo mwaga mabasi kama pipi, hiyo kampuni itaweza kusustain margina profit.

    Lakini mtu ana kabasi kamoja, mafuta ya kipanda kwa 10%, yeye lazima apandishe price kwa 10% kucover cost.

    CCM wanatupa starehe, wacheni kwanza nauli zipande mpaka 1000 kwa njia moja. then mtalearn something watanzania

    Mdau wa US

    ReplyDelete
  6. Duh hapo kiama kama unaishi Maili Sita halafu unafanya kazi KCMC itabidi tu uombe kuhamishiwa Mawenzi, au uanzishe kioski chako cha kuchoma sindano nyumbani! Maana itakubidi utoke Maili Sita hadi mjini, kisha upande basi ingine kwenda KCMC. Kama ndio hiyo 450, inamaana nauli peke yake kwa siku ni 1,800, kwa mwezi ni 54,000. Mfanyakazi mwenye mshahara ghafi wa sh 84,000 kwa mwezi, akikatwa kodi na masuala mengine anabaki na wastani wa 60,000, akitoa hiyo nauli anabaki na 6,000 kwa mwezi! Hapo hajathubutu hata kula chakula cha mchana huko kazini, akijaribu tu anabakia na urari hasi! Hii ni biashara kichaa kabisa! Sasa tutashangaa nini hawa wafanyakazi wakikwiba dawa au kulazimisha rushwa toka kwa wagonjwa? Kweli hali ni ngumu sana jamani.

    ReplyDelete
  7. Inasikitisha sana kuna serekali lakini, lakini utadhani tupo porini.Kila kukicha Zinaanzishwa mamlaka za kusimamia sehemu nyeti mbali mbali,ukiwemo usafiri na Nishati.Wapo wachumi waliobobea kabisa ktk nchi hii.
    Pia hata wasomi tunao wakutosha lakini inasikitisha sana mambo yanaendelea kuwa hivi.
    Mbali ya mabo mengine yote sisi watanzania ni wabinafsi, wachoyo ,hatuna uchungu na nchi yetu, hatuwajibiki kati yetu watu wanaangalia wakati huu tu.
    Ila siku moja litakuja kutokea fundisho kama kwa majirani zetu huko.Hapo Sasa ndio watu tuheshimiana na hili suala la Sentence za " UFISADI" RUSHWA na Urasimu vitaisha.
    Pia ndipo hata watuhumiwa watachukuliwa hatua ipaswavyo.
    Sasa hivi DEAL limekuwa KULA na KUJIUZULU saafi bila bughudha unaendelea na matumizi ya ulichochuma.
    LAZIMA NAULI IPANDE!!!!!!!!!
    UMEME NAO............

    ReplyDelete
  8. Jamani hili swala sio la `utani', hili ni tatizo ambalo Watanzania wote tunatakiwa tuamuke tuwe kitu kimoja. Hapa tunachoangalia ni maisha yetu na familia zetu, kwa upande wetu na faida na maslahi kwa upande wa wenye magari/serikali. Serikali itaneemeka kwa kodi kutokana na kupanda kwa nauli hii, kwahiyo wapo upande mmoja na wenye magari kutunyonya.
    Sasa wewe hata kama upo Ulaya, au wapi, jua kuwa wapo ndugu zako huku wanaumia, na kesho kesho kutwa utarejea, utaikuta hali ni mbaya. Ni vyema tukaamua/tukasaidiana wote sasa.
    Ni kweli mengine tumejitakiwa wenyewe. Siku unapiga kura yako ulikuwa mwenyewe, ukaamua kuwapigia `mafisadi'. Sasa gharama zake ndio hizo.
    Gharama za umeme zinapanda, kwasababu ya gharama za kuwalipa mafisadi, hata kama wamezalisha au la. Mafisadi wanatoka wapi kama sio wewe uliyewapigia kura.
    Hali kidunia inajulikana kuwa bei ya mafuta imepanda, lakini sio kwa kiasi tunachopandishiwa hapa nchini. Lazima kuwe na malipo kutokana na umbali. Barabara nyingi mbovu. Magari yenyewe ni ya kugombea. Wengine tunapanda magari matatu hadi manne ndipo tufike ofisini. Fikiria hii hali..
    Na kama tunaangalia hali ilivyo kidunia, kwanini hatuangalii kipato chetu pia kidunia.
    Jamani wananchi..., nyie ndio wenye uamuzi, hata kama wao wataamua kupandisha lakini kama mtakuwa na umoja, hawawezi kuwalazimisha, lakini je huo umoja mnao. Wapo wenzenu wenye uwezo hata kama watasema nauli ni elifu watapanda, na hawajali kama nyie mnaumia au la!!!
    Huu ni mwanzo tu, nasikia mpaka lengo lao la `gwalagwala' lifikie.

    M3

    ReplyDelete
  9. Tumieni baiskeli. Inashangaza mtu anaishi kilometa 1 na anakofanyia kazi lakini bado anagombania daladala badala ya kupunguza matumizi. Ni kweli mishahara haitoshi lakini tatitizo ni usimamizi wa biashara huria kwani bei ya mafuta ikipanda kidogo tu wanapandisha nauli lakini ikishuka nao hawashushi nauli. Serikali inabidi iwe kali kidogo kwani nauli zikipanda holela itasababisha migomo ya wafanyakazi

    ReplyDelete
  10. jamani baiskeli zianze kufanya kazi kama mambo yenyewe ndiyo hivyo duu twaumia wananchi wajameni.

    sweet
    Arusha

    ReplyDelete
  11. Mimi nadhani watanzania tuwe watu wa kuchambua mambo na siyo kukurupuka na kuanza kulaumu upande mmoja na pia bila kutoa njia mbadala. Wananchi wa tanzania tuna matatizo ya kuacha kila kitu kifanywe na serikali hata mahali ambapo serikali imeweka mazingira mazuri ila utekelezaji wake unahujumiwa. Kupanda kwa nauli haikuanza leo, serikali imepanga bei lakini baadhi ya daladala zilkuwa zinachukua bei zaidi ya ile halali na watanzania tumekaa kimya na kulalamikia serikali, CCM, Mafisadi etc. kwa namna hii ndugu zangu watu wasiokuwa waungwana watatumiza. Serikali imeanzisha biashara huria ya daladala ili wananchi wajipatie kipato lakini kwa sababu ya umasikini wetu, mtu ana gari moja lakini ana nyumba ndogo balaa na pia matumizi yote yanatoka humo, matokeo yake kuwaumiza wananchi kwa kisingizio cha mafuta na vipuri. Mimi naomba wananchi wenzangu sasa tuwe wakali kama wajeshi, anayelipisha nauli zaidi ya ile halali tumshughulikie kama mwizi. Anaeona nauli ya sasa hailipi aegeshe gari lake nyumbani na siyo kutapeli watu. Tusipoamua sasa tutazidi kulalamika mpaka Yesu arudi na hakuna mafanikio. Amkeni na msisubiri kuumia zaidi kwani serikali ilishaweka nauli halali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...