CHAMA CHA MAPINDUZI

Shina la Reading

MKUTANO WA PILI WA SHINA LA READING

Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Wanachama Wote - C C M - Reading
Wakereketwa Wote - C C M - Reading
Wapenzi Na Wana-Mapinduzi Wote wa Reading
Tarehe: 04/05/2008 Saa: 08:00 Mchana - Saa 12:00 Jioni

WAPI:
UKUMBI WA: 79 (Kijiweni)
79 LONDON ROAD
READING
RG1 5BY

Watanzania ambao wangependa kujiandikisha, mnaombwa kuleta picha zenu za passport size mbili na paundi kumi na tano (paundi tatu kwa kadi, halafu paundi kumi na mbili kwa ada ya uanachama ya mwaka mzima).

Kwa ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana na:

MAIRA MIGIRE – 07799212095
Katibu wa CCM Shina la Reading

Wote Mnakaribishwa – Kutakuwa na Vinywaji, Nyama choma na Muziki Baada ya Shughuli Zote.
Kiingilio – BURE!!!-- Best RegardsSoames PharesReadingUnited Kingdom

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Nyie ndugu zangu haya mambo ya kuitisha mikutano ya CCM huko majuu mngeya-'suspend' kwa sasa wakati nchi yetu iko kwenye 'boiling point' ya Ufisadi.Tutawaaminije kama hamkwenda kwenda huko kwa fedha ya ufisadi?Take care.Michuzi wewe ni kada uliyeelimika,sitegemei kama utaiminya hii.Iweke ili wajue hatari wanayojitafutia hawa ndugu zangu wa Reading

    ReplyDelete
  2. pound tano kwa kadi? huko nyumbani kadi ni kiasi gani na ada ya mwaka ni kiasi gani? naona kama watu wamegundua mradi wa kupata pesa za haraka haraka ni kuanzisha tawi la ccm nje ya nchi. Zamani ilikuwa kuanzisha charity sasa ni matawi ya ccm. Hebu nambieni kuna faida gani ya kuwa na matawi haya nje ya nchi? zaidi ya kujipatia pesa kwa wachache na kuwagawa watanzania tulio nje kwa sababu ya vyama vya siasa? sioni jengine, huwezi kuchagua raisi wala mbunge ukiwa nje ya nchi sasa faida iko wapi? kama ni kuunganisha watanzania jumuia tele zipo za watanzania takriban kila mji, hatuhitaji matawi ya ccm kutugawa! Jambo jengine ni kwa nini kila leo tunasikia ni matawi ya ccm tu ndiyo yanayofunguliwa huku nje? ni kama kwamba kila alo nje ni mwana ccm jambo ambalo sio kweli!!!

    ReplyDelete
  3. I love America !! ushenzi huo hakuna !!

    ReplyDelete
  4. Nimefurahishwa sana na comments za wenzangu hawa wawili hapo juu kwa kuwa nimekuwa nashangaa sana kwamba hata BALOZI wetu (sitaji jina wala nchi maana wote tunamsoma huku kwa Misupu...)kwamba eti kazi kubwa aliyotumwa huko na nchi yetu tukufu ni kufungua au kuhudhuria mikutano ya CCM. Jamani! Balozi hakuambiwa kazi yake akiwa huku nje ni nini? Maana hatumsikii kwa jingine lolote lile! Nadhani nalo hilo linaweza kuitwa "ufisadi" wa aina yake...

    ReplyDelete
  5. Kidumu chama cha Mapinduzi!
    Idumu Siasa ya Ujamaa na kujitegemea!
    Zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM! YUPI????????......

    ReplyDelete
  6. We know Who you are!you are all nothing but Pretenders.Gone are the dayz when CCM used to enjoy its credibility as a political party for the Patriots.Hivi sasa chama cha CCM kimegeuzwa kichaka cha Mafisadi.Kila mwenye pesa haramu salama yake na mali yake ni kujificha nyuma ya mgongo wa CCM apende asipende.Matokeo yake kimechafuliwa sifa zake kwelikweli.It doesn't make you proud at all to assparade as a CCM zeolot!Nani Mjamaa miongoni mwenu?Nani Mzalendo wa kweli miongoni mwenu?Uingereza mnatafuta nini?Muda gani utakaa huko kwa masomo ushindwe uvumilivu wa kuja kujiunga na CCM huku nyumbani utakapo rejea?Ulishindwa kujiunga na CCM ukiwa huku nyumbani leo ujifanye 'MLOKOLE WA KISIASA'na uokovu huo Yesu amekushukia ukiwa London Uingereza na kuuona Wokovu wa Bwana?Jamani acheni UNAFIKI.Watanzania hivi sasa sio wale mazumbukuku mliozoea kuwafuga kama Kunguru enzi zile za 'Ndiyo Mzee'!Wenzenu wenye akili wapo huko wakiwaza watawezaje kiba teknolojia mbalimbali za Nuklea na Makompyuta ili waje waziendeleze nchi zao!Nyie mmekaa mkiwaza kadi ya CCM itakuwezesha kupenyeza mambo yako binafsi ili yakunyookee!Wajinga kwelikweli.Hatuna noma na hilo,lakini mnamtangazia nani?Si mfanya mambo yeni kivyenu yawanyookee?Ulimbukeni huo ndugu zangu,mnatutia aibu kubwa!

    ReplyDelete
  7. HONGERA CCM KWA KUENDELEA KUWA CHAMA KINACHOWAFIKIA WANANCHI POPOTE PALE.MIMI NI CHADEMA LAKINI NAWAONEA WIVU CCM KWA MIKAKATI YAO YA KUWAFIKIA WANAOKIHITAJI,SISI WAPINZANI VIONGOZI WETU WANAJAZA MATUMBO YAO TU,HAWATAKI KUTUMIA PESA ZA RUZUKU KUJENGA VYAMA KUANZIA CHINI.HAKI YA MUNGU CCM ITAENDELEA KUPENDWA KWA DEMOKRASIA YAKE,NDIO WAPO WACHAFU LAKINI KWA CCM KULETA JUKWAA LA KISIASA NJE KUTAWAVUA VIONGOZI SAFI KURUDI NYUMBANI NA KUPAMBANA NA MAFISADI,BIG UP CCM LAKINI SITOKI CHADEMA ILI NIKUPE PRESSURE..SIKUBALIANI NA HUYO HAPO JUU ANAESEMA CCM INAWAGAWA WATANZANIA,KWA MAONI YANGU WATU WA AINA YAKO WEWE NI WALE WA KULAUMU TU BILA FACT.CCM TOKA IANZE HAPA UK IMESAMBAA MIJI KARIBU 7 NA KUWAUNGANISHA WATANZANIA WANAOAMINI KWAYO,VYAMA VINGI UNAVYOVIZUNGUMZIA VIPO KATIKA MIJI LAKINI HAVINA LINK NA MIJI MINGINE HIVYO KUWAUNGANISHA WATANZANIA,CCM INACHOFANYA NI KUWAUNGANISHA WATU.SIKUSHAURI USEME SIASA KAMA HUITAKI LAKINI KAMA WEWE NI CUF BASI NYIE NA SIE CHADEMA TUIGE MFANO WA CCM HAPA UK WA KUJISAMBAZA KAMA TUNA UBAVU WA DEMOKRASIA HIYO YA WENZETU.RAIS AMBAE NI MWENYEKITI WA CCM ANACHUKIZWA NA MAFISADI NYUMBANI NDIO MAANA KAIDHINISHA KUPITIA KAMATI KUU YA CHAMA UANZISHWAJI WA MATAWI YA CCM NJE YA NCHI ILI WALIO SAFI NA WASIO DEBE TUPU KAMA WEWE HAPO JUU KUJIUNGA NA HATIMAE UKAOKOE NCHI NYUMBANI KAMA KIONGOZI SAFI.WENGI WETU TUNAOPINGA CCM HAPA UK NIKIWEMO MIMI TUMEJILIPUA,LAKINI TUSICHUKIE TANZANIA KIASI HICHO HASA KWA VIONGOZI WAPENDA MAGEUZI KAMA [OBAMA KIKWETE].....MICHUZI USSBANIE HIII,HATA KAMA CHADEMA WATANINYANG'ANYA KADI,LAKINI UKWELI LAZIMA TUUSEME TU,KWANZA MIMI NI MANGI NI MWENZAO[CHAMA CHETU HICHO]

    ReplyDelete
  8. CCM TOKA IANZE HAPA UK MWAKA JANA JANUARY INA WANACHAMA HAI 550,TANZANIA ASSOCIATION INA 87,SLOUGH TANZANIA ASSOCIATION INA 60,NA SCOTLAND T.A.INA 62....MFANO HAPO JUU UNAONYESHA JINSI GANI WATU WANAIKUBALI CCM TENA BAADA YA MUDA MFUPI TU,TUTUMIENI DHAMIRA YA KAMATI KUU YA CCM NA KIKWETE KUFUNGUA MATAWI NJE KUINUSURU NCHI KWA MAWAZO NDANI YA VIKAO VYA CHAMA YATAKAYOFIKA HADI JUU KABISA.KWANI TUKUMBUKE MAAMUZI YOTE YA SERIKALI HUAMULIWA NA CCM,BE PART OF IT,JOIN IN AND TOGETHER WE CAN PUSH FOR CHANGE...MICHUZI KIAMA CHAKO JUMATANO NA CHELSEA,HAHAAAA HAAAA....

    ReplyDelete
  9. NASIKIA HAWA VIONGOZI WA CCM UK WANAOTUMIA PESA ZAO KUFUNGUA MASHINA KILA PEMBE YA UK WAMEOMBA KWENDA ZANZBAR MWAKANI NA WENZAO WA CUF NA CHADEMA KUFANYA SHUGHULI ZA MAENDELEO ILI KUONYESHA UMOJA WA WATANZANIA HALAFU MBUNGE WA CCM WANAWAKE MARTHA MLATA AKAWAKEMEA KAMA WATOTO KWA WAZO LAO HILO LA KIMAPINDUZI.....KAMA NI KWELI NAOMBA CCM IMSHUGHULIKIE MAMA HUYO ANAEDAI CCM HAIPASWI KUWABEBA CUF...SASA NAANZA KUONA KWANINI KIKWETE ALIKUWA RIGHT KUTULETEA CCM ABROAD,MAANA ALIONAO NYUMBANI KAMA NI KAMA HUYO MAMA,KAAAAAZI KWELIKWELIIII.

    ReplyDelete
  10. CCM HOYEEEEE,CHADEMA HOYEEEEE,CUF HOYEEEE,TLP HOYEEEEEE..PLEASE KIKWETE FANYA KWELI,MWITE MREMA IKULU MTIE YAMINI NA UMPE WIZARA YA KUPAMBANA NA UFISADI NA IWE INASIMAMIA TAKUKURU.LAKINI AWE NA ADABU ASIKUGUSE WEWE MAANA TUNAJUA WEWE NI SAFI NA SI FISADI.MAANA MREMA NAE HUWA HAKUMBUKI FADHILA ANAWEZA KUKURUDI BUREEEEE.......

    ReplyDelete
  11. Michuzi acha unafiki ndugu yangu basi iite hii blog ya CCM, watu wakiandika comment kuiponda CCM unazibania. Iko siku Mungu atawahukumu nyinyi MAFISADI wote, maana nadhani wewe Michuzi unapenda kuona watanzania wanazidi kunyanyasika na umasikini unaoletwa na CCM, tumeona juzi tu hapa watanzania wanavyoteseka kwa kukosa hata ambulance na kuishia kumbeba mgonjwa wao kwa njia zisizo salama, hata kama ni UKADA wako ndani ya CCM, ujue una ukomo wake. Inshallah Mwenyezi Mungu ataamua mwenyewe kutokana na wewe kuendelea kusaidia kuficha maovu ya CCM.

    ReplyDelete
  12. Nyie mnaolilia mapinduzi sasa hayo mapinduzi yatakuja kwa kupiga kelele kwenye blogu? Jamani jiungeni na vyama muwatoe hao wazee wenye mawazo ya mwaka 47 mje na mawazo mapya. Yes tunataka mabadiliko lakini ni nani wa kuleta hayo mabadiliko kama sio nyie mlio nje angalau mmefunguka macho mmeona dunia inaendaje kitu gani hatufanyi vizuri mje mrekebishe mambo.

    Na watu wasiiseme CCM peke yake kwa sababu wao wanatangaza hadharani kwani hata Chadema inaandikisha wanachama nje kupitia kwenye mtandao wao sasa kama unaona huwezi jiunga CCM jiunge Chadema, mwende mkalete mabadiliko na changamoto katika nchi. Umepita ule wakati wa vijana kukaa pembeni na kusema 'vijana taifa la kesho' wakati mnaishi leo na nguvu yenu ipo leo, kesho si mshakuwa wazee tena!

    ReplyDelete
  13. Kweli u can take a man from the bush but not the bush from a man!!

    Yaani pamoja na ufisadi wote unaoendelea badala ya wao kudai accountability na usawa wao wameamua kukumbatia mafisadi!!

    Ndio maana nchi yenu haiendelei, wenyewe hamyna uchungu na nchi yenu! Munaona mafisadi bora kuliko maslahi ya taifa.

    Nyoooooooni!!!

    ReplyDelete
  14. Mmegundua huyo Anon ALIYEANDIKA KWA herufu kubwa hapo juu ni mtu yule yule??? Ama kweli Tanzania tuna mambo na watu. watu mnakosa kuiba ujuzi mlete huku nyumbani mnatafuta kadi za kijani? No wonder we are where we are!

    ReplyDelete
  15. Anonym wa April 29,2008: 3:46 pm Shikamoo Mzee kwa hekima zako! Hawa jamaa zetu wa UK achana nao.Hawa siyo watanzania wenzetu,hawa ni vibaraka walioamua kuwasaliti watanzania masikini vijijini baba zao na mama zao kwa kuwalea mafisadi ili wazidi kuiangamiza nchi yetu.Ole wenu,mtakapo rejea tukiwafahamu mtakifahamu kilichomfanya Kanga akakosa manyoya shingoni!Nyinyi kuleni tu hizo fedha za kifisadi.Mnashindwa hata kukemea maovu ya dhahiri yanayo fanywa na hao viongozi mnao washabikia,tuwaeleweje nyie vimbwengu?

    ReplyDelete
  16. DUH!KWELI UFISADI HAUTOISHA!SASA HAWA WANAFANYA NINI KUSAIDIANA NA WATANZANIA WENZAO WAISHIO NJE YA NCHI????KILA SIKU MIKUTANO,MIKUTANO????CHA MAANA HAKUNA ZAIDI YA POMBE,NYAMA NA KUCHUKUA PESA ZA WATU???ETI KUJIANDIKISHA?????SASA NIKIWA KAMA MWANACHAMA MTANISAIDIAJE???HAO WENYEWE WALIOJIANDIKISHA WANAPANGA KWENDA KUDAI FIDIA ZAO???JAMANI ACHENI UTAPELI MSITUFANYE WATOTO WADOGO BWANA!KAMA WATU WANATAKA KUFANYA BIASHARA WATU NI HERI WAANZISHE MAMBO YA MAANA KULIKO UJANJA UJANJA TU!MAFISADI WAKUBWA NYIE!nyooooooo!NYOOOOOOOOOOOOO!WANAFKI TU.....MPENDA HAKI TOKA SLOUGH.
    ASANTE SANA MICHUZI KWA KUTUPA NAFASI.

    ReplyDelete
  17. Chadema hoyee.Wewe uliesema kuwa vijana tuache kupiga makelele bali tujiunge na siasa ili kuikomboa nchi UKO right.Hata huko Marekani kuna Mafisadi ndo maana makamu wa RAIS wao ana kampuni inayogawa chakula jeshini huko Iraq na ime over charge serikali,skendo lipo moto saa hii USA.Dawa si kupiga makelele dawa ni kujiunga na siasa ili kupambana na walaji.Walaji wapo dunia yote,ni vijana wa kizazi kipya kupambana na mizee kama hiyo duniani pote.KUJIUNGA na CHADEMA,CUF hata CCM si kuwakumbatia mafisadi bali ni kuwafuata huko waliko na kuwabanjua chini kama anvyowabanjua KIKWETE.Wa kuziba mapengo ya wabanjuliwaji hao ni sisi tulio na maono ya usawa.Naomba CUF na CHADEMA tuige mfano wa CCM UK,na sisi tuanzishe mashina UK yote na ikiwezekana tuunde coalition na CCM UK,YA UMOJA WA KITAIFA na tuisaidie nchi yetu.Wimbi la CCM kuvuka mipaka ya nchi na kufikia watanzania tulio na upeo linawatisha mafisadi nyumbani,maana wanajua sasa wajanja wanadandia jukwaa wanalotumia wao kuiba na watasukumwa chini.Kikwete amekaa mambo ya nje miaka kumi anajua hazina ya vipaji vya watanzania nje ndo maana anatupigia shavu tujiunge na siasa na hasira zetu tuzimalize kwa kufanya mema kwa jamiii.Hana watu nyumbani amezungukwa na walaji na watu wenye mawazo ya mwaka 47.Sisi wapinzani tulio nje tuwe moderate kidogo na tuige mfano wa CCM,TUKAINUSURU NCHI,TUACHE KULALAMIKA NA KUWAONA WASALITI WANAO JIUNGA NAO.[If you cant beat them as an outsider,join them and kill them face to face by legitimate meetings......MREMA for home office bongo,please KIKWETE.

    ReplyDelete
  18. ccm london na wenzenu inaonesha mko kwenye full kaputi ingekuwa nusu kaputi mgezinduka. Tumasikitika tumewapoteza hivi hivi
    Tumaini Geofrey

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 01, 2008

    CUF HOYEEEEE.Wewe unaewaita watanzania wenzako wana full kaputi,ukijiupeleleza sana yakhe elimu yako yawa duni mno.Makelele tunayopiga juu ya wanaomsaliti KIKWETE home kama hatujiungi na siasa na kupambana nao ktk mkondo wanaotumia kutuumiza[sisa]basi tutapiga kelele mpaka kiama ataporudi mtume kutuokoa.Naanza kuwaheshimu new generation ya CCM hapa UK hasa kwa wazo lao la mwakani kusahau propaganda za siasa na kuungana na sisi kwenda Zenj kufanya shughuli za maendeleo.Hiyo tutawaonyesha viongozi wetu wenye tongotongo home jinsi gani watoto wao huku majuu tumeiva UZALENDO...Nyie CCM UK,Msikubali wazo lenu hilo zuri kutekwa na [CCM 47cc] Nyie sasa ndio wa kuinusuru CCM maana nyie ni [CCM 3500cc]New generation.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...