Ero Mishuzi!
Saidia tasafali. Hii kitu nachengua mimi sana... iko hiine watu nyingeni nasema "anatikisa kibiriti" then ingine nasema "anatingisa kibiriti" wengine iko nasema " anatikisha kiberiti" na ingine "anatingisha kiberiti".
Naomba elekesa mimi ipi iko mahala yake
* Natangulisa sanks sangu
mdau Endulen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. mimi kwa upeo wangu hapo kuna viswahili viwili. Cha zanzibar na cha bara. Zanzibar tunasema 'tikisa kibiriti' (formal)na wengine husema 'tikisha kibiriti' hasa vijana na watoto na wakubwa katika lugha ya maongezi kwa iyo inaweza kuwa ni informal way lakini zote zinatumika sawa.'Tingisha' na 'kiberiti' misamiati hiyo haitumiki kabisaa kule visiwani kwa maana hiyo inatumika bara. Mfano ile nyimbo ya bongo flavor (bara) 'tingisha tingisha kama kib........

    ReplyDelete
  2. Na ile ingine inatingisa kibuyu ya kiloriti

    ReplyDelete
  3. duh balaah!! kwanza kiswahili chote hapo hakijanyooka!
    anyway. "anatikisa kiberiti" ndio sawa.

    ReplyDelete
  4. EErooo mi nafikiri neno sahihi ni ANATIKISA kiberiti hayo mengine ni yaja kwa watu kuathiriwa na lughas za mamaas zetu.

    ReplyDelete
  5. Wewe mdau wa Endulen unapomuita mwenzio "Mishuzi" unaleta maana tofauti kabisa, kama una utani na bwana Michuzi useme, lakini utani kama huu mimi nisingeuvumilia hata kidogo!

    ReplyDelete
  6. Ero rafiki sasa naona ewe uko na utani na CHIBIRITI, atakurushia mawe mpaka usahau sime yako
    Ngorotik wewe haha

    ReplyDelete
  7. Tikisa kiberiti, tingisha matako hapo ndio kiswahili kimesimama

    ReplyDelete
  8. Yoleleee

    tikis.a kt [ele] shake, wave sth: (tde) tikisia; (tdk) tikisika; (tdn) tikisana; (tds) tikisisha; (tdw) tikiswa.
    tikisik.a kt [sie] be shaky, unsteady. (tde) tikisikia; (tdk) tikisikika;
    (tds) tikisikisha.
    tingish.a kt [sie/ele] shake, shake up. (tde) tingishia; (tdk) tingishika; (tdn) tingishana; (tdw) tingishwa.
    PIA ONA MAANA YA ting.a1 kt [sie] swing. (tde) tingia; (tdk) tingika; (tds) tingisha.
    ting.a2 kt [sie] encircle, hem in, entwine. (tde) tingia; (tdk) tingika; (tds) tingisha.
    kibiriti1* nm vi- [ki-/vi-] matchbox; lighter, (zamani) flint, brimstone. (Kar)
    kibiritingoma1 nm vi- [a-/wa-] prostitute, whore. (haha hah aha hahahaha!)
    kibiritingoma 2nm vi-[ki-/vi-] short dress. (kwaio Michuzi unaweza sema Kibiritingoma amevaa Kibiriti ngoma)

    MENGINE (tingisa, anatikisha,, kiberiti) SI KISWAHILI!

    BADO NAULIZA MAMA WA KWANZA (MKE WA RAIS ANAITWAJE KWA KISWAHILI, JE RAIS AKIWA MWANAMKE MUMEWE ANAITWAJE? Majibu tuma kwa apakati_ya_chembe_au_kidevu@yahoo.com

    Aminia

    ReplyDelete
  9. Michuzi mimi nina matikisiko makubwa sana juu yako yaani wewe watu tukiweka posti za maana na majadiliano muhimu katika jamii yetu hutoi kwenye blogu unayapiga bani kiaina kazi yako kuweka huu upuuzi wa wasiojua lugha wanatikisa vibiriti na kwansa mmasai gani anasema nachengua kwa nini lakini ? kwa nini unatunyanyasa hutupi haki ya kujiexpress mawazo yetu kwa wengi ? sisi tunakuja humu tukijua fika ya kwamba unafanya kazi nzuri na kutokana na hili blogu yako inaunganisha wabongo tofauti ulimwenguni kote nikiwa na maana ya kuwa ni blogu mashuhuri sana sasa mimi nilitoa posti kwenye elimu ya juu kwa wale waliohitimu huko uholanzi na kwa nini kuna tofauti za idadi ya wasomi na idadi ya viongozi serikalini katika dini zetu kuu mbili nikakuomba uianike barazani siioni sijui umeipiga red card ? hii siyo democrasia kaka yangu najua wewe ndio blogu owner lakini hii ni blogu yetu kwani ndio sehemu ambayo hasa sisi wanyonge tunajiona tuna uwezo wa kusikilizwa, sasa wewe mwenyewe ndio ulikaribisha maoni na watu tuandike posti zetu sasa inakuwaje unabadilisha game na kumove goalposti katikati ya mchezo ? kwa kweli hii sio fair, na hii sio mara ya kwanza wewe kutokutoa posti zangu najua hata hii kwa kuwa nakupa ukweli hutaiposti lakini mimi shida yangu ni kukufikishia wewe salamu hivyo najua utazisoma na zitafika ingawa utaitia kapuni hiyo haina noma wala kelele sema kwa kweli roho inaniuma sana mimi nimepoteza time yangu na kuandika subject muhimu kwenye jamii na sio kama nilitukana mtu wala nini la hasha nilikuwa tu nasema ukweli ulivyo ama ninavyouona mimi wewe ulikuwa ni kuiposti hivyo labda ninakosea watu wangenikosoa lakini ukaimaindisha ukaitelekeza sijapenda kabisa sema nitafanyaje bwana mimi ni mnyonge na kilio cha mnyonge huwa hakisikiki sawa bwana mimi naona wewe hutaki niwe nacomment humu mana kila nikicomment unakaa nazo nmwenyewe basi kuanzia leo umeshinda kaka yangu sio kama nitasusa kuingia bloguni kwako la hasha nitapita kila siku kutwa mara tatu kama kawa sema huu ndio mwisho wangu wa kucomment chochote mana naona kaka yangu labda unaniona vipi sijui lakini hamna noma , nashukuru sana kwa hili,lakini napenda tuu kukukumbusha ya kwamba hii blogu yako ni dhamani umepewa na MWenyezi Mungu ili ufikishie watu habari na kwa usawa hivyo ni budi wewe utende haki kwani kila mtu hapa duniani ni mchunga na kila mchunga atakuja ulizwa kwa kile alichokichunga!! kwani wangapi wana mablogu lakini watu hatuna time nayo kila kukicha tuko kwa Michuzi wewe huoni kama wewe ni the chosen one and this is a very powerful tool for us to express ourselves?? sasa kwa nini unakuwa unatubania wengine na wakati tunafuata sheria za blogu sio kama tunatukana mtu ama nini? Mimi niliuliza tuu swali ili wadau wenzangu wanipe kipindi nielewe ni katika kutafuka habari sahihi sasa wewe unanikosesha mimi kufahamu ukweli wa mambo !! Yaani unanifanyia kauzibe !Anyway hamna noma wala kokoro sema hapa nina machungu wacha tuu nimalizie hapa nisije nikatoa michozi bure na niko kwenye kadamnasi hapa, but seriously nakutakia kila la heri katika kuendeleza libeneke na Mwenyezi mungu akujaalie guts za kutohofia hisia za watu juu ya yanayoandikwa humu na akupe nguvu ya kuposti na posti za sie wanyonge hata kama wewe unaziona hazifai machoni mwako ili watu wengine waamue.Amen.

    ReplyDelete
  10. wewe unayejiita mnyonge unaonekana una DHARAU ndio maana maoni yako yanabanwa na kwa TAARIFA YAKO MISHUZI ANAWEKA MBELE KESHO JE HUWA TUNASEMA KWANZA AU KWANSA, UMEONA MWENZAKO MJINGA KUULIZA WAKATI WEWE HUJU TUNATUMIA KWANZA AU KWANSA EBU MSIKIENI ALIVYOSEMA '.....kuweka huu upuuzi wa wasiojua lugha wanatikisa vibiriti na kwansa mmasai gani anasema nachengua kwa nini lakini ?

    USILOLIJUA NI HERI KUULIZA, MADA YAKO ILIYOBANIWA HAIJAKAA KIDINI KWELI MAANA MHH AU SIJAKUPATA??

    ReplyDelete
  11. wewe mnyonge usiyekiburi unanifanya nirudi kucomment humu bloguni wakati mimi nimeshamwambia Michuzi sifanyi hivyo tena. sasa kwa taarifa yako hivyo nilivyoandika ndivyo nilivyokusudia isomeke kama ilivyo nikiwa na maana ya KWANSA na sio unavyonirekebisha wewe KWANZA, yes I was taking the mickey out of huyo jamaa muulizaji kutokana na jinsi yeye mwenyewe alivyoiandika posti yake yote and with all due respect sikuwa namdharau Mdau mwenzangu it was just as a joke so wewe wala usitake kuleta ligi nyingine hapa mimi machungu yangu yalikuwa kwa kaka Michuzi tena hapa amenikata kilimi maana at least hiyo hapo juu kaiposti so sitaki kuongea sana , labda nikuulize wewe unamuita kaka Michuzi ukamgeuzie jina MISHUZI haya kulikoni ? Unataka kukaa unanikosoa kuandika kwangu wewe ya kwako huyaoni ? Na huju ndio nini tena sio huju ni HUJUI? Na kwa taarifa yako kiswahili hakuna EBU MSIKIENI ni HEBU MSIKILIZENI ! Ndugu tahadhari na kutuharibia lugha yetu tukufu na ukae ukijua Computer haina spelling check kwa kiswahili eeh! naona inabidi kaka Michuzi umtafute Mzee kifimbo cheza atoe darasa kwa wadau! Na ukitaka kujua swali la jibu lako kuhusu mada yangu whether imekaa kidini kwa zaidi muombe kaka Michuzi labda wewe atakusikiliza manake mimi sina tena nafasi labda aibandike then uamue mwenyewe lakini mimi personally siioni kama iko kidini narudia tena SIJATUKANA MTU WA KUDHARAU DINI YA MTU , ingawa mimi nilijieleza tuu na kutaka kujua kwa nini hatuna uwiano sawa kielimu na Kiuongozi wa serikali kati ta dini zetu kubwa mbili nchini ? sasa hapo udini uko wapi? anyway kama Michuzi akikuletea hii wewe ongea nae labda atakusikiliza. Kaka Michuzi asante sana kwa kuonyesha ujasiri wa kuposti comment yangu I see we will get there in the end!.

    ReplyDelete
  12. Mnyonge, kwa kweli mada yako ni wazi kuwa ni ya kidini na ndiyo sababu michuzi ameibania. Na kwa hilo mimi nampongeza sababu hata wewe jibu usingepata ingekuwa ya mwamba ngoma kila mmoja angevutia ngozi upande wake, nadhani umenipata hapo! ungeambulia majibu ya jazba kama si matusi na kuchafua hali ya hewa kwa baadhi ya watu kukashifu dini za wenzi wao. kwa hiyo usikasirike leta mada ambazo hazitatugawanya kidini humu.

    ReplyDelete
  13. Huyu mnyonge sioni analalamika nini!

    Kuja kwenye blog ya Michuzi ni hiari yako, sio suala la kusema amepewa na Mungu. Amepewa na Mungu ndio sio uongo, ila hata wengine pia wana wanazo blog, lakini ni Michuzi pekee ambaye blog yake iko active na inavutia. Sasa unategemea niende kwenye blog yenye mambo yaleyale wiki nzima?!

    Sasa kama wewe unajua kususa acha basi usije blogini, wenzio tutaendelea kama kawaida ili mradi awe active. Akiacha kuwa active basi tutatafuta ingine, hiyo ndio formula. Kwahiyo mada yako haina msingi.

    Pia kuhusu kuweka post au kutoweka hilo linalomhusu yeye na ana haki hiyo, jua kuwa ni yeye tu mwenye ku-control ubora wa hii blog. Unakuja ku-blog kutokana na ubora huo. Akiacha kuchuja hizo post zako kila mtu atamshangaa, ni kama vile lilipotokea suala na Lady Mercky wa UK. Kwahiyo ukiona hajaweka post yako, usimshambulie, ila jiulize maudhui yake, au maadili yake kwenye jamii.

    Hata hivyo naona post zako ni lazima zitakuwa zina-m-bore tu maana hizo comment zako hata paragraph hamna, wala hatujui sentensi inaanzia wapi au inaishia wapi.

    Mwisho, Michuzi ana haki juu ya nini kiandikwe kwenye blog yake. Ndio maana hata comment ukituma haiendi moja kwa moja mpaka asome.

    Tunaomba usimchanganye. Sisi tuko mbali na nyumbani, Michuzi anatuletea Tanzania karibu.

    Kaka Michuzi keep it up. Pls control the quality of this blog as you always do.

    Mdau- Amsterdam

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...