Braza Michu Habari,

Naomba wadau wanisaidie kidhungu hapa.
Hivi kama naandika e-mail ama naongea na mtu kidhungu nataka kumwambia “POLE KWA KAZI” namwambieje????



Mdau wa Mayfair Plaza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. sasa ni nini kigumu hapo? Kama hujui Kiingreza sii ukachukua madarasa tu?
    Hapo unasema sorry for job. kwisha.

    ReplyDelete
  2. Sorry for the job!

    ReplyDelete
  3. Wamarekani wanasema
    " are you having fun yet?", na jibu lake ni "oh,i am having a blast!!", au jibu lingine ni "i am busting my ass off"

    asante kwa kunipa fursa ya kujibu.

    ReplyDelete
  4. Michuzi sioni sababu ya kuchelewesha maoni yetu atu yanapitiwa na Blog owner afu unapitisha lugha ambazo Tanzania hazijaruhusiwa hiyo As** off haijatulia we vip kaka unalemewa? Tuajiri mkuu!
    umenikumbusha chuo kuna jamaa alipata SMS toka kwa demu wake 'sorry for paper' yani pole kwa mtihani!

    Kiswahili si sawa na Kiingereza na neno Pole halina kiingereza cha moja kwa moja Mfano Hodi haina kiingereza cha moja kwa moja na huwezi epuka Knock at the Door! Pole inaendana na my sympathy! sorry! take it easy! ila inategemea unafanya nini, mfano msibani si twasema pole, ukimkanyaga mtu pole, ukikosa daladala pole, so ktk English unachek ni ishu gani!
    Kumbuka Soorry? inamaanisha 'sija sikia ebu rudia tena' kwa kishwahili km hujasikia huwezi mwambia mtu "Polee??" labda eeehhh???
    Hah ahhahah inatosha jamani

    ReplyDelete
  5. Ndugu muuliza swali, kwanza lazima utambuwe kwamba si kila neno katika lugha moja linaweza kutafsirika kwa lugha nyengine! Huo ndo utashi wa lugha.

    Hata kama utajiribu kulitafsiri neno bado halitokidhi haja maridhawa,kwa maana halisi kwenye uhalisia wake haitopatikana!Ndo maana lugha moja huazima baadhi ya maneno kutoka lugha nyengine.

    Hakuna neno linaloleta maana ya "pole" kwenye lugha ya kikristo aah samahani lugha ya bibi aka English!
    Ukisema "sorry" just utafikisha ujumbe tu, lakini haileti maana kama neno "pole" lenyewe.

    Lugha huakisi mila na desutri za wahusika (wenye lugha), kwa hiyo moja ya mila na desturi za wasawahili ni huruma na upendo, ndo maana wanapoumwa au kufiwa watu hupeana pole, si desturi za wazungu, msiba utabaki kuwa wako mwenyewe na familia yako,na kama ni kuuumwa ndo hivyo watoto na mkeo, neno kubwa ni "get well soon" kutoka kwa familia au rafiki zako, yaani poa haraka ili urudi kututumikia!

    Kwa hiyo "Neno pole kwa kazi" litabaki na maana asili yake katika kiswahili na si english, ni muda wao, nawao wazungu (wa english) kuazima maneno katika lugha ya kiswahili.

    Kuna siku ilinipata kazi, maana ilibidi ni tafsir wimbo wa sabahi "Tamba" sababu msikilizaji mwenzangu haelewi kiswahili, kilichotokea hapo najuwa mwenyewe...!

    Kila lugha ina ladha yake, utamu wa baadhi ya maneno ya kiswahili huwezi kuyapata kwenye lugha nyengine!

    ReplyDelete
  6. in modern world or in western countries people dont have sympathy for working because it is an obligation/responsibility but it depends if its your wife ,she will tell you "hello darling you must be tired do you need tea or a shower first?" kama ni boss wako atakuambia thanks for today kwisha menipata hapo

    mdau

    ReplyDelete
  7. I was involved at one time in a major debate with distinguished swahili/english schoolars and this same question was raised
    The answer is simple really, before you give pole to anyone you must first establish if it is north pole or south pole, beware of bears if it is north pole

    ReplyDelete
  8. Katika utamaduni wa kiingereza hawapeani pole kwa kazi bali hupongezana tu. Ukitaka kutafsiri kiswahili kutumia maneno ya kiingereza basi utasema "My sympathies to you for your job." Na mtu huyo atakushangaa sana.

    ReplyDelete
  9. WEEE ANOMYMOUS ULIYE MWAMBIA MWEZIO AKACHUKUE MADARASA ETI KWA SABABU KATAKA KUJUA MAANA ''POLE KWA KAZI'' KWA KINGEREZA ACHA USHAMBA KUBABAKIA LUGHA ZA WATU NYIE WABONGO UNAONA KUJUA KINGERZAA NDO USOMI WADENISHI AU KWA WENGI HAWAJUI KINGEREZA NA HAWANA PRESSURE WALA NINI!! WAJERUMANI NDO KABISA TENA ANAJUA KINGEREZA NA AKAJIFNYA HAJUI WAFARANSA NDO DUUU OH MY GOD!!NDO WANAKIDHARAU HII YOOTE NIKUTAKA KUJIVUNA LUNGHA YAKE LABDA AJE TZ ATAONGEA NA WEWE KWA SABABU YUKO UGENINI

    ReplyDelete
  10. Wewe wa kwanza hapo juu umejibu kwa kebehi wakati na wewe umechemsha.. Ndio English za Dictionary hizo... Kusoma kidhungu sio kuweza kuongea. Unatakiwa upractise ndio utajua kuongea na sorry for Job ndio nini??? Afadhali hata huyo aliyesema Sorry for the job anamake sense. Sorry means regret..What are you regrating for?

    Kuongea kidhungu sio neno kwa neno...mtu atakueleza kwa maneno mengine lakini ujumbe utafika. Kama mtu wa tatu alivyoeleza.

    Halafu maneno na misemo yanatengenezwa kutokana na culture. Culture yetu ni kuwa mwanamke anakaa nyumbani halafu mume akirudi kutoka kazini..."heee mume wangu pole kwa kazi", watoto nao "Shikamoo pole baba kwa kazi"

    Huku wote tunachapa kazi...mkirudi home wote mmechoka swali ni "how was your day? Na linalofuata ni "what's for dinner? Na kama watoto wako wanajua kuongea utasikia "daddy is home", Hamna cha Shikamoo baba huku.....Manake Kesho tutaona mtu anaomba kuelezwa jinsi ya kusema SHIKAMOO kwa kidhungu ouch!

    Wa kumpa pole mwenzake hamna huku kwa vile huku hata kuka nyumbani kama ni mwanamke unajulikana kama ni house wife na ni kazi vilevile. Hivyo hata kama mwanamke akiwa haendi kazini naye yupo nyumbani ni kazi tu. Hivyo neno hilo wadhungu hawakulianzisha...

    ReplyDelete
  11. Kazi ni wajibu bwana, sio ridhaa. Wenzetu wanafahamu hilo ndio maana hakuna tafsiri sahihi ya salamu hii. Wabongo tumezidi uvivu ndio maana tunapeana pole kwa kazi.

    ReplyDelete
  12. Jaribu: Your Job is sorry!

    ReplyDelete
  13. vipi umeopoa "dhungu" nini?

    ReplyDelete
  14. My friend, the sentence is difficult 2 translate in English. All that it depends with the conversation, i think some words in swahili can not directly be change in english n if they do they don't make sense. i.e pole=sorry but u can't say "sorry for job" its doesn't make sense. Most people (how use english)ask questions to get the feeling on how someones day was.
    Examlpe: "How was ur day?" reply can be: Awful meaning extremly bad or it was a blast meaning can be gud or bad, or i work ma ass off.
    To reply to this person u might say "i hear you" or "i feel you" that show a little bit of sympathy but u can't say "SORRY FOR JOB"
    Mdau T-dot

    ReplyDelete
  15. wenzetu hawapeani pole ktk masuala ya kazi. Kama ni wajibu wako ktk kazi haina haja ya kupeana pole. It is much better kumpa mtu hongera. Mugisha

    ReplyDelete
  16. hakuna neno pole na kazi kwa kizungu kwa kuwa wenzetu kazi siyo hawaichukulii kama ni shida au kalaaa.

    ReplyDelete
  17. Hii ndiyo shida ya English Medium Schools. Tunajifunza lugha tu lakini utamaduni wetu ni tofauti na wa lugha tunazojifunza! Hapa kazi ipo!
    Laiti kama tungejifunza na utamaduni wa wenye English natumaini uchapakazi ungeongezeka maana kazi ni wajibu siyo mateso! Watu wangependa kazi!

    ReplyDelete
  18. Mijitu mijinga humu,inaropoka.Hata kama haijuwi inapandisha midadi,ona hawa wengine sorry for the job,kama wakenya.What is sorry for the job??? think people

    ReplyDelete
  19. Jamani hizi lugha za watu hizi, msijaribu mambo ya direct translation ya "watch mosquito watch" (sambusa) mtajiumbua! Kitu muhimu unaangalia unamaanisha nini, halafu unatafuta maneno ya lugha hiyo yenye kumaanisha hivyo hivyo.
    Na ukumbuke kuwa mara nyingi sisi tunavyosema "pole kwa kazi" mara nyingi ni kumjuliahali huyo ambaye hatujamuona kwa masaa hayo aliyokuwepo kazini na pia na huyo aliyebakia kufanya kazi za nyumbani. Kwa hiyo kwa kiingereza watu watokao makazini huambiana "how was your day"

    ReplyDelete
  20. MDAU USIWE NA WASIWASI NA SWALI LAKO. KATIKA VIUMBE WALIOKO DUNIANI INAONEKA NENO POLE LINA TAFASIRI YA MAANA KATIKA LUGHA NYINGE NA SIO KIINGEREZA. HAWA WATU WANAISHI MAISHA AMBAYO KILA MTU YUKO KIVYAKE AKIKWAMBIA POLE KAMA SORRY MAANA YAKE HAWEZI KUKUSAIDA MPISHE. SASA WASOMI DINIANI WAKATI WA KUANZISHA MAMBO YA ELIMU WALISHINDWA KUTIA MAANANI TOFAUTI YA NENO FULANI KWA LUGHA NYINGINE AU MAANA YA NENO FULANI KWA LUGHA YAANI KWA KIZUNGU TRANSILATION BY CONVERTION AU TRASNLATION BY DEFINITION. MFANO TAFRISI YA BABA KWA KIZUNGU NI FATHER( BY CONVERTION) ILA MAANA YA BABA KWA KISWAHILI NI MZANI WA KIUME( BY DIFINITION). NAMAANA YA FATHER KWA KIZUNGU NI MALE PARENT(BY DIFINITION), SASA TAFSIRI ZOTE UNAZOZIONA SASA ZINA MISINGI YA MAKOSA KWA KUSHINDWA KUTAFSIRI DEFINITIVE AU CONVERCTIVE. KWA HIYO POLE NI NENO LINAWEZA TU KUWA DEFINE AND IT IS NOT COVERTABLE .YOU CAN DEFINE POLE AS A WORD OF COMPATION AND EMPATHETICAL SHOWING SOME ONE THAT YOU FEEL HOW HE WORKED HARD OR HOW IS SUFERINGS.

    academia TUMAINI GEOFREY TUMU
    MOSHI TANANIA

    ReplyDelete
  21. Nimewapata vizuri sana katika huu mjadala lugha lazima u practise na sio tu kusoma school

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...