Wakati waandishi wa habari kutoka duniani kote wanafika kwa wengi katika mji mdogo wa Amstetten nchini Austria, polisi imeendelea kuchunguza nyumba ya familia ya mzee Josef Fritzl kutafuta ushahidi mwingine.
Wengi wanajiuliza vipi mzee huyu mwenye umri wa miaka 73 aliweza kumficha binti yake Elisabeth kwa muda huu mrefu wa miaka 24 pamoja na watoto wao katika chumba cha chini ya ardhi bila ya wengine kujua. Kwa muda huu wote alimbaka Elisabeth.

Polisi leo imechunguza ikiwa mlango wa chumba hiko uliweza kuwekwa na mtu mmoja bila ya msaada. Mlango huu una uzito wa kilogram 300 ulio wa chuma cha pua na mazege na wenye ufunguo wa elektroniki na unafunguliwa kwa kutia nambari ya siri. Mkuu wa upepelezi wa makosa ya jinai nchini Austria, Franz Polzer, alikanusha kwamba mzee Fritzl alikuwa na wasaidizi.

Bw. Joseph Fritzl alianza kumbaka binti yake Elisabeth alipokuwa na umri wa miaka 11. Wakati mtoto alifika umri wa miaka 18, baba yake alimtega kwenye chumba cha chini ya ardhi na kumficha huko.
Tangu hapo hakuwa tena na dalili yeyeto kuhusu binti huyo. Katika muda huu wa miaka 24 katika gereza lake, Elisabeth alizaa watoto saba, baba yake akiwa pia baba wa watoto hao.
Mtoto mmoja alikufa, wengine watatu mzee aliwapeleka juu kwenye nyumba na kumwambia mke wake kwamba Elisabeth aliwaacha mlangoni. Mbele ya familia yake, mzee huyu alisema, binti yake Elisabeth alikimbia nje ya Austria kuishi na kundi la kidini. Watoto wengine watatu waliishi na mama yao katika chumba cha chini ya ardhi.

Kulingana na mkuu wa polisi ya mji, Bw. Heinz Lenze, hakuna aliyejua kuhusu maisha ya wafungwa hao. Afisa alisema: “Aliunda picha kamili kabisa na mtuhumiwa alikuwa mwenye madaraka katika familia yake. Kulingana na uchunguzi wetu, si mke wala familia waliojua kuhusu maovu ya mzee huyo.”
Hata maafisa wa idara za serikali waliochunguza nyumba nzima miaka 9 iliyopita hawakugunda maficho chini ya ardhi.
Utekaji huu mzima uligunduliwa baada ya mfungwa Elisabeth aliweza kuzungumza na polisi baada ya kumsindikiza mtoto mmoja hospitalini. Polisi ilisema hali ya binti huyu ni mbaya sana, anaonekana kuwa miaka 20 mzee kuliko umri wake.

Kwenye picha zilizochapishwa na polisi unaweza kuona sehemu fulani ya maficho yaliyokuwa na jiko, choo na bafu pamoja na vyumba viwili vya kulala. Kwa ujumla maficho haya yalikuwa na ukubwa wa mita 60 za mraba.

Majirani wa familia hiyo bado wanashindwa kuelezea yaliyoendelea. Mmoja alieleza kuhusu namna, mzee aliweza kununua vyakula: “Alikwenda madukani kwa gari, lakini alikwenda hadi miji mingine, kwa hivyo haikujulikana kwamba ananunua vyakula vingi hivi.”

Kwa wakati huu, polisi pia inachunguza kesi nyingine ya mauaji na ikiwa mzee Fritzl alihusika naye. Pia kuna tuhuma nyingine ya ubakaji dhidi ya mzee huyu. Polisi inafikiria sasa kuwapa wahanga wa familia hiyo majina mapya.
HABARI HIZI ZINAKUJIA KUPITIA KWA www.malumbosjr.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2008

    MIMI SIONI KOSA LA HUYU BWANA KWA SABABU AMEAMUA KULA KUKU NA MAYAI YAKE NI BORA KULIKO WAZAZI WA HUYO DOGO WALIYE MFANYA ALE KICHWA CHA MTU TENA KATOTO KA MIAKA MITATU.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2008

    wewe hapo juu huna hata ubinadamu, wala akili sawa sawa. Labda wewe ni mojawapo wa watu kama hawa. Hamna hata afadhali, vyote ni vitendo vya kinyama, hakuna bindadamu yoyote wenye akili timamu anaweza kufanya vitendo vyakinyama kama hivyo. Nadhani unahitaja kuomba msamaha kwa wasomaji wa blog hii. Mawazo finju kama hayo hayafai, hata kama unataka kuanzisha mjadala.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2008

    KWA TAARIFA TU, MKEWE ALIYEMKIMBIA MIAKA MINGI AMEMRUDIA MZEE ILI WASAIDIANE KULEA WATOTO WAJUKUU!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2008

    BABA KUZAA NA BINTI YAKE HAKUNA KOSA LOLOTE KWANI WANAENDELEZA UKOO,PIA NI MUHIMU KWA BABA ASIYETAKA KUPOTEZA "U GENEOUS" WAKE. SI HIVYO TU BALI INASAIDIA KUPUNGUZA KUENEA KWA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KWANI WATOTO WA SIKU HIZI HAWAJATURIA HATA SEKUNDE!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2008

    JAMANI, JAMANI, JAMANI, MUNGU WETU MBONA TUMEMSAHAU??? KUTEMBEA NA MTOTO WAKO MPAKA KUMPA MIMBA YA WATOTO 7 NI HATARI NA INASIKITISHA SANA. NDUGU ZANGU HUU NI MWISHO WA ULIMWENGU NA MUNGU ATATEKETEZA VYOTE.. HII NI HATARI KUBWA SANA NA INATISHA SANA...JAMANI, HAKIKA KITENDO HIKI KWA MAONI YANGU NI CHA KIGAIDI. KUMFICHA MTU KWENYE MAHANDAKI KWA MIAKA 24 NI UGAIDI USIOELEZEKA!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...