MDAU,

ENDAPO KAMA UNA GARI AINA YA MERCEDES BENZ , RANGI NYEUSI AMA NAVY BLUE MUUNDO WA E200, E250, E300 NA E500 NA IKO KWENYE HALI NZURI WASILIANA NA KITENGO CHA SULLIVAN WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA AMBACHO KINAKUSUDIA KUKODISHA MAGARI AINA YA MERCEDES BENZ SALOON KWA MUDA WA SIKU 10 KUANZIA MEI 28, 2008 HAD JUNI 6, 2008 KWA AJILI YA MKUTANO WA SULLIVAN UTAOFANYIKA ARUSHA KATI YA JUNI 2 HADI 6. 2008.

PELEKA GARI LAKO KWA UKAGUZI GOVERNMENT TRANSPORT AGENCY (GTA) PALE BOHARI KUU BARABARA YA NYERERE KUANZIA MEI 3, 2008 KATI YA SAA MBILI UNUSU ASUBUHI NA SAA TISA UNUSU ALASIRI.

KITENGO CHA SULLIVAN TANZANIA KITAKODISHA GARI LAKO KWA GHARAMA ISIYOZIDI SHILINGI 150,000/- KWA SIKU.

KWA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NA KITENGO CHA SULLIVAN SIMU NAMBA

022 2111906/11,

2110185,

2128336,

AMA

0787 245424,

0715 599 299

KWA HABARI ZAIDI JUU YA MKUTANO WA SULLIVAN

http://www.thesullivansummit.go.tz/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Kwanza naomba kujua kuwa baada ya kuwakodosha je, Dereve ni wao au naleta dereva wangu?
    Kama dereve ni wa kwao, mhh! Nasita kidogo kupeleka gari langu.
    Wabongo sisi si tunajuana wenyewe jamani?
    Gari hilo linaweza kurudi kimeng'olewa hiki, kimeng'olewa kile, mpaka ukajikuta hiyo 1.5m yote ikaishia kwenye kurudishia vifaa vilivyong'olewa au kubadilishwa.
    Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  2. Mh Issa Michuzi Mie NAomba kuuliza kwani Lazima kwenye mikutano kwenda na "Benz" Bike ya Swala Au Phonex kama unauwezo siunafika na kueleza yaliokupeleka? pesa zote hizo tungezifanyia vitu vya maana vingi tu Tanzania. mambo mengine sawa na Watu wa Ma bara ya ulaya au Marekani ya Kaskazini kuvaa suti na tai kwenye mikutano, na sie waswahili tuna iga kuvaa hivyohivyo tungevaa Flana nyeupe na msuli au kama wa Ghana sindio mwanzo Nyerere alivaa hivyo? tizama Waarabu wanavaa mavazi yao hata nje kwenye mikutano UK au USA. wa nigeria na wa ghana pia bora kaunda suti nakubaliana nayo kidogo. kama gari jamani linakufikisha kwenye mkutano nenda sio mpaka foleni yote iwe benz. mnapenda kujipenda wenyewe viongozi watu wenu mnawaumizaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  3. hizo benz ni za kuwabeba marais watakauudhuria mkutano i think,maana kutakuwa na viongozi wengi sana wa africa,pamoja na baadhi wa asia,na ikulu haina benzi nyingi,ndo maana hata sherehe za muungano viongozi wa zanzibar huwa wanakuja na gari zao,wadau changamkieni dili hizo,kwa wakazi wa arusha hizo wamezizoea,kutoka na ikutano ya mara kwa mara huwa wanazikodisha gari zao sana,kuna watu arusha huwa wanaishi kwa hizi dili,mkutano unakuja na dili za kumwaga,wadau kuweni makini msizidiwe akili na watani wetu,maana wameshaomba kushiriki kwenye mkutano kuliko wa tz wenyewe,na wanauwania mkutano mwakani waupeleke kwao,wameanzisha kampeni kuwa arusha hakuna hotel za kutosha so wawapeleke wengine nairobi,´wakati arusha hotel saa hivi za kumwaga na dar tunazo pia hotel,na kama umbali ticket ua bus ni same dar arusha,na arusha nairobi.wabongo tukizubaa tunapigwa bao la kisigino kama kawa.

    ReplyDelete
  4. Mbona kila kitu ni ishu? duuh ila kweli mawazo ya mtu tuyaheshimu, Mtoa maoni wa April 29, 2008 1:34 PM si lazima Benzi ila bajeti inaruhusu, sijui hata nielezeje ila tukisema hivyo basi hata hapa blogini kukomenti ingekua duuh mtu angesema gharama za saa nzima internet ni Tsh 500 kwingi sana tsh 1000 si heri ungempa mama aliye Muhimbili anunue machungwa arejeshe afya aliyopoteza kwa kujifungua?, vingine tuanche naona wanataka kupendeza na kufanana na kumbuka Benzi ina Hadhi

    ReplyDelete
  5. mi ninayo ya damu ya mzee mkiitaji wasiliana nami

    Proditram@gmail.com

    ReplyDelete
  6. Nilizania wanakwenda green. Nilitegemea watatangaza kuwa wanatafuta watu wenye TOTOTA PRIUS HYBRID.

    Kwani serikali haina tena yale mabenz yao yalikuwa yanamwagwa kila corner ya Arusha ikija mikutano ya kimataifa...Enzi zile STD tukiwa wadogo yalikuwako hayo.

    ReplyDelete
  7. Mimi nina E320, mumeisahau ama hamuitaki kwa makusudi?

    ReplyDelete
  8. Dooh amakweli nimeamini Tz sio masikini ila masikini ni watz, Hizo tenda za mafisadi si walala hoi tutaweza wapi? Mie nina maki 11 ila haina AC nitaweka kafeni kadogo. wakihitaji Pls Michuzi utanishtua.

    ReplyDelete
  9. Kenya tunayo mabenzi hayo kibao mnahitaji mangapi watanzania tuwaletee? Ila mtalipa kwa dola.

    Kama mnayahitaji wasilianeni na Balozi wa wewtu wa Kenya hapo Tanzania na yeye atajua yatoke wapi bila tatizo.Mabalozi wetu wanajua nini kifanyike mkitoa hayo maombi.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 01, 2008

    Machalii wa A.City tunayasubiri hayo mabenz hasa za wabongo(machalii wa Dar)lazima kadhaa tuyakimbize hapo Kenya.Madreva tuko camp tunajinoa,benz tukiiweka mikononi break Isilii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...