BENDI YA MUZIKI WA DANSI YA AFRICAN STARS “TWANGA PEPETA INTERNATIONAL” INATARAJIWA KUONDOKA MJINI DAR ES SALAAM LEO JUMANNE USIKU KWA “ SHUTTLE” KWENDA MJINI NAIROBI, KENYA KWA AJILI YA KUTUMBUIZA MAONYESHO MANNE NCHINI HUMO.

MAANDALIZI YOTE KWA AJILI YA SAFARI HIYO YAMEKWISHA KAMILIKA NA BENDI IPO KAMILIFU KWA AJILI YA KUKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WA HUKO.

ZIARA YA TWANGA PEPETA NCHINI KENYA IMETOKANA NA MWALIKO MAALUM KUTOKA KWA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA KITAIFA CHA WAFANYAKAZI NCHINI KENYA(COTU) MR FRANSIS ATWOLI NA PIA ROTAMU PROMOTIONS YA NCHINI HUMO NA ZIARA HIYO ITAFAHAMIKA KWA JINA LA “AMANI TOUR” LENGO L IKIWA NI KUSAMBAZA UJUMBE WA AMANI NCHINI KENYA KWA NJIA YA MUZIKI KUFUATIA MACHAFUKO NA VURUGU KUBWA ZA KISIASA ZILIZOKUWA ZIMEIKUMBA NCHI HIYO HIVI KARIBUNI MARA BAADA YA UCHAGUZI MKUU.

BENDI INATARAJIWA KUONDOKA NA WANAMUZIKI WAKE WOTE NYOTA WAKIONGOZWA NA KIONGOZI MKUU KHAMIS AMIGOLAS NA KIONGOZI MSAIDIZI LUIZER MBUTU CHINI YA MENEJA WAO ABOU SEMHANDO.

BENDI INATARAJIWA KUREJEA NCHINI WIKI IJAYO JUMATATU YA TAREHE 5-05-08 ILI KUENDELEA NA RATIBA YAKE YA KILA WIKIENDI JIJINI DAR ES SALAAM.

ITAPOKUWA HUKO ONYESHO LA KWANZA LITAFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA UHURU PARK KATIKA KILELE CHA SHEREHE ZA SIKU YA WAFANYAKAZI (MEI MOSI) KUANZIA SAA NNE ASUBUHI AMBAPO MGENI RASMI ANATARAJIWA KUWA RAIS WA JAMUHURI YA KENYA MHESHIMIWA MWAI KIBAKI.

ONYESHO LA PILI LITAFANYIKA SIKU YA IJUMAA TAREHE 02-05-08 KUANZIA SAA TATU USIKU KATIKA KLABU YA USIKU YA NEW DEEP WEST RESORT ILIYOPO JIJINI NAIROBI, ONYESHO LA TATU LITAFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 03-05-08 KUANZIA SAA MBILI USIKU KATIKA KLABU YA CASAURINA (ZAMANI ILIKUWA IKIJULIKANA KAMA COCO BEACH), NA ONYESHO LA NNE NA LA MWISHO AMBALO NI MAALUM KWA AJILI YA FAMILIA LITAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA NEW DEEP WEST RESORT JUMAPILI, MEI 4 KUANZIA SAA KUMI JIONI HAPO HAPO MJINI NAIROBI.

HII ITAKUWA NI MARA YA PILI KWA BENDI YA AFRICAN STARS “ TWANGA PEPETA” KUZURU NCHINI KENYA KWA MUALIKO BAADA YA MWAKA JANA MNAMO MWEZI WA SITA KUZURU CHINI HUMO KWA MAONYESHO KATIKA MIJI YA NAIROBI NA MOMBASA.

BARAKA MSIILWA
MWENYEKITI
AFRICAN STARS ENTERTAINMENT (ASET)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. heee mazei,waKenya halahala masupuu wetu,muwatue.udenda unawatoka nishaona.

    ReplyDelete
  2. Hi!Kaka Michuzi kwa pongezi sana kwa kutuwekea tangazo hili,kuwa
    Twanga Pepeta watoto wa Nyumbani,watapeperusha bendera kwa watani wa jadi!
    Hi!iiiii!!!!!Raha tupu Twanga fanyeni kweli

    ReplyDelete
  3. HIVI KUMBE ZILE STYLE ZA KICHUPI CHUPI BADO ZINAENDELEA NILISHASAHAU. UKIMWI OYEEEEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  4. Dada Aisha naona sasa ni wakati wa kuchukua image right

    ReplyDelete
  5. Kwanini kila wakati Kaka Michuzi ukitonyesha picha za bendi ya Twanga wanenguaji wake picha ni ya Dada Aisha? Kwani mcheza show ni yeye peke yake??? So Booring.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...