wadau kunradhi,

habari za aliyekuwa gavana wa benki kuu mh. balali nimezipata toka jana, ila bado sijazithibitisha, ingawa vyombo kadhaa vimerusha. tutapashana mara mambo yatapokuwa tayari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2008

    vipi keshafleti?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2008

    Michuzi ni zakweli, mimi nakusibitishia kwani nimeongea na watu wake wa karibu jana mchana.

    Sasa kama unataka kupata confirmation kutoka kwa Rweymamu au JK mwenye then sahau sababu Balali hakuwa muajiriwa wa Serikali, so serikali hana say ya lolote lilotokea.

    Wasilina na mimi nitakupa simu ya muwakilishi wa familia

    Mdau wa DC

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2008

    Mjomba ukisema kuwa ameondoka nitafikiria vitu vitatu:
    1. Kuna mtu anatuyeyusha na anataka kutuacha ktk mataa.
    2. Ktk serikari yetu kuna special force ya kufuta watu wanaoiharibia heshima. May be they use Polonium 210 too.
    3. Tusipoona mwili nitaamini kuwa jamaa kafanya plastic surgery na kuingia mitini na sie tutalilia ndondocha...
    Kama ni kweli RIP ila umeondoka na siri nyingi mno
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2008

    vipi tena mtu wangu? huyu jamaa mnataka kufanya nini tena mbona kama mambo yake yalishakwisha? Sijui

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 21, 2008

    Hakuna lolote,

    Hilo watoto wa mjini tunaita ni "CHEZO" limechezeka,

    Hapo inatafutwa maiti ya mtu mwingine na kusingiziwa ni ya Balali kisha watu wanazika,

    Kwa kua ni Muislamu hakuna mambo ya kuacha sura wazi

    Then Jamaa anahamia kwengine na hakuna atakaemjua na ndio wa mwisho wa skendo wa EPA,

    Wajanja tumeshtuka,

    Plse michuzi, kapuni NO

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 21, 2008

    MUNGU MKUBWA...KAMA KWELI JAMAA KADONDOKA...itakuwa kadondoshwa na Waheshimiwa ili kuficha skandali zima la waliotafuna hela ya EPA...ILA jasho la wanyonge halipotei na halitakauka bure. Hata kama WAMEMMALIZA wakidhani wamenusurika, siku zinakuwa watarudisha haki zote wamekula. Jiulizeni..inakuwaje hela inarudishwa halafu hakuna anayejua ni nani anairudisha Benki? Linawezekana hilo? ..WAJINGA NDIO WALIWAO...Wamemmaliza nani atakuwa na ushahidi kuliko aliyewakabidhi ambaye hayupo tena??..NDIO WALILOKUWA WANALITAFUTA HILO ndio maana walichelesha kumleta nchini..HABARI NDIO HIYO!!!
    ----------
    By Mangi-08

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 21, 2008

    Na mimi nilitaka kushangaa....iweje MZEE WA BREAKING NEWS umekauka mpaka sasa. Nikadhani labda unawaogopa waosha vinywa watakavyolia kwa uchungu wa kuondokewa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 21, 2008

    Katika toleo lake la leo, gazeti la "Tanzania Daima" limetoa makala marefu ya Front Page (na kuendelea page 2) kuhusu kufariki kwa Daudi Ballali tangu Ijumaa iliyopita, na kwamba atazikwa Ijumaa ijayo hukohuko Washington DC.

    Taarifa hiyo sasa ipo pia kwenye tovuti yao katika anwani ifuatayo:
    http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/5/21/habari8.php

    Poleni sana kwa wote wale wanaohusika nae kama ndugu, marafiki au majirani.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 21, 2008

    Michuzi ee, wewe mtu mzima na unaakili pevu, kwa issue iliyotokea kuambiwa huyu mtu kafa haiingii akilini, anyway publish tu ili watanzania tutoe hasira zetu kwa maandishi.ila wote tunajua jamaa hajafa, serikali inaficha ukweli, jamaa anahimia state nyingine ya marekani yenye watu weusi wachache,pesa alizoiba zinamtosha kukaa residents za matajiri. Kisha watanzania tulivyo wapumbavu tutaendelea kuwa wapumbavu. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WAPUMBAVU WAKE

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 21, 2008

    UZURI WA BONGO HUITAJI KUWA SHEIKH YAHAYA HUSSEIN KUTABIRI MAMBO,TULIYASEMA HAYA JAMANI KUHUSU KIMYA CHA BALALI KITU KITAFANYIKA JAMANI.HAYA SINA MENGI .

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 21, 2008

    Hili chenga la macho! Ni vigumu kuamini sasa tutasikia hooo vijisenti vyote balali ndo alichukua! Wajanja sana

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 21, 2008

    Habari za kusikitisha kama ni kweli. Ila inabidi kuwa cautious hapa.. isije kuwa jamaa ama ndugu zake waka-fake death news ili ndugu yao aweze kuibuka na identity ingine kukwepa mkondo wa sheria. Cases kama hizo zipo nyingi tu.. proof is needed here kama ni yeye kweli na sio tell-tale.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 23, 2008

    KUMBUKA ZITTO ALIKUJA USA AKAWEKA MAMBO SAWA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...