JK na (kutoka shoto) Mhe. John Cheyo, Jaji Mark Bomani, Mhe Iddi Simba na Mhe. Zitto Kabwe wakiwa katika mazungumzo ya kukabidhi ripoti ya madini leo huko ikulu, dar. chini JK akiwa katika picha ya pamoja na kamati teuli ya madini ikulu



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2008

    Huyu msukuma (Cheyo) anataka kupiga mtu nini!! mbona inaonekana yupo ngangari!!
    Mheshimiwa zito nae inaonyesha hajafurahi maana amekunja uso wake huyo!!
    Jamani msihofu, hapo ni ikulu hivyo kunyweni na mfurahi kwani hamuwezi kubalaliwa. tehee!!! teheee!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2008

    mzee wa kaya matiz kidogo usijiachie muheshimiwa, 2010 bado unaitajika kuwatokomeza mafisihard bila ya wenyewe kutambua nini kinaendelea

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2008

    siasa ni mchezo mchafu.

    raila odinga alihamasisha wananchi pale kenya, sasa kawa PM na mpira umekwisha (wakenya kama walitegemea neema basi wasahau)

    kuna jamaa wa upinzani kule zimbabwe naye kama atashinda sitegemei jipya

    zambia walipurukushana sana na mzee KK, kawaachia nchi, kiko wapi!

    M7 kang'ang'ania! na usitaje akina taylor wa liberia nk..

    ukija kwetu ni yaleyale ya akina akina charles taylor.. wao walitumia mtutu wa bunduki kuchukua uchumi wa nchi lakini hawa wanatumia ujanja wa "karata tatu' kufanya unyama uleule.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2008

    1CHENGE=1MILLION USD(NATANIA)

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2008

    Mimi nadhani sasa wakati umefika kwa viongozi wetu wa dini kubadili mahubiri yao yanayosema kwamba mtu ukishatubu basi unasamehewa madhambi yako na mungu ili kuikoa dunia na maovu na maangamizi dhidi ya raia walio wanyonge. Kama tunaruhusu mashoga kuwa viongozi wa dini basi na hili najua linawezekana. nasema hivyo kwa sababu majambazi, mafisadi wanaua na kutesa viumbe na baadae kwenda kutubu ili wasemehewe lakini huku tayari wameshaua au wanatesa watu kwa kuwafanya vilema au kuwakosesha huduma wanazostahili kama binadamu. nadhani sasa tubadili staili ya kuhubiri na watu waambiwe kwa mungu ni JINO KWA JINO ili kupunguza ukatili wanaofanyiwa binadamu. mfano ni ule wa mzee wa vijisenti, wakati yeye anasema 1.0 bil ni vijisenti huku watu wengine wanakosa mlo ili waokoe maisha yao. Lakini utawasikia wahubiri wakisema akitubu ataenda mbinguni, hivi mungu kama ndiyo yuko rahisi kiasi hicho basi atakuwa hawatendei haki wanyonge

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2008

    hahahha anon wa 1:13


    WWW.UFISADI.COM hapo,mwanakwetu .. ivi hawana aibu??????

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2008

    vitambi vya wizi tu hapo!

    HELA ZETU ZIKO WAPI???

    nawauuliza tena enyi watu hapo kwenye picha HELA ZETU ZIKO WAPI?aha,nilikua sijasikia,kumbe kitambini

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 26, 2008

    MICHUZI, CAN WE HAVE AN EXCERPT OF THE REPORT?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 27, 2008

    Haya sasa na tumuone Mhishimiwa Raisi ripoti hii ataifanya vipi ? Maana ya EPA , Ballali and Co ndio hivyo ten akafa nayo Ballali itaishia hewani. Haya Chenge ndio huyo hana wasiwasi yuko mjini anakula starehe. Lowassa katulia hatoki magazetini anakula kuku polepole anavuta time akakusanye na zile pesa za Richi Monduli kwenye account isiyo na jina libeneke la Ufisadi kama kawa,Ukija kwa baba lao Mhishimiwa Rais mstaafu tunaambiwa tena tusithubutu hata kumtaja taja na kumtupia kashfa wakati ziko wazi !!!! hawa wengine wadogo wadogo woote bado wanaendelea na Ufisadi na hamna mtu anaewagusa.Sasa hii Ripoti ya Madini ilishaleak siku nyingi watu tunayo na kwa kweli ukiiona machozi yanakutoka kama mtoto mdogo yaani hii ndio baba lao , Wadau wenzangu subirini mtajionea !!! kaka Michuzi naomba utoe posti yangu usiibanie kwa kuwa nimewataja wazee wakuu wako!! JAMANI TUTAFIKA ???? AMA KWELI BONGO TAMBARARE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...