nimefurahi kukuta mambo haya kwenye vyoo vingi vya ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa aicc, kuonesha kuwa wanaafiki kwamba kinga ni bora kuliko tiba. na hii siyo kwa nanihii tu bali pia hata fegi. huu ni mfano wa kuigwa, mnasemaje wadau - hala hala waosha vinywa msianze... huo mkono si wangu.....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2008

    Kwa kweli hayo ndo mambo;
    Ila michuzi sasa hapo umejishusha; huo mkono ungekuwa wako mi nigekupa BIG UP kubwa kwa maana kwamba unajikinga; hata kama ulienda na mywaifu wako tungejua hamtaki kupata mabebi wengii;
    Sasa umekataa mkono si wako sisi tujue nini? JE wewe hizo Kinga hazikuhusu?
    Mi ningependa uwe mkono wangu na ningejidai sana kama mimi ni mtumia Kinga...

    Tafadhali usinibanie comment yangu...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2008

    Misupu; ninaharusi mwez wa tisa ya mdogo wangu sasa nitakuptaje kwa ajili picha??
    Ningependa utuwekee tangazo lako kama unafanya picha za still hapa kwenye blog ili tujue kama ni business au nimjuano? manake nasikia unapiga lakini sasa details hazitufiki vizurii
    Pliz nipe details:
    Waridi

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2008

    Unajitetea nini Michu, kwani wewe si mmojawapo wa walengwa wa bidhaa hiyo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2008

    Huo mkono wa kwako kabisa mzee wa Mikonooozzz!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 21, 2008

    Hiyo diameter si mchezo!
    Kweli kuna watu wana vitu jamani!
    Mbona mnatutisha sie wadada, au kaka michuzi hayo ni mambo yako ya fotoshop?
    Mzingo = Pie * Kipenyo, sasa kwa hicho kipenyo kunamtu atatoka salama hapo, maana ukizidisha na Pie unapata ingo hilo!
    Kaazi kwelikweli!!!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 21, 2008

    Yah wazo zuri. Lakini sisi tmechelewa kuanza. Hizi kinga kawaida zinatakiwa sehemu zote za public. Watu wengine wamekuwa wakifanya siku nyingi zaidi. Na inawezekana wanaweka tu kwa muda mpaka tarehe 04/06. Kwa hiyo tusubiri kidogo

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 21, 2008

    Nasikia kuna wahuni wanazipa sindano then wanazirudisha kwenye box. Mtu ukija, unachukua kwenda kutumia ukidhani haipitishi ngoma!!
    Inabidi hiyo box iwe sealed kama za mtoni!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 21, 2008

    Hahaa,
    Kwa kweli mimi nadhani hiyo ni njia nzuri tu ya kuwakumbusha watu wajibu wao.
    Umefikia wakati tuwe wawazi kwamba ABSTINENCE is a difficult option, it doesnt work. So, give them condoms so that they may use them in the next sexual contact.
    Nikiwa mwanafunzi wa Afya ya Jamii, nimefurahishwa sana na hiyo hatua ambayo mwenzetu Michuzi uliikuta huko AICC.
    Michuzi, mimi nakufahamu sana. Tumeshasalimiana sana pale SKYWAY BUILDING, HUO MKONO NI WAKO na natumaini hutapata matatizo kwa MRS kwani atajua UNATAMBUA WAJIBU WAKO.
    Asante.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 21, 2008

    Hii idea nzuri ila kondumu za bure Tanzania ni kama zimetengenezwa kwa mfuko wa rambo...ngumu ajabu.!!!

    Wajitahidi kuweka kondomu zenye quality kidogo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 21, 2008

    MBONA HAUJATULEZA KAMA VYOO HIVYO HUTUMIWA NA JINSIA ZOTE BILA UBAGUZI? KAMA NI CHA WANAUME TU, MNAHITAJI KINGA GANI ZAIDI KWANI UKIMWI HAUAMBUKIZI KWA KUTUMIA CHOO KIMOJA. HIVI HUMO CHOONI KUNA VITANDA AU NIKUKANDAMIZA UKUTA? NAJUA GESTI NYINGI HIZO ZANA UTAZIKUTA VYUMBANI NADHANI KUNA KITU FISHY WALIOZIWEKA WANATEGEMEA KUTOKEA, MIMI SIJUI.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 21, 2008

    kono lako michuzi jeusi ka la obama kwa kuvuta

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 21, 2008

    Kwani michuzi hata huo mkono ukiwa wako kuna ubaya gani? si inaonyesha ni namna gani unajali, siku hizi hakuna mtu anayeona noma kutumia hayo mavituz hali imekuwa mbaya sana ndo maana siku hizi mambo ni wazi wazi

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 21, 2008

    viongozi wetu wakiafrika huwendesha mambo kiafrika wakitaka waonekane nao wamo katika ulimwengu wakileo sasa tuangalie hii ni kwa hao watu maalum na sio kwa kila binadamu hasa kwa wale waliokuwa hawana uwezo ????????

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 21, 2008

    SIJUI MLIOCHANGIA HAPO JUU NA ALIYETOA HII MADA NI DINI GANI NA WALA SIINGILII UHURU WENU WA KUABUDU, ILA FAHAMU MIMI NI MKRISTO, HATURUHUSIWI, MKE WANGU MWISILAMU SAFI, HARUHUSIWI PIA. NIMEMALIZA


    KWa wale wanaopenda ubishi:
    Tafuta mazingira yoyote ya utumiaji wa hizo kama si kwa ajili ya uzinzi, na uzinzi umekatazwa.
    PILI suala la kubajeti idadi ya watoto Mola alishaliona hilo, mtuna mfumo sawa na Sokwe, nao je tuwape Kondom?
    Mwisho kabisa siziamini, nashukuru na aliyeongeza kuwa HUTOBOLEWA KWA MAKUSUDI!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 21, 2008

    mkono wako huo usijishaue hapa

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 21, 2008

    Anonymous wa May 21 8:11 am napenda kukutoa wasiwasi kidogo kwamba masuala ya kugawa hii mipira si kwa hapo aicc peke yake bali ni maeneo mengi wanafanya hivyo. Kwa mfano ungekwenda kwenye vituo vyote vya afya huduma kama hiyo ni bure na iko hadharani tu bila woga, pia katika idara na wizara zote za serikali hii huduma iko bure tu. Na mimi naamini kwamba kwa hapo aicc si kwa ajili ya mkutano wa sasaivi tu bali kila siku zipo kama vile chooni hapakosi tishu (eti mnaita toilet pepa)
    Mimi
    Sipendi

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 21, 2008

    ooossshhh!!
    hizi nini vile?thijui ni pipi!!au ndo dhile dhinadhofanana na maputo?
    ila wamefanya la maana kudhiweka kila sehem lol!!
    ila na uhakika huu mkono sio wa michuzi maana yeye anavaaga fulana tuu na huyu muhusika kavaa koti.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 21, 2008

    mkono ni wako si ulivaa suti ulivypiga picha na maprofesa sasa kuibadilisha rangi maana yake nini wacha hizo michu.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 21, 2008

    MICHUZI MIMI USHAURI WANGU KILA NYUMBA YA MJUMBE WA NYUMBA KUMIMI LIWEKWE KAPU KUBWA LA KONDOMU NJE HILI WADAU WAWE WANA CHOTA TU NA ZINGINE TUWE TUNAGAWA MICHEZONI KAMA MECHI ZA MCHANGANI NA KILA KONA.HIO INAWEZA KUSAIDIA SANA.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 21, 2008

    WE ANON WA 21 MAY 9:56
    UNANICHEKESHA SANA WE MKRITO NA MKEO MUISILAMU .KATIKA DINI HIZI MBILI NAONA HAZIOANI ; SASA HUONI WE NA MKEO MUISLAMU KUWA MWA ZINI? TENA NYIE NI WAZINZI WA KWANZA NYAMBAFU TUMIA KONDOMU , KWANI NIBORA KULIKO HIVYO UFANYAVYO NA BINTI WA KIJAHIDINA

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 21, 2008

    Mimi ni voda to voda tu(Usiibane michuzi nimetumia lugha fasihi)

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 21, 2008

    That's very good! Tatizo kubwa ni how to overcome woga na aibu ya kuzitumia. Kwa mfano, Misupu hapo ameanza kujitete "mkono si wangu..." kwani wewe hupaswi kutumia? Jamani, hata zile zinazotolewa bure ni zimethibitishwa ubora. Utamu wake inategemea, wakati mwingine ni mambo ya kisaikolojia pia, anyway.

    Seve

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 21, 2008

    WE anony wa SAA8:55[MKRISTO mme wa MWISILAMU]
    kuhusi swala la imani yako[yenu] siwaingilii hata kidogo kwa mambo ya ZINAA[uzinzi,uasherati,n.k] lakini kusu swala la kupanga uzazi napenda ni kuhakikishie kuwa wewe una wajibika pia kufanya hilo.USIJILINGANISHE NA SOKWE!!maana wale niwanyama,na kitaalam wanyama rythm yao inakuwa controlled na hormones tena pale tu wanapohiaji kujamiiana kwa kuzaa.lakini kwa binadamu wewe mwenyewe ni shahidi ni marangapi umemhitaji huyo mwenzio kwa casual sex?i.e kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kisaikolojia na kimwili pia?kwa wanyama hicho kitu hakipo.wa hu-detect ferromones zinazo tolewa mwilini kwa wakati maalum tu ambao wanaweza kutunga mimba!na dume anaweza kunusa ferromones hizo hata kwa umbali mrefusana,[mfano mbwa,vipepeo,ng'ombe n.k] pia milio fulani.
    PIA Kumbuka wanyama hawahitaji mahitaji kama shule,mavazi,tofauti na binadamu ambaye yuko organised.
    WEWE MUNGU KAKUPA UWEZO WA KUITAWALA NATURE kwa kui-manipulate ili ikusaidie!sasa mfano simu,computer,madawa ya hospitalini,n.k unadhani itakuwa sahihi kusema vitu hivyo nidhambi?
    mimi ninaweza kukupa mifano hata ya dawa ambazo basi unaweza kuziona ni haramu kwa imani yako kama unamtizamo huo hasi[hapa si challenge dini,nachallenge mtizamo wako]!pia kuna baadhi ya huduma kwa mfano MTOTO WAKO AU MKEO anatatizo la kupungukiwa damu[ANEMIA]JE UTAMPELEKA AONGEZEWE DAMU YA MTU? je hiyo kwako sio dhambi?au mtu amepata ajali akakatika miguu,je AKIPEWA MIGUU YA BANDIA sio dhambi kwako?huoni basi huo utakuwa unamsaidia mungu kuumba?au mtu kazaliwa na ulemavu unao weza kutibika kwa upasuaji[reconstructive surgery] je sio dhambi kwako?
    au wewe ukijijuwa kuwa ni carrier wa ugonjwa unaoweza kumuambukiza mkeo nao hautibiki je utafanya tendo hilo ili naye amambukizwe kisha afe kwa makusudi?
    hiyo ni mifano michache tu,najuwa sio wewetu peke yako kunawengi wanao sumbuliwa na uelewa wa mambo,ila ungekuwa umesoma philosophy,theology,na divinity[sio hiyo ya form six] ungeweza kuelewa namna ya kuchambua mambo yanayo husu imani kwa kina.hapa hapatoshi kukupa shule ya kutosha,lakini mimi kama daktari na mkristo kama wewe pia,nakushauri utafute elimu[ya mungu na yadunia] ufute vumbi machoni.usiwe kama watu wale wanaougua wanashindwa kujuwa kuwa mungu katoa elimu ya tiba kwa watu ili waitumie,au ndege waangani pia huruka ili wafike pale ambapo mungu kawawekea chakula ili wale,na wala hawasubiri awawekee midomoni mwao ili wameze!!!!! hope you understand,

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 22, 2008

    MASKINI CHELSEA TUMEKOSA UEFA

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 22, 2008

    Mi nimeupenda huu mdahalo wa Dr na mme wa mwislam,mipambano kama hii ndo inachangamsha blog ya michuzi hasa jamani, tunajifunza vingi humu kwenye kujikwaa ulimi ukweli masikio huwa juu kama popo na macho kama bundi wakati wa kusoma hapo ujue tunatoa vumbi sie wengine hapahapa bure bila gharama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...