Cinderella"," Nakshi nakshi" na Miss Schengen 2008 ndani ya Germany kufanyika tarehe 28.06.08, Essen
Katika shindano la kumsaka mrembo wa Schengen 2008 , burudani itatolewa na msanii Ali Kiba ambaye ameahidi kurusha nyoyo za wapenzi wake usiku huo wa raha. Katika sakata hilo Mgeni rasmi atakua ni Balozi wa Tanzania nchini Germany Balozi A.R. Ngemera.
Wageni wengine maalum ni mratibu wa Kitengo cha kiswahili radio Deutsche Welle bi Andrea Schimdt, Mratibu wa Beautiful tanzania Agency bi Irene Kiwia na Miss World Africa Nancy Sumari.
Akifafanua zaidi Mratibu wa Shindano la Miss Tanzania Schengen bi Nashe Mvungi ameelezea kuwa kwa mara ya kwanza Miss Tanzania kushirikisha mrembo kutoka Schengen 2008, Ambapo mwaka jana UK ilikuwa ya kwanza kushirikisha mrembo kutoka nje ya bara la Afrika.
Nia ni kutaka kupanua utamaduni na mila ya mtanzania ulimwenguni, kushirikisha watanzania walio masomoni au wanaoishi ughaibuni katika kuchangia maendeleo ya tanzania kiutalii na elimu na kuweka uhusinao katika ya jamii iliyoko nyumbani na Ulaya.
Pia alipenda kufafanua kuwa shindano hili limepitishwa na kupewa baraka zote na Uncle Hashim Lundenga wa LINO International agency waandaaji wa miss Tanzania.
Mshindi wa shindano hili atajipatia zawadi ya ticket na nafasi ya kushiriki shindano la kitaifa mwezi August 2008 Dar es salaam.

info@misstanzania.eu
+49 1520 588 0863

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2008

    watu wenye sura zao hawaendagi kushiriki manake ni uzushi mtupu..mtaona atakaeshinda,kwa anaebisha

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2008

    Wameiita 'Miss EU Schengen 2008'. EU ina nchi 27. Schengen nchi 15. Kwanini wamewatenga watanzania wenzao (kwenye warembo wazuri zaidi)?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2008

    OHOOO!! sasa hii ya mshindi atapelekwa kwenye mashindano ya Taifa huko Bongo mtawakosa washindani wengi wazuri wenye sifa za kushinda hapo EU maana wataogopa wakishinda itakuaje akiambiwa aende akashiriki TZ na hana vitu vitakavyomfanya arudi tena EU (Mapepa mwanawani!!!) pagumu hapo!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...