HAPA MWILI WA MAREHEMU DAUDI BALALI UKIWA KANISANI. SAMAHANI SIKUWEZA KUCHUKUA PICHA VIZURI NDANI YA KANISA. LAKINI KAMA UNAVYOONA KWA MBALI KUNA JENEZA .

PICHA NA MDAU WASHINGTON DC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 43 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2008

    Kwa mtazamo wangu Rais alipotoka kimaamuzi.
    Nadhani mheshimiwa alimuonea Balali kwa kitendo chake cha kumfukuza kazi,kama hakumuonea alitenda haki je ,alimfukuza kwa kosa gani?
    Kama ni kweli Balali alifukuzwa kazi kwa kuhusika katika upotevu wa mabilioni ya EPA,si ni sawa na muhujumu Uchumi?
    Je mhujumu uchumi si hushitakiwa kwa kosa hilo alilolitenda au hufukuzwa tu kisha basi?
    Mbona Prof.Mahalu anashitakiwa ati amehujumu,Je kuna kiwango cha hujuma ambacho ukifikia basi wewe unakua huru juu ya sheria?
    Nikijiuliza maswali hayo majibu nakosa kabisa nabaki kujiuliza tu kuhusu Mr.Prezi..........
    gEoRGe

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2008

    Acha kujidhalilisha michuzi. Au ndo umepewa tenda ya kusafisha jina lake? Hizo njaa mbaya msidhani ndo njia ya kuaminisha watu. Shame!!! Najua utaibania sijali kwani ujumbe wangu ni kwako michuzi si kwa wengine we bana tu. Message sent and RECEIVED

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2008

    msitufanyie usanii na kutufanya sie watoto,tutapataje uhakika kuwa aliyefariki ni yule mmojawapo wa wahusika na fweza zetu akiwa BOT? wakristo wakitoa heshima za mwisho kunakuwaga na kufunguliwa jeneza mboni hapa hamna?hamna hata picha za mwili in jeneza?na mama yake bongo amehakikishiwaje kuwa aliyekufa ni mwanae?
    msiba gan mpaka upate mwaliko kushiriki?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2008

    REST IN PEACE.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2008

    sie sio watotoooooo kutubeba kirahisi hivyoo wadanganyeni hao haooo sio sie tulioko huku..
    hizo picha sasa ndo zathibitisha nini juu y ahuo msiba wakati hazionyeshi hata balozi wetu,mkewe,dada zake na marehemu mwenye ndani ya jeneza..

    najua hii nayo mtaibania kwa sababu na nyie si mko ndani ya system....Mungu atazidi waumbua tu!na badooo kwa hili movie la Balali mmechemka njooni na nyingine

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 24, 2008

    kama sijakosea mwanzo nilisikia balali ni muislamu,inakuaje tena na mambo ya kanisani?
    anyway,imekuwa vizuri zaidi kama ni mkristo kumbe tunaweza kupata picha zake akiwa kwenye jeneza,tafadhali,sogea mbele zaidi upate uso wake ili tuwe na uhakika zaidi.
    maana angekuwa muislamu tusingeweza kuona sura yake.
    MANYUNYU

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2008

    CHANGA LA MACHO HILOOOOO...

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 24, 2008

    Poa Tu Najua Hii Hutaitoa Ila wewe Utaisoma.Muwatie Changa La Macho Hao Hao Mlionao Hapo Bongo.Sie Wajanja Tumekimbia Kama Alivosema Juma Nature Waliobaki Mnaumia. Hivi Hata Kama Ni Huo Ufisadi Serikali Gani Inachukulia Juju Ya Kifo Cha Mtu Aliekua anaweka hadi Sign Yake Kwenye Hela Za Nchi??? Leo Anakufa Mkwere Anatoa Rambirambi zuga!!! Ila Mjue Iko Siku Hata Hao Walioko Tunduni Watachoka

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 24, 2008

    I could say the winners here, are all culprits in EPA scandal. It doesn’t matter whether they come from ruling party, government or private sector; these are the people who will be laughing behind the scene and crying with crocodile tears in the public!

    Sadly and unfortunately, ‘we’, as normal citizens are the losers in this case, big time! Why? The simple reason is “we’ll never be able to see the light at the end of tunnel regarding this matter”. The money is gone and so do the ‘number one’ suspect. There are ‘stories’ that those involved in the ‘saga’ started to return back the money they have ripped off, but still can’t convince many as to be the case. Even if it’s going to be the case, these ‘perpetrators’ should face the music for what they have done!

    My worries are, for how long the people who ‘steal’ such a big amount of tax payers’ or donors’ money will continue to get away with it?

    The present situation doesn’t do any favour to Mr JK's government and its party; instead, it continues to put his reputation in tatters.

    Mzee Wauyagauyaga

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 25, 2008

    Trust me. kikwete know everything. baralali yeye akuiba pesa hizo.. ila siri ni ndogo sana. kikwete be honest. you new everthing n u new the dill. balali was sick time to time. so he wasnt in the office at the time. the New governor knows the way how that money is transported. n we al no the people who did this. so plz Mr president tells us what's moving on. kikwete kikwete kikwete. moogope Mungu toa siri yote.Ubalozi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 25, 2008

    jeneza halina kitu

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 25, 2008

    anonymous wa 2 wewe ndio mejidhalilisha!!!!!!!!!!!




    hayawiiiiii hayawiiiiii leo yamekuaaa hayaa jeneza ilooooooo

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 25, 2008

    Tanzanians hebu kuweni wastaarabu na moyo wa huruma, mtu amekufa mwacheni aende salama, hata Mungu atakuwa keshamsamehe kama alitubu, vije nyinyi hamtaki kusamehe na kusahau, wengine hapa mgebahatika kupata nafasi aliyoipata yeye duniani enzi za uhai wake mngefanya worse than he did, tena kama alifanya hayo maana inawezekana yeye ndio alitolewa kafara wengine wapone, acheni kumsimanga mtu kesharudisha number, Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 25, 2008

    Wabomgo tuwe wakweli kwa nini kama kweli huyu jamaa muhimu amefariki iweje msiba wake uwe ni kitu cha siri sana hadi kuingia kwa kadi mazishini?.

    Uongo wa aina hii ni hatari ila kama kweli amefariki Mungu ailaze roho yake mahali pema ila kama ni usanii Mungu awalaani ninyi na vizazi vyenu kwani mtu hutu amesababisha upotevu wa fedha za Watu wa Mungu ambao wanalipa kodi kwa mujibu wa maandiko matakatifu.

    Tunaomba tuambiwe ukweli kwa maaana yawezekana tunajiuliza ukweli huu kumbe mtu anakula raha Brunei au Malta.

    Kwa maana kuna wakati nilikuwa nchi fulani ikatokea tapeli mmoja akafa kwa kujizushia lakini kumbe hakufa na baada ya wiki tatu akakutwa nchini Brunei akiwa katika hoteli moja ya kifahari akila raha na vimwana kadhaa.

    Kwa picha ya namna hii inazidisha mashwali mengi, Broo Michuzi naomba utueleze ukweli ambao wewe unaujua, pls my broooo do.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 25, 2008

    Kama kweli Ballali kafariki dunia, alale mahali pema ila kama ni usanii laana hii iwaangukie wote waliohuisika kwa kuwaudanganya umma na watu wa Mungu.

    Nasema hivyo kwa maana kuna wakati fulani liwahi kutembelea moja ya nchi barani Ulaya ikasemekana kuwa Waziri wao mmoja aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya ufisadi amefariki kumbe ilikuwa ni mchanga wa macho.

    Ilibainika kwamba jamaa huyo alikimbilia nchini Brunei ambapo alikuwa akiishi katika hoteli moja huku akiendelea kupnda raha bila shaka shaka yoyote.

    kwa hiyo utata huu wa kifo cha Ballali ni moja ya vitendawili vinavyoisuimbua nchi kwa sasa.

    Tunaomba ukweli kwani haingii akili kuiona kuwa Mwafrika anakufa alafu msiba unakuwa wa watu maalum pekee, hili sijawahi kuliona na kwangu ni kituko cha mwaka ambacho kinastahili kuwekwa kwenye kitabu cha maajabu cha Genes.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 25, 2008

    we anony wa 8.06 unasema jamaa kafa! umeiona maiti? ktk mazingira ya kawaida mtu anakufa jeneza linafunguliwa watu wanapita kuona sura kwa mara ya mwisho, na kama tukio linatokea mbali basi picha zinapigwa na wengine wanaona. sasa hapa jeneza limefunikwa! unaaminije kuwa aliyemo humo ni balali? na kutokana na mazingira ya kifo chake na shutuma alizokuwa anahusishwa nazo huoni hapa kuna ka mchezo kamefanywa? hiyo kafara unayoisema ndio inayonifanya niulize maswali, kwa sababu kama kweli alitolewa kafara basi watuoneshe maiti yake. ina maana hata wewe unaamini kafara imefanyika?! hakyanani @€*%("!§/&

    karamagi

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 25, 2008

    Anon no 14, usijali, next time im at the Empire hotel in Brunei I'll look for him, I'll try Bali, St. Nevis and elsewhere too... but let's be serious..GET OVER IT..Wabongo mnajifanya siku hizi mmeamka na mahasira na kutaka kujua..basi wafuateni Mkapa na hao wengine..mbona hamuwataji..and they're one of the main sources katika hii kitu yote.. If he was the signature messenger so what? What was divides was taken by him..ndo shida ya wabongo...mnamfakamia aliyekufa toka ugonjwa wake na hamna nguvu wala nyuso za kuuliza wanaoishi..Mfuateni Chenge basi mmuulize ile scandal yake niaje.. MNAJIFANYA WANAUME MIDOMO TU HAKUNA COURAGE WALA VINGINEVYO......LET THE MAN REST IN PEACE..Pesa zenu walipa kodi half of you ran away ages na hamjawahi lipa kodi bongo msituletee hadithi za kaskazini saa hizi...kabebeni maboksi mlipo tena huko nako muanze kulipa kodi sio tu black jobs za kutumia numbers za watu wengine..

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 25, 2008

    Hebu Tazama picha za ndani ya kanisa

    http://www.ststephens.us/info/info.html

    Hakuna giza kabisa...

    Hii picha imepigwa kwenye pango gani?

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 25, 2008

    Anaishi kwenye villa lake Monaco bania hii najua utotoa ila ndio hivyo

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 25, 2008

    Rest in peace balaa li,mazishi gani hata ndugu wa marehemu hatuwaoni au mpiga picha ulishindwa pia kuwafikia hata walipokua wanatoka kanisani au kuingia? matokeo yake unapiga wazungu tu,tutamtafuta hata huyo mzungu atoeleze hiyo picha imepigwa siku gani na ilikua ni msiba wa nani hakuna kitakacho shindikana chini ya jua mpaka kieleweke...pls mmithipu hii ni muhimu pls usibane

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 25, 2008

    Annony wa 1.30 AM. is an idiot i've never seen before.

    Kila kilichoumbwa kitakufa na wewe na mimi ni marehemu watalajiwa, the only difference ni kwamba yeye amefia mbele ya mke na watoto wake na ameweza kuongea na kutoa wosia wake kwao na amewaeleza fundisho alilolipata katika maisha yake...lakini mimi na wewe hatujui hata tutakufaje!!! Sioni sababu yako wewe kufurahia kifo cha ndugu yako, mtanzania mwenzako ambaye jamii aliyoitumiakia imemnyanyasa kwa kumnyima haki ya kujitetea kwa hayo aliyotuhumiwa.

    In few words, this is just poli-trix...Balali was just a scape goat, don't be deceived that the late Balali as they say did all the evils as you've been exposed to.
    He was a good man working under Govt mandate, he was put there by President and all his autholities was under presidential directions...
    Do you think, by using your common sense that Prof. Ndulu,the current governor didn't know what was going on? If he didn't, then he is not fit for purpose. And if he did, why is he there!!!
    Before,we were witnessing "watu wakiwajibishwa kwa manufaa ya umma"...nowadays "watu wanawajibishwa kwa manufaa ya chama"...ndiyo maana tuhuma za kweli, watuhumiwa hupokelewa kwenye majimbo yao kwa nderemo na vifijo...chama au makada wa chama ndio huongoza mapokezi...tumeona kwa chenge...tumeona kwa Lowassa.

    Use your common sense and try to be human.

    Dr, Mwa-Balali rest in peace (RIP)

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 25, 2008

    Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

    Ingekuwa kuhusishwa na ufisadi ni sababu za kufanya mtu ajizushie kifo mzee wa vijisenti si angeishafanya kweli? Mbona yupo anatamba mitaa ya Usukumani kwa kupokelewa kwa hoi hoi, nderemo na vifijo?

    Wadau, mjumbe hauwawi. Mkuu wa wilaya ya nanihii amewasilisha tu, vipi wadau mnaomshambulia yeye kana kwamba yeye ndiye alikuwepo kwenye msiba huko DC?

    Mungu ampumzishe pema, Amina.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 25, 2008

    mie nikifa naombeni mnitie tu kwa tanuru halafu mtaona majivu. marekani misiba siyo kama africa, lazima ualikwe kama siyo ndugu siyo unazamia tu. labda na huu wameamua kufanya kimarekani. mtasema weee lakini ndo imeshatoka hiyo, wanga nendeni mkafukue kaburi. mwacheni baba wa watu a-rest in peace!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 25, 2008

    Wewe Amina acha unafiki, unakuwa kama umepewa hela. Au, na hii picha yenye mashaka umeituma wewe? Kama unaujua ukweli kaa kimyaaaa!

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 26, 2008

    hili jizi la mamilioni ya taifa halijafa bali huu ni mchanga wa macho eti azikwe marekani kamaoniiiiiiiiiiiiii givu mi a bureki ansi aponi time kulikuwako na watuhumiew wa hitla wakahamia cuba na sasa mamambo hayoooooooooooooooo kikwete ngoma nzito mwanakwetu ................huyu mhujumu uchumi hajafa bali ni mbwembwe za watu wenye hela

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 26, 2008

    teh teh teh anony wa 2:46 sasa hiyo picha ya kanisa la http://www.ststephens.us/info/info.html
    inahusiana nini na huu msiba? huko hilo kanisa unaloonyesha ni washington state na huyu tunaambiwa kazikwa washington DC.....
    Well Mungu anajau yote kama ni kitu tunadanganywa Mungu anajua ...Payback ni hapa hapa...wasicheze na machozi ya mnyonge

    I hope mafisadi watajifunza kutoka hili. Kuzikwa nje ya nchi ni kwa wakimbizi tu lakini mtu mwenye kwao ni vema kuzikwa nyumbani..Watoto wajukuu na jamaa watapenda kuzuru hata hilo kaburi sasa huku mbali kote si shida tu? Maisha haya...!!!!!!!!!!

    RIP

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 26, 2008

    MMH MIMI HUU MSIBA KWAKWELI KWANGU BADO KIZUNGUNKUTI HATA SIAMINI AKAMA KWELI KAFWA NA WALA SIAMINI KAMA HAJAKUFWA ASA SIJUI ITAKUAJE. NATULE TUVISENT VYETU INAMANA NDIO TUMEKUFWA NAVYO?

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 26, 2008

    HIVI KUWEPO KWA JENEZA KANISANI SIKU HIYO NDICHO KITHIBITISHO CHA KIFO CHA BALALI?

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 26, 2008

    MIMI SIAMINI HIKI UNACHOKIONYESHA HAPA KAMA KINA UHUSIANO WOWOTE NA MAISHA YA BALLALI. NAOMBA UTAFUTE HABARI NYINGINE

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 26, 2008

    Jamani mimi sioni cha ajabu hapo hata kama amekufa au hajafa ilikua lazima tudanganywe na hiyo ishu ingisha hivi hivi! Watu wanarudisha pesa za EPA lakini wana makapuni hewa pesa zinapokelewa wananchi tunaguna tu. ni kina nani wanaorudisha hatutajiwi majina wala kiasi. Haya balali alikua mtuhumiwa namba 1 na tume ilikua kwenye uchunguzi hakuwahi kuhojiwa hata siku moja ambapo kama muhusika mkuu angewarahisishia kazi kina mwema kwani ndiye signatory. Wakadai hawamtafuti yuko huru na asibugudhiwe. Sasa mnachoshangaa kutengeneza kifo ni nini? Nyerere watu kama hawa walifilisiwa na kustaafishwa kwa manufaa ya Umma sasa hivi unakumbatiwa na kuambiwa kula pesa zako kwa amani. Leo mimi nina vijisenti kama 10bln naambiwa uwaziri basi nini wasiwasi gani nina nyumba marekani. USIBANE MISUPU

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 26, 2008

    WADAU,MIMI NINA SWALI


    LINI TUTAAACHA U-TOMASO??

    NAOMBA WOTE MNJIBU KABLA YA KUENDELEA KUTOA MADA


    AMINA YUSUF

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 26, 2008

    jamani nikweli au !!!!!!!!!!
    mirojo nakuomba onyesha picha yake akiwa kaburini kabla hajazikwa ndiyo nitaamini ila usipo onyesha itakuwa unauza mbuzi kwenye gunia,
    sweet,
    Arusha.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 26, 2008

    Amina, sie utomaso na Udaku hatutaacha kamwe maana ndio hulka yetu iko ndani ya damu zetu inatiririka, kila kitu tunajua sie, kila jambo tunataka kuona sie, yaani hatuna mipaka. Na hata kama ndugu za Balali wangesema msiba uwazi na kila mtu aje aage, na jeneza lifunguliwe, bado watu wangesema siye yeye, imechukuliwa maiti ikafanyiwa plastic surgery kuwekewa sura ya Balali kitu ambacho sidhani kama kinawezekana medically, au tungekuja na tuhuma kuwa hiyo maiti imevishwa sura ya marehemu Balali iliyotengenezwa. Sasa nafikiri walichokifanya familia ya marehemu Balali ni sawa sawa, kwa sababu wangeonesha mwili wa marehemu kisha watu wakaja na utomaso wao na kusema kimefanywa hiki kimefanywa kile, nafikiri wangeumia zaidi kuliko hivi sasa.

    Rest In Peace Balali. Hakuna wa kutoa hukumu ila ni Muumba tu, na dunia ni mapito.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 26, 2008

    Haya kaka Michuzi tuambie kuhusu hiili jambo:
    Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuwa, Ballali aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Permian iliyopo Boston, Massachusetts, huku Serikali ikidai haijui halipo, mbali na kudaiwa kutendwa vibaya pia alipata hofu pale alipojisikia vibaya alipokula chakula wakati alipokuwa anatoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma.

    Chanzo chetu cha kuaminika na kisichotia shaka, kilitupasha kuwa Ballali alijua kinachoendelea kabla ya kuenguliwa katika nafasi yake na ndiyo kiini cha kuomba kwenda kutibiwa Marekani, ambako mke wake Anna Muganda ana uraia wa huko.

    Mtoa habari wetu alitupasha kuwa, mwishoni mwa mwaka jana Ballali alikuwepo nchini ambako aliitwa Dodoma na kufanyiwa mahojiano ‘maalumu’.

    Habari hizo zinasema kuwa Ballali alishangaa ni kwa nini aliitwa Dodoma wakati mahojiano yaliyotakiwa kufanywa yangewezekana hata Dar es Salaam.

    Inadaiwa Ballali alisindikizwa na mtu mmoja ‘mzito’ katika safari yake hiyo ya kwenda Dodoma, huku kile alichokula na kunywa alipokuwa kwenye ndege hiyo maalumu ikiwa ni utata mtupu.

    Chanzo chetu hicho kilizidi kutupasha mara baada ya kutoka Dodoma, Ballali alianza kulalamika kwa kutojisikia vizuri kitu alichotilia shaka kile alichotendwa katika safari yake.


    Mara baada ya kurejea Marekani, Ballali alifuatwa tena na afisa mmoja wa ngazi za juu wa usalama ili kumjulia hali wakati huo akiwa amelazwa katika Hospitali ya Permian.

    “Kubwa zaidi la kujiuliza ni kwamba watu wengi walipenda na walitaka kumuona Ballali akiwa katika hali mbaya na isiyo na matumaini. Tatizo linaanzia hapa,” kilisema chanzo chetu bila kufafanua.

    Awali gazeti hili lilikuwa la kwanza kufichua mahali alipolazwa Ballali, huku Serikali ikiendelea kufanya juhudi za kudai haijui mahali alipo.

    Uongozi wa hospitali hiyo iliyopo eneo la Andrews, Boston, Massachusetts ulipopigiwa simu na kutumiwa fax, ili kueleza kiini halisi cha ugonjwa uliokuwa unamsumbua Ballali haukutoa ushirikiano wa kutosha.

    Aidha, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu, aliendelea kushikilia msimamo wa Serikali na kudai hawana mawasiliano yoyote kuhusu mahali alipo Ballali, ingawa alisema kama wangemuhitaji wangeweza kumpata kwani wana mkono mrefu.

    Ilidaiwa kuwa makachero wa Tanzania walivamia Marekani kwa ajili ya kupeleleza nyendo na kujua mahali aliko Ballali, ili pale watakapomuhitaji kujua kuhusu fedha za EPA zipatazo Sh bilioni 133 isiwe shida kumpata.

    Naye Balozi wa Marekani, Mark Green Januari 28, mwaka huu alitoa taarifa ya Serikali yake na kudai hawajaombwa na Tanzania kumrudisha nchini Ballali na iwapo wangehitajika wangefanya hivyo.

    Green alisema wao walikuwa tayari kumsaidia Rais Jakaya Kikwete, kushughulikia ombi ambalo lingesaidia katika kutekeleza azma ya kumrudisha Ballali.

    Balozi huyo pia alipobanwa kueleza mahali alikokuwa Ballali, alidai hapafahamu na kuongeza kwamba sheria za Marekani hazimruhusu kutangaza nyendo na mahali walipo watu wanaoishi nchini humo.

    “Kila kitu hata kama ni fedha zilizoibwa BoT au Ballali kurejeshwa nchini kutategemea maamuzi ya Serikali ya Tanzania,” alisema Green.
    Habari hizi zilifuatiwa na kuyeyuka kwa Ballali nchini Marekani na kudaiwa kukimbilia katika Kisiwa cha Malta.

    Wakati anatangaza maamuzi ya Rais Kikwete kutengua uteuzi wa Ballali, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo alisema rais alifikia maamuzi hayo baada ya kukasirishwa na ripoti za kuwepo kwa ukiukwaji wa makusudi wa sheria, kanuni na taratibu za uuzaji wa madeni ya nje katika taasisi muhimu na nyeti kama BoT.

    “Kwahiyo ameamua hatua za kisheria na kiutawala zichukuliwe dhidi ya watu na kampuni zilizohusika na kashfa hiyo,” alisema.

    Luhanjo alisema kampuni 13 kati ya hizo 22 zilipokea zaidi ya Sh bilioni 90.3 kwa kutumia kumbukumbu, nyaraka, hati batili na za kughushi, wakati nyingine tisa zilipata zaidi ya Sh bilioni 42 bila kuonyesha nyaraka zozote za kuhakiki malipo hayo.

    Alitaja kampuni mbili miongoni mwa hizo kuwa ni Rashtas (T) na G & T International Limited zililipwa fedha pamoja na kutosajiliwa na Msajili wa Makampuni (BRELA).

    Kampuni zilizovuna mabilioni ya shilingi kwa mujibu wa taarifa ya Luhanjo ni Bencon International Ltd of Tanzania, VB & Associates Ltd, Bina Resorts Ltd, Venus Hotel Ltd, Njake Hotel & Tours Ltd, Maltan Mining Company na Money Planners & Consultant.

    Nyingine ni Bora Hotels & Apartments Ltd, B.V. Holdings Ltd, Ndovu Soaps Ltd, Navy Cuts Tobacco Ltd, Changanyikeni Residential Complex, Kagoda Agriculture Ltd, G&T International Ltd, Excellent Services Ltd, Mibale Farm , Liquidity Service Ltd, Clayton Marketing Ltd, M/s Rastash, Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloloma and Brothers na Karnel Ltd .

    Luhanjo alitaja kampuni ambazo ripoti ilisema yalilipwa zaidi ya Sh bilioni 90.3 kwa kutumia vielelezo vya kughushi na hati bandia ni, Bencon International Ltd of Tanzania, VB & Associates Ltd , Bina Resorts Ltd, Venus Hotel Ltd, Njake Hotel & Tours Ltd, Maltan Mining Company na Money Planners & Consultant.

    Nyingine ni Bora Hotels & Apartments Ltd, B.V. Holdings Ltd, Ndovu Soaps Ltd, Navy Cuts Tobacco Ltd, Changanyikeni Residential Complex, Kagoda Agriculture Ltd.

    Baada ya kashfa hiyo, Rais Kikwete aliunda timu iliyoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, John Mwanyika ili kushughulikia suala hilo kwa kuchunguza na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watuhumiwa.
    Ballali amekufa wakati tume iliyoundwa na Rais Kikwete kuhusu upotevu wa fedha za EPA ikiwa inaendelea na uchunguzi wake.

    Mbali na hilo, Ballali anakuwa gavana wa kwanza kuenguliwa katika nafasi yake tangu nchi ipate uhuru mwaka 1961.

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 26, 2008

    kamkabeni MH Kikwete,ndiyo mwenye hizo hela

    michuzi usinibanie!

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 26, 2008

    No pun intended, lakini nadhani wengi wetu tunapelekwa na mkondo, whether ni kwa kusoma kilichoandikwa through different media outlets au word of mouth.

    Hivi msomi gani asiyejua kuwa Governor wa Central Bank is just a banker na hana any authority na sio signatory wa Serikali? Lakini badala ya kuelewesha jamii wengi wetu tunatoa frustrations zetu kwa kumhukumu Balali.

    As much as we spend time kusoma na ku-post comments kwenye blogs, tu-research na kujua Central Banking System ainavyo-operate, na tuwasaidie wengine waelewe.

    Signatories ni watatu tu, na Governor sio mmoja wao.....

    Let him rest in peace.....

    Malima died mysteriously tukaletewa jeneza na halikufunguliwa, nani anajua kilichokuwa ndani? Kutokufunguliwa kwa jeneza isiwe nongwa!

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 27, 2008

    Anony May 26, 10:35: Aliyekuambia kuwa waislamu huwa wanazikwa na Jeneza nani? Unajifanya unajua kumbe hujui-Acha porojo!

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 27, 2008

    Ndugu zangu Watanzania,mbona imekuwa matatizo kuonyeshwa hizi picha.Je ningekaa kimya nisingemtumia kaka michuzi mngeona wapi?mngekuwa na uhakika gani?.Kwa nini mnamwonea Kaka michuzi,yeye hana kosa lolote lile.Amewawekea picha ili kujua kulikuwa na ibada huko.Na nina kuambieni kuwa kulikuwepo pia na watu kutoka world bank pia ,ambako marehemu aliwahi kufanya kazi huko.sasa tusimlaumu na kumtukana Kaka michuzi.kama hamuamini kuna baadhi watanzania tuliudhuria ,jaribu kuuliza ubalozini,mimi nilipata kuongea na watoto wake pale pale mara baada ya misa[wa kiume na wa kike].

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 27, 2008

    Anony May 27th 1:00am, soma vizuri usipayuke tu, nimeandika kuletwa sio kuzikwa! Kumbuka alifia England, kwa akili yako unadhani aliletwa na sanda? Na nani anajua kilichokuwa ndani ya sanda na mkeka kabla ya kuzikwa?

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 27, 2008

    Wewe Michuzi, usitufanye sisi ni wajinga sawa!!!, usipate kiburi kwa kuwa wewe ni kibaraka wa serkali, yaani unaungana na mafisadi kutudanganya, na kinamama wajawazito wangapi wangekuwa hai leo kama hao mafisadi wakiongozwa na RA, balali, etc wasingepokonya pesa za walala hoi,!!!??? upost usipost hii message utajijua, ila huuu ndio ukweli,

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 27, 2008

    HAKUNA HOSPITALI IITWAYO PERMIAN WALA ANDREWS HAPA BOSTON, MA! MMEDANGANYWA! HEBU FANYA GOOGLE SECHI KAMA HAMNIAMINI!

    Mdau Boston

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 28, 2008

    Anony May 26, 10:35: nanukuu "tukaletewa jeneza na halikufunguliwa, nani anajua kilichokuwa ndani?", kauli zako mwenyewe zitakufunga, haya endelea na porojo zako!

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 28, 2008

    Kwa Kweli Watanzania Tutajuaje kuwa huyo aliye kufa ni Balali. Msiba wake ulikuwa sio wakawaida. Kwanza tangia lini waTanzania tunakuwa cremated? Kama sio wahindi tu Tanzania. Kati msiba wake huko D.C kulikuwa hamna hata maua na familia ilikuwa haionyeshi majonzi yoyote. Mimi nadhani kuwa huyu mtu bado huko hai na anachekelea saa hi. Bila shaka hii kitu yote was planned. Wote tunajua kuwa aliiba hela BOT sasa mbona serekali haifanyi kitu, hata kuzirudisha hizo hela basi. Watanzania wenzangu naomba maoni yenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...